Mbasha Ajitapa Kuteketeza Pesa Kwenye Vazi La Suti

Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka na kuweka wazi kuwa anatumia pesa nyingi kwenye kununua vazi analodai linamuweka smart la suti.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Mbasha alisema kuwa yeye Mavazi yake hajawahi kuvalishwa na mtu, huwa ananunua nguo kisha anaondoka dukani tofauti na wale ambao huvalishwa na maduka mbalimbali.

Ni kweli nina suti nyingi na sina anayenivalisha wala ‘sponsor’, unajua mimi napenda sana kuvaa, napenda ‘usmart’ na kunukia vizuri, naamini hata jamii imenizoea hivyo. Hapa kwenye suala la kuvaa huwa natumia pesa yangu“.

Mbasha alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuwepo mtu ambaye anamvalisha bure kwa lengo la kumtangazia biashara Mbasha alikana kabisa:

 

Nikwambie tu uelewe kuwa mimi najivalisha kwa pesa yangu na kama sikununua dukani huwa nashonesha kwa fundi wangu maalumu ambaye huwa nampa laki tatu ananitafutia kitambaa na kunishonea, linapokuja suala la mavazi huwa sina mchezo, nateketeza fedha bila kujali”.

Lakini pia Mbasha alijitapa kutokurudia rudia nguo Lakini pia alikiri hajui thamani ya nguo zake zote:

Ukweli siwezi kuwa na hesabu ya haraka haraka ila najua kila suti nimenunua bei gani kwani mara nyingi natumia kuanzia laki moja na nusu mpaka laki tano, inategemea aina ya suti na kitambaa chake.

Kurudia nguo kwangu ni mara chache sana, kwani kama ni suti moja naweza kuivaa mara mbili tu kwa mwezi lakini siwezi kurudia zaidi ya hapo kwani ninazo nyingi“.

 

Bado Niko Single Sana :-Emmanuel Mbasha

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania,  Emmanuel Mbasha amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mahusiano yake kama amepata ubavu mpya baada ya kuachana na Flora . Mbasha amesema kuwa kwa sasa yupo single, bado anasubiri mwanamke atakayechaguliwa na Mungu.

Namuomba Mungu Mimi bado kijana siwezi kusema miaka yote nitaishi peke yangu.  Namuomba Mungu aje anipe mke mwema na sahihi wa kufanya nae maisha na kukamilisha taratibu zote za kiheshima.”amefunguka Mbasha kwenye kipindi cha E-Gospel cha EFM. “Kwa sasa hivi bado nipo single, Sina mchumba wala Girlfriend, nimeshachoka kuumizwa,”. 

Mbasha amefunguka hayo, baada ya tetesi kuwa amepata mchumba mpya, ambaye mara kwa mara amekuwa akimposti kwenye ukurasa wake wa instagram.

Mbasha Atangaza Kutenga Siku Maalumu Ya Kumuombea Ruge

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kutenga siku maalumu ambayo ataitumia kwa ajili ya kumuombea Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba.

Mbasha ametenga siku ya Ijumaa ya wiki hii Novemba 30 kufanya mkesha wa kufunga na kufungua  mwezi Desemba.

Lakini pia Mbasha amewataka Wasanii wenzake, waache mambo ya utimu na waungane katika maombi ili afya ya Ruge iweze kuimarika na arudi kwenye majukumu yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbasha ameandika ujumbe huu mrefu:

Ijumaa hii nitakuwa kwenye mkesha wa kufunga na kufungua mwezi, na katika mkesha huu nitakuwa na maombi maalum ya kumuombea Ruge Mutahaba ambaye yuko nchini Afrika kusini kwa matibabu. Huyu ndugu binafsi tunafahamiana vizuri sana, maana alikuwa mtu wa karibu sana kwangu. Najua wengi hawajui kuwa Ruge ndiye aliyekuwa meneja wetu aliyeisimamia albam yetu ya kwanza na ya pili wakati tunaimba na mke wangu, na hata baadhi ya nyimbo zetu ni yeye alisimamia kwa umakini mkubwa nikishirikiana nae kwa ukaribu sana, na kuzisimamia hadi zikavuma kila kona na kujulikana. Na kupitia usimamizi huu wa Ruge tulisaini mikataba mingi sana iliyokuwa ya faida. Hata katika ndoa yangu Ruge alipenda kunitia moyo na kuniambia kuwa “anafurahi kuona jinsi ninavyompenda mke wangu na kumsimamia vizuri, jambo ambalo ni gumu sana kufanywa na wanaume wengi wa kiafrika. Kwa kweli katika mambo yanayohusu tasnia ya muziki Tanzania kwa ujumla Ruge ana mchango mkubwa sana kwenye hii sanaa. Sio tu kwenye bongo fleva bali hata nyimbo za injili maana hadi leo hii ukitazama wanamuziki wengi wa nyimbo za injili ambao umaarufu wao umevuka ile mipaka ya kujulikana ndani ya kanisa tu, asilimia kubwa utakuta nyuma yao kuna support ya Ruge Mutahaba. Hivyo naamini hata katika ufalme wa Mungu huyu ni mtu wa faida sana. Na umuhimu wa wake umezidi kuonekana katika tukio la juzi la Fiesta, maana naamini kabisa endapo angekuwepo kila kitu kingeenda sawa. Nikiwa kama baba wa kiroho na mlezi mkuu wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania, napenda kutoa rai kwa wasanii wote Tanzania, huu ni wakati muafaka wa kila mmoja kuweka pembeni tofauti zake za u team na tuungane kwa pamoja kumuombea dua njema ndugu yetu Ruge Mutahaba, na huu ndiyo moyo wa binadamu muungwana anaejua utu ni nini.
Ila kwa yule atakaefurahia matatizo yake hakika atakuwa mchawi hata kama hajawahi kupaa na ungo. Maana ugonjwa ni hali inayompata mtu yeyote, leo kwake kesho kwako.
Asanteni….Get well soon brother ruge”.

 

Emmanuel Mbasha Ateswa na Mzimu wa Kutomuona Mwanae kwa Muda Mrefu

Mwanamuziki wa Injili Bongo Emmanuel Mbasha ambaye hivi karibuni alitengana na aliyekuwa mke wake Flora Mbasha, ameelezea machungu aliyonayo kwa kutomuona mtoto wake aliyezaa na Flora, wakati wa uhai wa ndoa yao.

Akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa na East Africa Television, Emanuel Mbasha amesema kwamba ni zaidi ya miaka miwili hajamtia machoni binti yake huyo, kutokana na kutokuwa na mawasiliano na mama yake, Flora Mbasha.

“Mwanangu sijaonana naye kipindi kirefu, mara ya mwisho kumuona ilikuwa mahakamani, mama yake mawasiliano sina naye, mzazi mwenzangu ametaka iwe hivyo, anaamini akininyima mtoto anajua ananikomoa, yule mtoto nimemmzaa, nimemlea mpaka alipofikia, ni mkubwa, anajua upendo wa baba”, ameelezea Emmanuel Mbasha.

Emmanuel Mbasha aliendelea kwa kusema kwamba hata hivyo aliamua kumuachia mama yake aishi naye, kwani kwa sasa yey yupo bachela hana mke, na ameamua kuishi hivyo kwa sasa akifuata mifano ya Mitume wa Mungu, Paulo na Yesu Kristo, na iwapo ataoa anaweza akadai kumchukua mtoto wake.

“Niliona kwakuwa bado niko bachela na nimeamua kuishi kama Paulo kama Yesu, na ukumbuke nilikataa kutoa talaka, nilijitunza mpaka leo hii, mtoto nitamchukua, lakini kwa sasa sijapata mwenza”, amesema Mbasha.

Emanuel Mbasha na aliyekuwa mke wake Flora waliachana na mahakama kuamuru itolewe talaka, na Flora kwenda kuolewa na mwanaume mwengine, kitendo ambaco Mbasha aliwahi kukitaja kuwa kinampa ugumu zaidi kuwasiliana naye ili aweze kumuona mtoto wake.

Mbasha Apangua Tetesi Za Kupombeka na Wolper

Msanii wa nyimbo za injili nchini Emmanuel Mbasha ameibuka na kupanguia tetesi zote zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba mtumishi huyo wa Mungu alikuwa amekaa na msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper wakinywa pombe.

