Rammy Galis Amtolea Povu Zito Duma

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis amekuja juu msanii mwenzake Duma na kumtolea Povu zito siku chache Baada ya Duma kutumia nyimbo vya habari na kuweka wazi kuwa msanii huyo haiwezi Sanaa.

Rammy Galis amefunguka na kudai kuwa Duma ni zero brain na mpiga  kelele ambaye anatumia vyombo vya habari na wana habari kwa ajili ya kumzungumzi yeye.

Katika mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Rammy Galis amefunguka haya:

Duma anapiga sana kelele kwenye media ilitakiwa kazi anazofanya haziendani na makelele yake anakuwa anaonekana Kama Zero brain na pia ni wazi Kama huwezi kutufananisha kwa sababu Mimi siendi kutafuta media ili nipige kelele nasubiria Media zinitafute niongee mambo ya maana”.

Siku chache zilizopita Duma alimtolea Povu zito Rammy Galis na kumchana kuwa hana kipaji cha kuwa kama Kanumba na hawezi kuwa kama Kanumba hata siku moja.

 

 

 

Meneja Maneno Amtetea Duma Kuhusu Swal la Ushirikina.

Meneja wa msanii wa bongo movies David maarufu kama Duma amefunguka na kutoa utetezi wake kwa msanii anaemsimania na kusema kuwa pamoja na kwamba watu wamekuwa wakisema kuwa msanii wake amekuwa akitumia ndumba lakini yeye anachoamini kuwa anachopitia Duma sasa hivi ni wakati wa mungu na wala sio kitu kingine kama watu wanavyosema.

Akiongea na EATV , meneja Maneno anasema kuwa pamoja na yote yanayoendelea kusemwa lakini anaamini kuwa kujituma ndiko kunakoleta mafanikio.

Tuhuma za ushirikina zipo maana huwezi kuwakataza watanzani kusema yale wanayoyasema hata siku moja, na ikifika siku Duma akifanikiwa watasema kuwa Duma ni Freemasons na kuongelewa mengi juu yake, lakini tu unapokuwa maarufu kuongelewa kupo na ni kawaida.

Hata hivo meneja maneno anasema kuwa amegundua kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa na mabadiliko hayo hayawezi kuja kama hakutatumika nguvu kubwa na nyingi kwa ajili ya kufanya hivyo na ndio maana yeye ameamua kujikita na kufanya kaz na Duma ili kufanikisha hayo.

Meneja huyo anasema kuwa pamoja na kwamba watu wamekuwa wakienda kwa waganga kuloga lakini mwisho wa siku unachotakiwa kujua ni kwamba hata waganga pia wanamtegemea mungu vilevile.

kwa mganga ni kama nyumba tu au gheto unakwenda unapiga stori tu fresh,nilikuwa sijajua kuwa kumbe hata mganga pia ana,tegemea mungu kwa sababu angekuwa anatumia nguvu zake basi angesababisha watoto wak waolewe na mawaziri na matajiri lakini mwisho wa siku wote tunabaki  kusugua rumba na kunyunyiza dawa.kwaio ukimuamini Mungu unafanikiwa kila kitu na ninachoamini kuwa Duma anachofanya kwa sasa ni wakati wa Mungu.”

 

Duma-Bongo Movie Inakuwa na Wasanii Tunafaidika

Msanii wa filamu za Bongo Movie Daud Michael maarufu kwa Jina la usanii kama Duma amefunguka na kudai sanaa ya Bongo Movie inakuwa kwa kasi.

Duma ambaye alifanya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Nipe Changu amedai kwa sasa Kikula kwa filamu za kibongo ni kwa kasi kubwa Lakini pia wasanii wanaona faida.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Duma Duma alisema sanaa ya Tanzania kwa sasa inakua na anaona jinsi ambavyo wasanii watanufaika.

Niseme tu kwamba nashukuru kwa sababu mifumo inayokuja ni ya faida, siyo mifumo ya kuuziana haki miliki hivyo naamini kila msanii ambaye atafanya kazi zake vizuri, anakwenda kunufaika nazo, kikubwa ni kumuomba Mungu ili tuweze kufikia malengo”.

