Faiza Asifiwa Kapendeza Baada Ya Kuacha Kuvaa Nusu Utupu

Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amesifiwa kupendeza na mavazi ya heshima baada ya kuachana na mavazi ya nusu uchi.

Mashabiki waliomuona kwenye moja ya Shughuli Hivi karibuni wamesema kwamba amebadilika katika suala zima la mavazi tofauti na zamani ambapo alikuwa akijiachia nusu utupu akiwa kwenye matamasha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Faiza amefunguka na kusema kuwa aliamua kuvaa vazi la heshima kwani hakutaka kuongelewa sana kwani amekuwa mtu wa kuongelewa kwenye kila red carpet event.

Faiza ameshawahi kuzua gumzo siku za nyuma Baada ya kuvaa nguo iliyokuwa inaacha makalio yake wazi kutokana na kuchanwa chanwa Lakini pia Faiza ameshawahi kuvaa shati la kiume tu na tai.

Nilipoachana na Sugu Niliogopa Kudhalilika :-Faiza Ally

Mwanadada Faiza Ally anafunmguka na kuongelea ugumu alioupata hasa baada ya kuchana na mwanaume aliwahi kuwa nae katika mahusiano na kuweza kupata nae mtoto wake kwa kwanza wa kike.

Faiza anasema kuwa mara alipoanza kugombana na sugu ambae ni mbunge wa mbeya mjini anasema kuwa ilimfanya kuwa katika wakati mgumu kwa sababu aliona kuwa akiachana nae basi atarudi katika maisha magumu tena watu watamcheka sana.

Faiza ambae anakiri kuumizwa na kuachana kwao kulimuumiza sana hasa ukiangalia kuwa alikuwa ayari ameshazoea maisha fulani ya pesa , ilikuwa inampa wakati mgumu sana kuamua kufanya maamuzi hayo.

Faiza anasema kuwa alikuwa anapata wakati mgumu kurudi yale maisha ya uswahili.

Faiza- Nikipata Ukimwi Nitajitangaza Hadharani

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kusababisha endapo siku akijigundua kuwa ni muathirika basi hatajificha bali atajitangaza hadharani.

Faiza amefunguka kuwa endapo itatokea bahati mbaya akakwaa ugonjwa wa Ukimwi a.k.a ngoma, kamwe hatajificha au kujiona tofauti, bali atajitangaza hadharani na kuwapa watu moyo kuwa wanaweza kuishi miaka mingi zaidi.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili alisema anawashangaa wenye tatizo hilo ambao hujificha na hata wengine kuambukiza wengine, lakini kwa upande wake ataweka hadharani ili kuwapa elimu wengine na kuzuia maambukizi mapya.

Kama mimi ningekuwa na Ukimwi, ningejitangaza hadharani bila woga wowote wala aibu na tena nitasaidia watu wengine wajiepushe na maambuzi mapya“.

Wiki iliyopita Faiza alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya kuposti video iliyomuonyesha akiwa anapima ugonjwa wa Ukimwi na kuanika majibu yake yaliyoonyesha hana maambukizi ya gonjwa hilo.

Faiza Ally Akiri Kuwahi Kuwa Mdangaji

Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, Faiza Ameibuka na kuweka wazi kuwa ameshawahi kudanga.

Faiza Ally ameeleza kuwa kudanga kwake siyo ishu kwani kama mtu anafanya hivyo kwa kufanya kitu cha maana siyo tatizo Kama atatumia kama njia ya kufanya mambo ya maana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Faiza alisema kama ni kudanga amedanga, lakini alifanya hivyo kwa malengo fulani kwa sababu hakuna anayependa kudanga, alipotatua shida yake kwa sasa amekuwa shujaa na anayejitokeza na kumcheka hajitambui.

Nilidanga kwa sababu zangu nilizokuwa nazo na mwisho wa siku naendelea na maisha yangu”.

