Fid Q Awatolea Povu Zito Waliokula Pesa Za Rambirambi

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefunguka na kuwajia juu watu ambao wamekimbia na   Rambirambi ya msiba wa Godzilla.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Fid Q amesema kwamba wachangishaji walikuwa wengi, lakini baadhi ya michango ilifika ikiwemo iliyokusanywa na Niki Mbishi, Soggy Dogy na Wakazi, lakini wale waliochangisha kwenye vidaftari kuna baadhi hawakufikisha kabisa pesa hizo za rambi rambi.

Kwa taarifa nilizotoka nazo kule watu ambao wamefikisha ni washakaji zetu tu wale ambao walichangisha ka njia ya simu, kule twitter, ambao wamewasilisha ni kina wakazi na Niki mbishi, kulikuwa na wachangishaji wengi, kulikuwa wenye vidaftari, sasa wale wenye vidaftari kuna ambao walifikisha na kuna wengine hawajafikisha kabisaaa”.

Kutokana na hayo Fid Q amesema watu hao bado wana nafasi ya kuzirudisha na kuwasilisha kwa familia ya Godzilla, lakini wasipofanya hivyo Mungu ndiye atawahukumu.

Wito wangu kwa wote ni sawa tu kupita na rambi rambi, wajue ile ni rambi rambi watu wametoa kusaidia pale palipopungua, kwa hiyo bado muda wanao, watumie fursa hii kurudisha kisichokuwa chao, na kama hawatarudisha basi tumuchie aliyeumba wahukumu yeye“.

 

Account Ya Marehemu Godzilla Yadukuliwa na Kugeuzwa Page Ya Umbea

Account ya mtandao wa Instagram ya Aliyekuwa Msanii wa Bongo fleva Godzilla, aliyefariki dunia siku chache zilizopita imedukuliwa.

Ni siku tano zimepita tokea Godzilla apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kindondoni jijini DSM February 16,2019, lakini jambo lililowahuzunisha wengi ni kitendo cha akaunti yake ya Instagram kua-hacked account na kufanywa page ya umbea.

Msanii wa Hip Hop Fid Q hakutaka kitu hiki kipite hivyo ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa taarifa kuwa account aliyokuwa akiitumia Marehemu Godzilla imechukuliwa na sasa inamilikiwa na Umbea Queen na ameonyesha kusikitishwa na kitendo hiko.

Daaah.. Yaani hatujafikisha hata wiki tangu tumpumzishe ndugu yetu kwenye makazi yake ya milele.. HACKERS washapita na page ya insta ya ZIZI..!!? ??”.

Fid Q Ampa Shavu Msanii wa Taarab

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amempa Shavu Msanii maarufu wa Taarabu nchini Isha Mashauzi katika kazi yake mpya.

Wimbo mpya wa Fid Q unaenda kwa jina la  ‘Bam Bam’ iliyowakutanisha Isha Mashauzi, Rich Mavoko na Big Jahman huku Wimbo huo ukimya umetengenezwa na Marco Chali toka Mj Records.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Fid Q amefunguka na kusema kuwa ameamua kumshirikisha Isha Mashauzi ambaye amezoeleka kuimba muziki wa Taarabu kwa sababu ya uwezo Wake wa kuimba kwa style nyingi.

Yaani kilichotokea Mpaka nikamfikiria nilikutana naye sehemu anaimba covers na nyimbo nyingine nyingine nikasema HA! Mbona mimi nilijua unaimba taarabu tu wewe, akasema hapana mimi naimba muziki aina tofauti tofauti.

Kwaiyo nilipokuwa studio nilisema nahitaji mtu ambaye ana tabia ya kupita na mistari yangu ndio ilifanya apate attention yangu”.

 

 

Fid Q Ataja Sababu Iliyomchelewesha Kuoa

Msanii wa Muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amefunguka na kuweka wazi sababu iliyomfabya Mpaka akachelewa kuoa.

Fid Q alifunga ndoa na Mpenzi Wake wa siku nchini ambaye ameshakuwa naye kwenye mahusiano kwa miaka mingi Lakini pia mwanamke ambaye amezaa naye Mtoto.

Ndoa hiyo ilifungwa mwaka jana mwishoni ambapo ilionekana kuhudhuriwa na ndugu wa karibu kwani wasanii hawakuonekana kwenye shughuli.

Lakini akiwa ndani ya ndoa Fid Q amefunguka na kuweza wazi sababu iliyomfanya Mpaka Akawa hajaoa mapema kama ambavyo alikuwa anategemewa.