Kauli hii ya Duma inatia moyo kwani kwa muda mrefu sasa tangu Steven Kanumba afariki dunia kumekuwa na pengo kubwa katika sanaa hiyo na hata watu kudai Kanumba alikufa na Matumaini ya kukua kwa sanaa.

Duma Afichua Siri ya Watu Kujaa Katika Uzinduzi wa Nipe Changu.

Msanii wa bongo movie David Michael amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kujaza watu wengi katika uzinduzi wa filamu yake mpya ya Nipe changu uliofanyika wikiendi iliyopita ni kutokana na nguvu kubwa alizopewa na mwenyezi mungu na wala sio uchawi kama watu wanavyosema katika mitandao ya kijamii.

Akiongeana EATV, Duma anasema kuwa Mungu amempa kipaji na nguvyu na wala sio kama minongono inayoendelea kuwa watu waliojaa Mlimani City Jumamosi ilikuwa ni utumiajiwa nguvu za giza alizotumia duma katika filamu iyokupata umaarufu.

Mimi kujaza watu huu ni ufalme na nguvu nilizopewa na mwenyezi Mungu, huu ni ufalme niliyopewa na mwenyezi Mungu na wala sio mimi, watu hawa wamekuja kwa mapenzi yao kwa DumaHakuna uchawi unaotumika kwangu bali ni kufanya kazi tu.

Lakini pia Duma anasema kuwa kupitiakazi hiyo ambayo yeye anaamini kuwaitafanya bizuri itawanyamazisha wale waliokuwa wanaongea kuwa hajui kazi.

Duma Akiri Kumkubali Sana Johari

Msanii wa filamu za kibongo Daudi Michael maarufu kama Duma amefunguka na kukiri kuwa hakuna msanii wa kike anayemkubali kama anavyomkubali Johari.

Duma amekiri kuwa Msanii huyo mkongwe (Johari) ndio aliyempa yeye hamasa ya kuweza kuingia kwenye filamu miaka ya nyuma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Duma amesema kuwa hata akiulizwa mahali popote kuhusu msanii aliyemfanya aingie kwenye uigizaji hawezi kuona aibu kusema ni Johari kwa sababu mpaka leo hii ndio msanii wa kike anayempenda sana.

Siwezi kuwa mnafiki hata kidogo ukweli ni kwamba Johari ndiye aliyenifanya niingie kwenye tasnia ya filamu kwa sababu alikuwa akiigiza kiuhalisia kwenye filamu yake ya Johari na mpaka leo ni mwanamke wa kwanza kumpenda Bongo Muvi“.

Johari alijizolea umaarufu miaka ya nyuma Kupitia maigizo kadhaa aliyokuwa anafanya na ambapo alikuwa anaigiza na wasanii kama Ray, Marehemu Kanumba na wengineo.

Gabo Hana Hadhi ya Kuwa na Bifu Na Mimi- Duma

Muigizaji wa Bongo movie Daudi Michael maarufu kwa Jina la usanii kama Duma amefunguka na kudai kuwa hana bifu na msanii mwenzake Gabo na wala hana hadhi hiyo.

Kwa muda mrefu kumekuwa na kama ugomvi fulani kati ya Duma na Gabo na hata juzi juzi tu wawili hao wameonekana wakirushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii na hata vyombo vya habari.

Lakini Duma amedai hana bifu na Gabo na taarifa zinazoendelea kusambaa Kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii sio za kweli.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Duma alisema hayupo katika bifu na Gabo kama watu wa mitandao wanavyovumisha ingawa hana mawasiliano naye kwa sababu hana kitu cha kuongea naye ila akiwa na kazi anaweza kufanya naye na akamlipa.

Sina bifu naye kabisa na wala hatuna mawasiliano kwa sababu mimi ni bosi wa kampuni yeye ni msanii wa kuigiza sasa tutaongea kuhusu nini? Labda nikiwa na kazi nitamwita afanye na nitamlipa ila najua yeye hawezi kuniita kwa sababu hajawahi kuzalisha filamu”.

