Lulu Afungukia Tetesi Za Kuwa na Mimba

Msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa sio mjamzito na hata alipotoka gerezani hakuwa mjamzito.

Lulu alitoka gerezani mwaka jana Baada ya kutumikia kifungo kwa miezi kadhaa lakini Baada ya kutoka kuna tetesi zilisambaa kuwa ametoka mapema kutokana na ujauzito na pia alikuwa ameongezeka kwa kiasi kikubwa.

Lakini siku ya Leo kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Lulu ameweka wazi kuwa hajawahi kuwa mjmzito kabisa bali alinenepa alipokuwa jela na kuongezeka karibia kilo 20.

Lulu amesema taarifa zilizowahi kusambaa kuwa alikuwa mjamzito hazily was za kweli bali alivyotoka jela alikuwa ameongezeka kilo 20 hivyo kupelekea mwili Wake kuwa mkubwa sana.

Lakini pia amefungukia tetesi za kugombana na Mpenzi Wake Majizzo ambapo amesema kuwa hawezi kuongea chochote kuhusu maisha yake binafsi:

Watu wanatengeneza vitu vyao ili wapate jambo kutoka kwako, watu wanatengeneza mambo yao, Mimi kuwa maarufu haimaanishi kila kitu katika miasha yangu lazima kiwe maarufu, hata mahusiano yangu yawe maarufu.

Juu ya hilo la kuvua pete Siwezi kukubali wala kukataa wacha waamini wanavyoamini”.

 

Lulu Apiga Mnada Nguo Zake Kusaidia Wasiojiweza

Msanii wa filamu za Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ameuza  nguo zake kwa nia ya kusaidia watu ambao wanaishi katika mazingira magumu.

 

Siku ya Jumamosi, Januari 26, 2019 Lulu aliwakabidhi nguo  watu walionunua katika zoezi lake la kuuza baadhi ya nguo zake kwaajili ya kukusanya fedha ili kuwezesha project yake ya Save My Valentine, alilolenga kuwasaidia wasiojiweza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari, Lulu alisema kuwa kwa siku ile alikabidhi takribani nguo 36 kati ya 40 ambazo tayari zilikuwa zimeshapata wateja na kwamba mwitikio wa zoezi hilo umekua mzuri na unatia moyo kwa sababu watu wamepokea wazo lake vizuri na kumsapoti.

Mimi nina nguo nyingi sana, hivyo nilifikiria baadhi ya nguo kuzigawa bure kwa watu wasiyojiweza, lakini zipo nilizokuwa nikenda nazo kwenye events na shoo, nikaja na wazo baada ya kuona bora niziuze ili nipate pesa ya kuwasaidia watu wasiyojiweza ambao kwangu mimi nitasherehekea nao Siku ya Wapendandanao kama Valentine wangu, Februari 14.

Zoezi bado linaendelea, nitaposti tena jumatatu na watu wanaohitaji tutawasiliana ili wanunue. Ninafanya hivi kwa sababu nataka siku moja nikiondoka duniani niache alama ya mazuri niliyofanya, nimefanya mabaya mengi, nimepitia magumu mengi katika maisha yangu, lakini sasa hivi ni wakati wa kufanya angalau mema ili siku moja nikumbukwe kwa hiki ninachiokifanya”.

 

 

Mh Makonda Atia Neno Mahusiano ya Lulu Michael.

Mh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefunguka na kuongelea mahusiano ya mwanadada lulu michael na mpenzi wake majizo hasa katika kila hatua wanayoipiga wawili hao ikiwa ni hatua kubwa kuelekea kufunga ndoa.

Ikumbukwe kuwa Majizo na Lulu wamekuwa wapenzi wa muda mrefu lakini hata baada ya Makonda kutangaza kuwa kama mwanaume huyo hatotaka kumuoa lulu  basi atamfunga,.

Katka ukurasa wake Paul Makonda aliandikahaya baada ya wiki iliyopita mwanadada huyo kutolewa mahali na mume wake huyo mtarajiwa “mafanikio yenu yanabeba watu wengi na katika kila hatua mnaonekana kuwa hamtanii,basi Mungu wangu akawaonyesha njia mfikeie mafanikio mpate kuwa msaada kwa wengine”

Mpaka sasa wawili hao wamesgafiki hatua nzuri ya kufikia ndoa yao.

