Vazi la Kiatu kirefu Kwa Wanawake

Wadada wengi  huvaa sana na kujali sana muonekano wa juu zaidi kuliko kuangalia nini anataka kuvaa chini kama kinaendana na kile anachovaa juu.

wataalamu wanashauri kuwa kwa mwanamke mwenye  mguu mnene  ni bora kuvaa kiatu ambacho hakina kifundo ili kisigawe mguu wake juu na chini na kuleta picha mbaya ya mguu.

Ni bora kuvaa kiatu chenye ncha mbele na uwazi ili kuleta muonekano mzuri zaidi.

 

Lakini pia kwa uchaguzi wa viatu angalia rangi ambayo haitakuwa inan’gaa sana katika miguu yako, jaribu sana kuvaa rangi zinazoendana na ngozi ya mwili wako na si vinginevyo.

kwa wanawake wenye miguu mirefu  ni vizuri kuvaa kiatu che kifundo inapendeza zaidi, lakini pia kiatu kiref cha kamba kinakuwa na muonekano mzuroi wa watu wa aina hii.

kwa wenye miguu miembamba, anashauri sana kuvaa kiatu chenye wedges ili kufanya miguu yako kujaa  na kuonekana imependeza katika kiatu husika.

kwa  wenye miguu mifupi,  vaa kiatu kifefu cha kuchongoka mbele na pia kiwe na uwazi kwa nyuma au mikanda.

 

 

 

Pajamas, Trending Fashion Kwa Kina Dada

Kuna fashion imekuwa ikitrend kwa muda kidogo , wadada wa mjini wamekuwa wa kivaa pamajas na kutoka katika matukio tofauti, ingawa hivi juzi pia nguo hii iliwaacha baadhi ya watu midomo wazi baada ya kuvaliwa na Zari The Bossy.

Zari alivaa nguo hii na kuwa na muonekano huu katika uzinduzi wa duka jipya la Mlimani City mali ya Gsm.Lakini watu katika mitandao walimkosoa na kuona kama amevaa nguo ya kulalia katika event kubwa kama ile.

Nguo hii ni moja ya fashion iliyo-trend sana katika mitandao kwa wakina dada, wengine wakivaa na raba chini au kiatu kirefu.Hawa ni baadhi ya mastaa wakubwa waliovaa kabla ya Zari lakini haikuwa imeongelewa kama ilivyoongelewa baada ya kuvaa Zari.

Millen Magesse alivaa nguo hii kipindi cha ujauzito wake , ni zaidi ya miezi mitaano imepita.Chini alipiga na raba zilizomfanya haonekane maridadi zaidi.

Vera Sidika alishawahi kuvaa aina hii ya nguo,huku akichagua rangi inayoenda na mwili wake na alioneka kuwa perfect!!

Vannesa Mdee akiwa ndani ya kivazi hiki cha  pajamas ikiwa ni trend fashion na alitoka vizuri  kwenye event kubwa ya utoaji wa tuzo za  billiboard music awards,chini akiwa amevaa high heels.

Kris Jenner, mama mzazi wa mwanamitindo maarufu Kim Kardashian, ni mmoja wa watu maarufu duniani ambae alishawahi kuonekana akiwa ametoka na style ya pamaja.

Tahiya, mmoja wa video queen wanaofanya vizuri bongo, alishawahi kutoka na kivazi hiki cha pamaja pia.

watu wengine maarufu kama jokate,k-lyn,rihana walishawahi kuonekana na kivazi cha pjama katika events kubwa , kwaio ni fashion inayoweza kumfit mwanadada yoyote ilimradi uweze kupangilia jinsi ya uvaaji wako na rangi gani inayoweza kukufaa ili uweze kuwa na muonekano mzuri.zipo za maua, zipo za mistari lakini pia zipo za rangi moja.