Kwa muda mrefu sasa wasanii hawa wamekuwa wakisikika wakirushiana madongo kama hayo lakini sababu kamili ya kutoelewana haijulikani.

Gabo na Duma Watoleana Maneno Kisa Kauli Ya ‘Kanumba Wapya’

Staa wa Bongo movie aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa kiume Gabo amejikuta katika vita ya maneno a Msanii mwenzake Duma baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu Marehemu Steven Kanumba.

Gabo alipofanya Interview na kituo kimoja cha habari, Gabo alisema ili kuiokoa Bongo Movie wanahitajika kuandaliwa wakina Kanumba wengine watakaoweza kuikoa tasnia hiyo.

Baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Gabo, Duma amemjia juu na kusema hajapendezwa na kauli hiyo kwani yeye na wasanii wenzake wana uwezo sana na watu waache kumtaja Steven Kanumba.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Duma alimwaga povu hili:

Kama kweli wewe unajiamini ni msanii mzuri Ian uwezo unapambana na unajituma huwezi ukasema tunahiyaji kanumba wengine kwani sisi hataweza kufanya alichofanya Kanumba? TUnaweza ila cha muhimu ni kujituma na kujua wapi tunapokosea.

Lakini pia Duma aliendelea kumtolea povu zito Gabo ikiwemo kumtolea maneno makali:

Unajua sio kila staa ana akili timamu kuna wengine mitambo tu tupo nao Kwenye Industry lakini ndio uwezo wao umeishia hapo lakini kama unajiamini uwezo wako unaweza kufanya kazi kubwa zaidi”.

Lakini pia Duma amewataka watu waache kumtaja taja Marehemu Kanumba lakini badala yake waelekeze juhudi zao Kwenye kupiga kazi nzuri zaidi.

Nataka Kuleta Heshima ya Bongo movie- Duma

Muigizaji wa Bongo movie Duma amefunguka na kusema anataka kurudisha heshima ya Bongo movie baada ya kupotea kwenye ramani.

Miaka Kama mitano nyuma Bongo movie ilikuwa mbali tofauti na ilipofikia Leo kwani hivi sasa no Kama imeshakufa kabisa hii yote ikisababishw na kukosekana kwa ubunifu.

Lakini mkali wa Bongo movie Duma amesema anataka kuketa heshima tena katika Bongo movie na ndiondio maana ameamua kmleta muigizaji John K kutoka Australia ambaye alikulia Tanzania na mwenye asili ya Burundi wafanye naye filamu hapa nchini.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv , Duma aamefungua haya kuhusu kuleta heshima kwenye tasnia hii ya Bongo movie.

Kwanza naomba Watanzania watusapoti Sana kwani tunataka kuleta heshima ya Bongo movie, nimemleta John K na tunarudisha heshima ya filamu Tanzania na kuonyesha jinsi gani Duma anapambana kwa ajili ya tasnia hii na sio ya mtu mmija mmoja so Mimi napambana kwa ajiki ya industry nzima na sina matatizo na mtu”.

Duma amesisituza anaamini yeye na John K watafanya vizuri kwa sababu John K ni staa anayefanya vizuri katika filamu nchini Australia.

Nay Wa Mitego na Duma Wameingia Kwenye Bifu Zito

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ney Wa Mitego na muigizaji wa Bongo movie Duma wamejikuta wakiwa katika pande mbili tofauti za shilingi baada ya kuingia kwenye bifu zito.

Bifu hili lilianzia kwenye mtandao wa kijamii huko Instagram baada ya Nay Wa Mitego kuweka maoni kwenye picha hiyo kulikuwa kuna wakali watatu wa Bongo movie ambao ni Rammy Gallis, Gabo na Duma na kisha ilisindikizwa na swali liliouliza ‘Je nani  mkali wa fasheni hapo?’ Basi baada ya kuona hivyo Nay Wa Mitego alienda ku-comment na kuandika ‘ Tafadhali msimfananishe Gabo na vitu vya kipuuzi’ maneno ambayo yalimkera sana Duma.

