Ben Pol Akana Kuwa Kwenye Penzi na Ebitoke

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amekana kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mchekeshaji kutoka Timamu Tv, Ebitoke.

Tetesi za Ben Pol na Ebitoke kuwa Kwenye Mahusiano zilianza kusikika Mara baada ya Ebitoke kukiri hadharani kuwa anampenda Ben Pol na kuwa angefurahi sana kuwa naye.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ben Pol alikataa kukubali kuwa Kwenye Mahusiano na Ebitoke au hata kuwahi kuwa naye tofauti na Ebitoke ambaye ameshasema mara kwa mara kuwa wapo Kwenye Mahusiano:

Kuhusiana na mahusiano hayo its Complicated ingawa kila kitu nilishaongea ila kila kitu kilichoonekana kwenye vyombo vya habari ni sehemu ya maisha yangu”.

Lakini pia Ben Pol alifunguka na kuendelea kunena:

Vyovyote mtu atakavyohisi aendelee kuhisi ila mimi siwezi kutamka chochote ila muda ukifika kama kweli niko kwenye mahusiano ntaweka wazi na kama siko nae pia itafahamika”.

Imeshawahi kusemekana kuwa Ben Pol hajawahi hata kuwa Kwenye Mahusiano na Ebitoke bali ilikuwa ni kiki tu.

“Sio Kiki Mimi na Ben Pol ni Wapenzi”- Ebitoke

Mchekeshaji kutoka Timamu tv asiyeisha vituko, Ebitoke amefunguka na kusisitiza kuwa yeye na staa wa Bongo fleva Ben Pol wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi na sio kiki kama wengi wanavyosema.

Tangu walivyotangaza kuwa wapo kwenye mahusiano Kumekuwa na tetesi nyingi huku watu wengi wakidai kuwa hawana mahusiano yoyote bali wanatafuta tu kiki ili Ben Pol auze mziki wake na Ebitoke ajulikane kwa komedi.

Lakini mara kwa mara Ebitoke amekuwa akisisitiza kuwa wenyewe wapo kwenye mahusiano na amekuwa akisisitiza kuwa anampenda sana Ben Pol ingawa inasemekana ana mpenzi mwingine.

Ebitoke ameendelea kukiri penzi lake na Ben Pol Kwenye interview aliyofanya na Bongo 5 ambapo amedai kuwa hawatafuti kiki bali wapo kwenye penzi zito:

Watu wengi wanajua mimi na yeye hatuna mahusiano na watu wameshakariri kama ni kiki ila tumewaacha waendelee kuwa na mtazamo huo wanaouona lakini mimi na Ben Pol tunaendeleza mahusiano yetu na tunafnya kimya kimya. Ben Pol amefikia hatua ya kunisapoti na mimi huwa namsapoti maana huwa tunasapotiana kwaiyo mkiwa pamoja lazima mambo yawe hivyo”.

Lakini pia Ebitoke amefungukia tetesi zinazomzunguka mchekeshaji mwenzake Mama Ashura ambapo inadaiwa Ebitoke alimuibia bwana, jambo ambalo amelikataa na kusema kuwa Mama Ashura yupo anatengeneza kazi zaidi siku si nyingi ataonekana.

 

Ebitoke Aibua Mapya Kuhusu Penzi lake na Ben Pol

Mchekeshaji kutoka timamu TV Ebitoke ameibuka upyaa na habari za kinachoendelea baina yake na mpenzi wake supastaa wa Bongo.fleva, Ben Pol.

Ben Pol na Ebitoke wamesemekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini mara imeonekana kwamba kuna utata Fulani kwemye mapenzi yao.

Ebitoke alianzisha mahusiano na Ben Pol baada ya kutangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa anavutiwa naye na angependa kuwa na mahusiano naye, baada ya muda mfupi mapicha picha talianza kusambaa mtandaobi zikiwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye mahaba mazito.

Miezi michache iliyopita wakati wa tamasha la Fiesta Ebitoke alitangaza kuwa ameamua kuachana na Ben pol kwa sababu ameona kama ni mtu ambaye haeleweki au hataki kuwa na yeye kwani amekuwa akimpotezea bila sababu akimtumia meseji hajibu na mengineyo.

Lakini Ben Pol aliibuka na kudai shutuma za Ebitoke kuwa anampotezea kwa kutojibu meseji zake wala kupokea simu zake sio za kweli kwani anafanya vile kwa sababu ya kazi nyingi na kwa kipindi kile alikuwa hawezi kupojea na zake kwa sababu walikuwa wanaenda mikoani kufanya Fiesta hivyo network ilikuwa mbovu ndio maana alikuwa akimpigia hampati.

Siku za hivi karibuni Ebitoke ameibuka na kudai kuwa hajawahi kuachana na Ben Pol bali kilichotokea ni kwamba aluona kama Ben Pol kama anampotezea Fulani hivi hivyo akaamua kumuweka kando na kukomaa na mishe mishe zake.

Ebitoke Amebwaga Manyanga Kwa Ben Pol

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu TV, Ebitoke amefunguka kuwa ameamua tu ayabwage manyanga kwa aliyekuwa anadaiwa mpenzi wake mwanamuziki wa bongo fleva Ben Pol.

Siku za nyuma habari zilivuma kuwa Ebitoke anatoka kimapenzi na Ben Pol hii ilikuja kutokana na Ebitoke kuweka wazi hisia zake kuwa anampenda Ben Pol jambo ambalo lililompelekea Ben Pol kumpokea  Ebitoke kwa mikono miwili na kumfanya mpenzi wake. Lakini siku mbili hizi kumekuwa na drama nyingi ambazo zinakuwa zinawahusisha wawili hao ambapo Ebitoke alienda kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa Ben Pol ameamua kumpotezea yaani hapokei simu zake akimpigia wala hataki kuongea naye kitendo alichodai kilimuumiza, lakini Ben Pol alipoulizwa alidai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka asipokee simu za Ebitoke sio kuwa anampotezea bali ni kwa sababu yupo kwenye tamasha la fiesta hivyo sehemu nyingi wanazoenda hakuna mtandao na pia yupo na ubize kidogo.

Kwenye mahojiano na TBC 1 katika kipindi cha Papaso, Ebitoke aliweka wazi kuwa kutokana  na ubize wa Ben Pol na malengo yake  ameamua tu kumuacha;

Unajua mapenzi ni hisia, nahisi ni kama nilikuwa kama namlazimisha lakini nimegundua siwezi nikakosa furaha nikashindwa kufanya baadhi ya malengo yangu, kwa hiyo nimeamua kumuacha afanye maisha yake, ameniacha na mimi nimemuacha tunimeamua kutulia nifanye mambo yangu”.

Amefunguka Ebitoke, lakini pia amesisitiza kuwa kuanzia hivi sasa hatarudia kosa la kumtangaza mpenzi wake kwenye mtandao wa kijamii tena yaani hata akipata mpenzi mpya hawezi kuja kumtangaza hadharani ni kitu alichojifunza ni kukaa kimya kuhusu uhusiano wake.