Kwenye interview aliyofanya na kituo kimoja habari, Mbasha amekanusha tetesi hizo na kudai kuwa alikuwa anakunywa soda. Mbasha amesema watu wamemjia juu kwa kukaa karibu na Wolper na kusema akiendelea kukaa karibu na  Wolper atampoteza na pengine anaweza akafanya mambo ambayo hayaendani na wokovu wake kama watu walivyomzoea kwamba yeye ni mtu wa dini.

Mimi na Wolper ni marafiki wa karibu na ukweli ni kwamba mimi nampenda Wolper kama dada yangu na namkubali kwa kazi zake anazozifanya hata hivyo naamini kwamba na yeye ananipenda kwa kuwa tumekuwa karibu kwa muda mrefu sasa”.

Lakini pia Mbasha alimalizia huku akitolea maelezo picha ambazo zimesambaa mitandano zikimuonyesha akiwa karibu na Wolper na kusema kwamba picha hizo zilitokana na kazi ambayo waliipata kwa pamoja ikawakutanisha na kuwaweka karibu.

 

 

Mbasha Azidi Kumchokonoa Mc Pilipili

Msanii wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha ameibuka na kumtupia madongo Mshehereshaji maarufu Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ baada ya kupiga picha akiwa na mpenzi wake.

Siku chache zilizopita Mc Pilipili aliposti picha Mtandaoni akiwa na mpenzi wake anajulikana kama Qute Mena lakini mara moja Mbasha alimtolea povu Mc Pilipili na kudai kwa kufanya hivyo amekiuka taratibu za kidini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mbasha alisema lengo la kumuandikia ujumbe mrefu MC Pilipili kwenye ukurasa wake wa Instagram, lilikuwa ni kumjenga pamoja na kumuelimisha kwamba kitendo anachokifanya sio sahihi.

Unajua sio vizuri kumuanika wazi wazi mchumba wala kuwa naye karibu kiasi ambacho hata watu wakiwaona watashangaa, kwa sababu tunafundishwa kwamba, ukishamchumbia mtoto wa kike hutakiwi kufanya naye kitu chochote mpaka pale utakapo muoa na kumfanya mke wako.

Sasa Napata wasiwasi kwa huyu ndugu yangu MC Pilipili na huyo mchumba wake, nimepata taarifa kwamba wapo Zanzibar sasa sijajua kama wamechukua vyumba tofauti au wanaishi kwenye chumba kimoja, kitendo ambacho si kizuri, ila lengo la kumuandikia ule ujumbe kwenye akaunti yangu ni kumuelisha kwa sababu yeye ni kioo cha jamii na watu wanahitaji kujifunza kutoka kwake”.

 

 

Mbasha Afungukia Majibu Yake Ya Ukimwi

Msanii wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kuanika majibu yake ya ugonjwa wa Ukimwi aliofungukia na kukiri kupima siku chache zilizopita.

Global Publishers wanaripoti kuwa mtu wa karibu wa Mbasha kilieleza kwamba mwanamuziki huyo alikwenda kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) na alipopatiwa majibu alijikuta akirukaruka kama yuko jukwaani akiimba nyimbo zake.

Mbasha, baada ya kupata majibu kwamba ni mzima, hanamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi alipagawa yaani kama mtu ambaye alikuwa aamini, hapo ndiyo utajua kila mtu duniani anaogopa Ukimwi iwe mtumishi wa Mungu au mtu wa kawaida”.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Risasi, Mbasha alikiri taarifa hizo na kudai alipagawa kwa furaha baada ya kujikuta hana magonjwa hayo:

Nilijikuta ninapagawa kwa sababu ya ile furaha ya kukutwa mzima wa afya na siyo kwamba nilikuwa sijiamini, unajua ukimwi hauambukizwi kwa ngono tu unaweza kupata kwa njia mbalimbali kwa hiyo hapa nina furaha ya ajabu“.

Mbasha alianika majibu yake Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kwenye insta story ili kuonyesha mashabiki zake kwamba yeye ni Mzima kabisa bila Shaka:

 

Majibu ya UKIMWI ya Mbasha Yamtia Wazimu.

UPIMA Ukimwi siyo jambo la mchezomchezo! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Emmanuel Mbasha kupagawa baada ya kupewa majibu ya kipimo hicho.

Chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa Mbasha kilieleza kwamba mwanamuziki huyo alikwenda kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) na alipopatiwa majibu alijikuta akirukaruka kama yuko jukwaani akiimba nyimbo zake.

