Esma Ageuka Chui Kuulizwa Malezi ya Watoto wa Zari

Dada wa msanii diamond platinumz amegeuka kuwa mbogo hasa baada ya mwandishi wa habari kumuuliza wao kama famili ya Diamond wanajiskiaje pale wanaposikia mama watoto wa watoto wa Diamond zari anapotangaza katika mitandao kuhusu kutelekeza watoto wake.

Zari amekuwa akisema kuwa baba wa watoto wake hana anachojali kuhusu watoto hao na kwamba kila kitu kwa sasa anajua yeye mwenyewe.

Mtangazaji alipouliza kuhusu swala hilo ESMA alikuwa mkali na kusema kuwa kuna baadhi ya mambo hana haja ya kuyajibu kwa sababu hayamhusu kuyaongelea.

sitaki kuulizwa habari zake, unaniuliza mimi kwani zinanihusu.Kwani mimi ni Diamond, sitaki mambo ya ajabu ajabu …(tusi)

 

 

Esma Apiga Dua Ndoa Ifanikiwe

Mwanadada esma platinumz ambae ni dada wa msanii Diamond platinumz amefunguka na kuonyesha wasiwasi wake katika swala zima la kufungwa kwa ndoa kati ya kaka yake na mwanadada tanasha kutoka nchini kenya.

Esma ameonekana kuwa na wasiwasi huo mpaka kufikia hatua ya kushusha sala katika moja ya picha aliweka kaka yake kuhusu mwanamke wake huku akiomba ndoa iyo itimie.

Ukiachana na walimwengu kuwa na wasiwasi na kusema ndoa  hiyo haiwezinkufanikiwa, hayo yote yanakuja kutokana na kutokuwa makini kwa Diamond platinumz amvae anakuwa na mahusiano na wamawake tofauti na kutangaza ndoa lakini kushindwa kuwaoa.

 

 

 

Esma Asema Hamisa Anaharibiwa na Watu

Dada wa msanii diamond platinumz amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu anavyojua kuhusu Hamisa Mobeto ambae aliwahi kuwa mpenzi wa kaka yakena hata kupata bahati ya kupata mtoto mmoja ni kwamba mwanadada huyo aana tabia nzuri sana lakini amekuwa akiharibiwa na watu.

Akijibu maoni na maswali ya mashabiki zake katika ukurasa wake, Esma anajibu swala liloulizwa na shabiki maoni yake juu ya Hamisa na ndipo anasema hivyo.

 

Ikumbukwe kuwa mwanadada hamisa na sma walikuwa marafiki wakubwa sana kipindi cha nyuma , lakini ghafla hamisa na familia yote na diamond walikuja na kuwa maadui na hata kufikia hatua ya kuitana wachawi mbele ya mashabiki mitandaoni.

Siwezi Kurudiana na Petit Hata Iweje :- Esma

Dada wa msanii Diamond Platinumz , maarufu kama Esma Platinumz amefunguka na kusema kuwa hata iweje hawei kurudiana na mzazi mwenzie petit man

Esma amefunguka hayo kufuatia kuvuja kwa video mtandaoni ikiwaone- sha wawili hao waki- wa pamoja na wadau kuanza kuwapongeza wakidhani wamerudiana.

“Hatujarudiana. Hiyo video ni ya siku nyingi, wewe an- galia hata hizo nguo tulizovaa sidhani hata kama wote tunazo hadi sasa, ni za siku nyingi sana. Kwa

sasa mimi jamani hata iweje siwezi kurudiana na Petit,” alisema Esma. Septemba, mwaka huu, Esma alitan- gaza rasmi kumwagana na Petit kwa kile ali- chodai kuwa jamaa huyo amekuwa akimkwami- sha katika mambo yake ya kimaendeleo.

Esma Amkana Tanasha , Asema Hajatambulishwa.

Dada wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kukanusha kauli yake aliyowahikusema hapo awali kuhusu kumpenda wifi yake  mpya tanasha ambae ndie anakwenda kuwa  kuolewa  mwaka 2019 na msanii huyo.

Hapo awali mwanadada huyo alisema kuwa anampenda sna wiifi yake na wanamkaribisha katika familia yao lakini ghafla mwanadada huyo amegeuka na kusema  kuwa hamjui kabisa mwanadada huyo na kwamba  mwanadada huyo hajatambulishwa kwao hivyo hawezi kusema chochote.