Faiza amefungukia biashara zake anazomiliki kwa Hivi sasa ikiwemo tenda ya kuagizia wateja bidhaa kutoka nchini China kuja Tanzania.

Faiza Ally- Ipo Siku Watu Wataelewa Ndoto Zangu

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini na msanii Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally ameibuka na kudai ipo siku watu wataelewa tu ndoto zake.

Faiza Ally amefunguka kuwa watu wengi wanaweza wasimuelewe kwa jinsi anavyopigana na maisha ili tu kutimiza ndoto yake ila ipo siku wataelewa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Faiza alisema anakesha China, kubeba mizigo ya watu waliyomuagiza vitu kwa sababu anatafuta pesa na nia yake kubwa ni kuwa tajiri tena kwa kutafuta kwa jasho.

Naona watu hawanielewi mimi ni kukesha na kubeba mizigo ya watu walioaniagiza ni kwa sababu nausaka utajiri tena siyo hela ya haramu ni ya jasho langu na ninataka kuonyesha watu inawezekana na ipo siku watanisimulia tu”.

Mpaka hivi sasa Faiza amekuwa nchini China kwa muda wa wiki kadhaa na amekuwa akionekana akiwa ananunua bidhaa  mbali mbali kwa ajili ya kufanyia biashara anazoagizwa na wateja Wake.

Faiza Ally- Bado Nampenda Sugu

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Faiza Ally amefunguka na kudai bado anampenda Baba wa Mtoto wake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Sugu na Faiza walikuwa kwenye mahusiano miaka kadhaa iliyopita lakini pamoja na kuachana wamendelea kukamata headlines kwa maugomvi yao ya mitandaoni.

Faiza pamoja na kumdhalilisha Sugu Mara kwa Mara kwenye mitandao ya kijamii huku akimtuhumu kwa kumtelekeza Mtoto wao bila huduma yoyote.

Pamoja na kukosa maelewano Faiza ameibuka na kudai kuwa bado anampenda sana Sugu na amejaribu kuwa na wanaume wengine lakini ameshindwa ikiwemo kuzaa na mwanaume mwingine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza ameandika maneno haya:

Baada ya kuandika maneno hayo mashabiki wengi walimjia juu wakidai kwa kuandika hivyo anakuwa anamkosea heshima mke wa Sugu ambaye hivi sasa ni mjamzito wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza.

Faiza Ally Awatolea Povu Zito Wanaotaka Kuongeza Makalio Kwa Madawa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amejikutwa akiwatolea Povu Zito wanawake ambao wamekuwa wakimsumbua kuhusu madawa ya kuongeza makalio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka wazi kuwa kuna wanawake wamekuwa wakimsumbua kwa kutaka kumtuma madawa ya kichina ya kuongeza makalio.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Faiza ambaye pia ni mfanyabiashara alisema hakuna jambo ambalo halipendi kama mtu kumuagiza dawa za kufanya mabadiliko kwenye mwili hivyo anawasihi wanawake wajikubali kama walivyoumbwa.

Sipendi wanawake kutojikubali. Mimi siwezi kumletea mtu dawa ya kuongeza makalio maana naona kama si za kweli, lakini pia ni vyema kujikubali, hicho ndicho kitu muhimu“.

Faiza ambaye hivi sasa yupo nchini China kwa ajili ya kufunga mizigo ya wateja alianika meseji za wanawake ambao wanaomba kuletewa madawa ya kuomgeza hipsi na makalio.

Biashara Zangu Ndio Zinanikondesha Sio Kingine-FaIza Ally

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza kwa Mbunge wa Mbeya Mjini Sugu, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi kuwa kinachomkondesha kwa hivi sasa ni biashara zake.