Nilichelewa kuoa kwa sababu nilichelewa kupata mwanamke ambaye tungeendana, kwani ambao nilikuwa nawapata tulikuwa hatuendani baadhi ya vitu Lakini nilivyompata mke Wangu kwa kweli naona kabisa kuna vitu vingi tunashabihana na vichache tupo tofauti”.

 

Fid Q Afunga Ndoa na Mpenzi Wake Wa Siku Nyingi

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Fid Q amefunga ndoa rasmi na Mpenzi Wake ambaye amezaa naye Mtoto mmoja.

Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q,  amefunga ndoa siku ya jana katika Msikiti wa Qiblatain Boko Jijini Dar es Salaam.

Fid Q alimvisha pete ya uchumba Mpenzi Wake huyo siku chache zilizopita katika mkesha wa mwaka mpya na kufunga naye ndoa siku ya jana mwaka mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Fid Q aliandika ujumbe huu Baada ya kumvisha pete Mpenzi Wake:

https://www.instagram.com/p/BsAK-gFD0rU/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=7zc1chke3w3b

Fid Q Afunga Ndoa

Msanii mkongwe Fid q amefanikisha safri yake ya mapenzi baada ya kuamua kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi ambae wiki iliyopita aliamua kumvisha pete ya uchumba na hata january 2019  kuamua kufunga nae pingu za maisha.

Mwaka 2018 umekuwa mwaka mwema kwa baadhi ya wasanii hasa wa kiume ndani ya bongo fleva kwa sababu idaidi kubwa ya wasanii hao wamefanikiwa katika swala la kufunga ndoa na kuachana na ubachela.

 

Fid Q Ajibu Tuhuma za Muziki Kumkosesha Mafanikio kwa Hili

msanii Fid q ameamua kuwajibu kwa vitendo wale wote ambao walimsema vibaya kwamba hana mafanikio yoyote katika maisha pamoja na kwamba amekuwa akifanya muzki kwa muda mrefu kulinganisha na baadhi ya wasanii.

Fid q anasema kuwa mara nyingi amekuwa hapendi kuweka maisha yake binafsi wazi sana kwa sababu ni maisha yake lakini maneno hayo yalimuumiza sana kiasi kwamba ameona ni bora aweke wazi swala hilo kwa vitendo.

Fid q ambae anasema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa yeye ni moja ya msanii mwenye ushawishi mkuwa katika muziki lakini hakuna cha maana cha maendeleo anafanya hata kwa maisha yake na ndio maana ameamua kuweka wazi gari yake ya thamani aina ya jeep yenye DJ set ya muziki nyuma.

kuna kitu kiliniumiza sana hasa ale waliosema kuwa mimi ni msanii mkubwa sana katika game na nimekuwa nina influence kubwa sana lakini mnavyosema sina mafanikio haileti maana ,, nieamua kufanya hivyo kuonyesha hii kitu kama kuwasaidia vijana kuwa kumbe hata hii inatija.

Gari hilo la Fid q , ina tahamni ya dola zaidi ya 33,320 ambayo ni zaidi ya milion 76 za kitanzania.

Fid Q Atangaza Kufunga Ndoa Kabla Ya Mwaka Kuisha

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu Kama Fid Q ameibuka na kuweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa mwaka huu Baadaye.

Fid Q ameweka wazi moja kati ya watu walimsukuma kufikia uamuzi huo ni Msanii mwenzake Stamina ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu.

Fid Q alifunguka hayo Wiki iliyopita kwenye sherehe fupi ya kumbu kumbu ya siku ya kuzaliwa Stamina, ambapo alieleza kuwa maisha ya ndoa yanambadilisha mtu.

Kitu ambacho hukifahamu wewe (STAMINA) au labda watu wengi hawakifahamu. Wewe pia unani-inspire mimi siku hizi unanielewa vizuri, Unani-inspire kama Artist, Lifestyle, umebadilika sana siku hizi umekuwa mtu wa familia.  Kwa kupitia wewe mimi nina mpango wa kuoa mwezi Desemba”.

Fid Q na mpenzi wake huyo wamefanikiwa kuzaa Mtoto mmoja.

Fid Q Awaomba Radhi WCB Baada Ya Mgogoro Wa Wasafi Festival na Fiesta

Mwanamuziki wa hop hop nchini Fid Q ameibuka na kumuandikia ujumbe wa kumuomba radhi meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale mara Baada ya mgogoro wao.

Sakata hilo kati ya Fid Q na Wasafi lilianza maraa Baada ya Fid Q kuamua kufanya shoo kwenye Fiesta ya Clouds na kukataa kufanya shoo Wasafi Festival siku ya jumamosi tarehe 24.