Mbasha, baada ya kupata majibu kwamba ni mzima, hanamaambukizi ya Virusi Vya Ukimwi alipagawa yaani kama mtu ambaye alikuwa aamini, hapo ndiyo utajua kila mtu duniani anaogopa Ukimwi iwe mtumishi wa Mungu au mtu wa kawaida,” kilieleza chanzo hicho.Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kupima ngoma na kujikuta akipagawa kwa furaha kutokana na kukutwa hana maambukizi.

Hata hivyo mbasha alikuja kuulizwa ni kitu gani kilimfanya achanganyikiwe alipopata majibu yake ndipo alipojibu kuwa UKIMWI hauambukizwi kwa ngono pekee hivyo unapokutwa mzima ni jambo la kushukuru Mungu.

“Nilijikuta ninapagawa kwa sababu ya ile furaha ya kukutwa mzima wa afya na siyo kwamba nilikuwa sijiamini, unajua ukimwi hauambukizwi kwa ngono tu unaweza kupata kwa njia mbalimbali kwa hiyo hapa nina furaha ya ajabu,” alisema Mbasha

Mbasha Akiri Kumkubali Wema, Amponda Mobetto

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ameibuka na kudai Wema Sepetu ndio Tanzania Sweetheart pekeee na sio vinginevyo.

Emanuel amesema hayo baada ya kuibuka kwa mjadala mzito katika siku za hivi Karibuni baada ya mashabiki kutaka kumvua cheo cha Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu na kumvalisha Hamisa Mobetto.

Katika Interview yake na Gazeti la Ijumaa, Mbasha alisema kuwa kwa upande wake, Tanzania Sweetheart kati ya warembo hao wawili, ni Wema kwani ndiye anayestahili na hilo halina hata mjadala.

Hilo jina linamfaa aliyekuwa nalo tangu zamani (Wema), kwani ndiye aliyepewa hilo jina, kwa hivyo acha tu aendelee nalo kwa sababu ndio linampendezea”.

Siku za hivi Karibuni Mbasha aliingia katika vita kali na mashabiki wa Mobetto baada ya kuweka picha yake akiwa anapaa na ungo kufuatia tuhuma za uchawi.

Emmanuel Mbasha Azungumzia Mtoto Aliezaa na Florah, Hawajaonana kwa Miaka 4

Msanii wa nyimbo za injili nchini ,Emanuel Mbasha amekuwa akiongea na kulalamika kwa uchungu sana tangu alipoachana kwa talaka na mzazi mwenzie Florah Mbasha miaka minne iliyopita  baada ya mwanamke huyo kumkatalia mtoto aliewahinkuzaa nae walipokuwa katika ndoa.

Emmanuel anasema kuwa kwa takribani miaka minne sasa hajawahi kuonana na mtoto wake na hata pich ya mwisho aliyokuwa nayo ya mtoto huyo ni ile aliyopiga nae siku ya mwisho walipokuwa mahakamani kufuatilia talaka.

Emmanuel anasema kuwa inazidi kumuumiza kwa sababu ndio mtoto pekee aliyenae aliempata akiwa kijana lakini alimlea kwa mapenzi tangu alipozaliwa akiwa mchanga na yeye ndio alikuwa akimlea mtoto huyo.

Unajua Liz ni mtoto wangu wa ujanani, nimemlea tangu akiwa mchanga kabisaa, mara ya mwisho kumuona  ni pale mahakamani mwaka 2014 tulipopeana talaka na mama yake  na nikapiga nae picha na baada ya hapo mama yake amekuwa akimkatalia  nisimuone kwaio imekuwa changamoto sana kwangu.

 

Emmanuel Mbasha Amshukia Shilole Baada Ya Kuomba Msaada Kwa Raisi

Msanii wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha amejikuta akimwagia povu zito Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, baada ya kuomba msaada kwa Raisi.

Siku chache zilizopita kuna video clip iliyosambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Shilole akimlilia Raisi Magufuli pesa kwa ajili ya kumsomesha mtoto wake.

Mbasha aliamua kuwatolea uvivu watu wote maarufu wanaomuandama Rais Magufuli kwa kutaka msaada wa mali ile hali wana uwezo kifedha, ikiwemo Shilole ambaye anafanya kazi za sanaa na mjasiriamali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbasha aliandika ujumbe huu:

 Habari za mda huu . Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost ????. Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili?.???. Leo nileshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba raisi akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu? Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ?

Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ? Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima.kajifunze kwa @munalove100 basi”.

Baada ya kusoma ujumbe huo Shilole alijibu kwa maneno machache tu Nakuheshimu sana kaka yangu please tulinde heshima yetu”.

Emmanuel Mbasha Aburuzwa Mahakamani Baada Ya Kutelekeza Mtoto

Mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye pia alijizolea umaarufu baada ya kumuoa muimbaji wa nyimbo za Injili Florah Mbasha, ameburuzwa mahakamani baada ya Kutelekeza mtoto.

Habari za chini ya kapeti zinazoripotiwa na gazeti la Risasi Mchanganyiko, zinadai kuwa Mbasha ameburuzwa mahakama ya Kisutu na mwanadada Miriam Kawishe ambaye amedai amemtelekeza mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Avantica bila matunzo yoyote.

Unajua Mbasha naye ameburuzwa mahakamani kwa kesi ya kushindwa kutoa matunzo ya mtoto tangu alipozaliwa hadi sasa ana miaka mitatu na ilianza kutajwa wiki iliyopita huku ikitarajiwa kuendelea tena mwisho wa mwezi huu. Ninyi mtafuteni huyo mzazi mwenzake atawaeleza vizuri”. Kilisema chanzo cha habari.

Baada ya taarifa hizo , Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mwanamama huyo aliyezaa na Mbasha, Miriam ambaye alikiri kwamba ni kweli, lakini hawezi kuzungumza sana kwani kwa sasa suala hilo liko mahakamani tayari pia ana wakili anayelisimamia.

 

Mbasha Akanusha Tetesi za Kutoka na Agness Mmassy

Msanii wa nyimbo za injili emmanuel mbasha amefunguka na kuamua kuweka wazi mahusiano yake na mwanamitindo maarufu nchini agnes mmasi na kusema kuwa watuwamekuwa wakizusha kuusu yeye kutoka kimapezni na mwanadada huyo lakini taarifa hizo sio za kweli.

atika UkIrasa wake wa instagram , Mbasha aliandika “Nakanusha yote ni uongo, sia mahusiano na huyu dada kabisa na wanaoendelea kuzusha  na kueneza huu uongo basi na mungu wangu atawalipa.sio kweli.”

                                

Kumekuwa na tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano kati ya mwimbaji huyo na mwanadada mabe ni mwanamitindo ambae amekuwa akipiga picha za utupu mara nyingi na kuziweka katika mitandao ya kijamii Agness Mmasy.

Hata hivyo kwa rekodi ya hivi karibuni, Emmanuel Mbasha alikiri kutokuwa na mwanamke tangu alipoachana na mke wake Florah na kusema kuwa kwa sasa hivi amejukita zaidi katika swala la uokovu na kwamba kuwa na mahusiano kabla ya ndoa ni kuzini na asingependa kufanya kitu hicho.

 

Mbasha:Tangu Niachane na Mke Wangu Sijawahi Kuzini.

Msanii wa nyimbo za injili  Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa kwa muda mrefu tangu ameachana na mke wake aliekuwa amefunga nae ndoa hajajiingiza tena katika mahusiano ya aina yoyote kwa sababu bado hajapata mwanamke wa kuingia nae katika mahusiano.

Emmanuel Mbasha anasema kuwa   ameamua kuishi bila kuoa  hata kama itamgharimu maisha kwa sababu hata yesu na paulo waliweza kusihi bila kuona na waliweza kuishi.mbasha anasema kuwa pamoja na kwamba yeye pia ni mwanaume aliyekamilika lakini bado amekuwa akimuomba mungu sana kushinda vishawishi vya shetani vya kujiingiiza katika mahusiano hayo.

ukiona niko na mwanamke ujue ni rafiki yangu tu wa kawaida na tangu nimeachana na mke wangu wa kwanza wa ndoa sijawahi kuzini tena,na niko kawaida tu sina matatizo yoyote yale na ukizingatia nafanya sana mazoezi.sina mpenzi wala mchumba kama watu wanavyokuwa wananizushia maneno ya uongo.