Faiza ambaye amesuka gumzo baada ya kuonekana anapukutika mwili wake amedai kuwa anakonda kutokana na mizigo ya watu kuchelewa kufika kwa wakati.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la  Ijumaa Wikienda, Faiza amesema kuwa watu wengi wanamzungumzia na kumshangaa jinsi alivyopungua, lakini hawajui ni jinsi gani hali wala halali usiku kwa sababu ya mizigo ya watu kuchelewa kufika bandarini.

Watu wengi wananiuliza ninakondeshwa na nini, lakini hawajui ni jinsi gani ninakosa amani mizigo ya watu walioniagiza isipofika kwa wakati ninachanganyikiwa kabisa”.

Faiza ni mmoja kati ya wajasiriamali wa Kwenye Instagram ambaye anafanya biashara ya Kukutwa watu vitu kutoka China kuja Tanzania.

 

Faiza Achukizwa na Ukaribu wa Mwanae na Mama wa Kambo.

Mwanadada Faiza Ally ameonekana kukwaza na ukaribu alionao mtoto wake wa kwanza wa kike na mke wa  baba wa mtoto huyo.

Faiza Ambae hapo awali aliwahi kutuma ujumb kwa baba wa mtoto kupitia ukurasa wake wa instagram akitaka mtoto huyo aawahi kurid kutokana na kufungua shule aliwafanya baadhi ya watu kumtolea mapovu kutokana na matatizo ya misba aliyokuwa nayo baba wa mtoto wake baada ya kufiwa na mama yake mzazi.

Hata hivyo kuna picha zimekuwa zikisambaa za mtoto wake na mama huyo ambae ni mke wa sugu , picha ambazo zimemkera sana faiza na kumtolea povu mwanamke huyo huku akimuonya kuacha ukaribu na mtoto wake na kumwambia kama anataka mtoto basi atafute wake.

koma kupiga picha na mwanangu zaa wako….baba sasha naomba mkataze mtu mwenye sura mbaya kutafuta kiki kupitia mtoto wangu…unachotaka ni kumtengansha sasg=ha na baba yake na sasa umefanikiwa, sasa mataishia kuona picha tu zake tu insta..

 

 

Faiza- Sijaenda Kwenye Msiba Wa Mama Sugu Sababu Alikuwa Hanipendi

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa Msanii wa Bongo fleva na Mbunge wa Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, Faiza Ally amefunguka na kuweka wazi sababu zilizompelekea mpaka kushindwa kuhudhuria msiba wa Mama Mkwe wake.

Siku chache zilizopita Mama mzazi wa Sugu Bi. Desderia Mbilinyi aliaga dunia baada ya kugua kwa muda mrefu ambapo siku ya jana ilifanyika ibada ya kuaga mwili wa marehemu katika kanisa la Muhimbili hospitali.

Lakini siku ya jana hapo kanisani Faiza hakuonekana kabisa na badala yake alionekana mtoto wake aliyezaa na Sugu hali iliyoibua maswali ya kwanini hakuhudhuria msiba.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Faiza amefunguka kuhusu kutohudhuria Kwenye msiba:

Sijaenda wala sijashiriki Kwenye msiba lakini Sasha ameniwakilisha yupo pale kwa ajili yangu kila mtu akimuona Sasha pale atajua amemuwakilisha Faiza.

Sikujisikia kwenda pale kwa mtu ambaye hajawahi kunipenda na mimi naamini ukienda Kwenye msiba wa mtu ambaye hajawahi kukupenda naamini unaenda kupata dhambi unatakiwa ukifika pale uwe na majonzi na mapenzi kwaiyo sikuhitaji kuwepo sehemu ambayo sijutakiwa kuwepo”.

Faiza amekuwa Kwenye mgogoro wa muda mrefu na Sugu pamoja na Familia yake yote kutokana na malezi ya mtoto wao Sasha.

 

Faiza Ally Azua Mjadala Baada ya Kuweka Picha Akiwa Ananyonyesha.