Baada ya kufikia uamuzi wa kufanya show Fiesta alifanya tangazo la Tigo Fiesta ambalo linasambaa mtandaoni akitafsirikiwa kwamba alitupa dongo kwa Wasafi Festival.

Kupitia video hiyo, Fid alisikika akisema “Yani nyinyi mnataka kusubiri watu wafanye halafu na nyie mfanye, kawambie acheni upumbavu ni moja kubwa” kauli ambayo ilitafsiriwa ni dongo kwa kwambi hiyo.

Baada ya sintofahamu hiyo Fid q aliamua kutoa kauli yake huku akiomba radhi wa WCB kama walimtafsiri vibaya kwani hakuwa na nia ya kuwarushia vidongo.

PART 1: Nimeonelea si vibaya nikifungua hiki kigazeti changu na sentensi hii—-.> “ Keki ya taifa ni kubwa sana na ina vipande vingi vya kuwatosha wachakarikaji wote wenye kuistahiki “

Na kwakua Allah ndio mtoaji riziki, mimi kama mimi sina hayo mamlaka au hata hiyo roho mbaya ya kutamani wachakarikaji wenzangu mkwame ktk harakati zenu, ninasema hivi ni kwasababu siku zote huwa siamini kama nitapungukiwa kitu nyinyi mkifanikiwa, na siamini hivyo kwasababu ninajiamini mimi ni mchakarikaji na kipande changu cha KEKI bado kipo mezani kinaningojea ( cha muhimu ni PUMZI na DUA tu ).. ni ukweli tupo kwenye tasnia moja na kila mmoja wetu anajaribu kufanya lile alionalo sahihi ili kusogea mbele, na iko wazi mmeshafanya na mnaendelea kufanya mengi makubwa, nami bila kusita siku zote nimekua ni mtu wa kuwapongeza iwe kwa njia ya mitandao au tukutanapo ana kwa ana.. mie hufanya vile kiroho safi pasina chembe yoyote ya unafiki. ••••••••••••
Nimeyasema hayo hapo juu ili tu uweze au muweze kupata picha halisi ya kilichomo moyoni mwangu na pia kuwakumbusha ya kwamba mimi pia ninao uhuru wa kufanya shughuli zangu za sanaa na yeyote ambaye nimeridhia nae kimaslahi pasina kujali kama jicho la pembeni yangu linaiona faida iliyopo au laah.. sioni ni busara kwa nyie kuja na kujaribu kunipangia yupi nifanye nae au yupi nisifanye nae ili kuwaridhisha machoni/ mioyoni mwenu.. na kama mnaamini ni haki yenu ya msingi mimi kuyafuata hayo matakwa yenu basi naomba nikujuzeni ndugu zangu mtakua mmeonyesha UBINAFSI wa hali ya juu kwenye hili.. pia kumbukeni mimi pia nishawahi kuwa na matatizo na MJENGO.. lakini nilijikuta ninapambana peke yangu hadi UTULIVU uliporejea pasina msaada wa mtu yeyote.. na sikupambana peke yangu kwasababu hamkua na taarifa, taarifa mlikua nazo lakini ninafikiri mlikua mmetingwa na shughuli zenu za ujenzi wa taifa kiasi kwamba hamkuona kama kuniongezea nguvu ingesaidia lile zoezi kuisha haraka.. amini msiamini sijawahi kumuwekea mtu yeyote kinyongo kwenye hilo, na hiyo kitu ilinifunza sana juu ya suala zima la KUJIPAMBANIA MIE MWENYEWE kwenye situation yoyote ile na KUTOKUPIGANA VITA NISIYOIJUA au ISIYONIHUSU.

PART 2: Yote na yote.. Kiukweli yale maneno ya kwenye promo ya “MOJA KUBWA” sikutegemea kama yangekua na uzito huu uliopelekea ndugu yangu uchafukwe kiasi cha kunifungulia bomba la matusi humu insta.. kwanza sikumbuki hata kama niliyatamka kwa nia ya kuleta msigishano huu.. Lakini kama kweli nimewakwaza… Naomba mnisamehe kibinadamu kwa hilo ,naomba tumuache SHETANI apite na mwisho naomba nimalize kwa kusema.. BURUDANI sio VITA <hivyo ninawatakia kila la heri/ MAFANIKIO ya hali ya juu ktk MAPINDUZI YA BURUDANI huko MTWARA.. KEKI YA TAIFA NI KUBWA SANA NA INA VIPANDE VINGI VINAVYOTOSHA KUMFIKIA KILA ANAYESTAHIKI KWA KUDRA ZAKE MUWEZA WA VYOTE…. MAULID NJEMA ??”.