Baada ya maneno hayo kuenea mtandaoni Gabo alimwaga povu lake kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa;

Kwanza nilikuwa Nairobi nafanya project nikaona hizo comments watu tofauti tofauti wakanitumia mimi nikafurahi nikaona ni kitu kizuri ila naomba nimwambie Bwana Emanuel,  Ney Wa Mitego ameingia choo cha Kasilo kwa sababu ameshawahi kumtibua Niva, alishawahi kumtibua Yusuphu Mlela akatulia tu ila mimi ni namba chafu asione watu wamenyamaza ila mimi peke yake namtosha Ney Wa Mitego yaani mimi ndio namwambia Ney asiingilie mambo ya Bongo movie kama anatafuta kiki akatafute huko huko kwa wanamuziki wenzake asituingilie Bongo movie kwa sababu ameshatuongelea sana mara oh Bongo movie imekufa mara nini sijui sasa basi inatosha namkanya Ney aachane na sisi kama hana ishu arudi kwao Manzese akawe mkabaji maana alijuwa kibaka zamani hivyo awe na heshima maana mwisho wa siku mziki wake umeshuka”.

Pia Duma amedai Ney hana haki ya kuiongelea vibaya Bongo movie kwa sababu pale alipo hana kolabo hata moja na nsanii wa nje lakini hao anaowasema Bongo movie wameigiza na wasanii mbali mbali wa nchi za nje.

Bifu La Gabo Na Duma Bado Linafukuta

ingawa wenyewe wanasema kuwa hawana ugomvi lakini kumekuwa na kurushiana kwa maneno baina ya wasanii wa Bongo movie kati ya Duma na Gabo Zigamba, bifu ili lilianza pale ambapo Duma alianza kwa kumponda sana Gabo na kumwambia kuwa hajui kuvaa, hata hivyo Duma amekuwa akikerwa na tabia ya Gabo kukaa kimya kwa muda mrefu bila kufanya filamu ili kikudhi kiu ya mashabiki zake.

Duma amekuwa akisema kuwa hana ugomvi wowote na Gabo ila tu anajaribu kumuweka sawa msanii mwenzie kwa sababu ni moja ya wasanii wa Bongo movie mwenye mashabiki wengi wanaopenda kazi zake, lakini ili aendelea kuwaweka msahabiki zake na kuwaongeza ni lazima  ajitaidi kutoa filamu mpya ili kuwafanya mashabiki waaendelee kumsapoti.

Hivi karibuni Duma alifunguka na kusema tena kuwa msanii Gabo amekwa akibweteka tu katika kufanya kazi, hayo yamekuja baada ya msanii Duma kufanya uzinduzi wa filamu yake ya ‘bei kali’, ambapo Duma alimualika Gabo katika uzinduzi huo lakini Gabo hakutokea.Akiongea na waandishi wa habari Duma nasema kuwa kilichomsikitisha ni kwanini Duma aliamua kutokutokea katika uzinduzi huo ilhali alipewa mwaliko.Kwa mujibu wa Duma, anasema kuwa katika sehemu kama hizo ndipo wasanii wanapopata nafasi ya kukutana na mashabiki wake na kujifunza mambo mengi anayohusiana na filamu kwa sababu kuna kuwa na mkusanyika wa watu wengi hivyo kuna mengi ya kujifunza.

alipopata nafasi ya kuongea na kuelezea kwanini gabo hakuonkana katika uzinduzi huo, msanii duma alisema “yeye kutokuwepo anakosa vitu vingi sana,gabo anashuka kimasoko,mimi na yeye hatuna mugogoro wowote ila tu tunaelezana ukweli wa mambo ilitueze kutoa tasnia hapa ilipo na  kuipeleka sehemu nyinginw.mimi simkosei heshima kwa sababu sijamkosea kitu chochote kwa sababu sijawai kumtukana tusi hata moja,Gabo ana mashabiki wengi  sana yeye anabweteka  tu, no man, fanya kazi” ameongea Duma

Inawezekana ikawa ni njia ambayo Duma anaitumia kukuza tasnia ya filamu lakini, nadhani njia inayokuwa bora zaidi ni wawili hao kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao ili kuunda mbinu itakayokuwa bora ya kukuza tasnia hiyo kwa pamoja.