Jeshi la Magereza Lakanusha Taarifa Za Lulu Kuwa Huru

Jeshi la magereza limekanusha taarifa zilizosambaa siku ya Jana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu amekuwa huru baada ya kumaliza kifungo chake.

Kupitia kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo, Amina Kavirondo, amesema kuwa muigizaji huyo bado ni mfungwa kwani kuna utaratibu uliowekwa ambao atapaswa kuufuata ili aweze kuachiwa huru na

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha EATV, Bi. Amina amefunguka na kusema:

Taratibu nafikiri zinaeleweka, (Lulu) anakuwa bado ni mfungwa, na anapokuwa na kifungo hicho cha nje kuna taratibu zake, akimaliza basi kuna taratibu kama mfungwa yeyote, hata kama ni maarufu. Kile ambacho Lulu atafanyiwa ndicho atakachofanyiwa mfungwa mwingine yeyote, ‘treatment’ yetu ni sawa na wafungwa wengine”.

Lakini pia Bi. Amina amesema kuwa Lulu mwenyewe anajua taratibu za kufuata ili aweze kuachiwa huru:

Mwenyewe anajua anatakiwa afanye nini, yule ni mfungwa kama wengine, hawezi kumaliza akaondokea kule kule”.

Taarufa za Lulu kumaliza kifungo zilikuja baada ya kudaiwa kumaliza rasmi kifungo chake cha nje siku ya jana.

Majjizo Amvisha Pete ya Uchumba Elizabeth Michael.

Ile ndoto na stori iliyokuwa ikisubiriwa kwamuda mrefu kuhusu mahusino ya mwanadada Lulu Michael na majizo ambae ni bosi wa EFM imkeuwa yenye kheri baada ya mwanaume huyo kuamua kumvisha pete ya uchumba mwandada lulu siku ya septemba 30.

Majizo na Lulu wamekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu na hata kwanadada lulu michael alipokuwa katika kesi yake ya kuuua bila kukusudia mwanaume huyo alikuwa nae bega kwa bega.

Hata hivyo kati ya watu waliohudhuria kitendo hicho ni pamoja na mh paul makonda amabe tangu hapo awali akithubutu kusema kuwa atahakikisha mwanadada lulu anafunga ndoia na bosi huyo la sivyo atadiriki kumfunga.

 

Lulu Aibuka na Kuvunja Ukimya.

Mwanadada Lulu Michael amejitokeza kwa mara nyingie ntena tangu alipotuma kwa mara ya kwanza katika ukurasa wake wa instagram kuhusu msiba wa mtoto wa muna na kuacha ku-post kitu chochote .Leo hii jumapili ya wikiend hii ambayo ilikuwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya mpenzi wake wa muda mrefu ambae pia ni meneja wa Efm Majjizo , Lulu amejitokeza kutuma salamu.

Katika ukurasa wake wa instagram, Lulu Michael aliandika maneno mazito yenye kumshukuru na kutia moyo kwa mpenzi wake huyo wa muda mrefu huku akimtakia siku njema ya kumbukumbu  yake ya kuzaliwa.

Lover, Best, Bussiness partner  Ride or Die and A Shoulder  always to cry for, Asante kwa kunionyesha maana ya upendo wa Agape (KIUNGU) , Baraka za mungu zikufuate siku zote za maisha yako.Happy birthday Baba G, I love You.

Tangu Mwanadada Lulu Michael ametoka gerezani amekuwa akitumia kwa mara chache sana mtandao wake wa instagram na hata mashabiki zake kuwa wakimuulizia sana.

Ray C Afunguka Kumzimikia Lulu Tangu Atoke Jela

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kueleza jinsi anavyovutiwa na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Ray C amedai kuwa tangu Lulu atoke jela Miezi michache iliyopita amebadilika sana kwani amekuwa mtu wa kumuabudu Mungu na kuoekana akiwa kanisani tu.

Ray C amesema Lulu amemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua, kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

Aisee, nimemfuatilia sana Lulu tangu ameanza kupata matatizo ya kesi yake (ya mauaji ya bila kukusudia dhidi ya msanii Steven Kanumba) amebadirika sana. Sasa amekuwa mtu wa kumtukuza Mungu.