Mwanadada Faiza ally  siku ya jana aliacha  watu hoi baada ya kuweka picha akiwa anamnyonyesha mtoto wake wa kiume mdogo huku akiwa ameweka picha ya sehemu yake ya maziwa wazi huku mtoto huyo akiwa ananyonya.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii faiza kufanya hivyo kwa sababu alishawahi kuweka picha kiwa leba anajifungua na kusababisha watu wengi kulalamikia picha hiyo huku ikionekana kama ni udhalilishaji kwa wakina mama kama yeye.

Watu wengi wali-react kupitia picha hiyo huku wakimtukana sana kwa kujikosea heshima yeye mwenyewe na wanawake wenzie kwa sababu maswala kama hayo yalipaswa kuwa si ya kuonyesha mpaka katika mitandao ya kijamii kama anavyotaka kufanya yeye.

 

 

Shamsa, Faiza Ally Wamshambulia Zari the Bossy.

Wasanii wa bongo movies nchini wamefunguka na kumshambulia mwanamama Zari The Bossy kwa kile kinachosemekana kuwa mwanadada huyo amekuwa na dharau sana kwa watanzania na kwamba amekuwa akimtesa sana ndugu yao diamond kuhusu watoto wake,

kwa upande wa Faiza Ally ambae yee amewatolea povu mpaka watanzania wenzake na kusema kuwa wamekuwa wakimuona zari kama mtu muhimu sana wakati hakuna chochote cha maana alichonacho mwanadada huyo.

katika ukurasa wake wa instagram ambapo aliweka picha hiyo na kisha baadae kuifuta , faiza laisema ” wanawake bhana mna ujinga mwingi sana , mnataka watu wote tumuone zari kama mnavyomuona ninyi, mimi ninamuona tu ni mshamba wa kiganda kama washamba wote….msinitagi up*** wenu, kwanza mi mzuri sema maisha tu ndo magumu.

katika posti hiyo hiyo, Shamsa nae akaja na kupigilia msumari na kusema “mtu asiyetabasama muda mwingi yeye kafumba mdomo na hana tabasamu mara nyingi anakuwaga sio mtu mzuri kabisa,wanakuwaga na roho mbaya sana zilizokomaa kiasi kwamba hata kujifanyisha hawezi…

Hata hivyo haya yote yanakuja baaada ya mwanamke huyo kuonekana kukataa kuwaona ndugu na watu wa karibu wa msanii Diamond katika birthday party ya mtoto wake huko Afrika ya Kusini.

 

Faiza Ally Adai Sugu Atakuwa Amelogwa

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amerudi tena kwenye headlines na sakata la mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Faiza amemtolea povu zito Sugu na kudai atakuwa amelogwa maana matendo anayefanya sio ya kawaida hata kidogo na anaamini hakuwa hivyo zamani wakati wako wote.

Faiza amefunguka hayo baada ya sakata lao la juzi ambapo Faiza alimtolea povu Sugu Kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka amuheshimu baada ya Sugu kumtuma Mke wake kufanya shopping ya Faiza badala ya kumpa pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Faiza ameongea haya:

Kwa jinsi ninavyomjua Baba Sasha ni mtu ambaye ana akili zake lakini sijui labda kalogwa kwa sababu nilijua naye mpaka mtoto akakua kuwa na alikuwa responsible father kwa wakati huo kwa nini sasa hivi amekuwa na mwanamke mwingine amebadilika”.

Faiza aliendelea kuelekeza tuhuma za kulogwa kwa Sugu:

Mimi nadhani atakuwa amelogwa tena atakuwa amelogwa milogo mibaya ambayo yeye mwenyewe hajui kwa sababu katika hali ya kawaida huwezi kuleta matatizo Kwenye kumlea mtoto mwenyewe mmoja halafu uwezo unao kama hajalogwa atakuwa na matatizo ya akili”.

 

Sugu Bado Ananipenda:-Faiza Ally Afunguka.