Pamoja na kwamba emmanuel amekuwa akikanusha kuwa na mahusiano na mwanamke yoyote lakini hivi karibuni amekuwa akiweka picha katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanawake tofauti tofauti na kusemekana kuwa ni mwanamke wake.

Emmanuel Mbasha aliwahi kuwa na mahusiano na msanii wa nyimbo za injili Florah Mbasha kwa na kufanikiwa kuzaa mtoto mmoja lakini baadae walikuja kuachana na kushindwana katika ndoa kwa sababu florah alimfungulia mashtaka kwa sababu ya kisingizio cha kumbaka mfanya kazi wake wa ndani.

 

 

Wanawake Wengi Wananitaka Kimapenzi- Emmanuel Mbasha

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Flora Mbasha, amekiri kuwa amekuwa akisumbuliwa sana na wanawake wanaomtaka kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa Emmanuel Mbasha amekiri kuwa amekuwa akipata usumbufu huo hasa kupitia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.

Kwenye kipindi cha Enews Mbasha alifunguka;

“Unajua watu wakiona umempost msichana kwenye page yako wanaamini ni mpenzi wako lakini sio kweli wengi wao no mashabiki tu nakutana nao wanaomba wapige picha na mimi basi ila kwa sasa sina mpenzi sina mke nipo tu mwenyewe na mambo yangu ila itakapofika wakati sahihi na ninaamini binti niyakayempata atakuwa ameletwa na Mungu hivyo sina sababu ya kukurupuka kwa sasa nimetulia nasubiria make sahihi, unajua nimetokea kwenye ndoa iliyokuwa na changamoto kubwa sana angepitia mtu mwingine angedata lakini mimi nashukuru nilisimama na Mungu nikamuomba anivushe salama na nashukuru nimevuka sasa sina sababu ya kuharakisha mambo kwa sasa”.

Pia Mbasha aliendelea kufunguka kuhusu changamoto anayopata kutoka kwa wanawake;

“Unajua wadada wengi wananipenda wa kila aina wote wanataka kuwa na mimi yaani nikikuonyesha meseji zangu wanazonitumia za kunitaka zimejaa kibao kwenye mitandao yote facebook, instagram kote huko lakini namshukuru Mungu kwakibali hicho maana kupendwa nako ni kibali jambo ambalo lipo wazi, Kwa sasa siwezi kukurupuka tu nikamchukua yoyote nisije nikaingia kwenye majanga namuomba Mungu anioneshe mwanamke mwema”.

Mbasha pia amekiri kuwa usumbufu huo anaopata kutoka kwa wanawake wengi ameuzoea kwani tangu kipindi  ameoa amekuwa akipata usumbufu huo huo kutoka kwao. Mbasha ameweka wazi hayo baada ya tetesi kuenea kuwa ana mpango wa kuoa hivi karibuni mara tu baada ya aliyekuwa mke wake Florah kuolewa tena.

Flora Mbasha na mumewe wa zamani wakorofishana tena

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha waliachana miaka mitatu zilizopita lakini bado wako wakorofishana kwenye mtandao.

Emmanuel amemtupia maneno mke wake wa zamani baada ya kuzuka uvumi kuwa Flora alichapisha kitabu chake kinachoitwa ‘Siri za Flora Mbasha’ ambacho kinazungumia vitu mbaya kuhusu Emmanuel Mbasha.

Flora Mbasha na Emmanuel Mbasha

Ijumaa Wikienda lilimtafuta Emmanuel ambaye alionekana kuwa mwenye hasira kali alipoulizwa kuhusu kitabu cha mke wake wa zamani.

“Sipendi ujinga kwani watu hawawezi kuuza hicho kidaftari chao mpaka watafute kiki kwangu? Mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri? Mimi ninaingiaje kwenye ishu za huyo Flora? Zaidi ya miaka mitatu sipo naye na ni mke wa mtu, ninamuomba atulie na akome kunitajataja,” Emmanuel Mbasha alisema.

Kwa upande wa Flora alipotafutwa kuhusu ishu ya kumchafulia jina mume wake wa zamani, alisisitiza kuwa habari hizo za mtandaoni hazikuwa za kweli isipokuwa ni kweli kitabu chake hicho kimeshatoka na kinaelezea kiundani mambo aliyoyapitia kwenye ndoa yake na Mbasha kabla ya kuolewa na David Kusekwa.