Yaani nikiwa namwangalia picha zake au video zake mitandaoni anazoimba nyimbo za dini mpaka machozi yananilenga, hadi fikra zinakuja maana sikumbuki mara ya mwisho lini niliingia kanisani.

Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali. Hakika nimejifunza kitu kutoka kwake, nawashauri watu wajirudi kwa kutubu kwa mwenyezi Mungu kutokana na makosa waliyofanya, wasisubiri hadi matatizo yawapate”.

Tangu Lulu atoke jela Miezi michache iliyopita baada ya kufungwa kwa Miezi kadhaa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba, Lulu amekuwa kimya hasa Kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana Makanisani tu.

Lulu Amuhamasisha Ray C Kumrudia Mungu

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kuweka wazi jinsi video ya msanii wa Bongo movie Elizabeth Michael ‘Lulu’ ilivyomuhamasisha kurudi Kanisani.

Siku chache zilizopita kuna video iliyomuonyesha Lulu kwa mara ya kwanza hadharani kwa ridges yake tangu atoke jela Miezi michache iliyopita kwa msamaha wa Raisi.

Video hiyo ilimuonyesha Lulu akiwa mwenye afya tele kanisani akioenekana akiimba na kumsifu Mungu kwa hisia kali pamoja na waumini wenzake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C aliandika kuwa video hiyo imemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

Lulu nimeangalia hii video zaid ya mara kumi nahisi!mpaka machozi yamenilenga kwakweli!Sikumbuki lini nimeingia kanisani.’

Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali! nimejifunza kitu kutoka kwako my dear! kikubwa sana. You Inspire Me”.

https://www.instagram.com/p/Blpj6psDs1Q/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=seqgtm1xok5m

Picha Mpya ya Lulu Iliyosambaa Katika Mitandao ya Kijamii

Tangu mwanadada elizabeth lulu michael ametoka gerezani hajaweka picha yake yoyote katika mitandao ya kijamii pamoja na kwamba kwa muda mwingi waandishi wa habari wamekuwa wakitafauta kwa udi na uvumba picha yake ili kuzisambaza katika mitandao.

Hata hivyo wikiend hii mwanadada lulu michael aliachia moja ya picha zake akiwa katika moja ya event moja jijini Dar Es Salaam ikimuonyesha akiwa mweny furaha na mwenye kupendeza na kuwafanya mashabiki wafurah na hata kuongea nae kupitia maoni juu ya picha hiyo.

Katika ukiurasa wake wa instagram, aliweka picha katika sehemu ya stories ikimuonyesha mwanadada.

 

Mama Kanumba- Siwezi Kuhudhuria Harusi Ya Lulu na Majizzo

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ ametoa povu zito hivi karibuni baada ya kuulizwa Kuhusu Ndoa ya Lulu na Majizzo.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na mpenzi wake Majizzo wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Mama Kanumba amefunguka kuwa, endapo atapelekewa kadi ya mwualiko wa harusi hiyo hawezi kwenda kwa sababu tangu atoke gerezani hawajawahi kuonana na Lulu wala kusalimiana naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mama Kanumba amedai kuwa, hata hiyo habari yenyewe ya Lulu kuolewa na Majizo anaisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba hajui lolote.

Kwanza hiyo habari yenyewe nimeisikia kwenye vyombo vya habari, lakini mimi sijui kabisa kama wanaweza kuniletea hiyo kadi ya mwaliko na hata wakiniletea siendi.

Najua itakuwa ngumu tu katika mazingira tuliyopitia sisi, kwanza mimi sasa hivi muda mwingi ninajikalia nyumbani tu kutoka na maradhi yangu haya presha”.

Mama Kanumba aliweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kutoka jela mapema baada ya kupata msamaha wa Raisi na kupewa kifungo cha nje mapema mwezi uliopita.

Baba Kanumba Afurahishwa na Kitendo Cha Lulu Kutoka Gerezani

Baba mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Charles Kusekwa Kanumba amefunguka na kuweka wazi furaha yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani kupewa kifungo cha nje.