Mwanadada Faiza Ally amefunguka alipokuwa akiongea na waandishi kuhusu mahusiano yake na baba watoto wake Mh Sugu , mbunge wa mbeya ambae amepata nae mtoto mmoja wa kike.

Faiza ambae mara nyingi amekuwa akiongea sana katika mitandao ya kamii akilalamika kuhshu mwanaume huyo kutotimiza mahitaji ya mtoto wake na kwamba amekuwa akimtumia mke mwenzake kutuma mahitaji ya mtoto wake anasema kuwa mwanaume huyo inaonekena anapenda anavyokuwa anamtukana katika mitandao ya kijamii na ndio maana hataki kujirekebisha.

Faiza anasema kuwa kamwe hatoacha kumsema Sugu mpaka pale atakapojirekebisha na kutimiza majukumu yake kama baba.

nadhani sugu bado ananipenda na ndio maana hatimizi vizuri majukumu yake ya malezi na matumizi kwa mwanae shasha.nadhani atakuwa anafurahi vile ninavyomsema na mimi sitakaa niache kumsema mpaka atakapoweza kutimiza mahitahi yake ya malezi.

kama huitaji kuwa na ishu na mtu basi unachopaswa ni kusihi na huyo mtu in a right way,lakini ukiona mt anakutafutia vitu vya kukuumiza ujue bado upo kwenye moyo wake. aweke matumizi ya mtoto kwenye akaunti kila mwezi aone kama mimi nitamsumbua tena.

Faiza Ally Awapa Somo Mabinti Kuhusu Wanaume

Msanii wa Filamu za Bongo Movie na mzazi mwenza wa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, Faiza Ally amefunguka na kuwapa somo watoto wa kike kuhusu wanaume.

Faiza amewasihi mabinti kutowaendekeza wanaume kiasi cha kukubali mapenzi yawarudishe nyuma kimaendeleo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza amewapa ushauri wasichana na kujitoa mfano na kuweka wazi kuwa amerudishwa nyuma kimaendeleo na mapenzi na sasa anakuwa kama anaanza upya:

Kama kuna binti anasoma haya naomba nikwambie tu tafuta maisha usikubali kuyumbishwa akili Wanaume wanaume wanarudisha wanawake nyuma mara nyingi sana.

Mimi ni mmoja ya Wanawake waliorudishwa nyuma na mapenzi na kwa sasa ni kama naanza upya kuna wakati mwingine nawish ningeona ya mbele ili nijiokoe lakini siri ya maisha anaijua Mungu pekee lakini pamoja na hayo yote kama bado unaishi unayo nafasi nyingine usikate tamaa”.

Faiza hakumtaja mwanaume aliyemrudisha nyuma kimaendeleo lakini siku za nyuma ameshawahi kumlaumu Baba mtoto wake Sugu kwa kumpumbaza kimapenzi.

Faiza Ally Athibitisha Kumaliza Bifu Lake na Sugu

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally na mzazi mwenzake ambaye ni  Mbunge wa Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wameonekana kumaliza bifu lao.

Faiza na Sugu wameshawahi kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii mara kwa mara na hata kufikia hatua ya Faiza kumtukana matusi ya nguoni mzazi mwenzake.

Hali ilikuwa mbaya baina yao hadi kufikia hatua ya Sugu kutopewa nafasi ya kumuona binti yao anayeitwa Sasha.

Lakini hivi sasa inaelekea hali ni shwari kwani Faiza ameweka picha Mtandaoni zinazomuonyesha Sugu akiwa na binti yake ambaye ameenda kumtembelea mkoani Mbeya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka picha ya Baba na mtoto na kusindika na ujumbe mfupi ili kudhihirisha kuwa hivi sasa hana tatizo na mzazi mwenzake huyo.

Faiza ameandika:

Najisikia vizuri kuwaona Baba na mtoto pamoja tena…. Nawapenda sana”

.