Esma anasema kuwa hajawahi kutambulishwa zaidi ya kumjua kutoka instagram , kwa hivyo wala hajui kitu na yeye anaona ni kama msinema tu.

Alipoulizwa kuhusu ni kitu gani anaenjoy kutoka kwa wifi yake Tanasha majibu ya Esma yalikuwa “ndugu yangu sina hata ninachoenjoy kutka kwa tanasha,kwa sababu simjui na yeye hanijui wala  kwaio tumekuwa tukionana tu huku instagram, lakini ukinuliza wala sijui chochote.bado hatujatambulishwa rasmi na sisi tunaona sinema kama nyinnyi mnavyoona tu.”

 

Esma Atangaza Kuwa Single, Yuko Tayari Kuolewa Tena.

Dada wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kutangaza kuwa single tangu hapo awali alipotangaa kuwa yeye na aliyekuwa mume wake petit man wameachan na kushindwa kuendelea kukaa katika ndoa yao.

Akiongea na waandishi wa habari alipokuwa akiingia katika ukumbi ilipofanyika birthday party ya mwanadada Wema Sepetu, Esma  amesema kuwa ni kweli ka sasa yuko single na ikitokea kuna mtu anataka kumuoa yuko tayari kwa sasa.

Hata hivyo, kuna tetesi zilizokuwa zikisambaa kuwa duka la vitenge na vipodozi la Esma alifunguliwa na mume wake huyo , kuhusu swala hilo Esma amaekanusha vikali swala hilo na kusema kuwa ni uongo.

Esma na Petiti walifunga ndoa miaka michache iliyopita na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, hata hivyo wawili hao wanaachana baaada ya mwanaume kuonekena kuwa na skendo nyingi za wanawake.

hata hivyo esma alipoulizwa swala la kurudiana na Petit alisema kuwa hajui kama anaweza kurudiana na petit kwa sasa.

Nitachagua Wanaume Kama Karanga;- Esma

Dada wamsanii Diamond amefunguka na kusema kuwa kwake kuwa na wanaume tofauti tofauti wala sio shida kwa sababu alishajifunza kutokana nawanaume wa nyuma ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano kipindi cha nyuma jinsi walivyomuumiza.

Esma anasema kuwa swala la kuumizwa limemfanya kuwa na muda mrefu sana wa kuchagua mwanaume kabla hajaingia nae katika mahusiano huku akisema kuwa atakuwa anachagua mwanaume kama karanga ili kujifunza kutokana na makosa aliyowahi kuyafanya na kuumizwa na mapenzi.

Esma anasema kuwa kwa muda mrefu sana amekuwa akivumilia kukaa kimya katika ndo yake na petit lakini alikuwa anaumia lakini hakutaka kuongea chochote mpaka yalipokuta kubumbuluka katika mitandao ya kijamii lakini amekuwa akiumia sana.

Ukiumwa na nyoka basi hata ukiona jani tu unakuwa unashtuka sana, na haya ndio yamenikuta na mimi sasa hivi, ila kwa sasa nimejifunza sana kabla yai. kumuamini mwanaume nitamkagua hata mwaka mzima ndio nianze kuwa na mhausiano nao la sio wala siwezi.

Wiki iliyopita Mange kimambi aliweka wazi mahusiano ya Petit na mwanamke mwingine wa kinyarwanda na ndipo Esma alipokuja kuongea katika vyombo vya habari na kusema kuwa walishaachana na Petit siku nyingi sana lakini hakutaka kuweka wazi.

 

 

Kisa Hamisa, Mange Kimambi Awashambulia Esma Na Mama yake .

Baada ya kuibukakwa tuhuma za uchawi kutoka kwa mwanadada Hamisa Mobeto kuwa amekuwa aikiiloga familia ya Diamond Platinumz, mwanaharakati mashghuli Mange Kimambi aliamua kuingilia kati swala hilo na kuamua kumtetea Hamisa dhidi ya wanafamilia ya Diamond.

Mambo yanazidi kuwa mambo baada ya Mange kuamua kuituka familia ya diamond na ndipo familia hiyo hasa dada wa Diamond alipoamua kujibizana na Mange katika mitandao ya kijamii.siku ya jana ilizid kuchafuka katika ukurasa wa instagram baadaya wawili hao kuingia katika ligi ya kutukanana matusi huku kila mmoja akijitaidi kutetea upande wake.

Kwa upande wa Mange anasema kuwa familia hiyo haukupaswa kumtuka hamisa ukizingatia wamekuwa wakimsema kuwa kila mtoto ana baba yake ilhali hata esma nae ana watoto ambao kila mtu na baba yake.