Tofauti na Mama Kanumba ambaye aliweka wazi kuwa alikasirishwa na Kitendo Cha Lulu kuachiwa huru, Baba Kanumba ameweka wazi kuwa hana neno na Lulu na amefurahi alivyotoka kwani hata kama angefungwa miaka 100 mwanaye hawezi rudi.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Ijumaa Wikienda Baba Kanumba amesema yeye ni mcha Mungu hivyo hawezi Kubeba kinyongo dhidi ya Lulu.

Kila kitu hapa duniani hupangwa na Mungu na kila kinachotokea ni mapenzi yake, siwezi kulaumu kwa nini Lulu ametoka bali nimefurahi kwa sababu hata angefungwa miaka mia moja, Kanumba tayari alishafariki dunia, hawezi kurudi duniani.

Silaumu kwa sababu mimi ni mcha Mungu hivyo Mungu ndiye amesema suala hilo lifikie tamati kwa namna hiyo, wanaopinga na kusema siyo haki, hayo ni mawazo yao maana kama ni kifo cha mwanangu kiliniuma sana, lakini sasa siwezi kumlazimisha Mungu afanye mimi binadamu ninavyotaka maana hata neno lake linatufundisha kwamba tusamehe“.

Lakini pia Baba Kanumba amempa masharti mazito  kwamba kama anataka maisha yake yaende vizuri, awe na familia nzuri kama watu wengine na amani moyoni, anatakiwa kwenda kufanya usafi kaburi la Kanumba kama ni kulia, alie na hapo atakuwa ameacha balaa na mikosi yote.

Kwa mila za kabila letu la Kisukuma ni kwamba, Lulu alitambulika kama mke wa Kanumba maana hakuna mwanamke mwingine tunayemfahamu sisi hivyo natamani angeachiwa huru kabisa asiwe na kifungo cha nje na aende tu kufagilia kaburi la mumewe Kanumba na hapo atakuwa amemaliza na kuwa huru.

Lulu Aanza Kutumikia Kifungo Chake Cha Nje Rasmi

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael ameanza kutumikia rasmi kifungo chake cha nje siku ya jana baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza alitoka katika jengo la Wizara ya nje.

Lulu amekuwa akioneka akifanya kazi ya usafi katika jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani jijijni Dar es Salaam tangu Jumatatu wiki hii Ikiwa ni sehemu ya kazi za jamii atakazofanya.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Global Publishers umebaini kuwa mrembo huyo amekuwa akifika makao makuu ya wizara hiyo asubuhi na kufanya majukumu yake na kuondoka mnamo saa 4 au 5, kabla ya mchana.

Baada ya kumaliza kazi zake hizo za kufagia na kudeki, Lulu ambaye hufika hapo kwa gari, pia huondoka kwa gari kurejea nyumbani.

Mama Kanumba: Lulu Angeachwa Atumikie Kifungo Kidogo

Mama mzazi wa aliyekuwa Muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa au na kama Mama Kanumba amesema hajafuraishwa na kitendo cha Lulu kutoka gerezani na anatamani angeachwa atumikie kifungo kidogo tu.

Lulu aliyekuwa akitumikia kifungo chake cha miaka miwili katika Gereza la Segerea, alipunguziwa adhabu hiyo Mei 12, mwaka huu kufuatia amri ya Mahakama Kuu huku taarifa ya magereza ikieleza kuwa mrembo huyo, alipunguziwa robo ya kifungo chake kutoka kwenye msamaha wa Rais Dk John Pombe Magufuli.

Lakini pamoja na watu wengi kufurahishwa na kitendo cha Lulu kuachwa huru lakini Mama Kanumba ni mtu mmoja ambaye hakupenda hata kidogo kitendo hicho ambapo Kwenye mahojiano na  Global Publishers alifunguka haya:

Najua Lulu na ndugu zake wanasherehekea sasa hivi lakini wakae wakijua sijafurahishwa na kilichotokea. Kanumba alikuwa akiwalipia kodi Lulu na mama yake lakini leo wanafanya haya wanayoyafanya kweli? Bora hata wangemuacha atumikie kidogo adhabu lakini namuachia Mungu”.

Baada ya kutoka jela Lulu ameendelea na kifungo cha nje ambapo ameonekana akiw anafanya usafi katika wizara ya mambo ya nje kama muendelezo wa kifungo chake cha nje.

