Esha Buheti Adai Atampokea Mtoto Wa Nje Wa Mumewe Kwa Mikono Miwili

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kudai hatakuwa na tatizo endapo mume Wake Atamletea Mtoto wa nje kwani atampokea na kumlea Kama mwanaye.

Esha buheti amefunguka kuwa ameishi na mume wake kwa takribani miaka 10 sasa, hivyo hata leo hii akiamua kumletea mtoto wa nje yupo tayari kulea ila tu huyo mwanamke akae mbali na anga zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Esha amefunguka na kusema haya zaidi kuhusu ishu hiyo:

Unajua mimi nimeishi na mume wangu kwa miaka 10 sasa, namjua vizuri sana, ila itakapokuja kutokea amezaa nje na akaniletea mtoto nimlee haina shida nitafanya hivyo, tena nitamlea kama mtoto wangu wa kumzaa ila tu huyo mwanamke ndio asije akasogea kwenye anga zangu kabisa”.

Kauli hiyo imeonekana kuwaacha midomo wazi mashabiki wa mwanamama huyo na wengi wao kuoenekana kupingana naye na kumshauri kutofanya hivyo kwani anakuwa kama anamruhusu mume Wake kufanya uchafu.

Jacqueline Wolper Ahaidi Kupambana na Marafiki Wanafki

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper ametoa neno kwa marafiki wote ambao wamekuwa na tabia za kinafki na kuhaidi kupambana nao.

Wolper amefunguka na kudai siku akimkamata mtu ambaye wanafahamiana vizuri akiwa anamsema kwenye Mtandao wa Instagram atafurahia shoo kwa atakachomfanya.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Wolper kama mtu mnajuana na ukaona amekosea ni vyema ukamfuata mwenyewe na kumwambia kuliko kuandika unavyotaka Instagram kwani huo ni unafiki.

Siamini kabisa mtu mwenye mapenzi ya dhati na wewe anaweza kukuandikia ujumbe kwenye Instagram. Mimi huo ninauita unafiki na siku nikimkamata mtu wa aina hiyo atanijua“.

Siku chache zilizopita Wolper aliingia kwenye mgogoro na msanii mwenzake Esha Buheti baada ya kuamua kumsema Wema Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Instagram jambo ambalo Wolper alidai hajapenda na kumtaka Esha amfuate pembeni na kumsema Wema badala ya kumsema Instagram.

Esha Buheti Amchana Wema Kwa Picha Chafu Alizovujisha

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kumchana Msanii mwenzake Wema Sepetu baada ya kuvujisha picha na video chafu zinazomuonyesha yeye na mume wake mtarajiwa.

Siku ya jana Wema alitengeneza headlines baada ya kumtambulisha mwanaume anayetambulika kama Patrick na kusema ndiye mume wake mtarajiwa lakini baada ya kuposti video iliyowaonyesha wawili hao wakibusiana ilizua gumzo zaidi.

Esha Buheti ambaye ni rafiki mkubwa wa Wema alishindwa kuvumilia na kumuandikia barua ya wazi ambapo amemchana laivu na kumtaka aache kufanya mambo ambayo yanamuaibisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esha Buheti aliandika ujumbe huu:

Wema ametangaza uhusiano na mwanaume ambaye anasemekana tayari ana wake wawili Lakini pia kijana huyo ameshawahi kumrushia maneno ya kejeli Wema na Familia yake Kupitia mitandao ya kijamii.

Esha Buheti Afunguka na Kueleza Jinsi Mtoto Wake Alivyoiokoa Ndoa Yake

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Esha Buheti amefunguka na kuweka wazi jinsi mtoto wake wa mwisho aliyemzaa alivyoikoa ndoa yake.

Esha amedai mtoto wake aitwaye Claribel ameweza kwa asilimia kubwa kuiokoa ndoa yake ambayo alikuwa kabisa anaiona kama imeshavunjika na kukosa kabisa matumaini ya Kurudi tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Esha amesema kila akimuangalia mtoto wake huyo anakuwa na sababu nyingi za kumshukuru Mungu, kwa kuwa ndiye chachu ya kumfanya awepo kwenye ndoa yake mpaka leo.

Unajua kabla ya ujauzito wa mtoto wangu huyu ndoa yangu ilikuwa haina uhai kabisa yaani ilishikiliwa na uzi mdogo sana, lakini Mungu alipomleta mwanangu huyu na ndoa yangu ikarudi upya kabisa, nashukuru kwa hilo nina maelewano vizuri na mume wangu”.

Esha: Jokate Usinichukie Mimi Ni Bendera Fuata Upepo

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameendelea kumtolea povu zito mwanadada Jokate Mwegelo huku akimsihi asimchukie kisa Ali Kiba kuoa kwani yeye ni bendera fuata upepo tu.

Siku chache zilizopita Esha alimtuhumu Jokate kwa kumchukia kisa na mkasa alihudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na mkewe Amina Mombasa nchini Kenya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Esha amedai kuwa  amesikia kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba mwanamitindo huyo anamchukia kwa sasa kutokana na kuwa karibu na Kiba kwenye harusi yake na mrembo Amina Khaleef.