Hata hivyo Mange anaendelea kutoa siri kuwa kutokana na maswala ya uchawi ndio maana hata aliwahi kumuua mtoto wake wa kwanza ambae watu wengi hawakuwahi kumjua alipokuwa akiumwa na kushindwa kumpelea hospitali kwa madai kuwa amelogwa hivyo kumpeleka kwa waganga.

Esma nae hakukaa kimya na kuseme akuwa mara nyingi mange amekuwa hajielewi na ndio maana amekuwa akiongea maneno yasiyokuwa na uhakika nayo na kikubwa zaidi ni pale Esma nae alipoamua kuanza kuongea kuhusu familia ya Mange huku akiwataja baba na mama yake mzazi na mtoto wa kwwanza wa kike wa mange ambae inasemekana amekuwa akifanya biashara ya ngono akiwa bado na umri mdogo.

Bado ligi inazidi kuendelea huku masabiki wakitaka kujua ni nani anaweza kukaa kimya baada ya kutukana na kwa muda mrefu.

Esma Awataja Zari na Wema kuwa na sifa za kuolewa na Diamond.

Esma platinumz ametaa sifa za mwanamke ambae anataka kaka yake amuoe huku akitaja kati ya wanawake wote ambao kaka yake amekuwa nao anaona kuwa Zari na Wema ndio wanaweza kuwa na kaka yake kutokana na sifa walizonazo.

Mwanamke classic, mwanake anaejielewa , mwanamke mwenye akili mwanamke aliyesoma, kwa mfano kama Zari yuko vizuri sana  ni mwanamke anaeielewa na yuko vizuri , pia amesoma lakini pia mwingine Wema, mwanamke ambae shule kidogo imeingia ingia .

Hata baada ya kuwataja wema na zari kama wanawake alioona wanaweza  kuolewa na kaka yake lakini pia esma amesema kuwa ikitokea akaletewa mwanamke tofauti na sifa alizozitaja basi kwake haitakuwa shida ataumia roho lakini baadae  atamzoea.

yoyote atakae niletea kwangu itakuwa sawa tu na siwezi kumsemea ni nai lakini hata kama atamleta na sijamkubali najua roho itaniuma lakini itaenda baadae nitamzoea.

Esma Aelezea Anavyojiskia Mama yake Akitukanwa Mitandaoni

Mwanadada Esma Platinumz, dada wa msanii mkubwa wa bongo fleva Diamond Platinumz,ameongea na waandishi wa habari wa wasafi tv na kufunguka ya moyoni kuhusu  jinsi anavyojisikia anapoona matusi katika mitandao ya kijamii kuhusu matusi yanayomuendea mama yake mzazi.

Esma anasema kuwa mara nyingi amekuwa akikaa kimya lakini kuna muda inamuumiza sana moaka kuamua kuwajibu wanaomtukana kwa sababu hata yeye anajisikia vibaya.

Esma anasema kuwa pamoja na  yote lakini wanaona saa zingine hakuna cha kufanya kutokana na kuwa tayari wameshaingia katika mitandao ya kijamii na kujulikana hivyo wanavumilia hivyo hivyo  na hakuna jinsi ya kufanya kwa yanayotokea.

Najiskia vibaya sana na unajua mimi huwa sipendagi sana kuingilia katika maswala kama hayo,ila kuna wakati ukisoma unajikuta unashindwa kuvumilia hasira zako kwaio unajikuta unasoma na wewe unajibu pale pale.ila ni kitu ambacho kinauma sana lakini hakikwepeki kwa sababu tayari tulishaingia katika ulimwengu wa kujulikana, watu wanakujua na kukufatilia.

Niko Bize Nafanya Maandalizi ya Kumpokea Wifi Yangu ;Esma

Dada wa staa maarufu bongo na nje ya bongo amefunguka na kusema kuwwa mwezi huu wote wa ramadhani yuko busy kufanya maandalizi ya kumpokea wifi yake zari kutoka Afrika ya Kusini.Esma anasema kuwa hawezi kuelezea furaha aliyonayo moyoni mwake kila anapofikiria kuwa wifi yake mpendwa anarudi nyumbani.