 

Lulu Kutumikia Kifungo Chake Cha Nje Kwa Kufanya Usafi Wizarani

Muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu alipata msamaha wa Raisi na kupunguziwa adhabu ya kifungo chake na hivyo kutoka gererzani na kutumikia nje.

Jeshi la Magereza lilitangaza taarifa hiyo kwa vyombo vya habari baada ya kumuachia mfungwa huyo ambaye alikuwa anatumikia kifungo chake Segerea baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba.

Akiwa nje, Lulu amepangiwa kufanya kazi mbali mbali za kijamii ikiwemo katika viunga vya wizara ya ndani ya nchi, kwa mujibu wa amri ya mahakama  kuu.

Inadaiwa kuwa Lulu akiwa na wenzake 10 wamepangiwa kufanya usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani zilizopo Posta Jiji la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka  Mkurugenzi wa Probesheni na Huduma za jamii, Charles Nsanze amesema kila siku mwigizaji huyo atatumia saa nne kusafisha mazingira kisha ataendelea na shughuli zake nyingine za ujenzi wa taifa.

Atapumzika siku za Jumamosi na Jumapili au siku za sikukuu, hatakuwa peke yake kwa kuwa tayari hapa wapo wafungwa wengine tisa wanaofanya kazi za usafi wa mazingira”.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Steve Nyerere Anena Haya Baada Ya Lulu Kuachiwa Huru

Muigizaji wa Bongo movie na Mwanaharakati wa siasa Steve Nyerere amefunguka baada ya Muigizaji mwenzake Elizabeth Michael kuachiwa huru mapema jana.

Siku ya jana Jeshi la Magereza lilitangaza rasmi kupitia barua yao walioiachia Kwenye vyombo vya habari kuwa Elizabeth Michael ameachiwa huru rasmi na kwenda kutumikia kifungo cha nje.

Baada ya Lulu kuachiwa rasmi Steve Nyerere ambaye pia ni kiongozi Kwenye tasnia ya Bongo movie amemualika rasmi Lulu katika harakati za kuijenga upya tasnia hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve Nyerere aliandika ujumbe huu:

LULU NI.JAMBO LA.KUSHUKURU SANA KWANI KILA PITO NAAMINI MUNGU YUPO.PAMOJA NAWE,NICHUKUE NAFASI HII KWA DHATI KABISA KUMSHUKURU MH RAIS JOHN POMBE MAGUFURI KWA MSAMAHA HUUU NAAMINI UMEFANYA JAMBO JEMA SANA RAIS WANGU,NIIPONGEZE MAHAKAMA PIA NA WADAU WOTE MLIO KUWA MNAMUOMBEA MWENZETU KUTOKA ,FAMILY, NJOO LULU TEJENGE TASNIA YETU SASA“.

Mara baada ya taarifa kusambaa kuwa Lilu ameachiwa huru wasanii wenzake wengi walionesha kufurahishwa na kitendo hiko.

Mama Kanumba Asononeshwa na Kitendo Cha Lulu Kutolewa Jela Mapema

Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba ameeleza machungu yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani jana.

Siku ya jana Jeshi la Magereza lilitangaza rasmi kuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameachiwa rasmi kutoka gerezani baada ya kukaa ndani kwa miezi mitano ambapo alitajwa kwenda kuendelea na kifungo chake nje.

Tangu Lulu afungwe Mama Kanumba aliweka wazi kuwa alifurahia kifungo cha Lulu na hata kudai kuwa kifungocha miaka miwili kilikuwa kidogo kwa mauaji ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na MCL digital, Mama Kanumba amefunguka kuwa tangu amepata taarifa kuwa Lulu ameachiwa amekuwa akikosa usingizi na hata presha kupanda kwani ameumizwa sana na taarifa hizo.

Tangu nilipopata taarifa hizi nimejikuta nakosa usingizi na kuumwa presha hivyo leo imenibidi niende kwenye maombi kwa ajili ya afya yangu.

Lakini siku zote naamini Kuwa maskini hana haki”.

Lakini Mama Kanumba amewashukuru wote walioshiriki katika kumtoa na kuongeza kuwa anaamini hiyo yote ni kwa sababu yeye hana hela.