Kama ni kweli Jokate atakuwa ananichukia kisa mpenzi wake wa zamani Kiba kuoa kama watu wanavyosema, basi atakuwa ananichukia bure“.

Lakini pia Esha ameweka wazi kuwa sio kosa lake kwani yeye ni kama bendera fuata upepo anafanya alichokuwa anaelekezwa kwani haikuwa harusi yake:

Mimi ni kama bendera tu nafuata upepo kwa hiyo wa kumchukia ni Kiba mwenyewe aliyeamua kumuacha yeye na kuoa mtu mwingine, na wala si yeyote yule ambaye yupo karibu na Kiba”.

Tangu Ali Kiba Afunge ndoa aliyekuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo hajaposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii.

Esha Buheti Amlipua Jokate na Kudai Anaona Wivu Baada Ya Alikiba Kuoa

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kumtupia tuhuma nzito mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ baada ya kudai kuwa tangu amehudhuria harusi ya staa wa Bongo fleva Ali Kiba na Amina mrembo huyo amekata naye mawasiliano.

Esha ni mtu ambaye ana ukaribu sana na familia ya Ali Kiba na hata kwenye harusi ya Ali Kiba alionekana mwanzo mwisho akishitiki kwani alienda hadi Mombasa.

Hapo nyuma kuna taarifa ilisambaa kuwa Esha ndiye aliyemtafutia mchumba huyo Ali Kiba (Amina) ingawa mwenyewe alishakataa na hata Ali Kiba na Amina waliweka wazi walikutana wenyewe Kwenye ndege.

Kwenye mahojiano na Shilawadu  Esha anadai kuwa tangu ahudhurie ndoa ya Ali Kiba basi Jokate kama kama kamkasirikia kwani zamani alikuwa anaangalia status zake WhatsApp lakini saivi ameacha.

Mimi na Jokate tukiongelea kuhusu kukutana basi tulikutana kama mara tatu tu lakini kama yeye ananichukia ni yeye tu lakini mimi siwezi kumchukia kwa sababu sio mimi niliyeoa aliyeoa ni Ali kiba, ingawa kabla alikuwa ana view status zangu lakini tangu niende Mombasa sijaona aki view tena Lakini sikuhangaika kuangalia kama ameniblock au vipi”.

Jokate hajaonekana aliposti kitu chochote Kwenye mitandao ya kijamii tangu harusi ya Ali Kiba hivyo pia hajajibu tuhuma hizi.

Mimi Sina Competition na Shiloleh:-Esha Buheti

Mwanadada wa bongo movie esha buheti amefunguka na kuongelea uhusiano wake na shiloleh kama watu ambavyo wamekuwa wakiwashindanisha katika swala zima la mapisha na kusemekana wawili hao kwa sasa hawaelewani kwa sababu hiyo,

Akiongea na mwandishi wa habari, esga anasema kuwa kwa upande wake hana ushindani na mtu yoyote zaidi ya kwamba anachojua kila mtu anafanya kazi zake mwenyewe na kila mtu ana wateja wake lakini pia anshangaa kwanini watu wengi wamekuwa wakimshindanisha na yeye wakati kuna wasanii wengi tu ambao ni wapishi.

Competion gani, mimi si-compet na mtu yoyote na hakuna biashara mamabyo ni ya mtu  au kuwa hii imepangwa kufanywa na mtu fulani tu hapana,na hayo ni maneno ya watu nimekuwa nikiyachukia sana kwa sababu mimi sina competition na shiloleh , kwanini mbona watu wengi wanapika tu kuna open kitchen anapika , uwoya anapika lakini wao wamekazana na shiloleh tu kuna nini au vigezo gani vya kunilinganisha nae.

Siwezi kulinganishwa na shilole kwa sababu yeye nilishamkuta akifanya alafu hata menu zetu ni tofauti sana.

Esha Buheti Amtetea Wema Sepetu Baada Ya Kuambiwa Hastaili Kushinda Tuzo

Msanii wa Bongo movie Esha Buheti amewajia juu wasanii wote wa Bongo movie wanaodai kuwa Wema Sepetu hakustahili kushinda tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Siku ya Jumapili pale Mlimani City hall Kulikuwa kuna ugawaji wa tuzo za Sinema Zetu (SZIFF) kwa wasanii wa filamu za Bongo movie na moja kati ya wasanii waliopata tuzo kubwa ni Wema Sepetu aliyejinyakulia tuzo ya msanii bora wa kike na Gabo aliyejipatia msanii bora wa kiume.

Kitendo cha Wema kushinda kiliibua hisia za wasanii wengi walioona Wema hajafanya movie nyingi mpaka kuweza kustahili kushinda tuzo hiyo na moja kati ya waaanii hao ni Irene Uwoya ambaye aliweka wazi kuwa Gabo alistahili tuzo ile lakini sio Wema.

Esha ameibuka na kumkingia kifua Wema na kusema hamna haja ya kumuonea wivu kwani wasanii walivyoambiwa wapeleke kazi zao kwa ajili ya kushindanishwa waligoma ila wachache waliopeleka kama Wema na Gabo wamefanikiwa kuibuka kidedea.

.