Ikumbukwe kuwa Zari alikuwa Afrika ya Kusini kwa muda mrefu na hata alipokuwa akija Tanzania alikuwa afikii kwa ndugu wa Diamond kwa sababu wawili hao hawakuwa na maelewano.

yaani sijui nisemeje lakini madale, tandare kote  anasubiriwa ndege tausi atue hapo,nikop bize mimi kumsubiriwifi yangu maana sio kwa kummisi huko nilikommisi.yaan natamanai sana sikukuu ya eid tukale wote

Esma Amkana Hamisa Mobeto Kweupe

Mwanadada Esma Platinumz amemkana Hamisa Mobeto kwamba  sio rafiki yake tena kwa sasa hivi na kusema kuwa hajui chochote kuhusu mahusiano ya rafiki yake huyo na  kaka yake Diamond Platinumz.

Akiongea katika sherehe waliofanya wikiend iliyopita walipokuwa wakiukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani, esma anasema kuwa hajui chochte kuhusu mahusiano ya wawili hao na ndio kwanza ameyasikia kutoka kwa mtangazaji huyo na kama ni kweli basi hana cha kuzungumza kuhusu hilo.

 Ndo kwanza nasikia kwako taarifa hizo wala hata sijui kama wamevalishana pete,hamisa mobeto alikuwa rafiki yangu lakini no comments,alikuwa rafiki yangu lakini sio kwa sasa hivi.

Esma Akubali Kumuonea Wivu Zabibu Kiba, Amtaka Kaka Yake Aoe

Wikiend iliyopita ,msanii alikiba alifunga ndoa na mwanamke kutoka kenya ambapo kati ya wasanii waliomtakia kheri siku ya ndoa yake ni msanii mwenzie Diamond Platinumz ambae watu wengi hawakuamiani kama angeweza kumpa hongera hizo.

Dada wa msanii diamond anaejulikana kwa jina la esma platinumz, alifunguka na kuandika katika ukurasa wake kuwa anamuonea wivu sana dada ayke na alikiba kwa furaha aliyonayo kuona kaka yake anaoa.

Akiongea tena kwa nara nyingine katika viwanja vya Leaders club , esma anakiri kuwa ni kweli amekuwa akimuonea wivu kwa sababu hata yeye anatamani sana kaka yake awe na mke mmoja wa halali na sio kucheouka kila siku na pia kaka yake akiona hiyo itawapa wao nguvu kwa sababu wamekuwa wakitukanwa sana na watu kutokana na tabia ya kaka yao kubadilisha wanawake lakini hawana cha kufanya.

sisi hatuna kosa kwamba ukiletewa mtu ukasema  huyu simtaki, inabidi umkubali tu, sasa anapooa unakua u ajua kabisa kuwa huyu ndo wa halali kwaio unakuwa na nguvu ya kusema kwanin upo na huyo wakati huyu yupo.nilijisiakia wivu kwakweli na hata nilivyoandika niliandika huku nikiwa nasisimuka mpka  nywele.

Esma Afunguka, Anatamani Diamond Nae Aoe

Dada wa msanii mkubwa nchini, Diamond Platinumz amefunguka mazito kuhusu maishaya ubachela aliyonayo mdogo wake diamond platinumz kwa sasa.Esma ambae anasema kuwa anatamani sana furaha aliyokuwa nayo dada yake na alikiba (zabibu kiba) siku ya harusi ya alikiba ambayo ilifanyika april 19 awe nayo yeye kumuona kaka yake anaoa.

Katika ukurasa wake wa instagram, Esma aliamua kumjibu kaka yake diamond ambae aliandika maneno yenye kumpongeza alikiba kuwa amesikia alikiba ameoa .

Sio mi suti tuu, mfanye na nyie muoe, sio mnatufanya tunatukanwa tu kila siku , tuheme na kina sie, miwani tu , kheri ya ndoa , mungu akawatangulie na kuwatia nguvu na furaha ndoa yenu idumu naimani na sisi ipo iku tutafurahi kama zabibu lo kama nakuona ulivyo na furaha daah naona donge mimi.

Diamond ambae mwaka huu alitangaza kuwa hauwezi kuisha bila kuoa ,anaonekana bado hajaamua kuona hasa baada ya kuonekana mitandaoni bado akiwa na kila dizaini ya wanawake hivyo hii inaonyesha kuwa bado hajachagua mwanamke wa kuoa.

Kifesi Amjibu Esma Kuhusu Kufukuzwa Kazi Wcb

Aliyekuwa mpiga picha maarufu kutoka kundi la Wcb ambae aliajiriwa kwa kazi maalum ya kupiga picha alitangaza kuacha kazi hiyo kwa madai kuwa anataka kuendelea na kufanikisha ndoto za maisha yake ambazo anaona kabisa hawezi kufanikiwa kama atakuwa hapohapo kila siku, lakini pia alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa sababu anataka kumrudia mungu wake kwa sababu kwa muda mrefu  amekuwa akifanya kazi kinyume na maadili ya dini yake.

Lakini cha kushangaza  na kwamba baada ya kifesi kutangaza na kutoa tamko ilo, dada wa msanii Diamond Platinumz aliweka comment chini ya post ya Kifesi katika ukurasa wake wa instagram na kufichua siri kuwa , kifesi ni muongo ajaacha kazi bali amefukuzwa na bosi wake.

acha uongo kifesi, umefukuzwa kazi kwa kucha kufatilia maisha ya bosi wako, yametushinda sisi wewe mtu baki utayaweza-Aliandika hivyo Esma.

Hata hivyo kifesi aliamua kujibu tuhuma hizo na kukanusha kuwa hajawahi kufukuzwa kazi WCB na hata swala la kuktetea zari hajaanza kulifanya leo.

Hapana sijawahi kuachishwa kazi na kama niliachishwa kazi basi sikuwahi kupewa taarifa,ninachofahamu ni kwamba nimechukua maamuzi haya na nai kitu nilichokuwa nimekipanga tangu siku nyingi, so jana nikasema i think its aright time to do this.

kumtetea zari sijaanza leo na hata ukiangalia katika post zangu za insta utaona,nilikuwa nafanya hivyo ingawa pia ni swala gumu kulielezea.

Kifesi alimtetea Zari kwa Diamond na kusema kuwa kitendo cha Diamond kuachana na zari atakuja kukijutia maishani.

 

 

Esma Aongelea Uhusiano Wake na Wema na Hamisa na Zari

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu mtandao wa instagram kuzizima kutokana na habari za Diamond kuachwa na mama wa watoto wake wawili Zari the Bossy, dada wa Diamond, Esma Platinumz aongelea swala hilo na kukori kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akikaa pembeni na kutofatilia mahusiano ya kaka yake kwa sababu hayo ni maswla yake binafsi hivyo hawezi kuyaingilia hata kidogo.

Esma anasemakuwa kwa  mahusiano ya kaka yake na mkewe yatabaki kuwa ni sehemu ya maisha yao ,na kama wanataka kuongea kitu na Diamond hatoweza kumuuliza kuhusu maswal hayo ya mapenzi zaidi ya maswala ya kifamilia tu.

kuna vitu vingine unawaachia wenyewe kwakweli, wao wenyewe watayaongea na kuyamaliza, hivyo havinihusu hata kidogo.hata mimi nikigombana na mtu wangu hawataingilia hayo ni ya kwao .tutakutana na kuongea maswala ya kifamilia tu hayo mengine wataongea wenyewe.

Akiongelea swala la watu latika mitandao kumuita mnafiki na kwamba amekuwa akiwafitinisha watu hasa wanawake aliowahi kutembea na kaka yake kwa kujifanya yupo kila sehemu Esma amejibu:

Mimi watu wote watu wangu, kimji chenyewe hiki kidogo unaweza kwenda sehemu ukakutana nao wote utaaacha kuongea nao, ukisema ugombane na kila aliegombana na kaka yako utakuwa mchawi wewe, mimi pia ni binadamu ninaweza nikadondoka sehemu nani ataniokota kama nitagombana na kila mtu.

Kuhusu uhusiano wake na wema esma anarudu tena na kusema hawezi kamwe kugombana na wea kwa sababu alimjua kabla ya kaka yake.hivyo hawezi kukutana na wema sehemu akamkimbia eti kwa sababu ni adui wa kaka yake.

mimi na wema ni kwa sababu tunajuana tangu zamani, siwezi kumuona sehemu alafu nikamchunia tu au nikae pembeni nisiongee nae lazima nitamfata na nitaongea nae kama ni msibani tutalia wote, pombe tutakunywa wote ,club tutacheza wote na hamisa pia ni hivyo hivyo.

Akimalizia kwa kusema pamoja na kwamba wanakuwa na mawasiliano na Diamond lakini hawezi kumuuliza chochote kuhusu kilichotokea juzi kati yake na Zari , hata kama wanaongea na mama yake mzazi lakini hawezi kufatilia kuhusu maswala ya mahusiano ya watu wengine na hata huko instagram huwa anaingia kwa ajili ya matangazo ya biashara zake tu.