 

Simuoni wa Kunipa Upinzani :-Fid Q

Rapper mkongwe nchini fareed kubanda maarufu kama Fid Q amefunguka na kusema kuwa kitu kikubwa kinachsababisha wasanii wengi na kazi zao kushindwa kufanya vizuri ni kutokana na upinzani mkubwa wanaotengeneza baina yao na kuweka mashindano sana.

Maswala ya mashindano mara nyingi mimi huwa siyapendi sana kwa sababu huwa yanatengeneza majkundi na ma-timu  mabvyo vinawadumaza wasanii wakashindwa kufikiria jinsi ya kukuza muziki wao, badala yake wanakuwa wanafanya muziki kwa ajili ya kupata nafasi kwa mashabiki badala ya kufanya muziki mzuri.

Fid q anasema kuwa swala hilo la upinzani linafanya kiasi kwamba  wasanii wapya wanaokuja wanaokuwa hawapati attention kubwa kwa mashabiki kwa sababu tu wanakuwa tayari wametengeneza upinzani wa Simba na Yanga.

hata hivyo fid q anasema kuwa kwa upande wake hana shida na wala hana mpinzani kwa sababu muziki wa aina yake hakuna wa kufanana nae.

 mimi binafsi sina chalenge kwa sababu nimekuwa nikifanya muziki wangu kwa muda mrefu na wala sina mpinzani wa kushindana nae.

Fid Q Akanusha Kuwa na Bifu na Joh Makini

Msanii wa hip hop nchini kwa muda mrefu Fid q amefunguka na kusema kuwa hana bifu lolote na msanii mwenzake joh makini kama ambavyo imekuwa ikisemekana katika mitandao ya kijamii kuhusu wao kuwa na bifu hasa baada ya kutoa wimbo wake mpya ambao kuna baadhi ya maneno yalionekana kumlenga msanii huyo.

Alipokuwa akiongea na Big Chawa kutoka planet bongo ya EATV , Fid q anasema kuwa kutokana na kuwepo na maneno katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa bifu kati yao ndio maana aliamua kumuimbia msanii huyo.

La hasha wimbo wangu wa kibiriti hauna  uhusiano owowte na  joh makini  kwa lolote bali ni wimbo ambao unanihusu mimi kwa 100% , kwa sababu ninaongelea wale watu waliokuwa wakiniponda kila ninapotoa kazi zangu, kwaio nimejilenga mwenyewe na wala sijatoa kwa ajili ya mtu yoyote.

Hata hivyo pia joh makini alisema kuwa atatoa wimbo kwa ajili ya msanii Fid q kwa sababu ya sikukuu yake ya kuzaliwa.

Fid q Apokea Tuzo ya Heshima , Wana Mwanza Wamshukuru kwa Kuwawakilisha Vizuri katika Muziki.

Rapa na Staa wa muziki kutoka Tanzania, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q amepokea tuzo ya heshima ya kuwakilisha vyema kanda ya Ziwa kupitia Muziki toka kwa wataalam wa masuala ya mazingira Tanzania ‘KIJANI CONSULT TZ’.

Kupitia Ukurasa wake rasmi wa Instagram, Rapa Fid Q aliweka Picha za mwanae wa kwanza wa Kiume, ‘Feisal’ akiwa kakaa kando ya Tuzo hiyo na kuandika:
Jana nimepokea TUZO YA HESHIMA YA KUIWAKILISHA VYEMA KANDA YA           ZIWA KUPITIA MZIKI toka kwa wataalam wa masuala ya mazingira waitwao                KIJANI CONSULT TZ… MWANZA ninakuja na team nzima ya SPORTS MUSIC               ili tusherehekee TUZO hii pale UWANJA WA KIRUMBA leo kuanzia mchana                    hadi mida mibovu.. karibuni sana.

Fid Q Aanza Kazi Rasmi TUMA kwa Kuwasilisha Maombi Serikalini.

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Fared Kubanda maarufu kama Fid q ameanz akazi rasmi kwa kutuma maombi kwa serikali kuwasaidia wasanii kutatua matatizo yao ya kimaslahi kwa kuwa wao hawana sehemu yoyote ambayo wanaweza wakalalamika kuhusu matatzo wanayoyapata wakiwa kazini.

Kwa kuitumia siku ya wafanyakazi, Fid  Q ambae siku moja iliyopita alitoka kuchaguliwa  kuwa mwenyekiti wa uchumi na fedha katika chama cha wasanii wa kizazi kipya Tanzania.

Sanaa ni sekta rasmi sasa hivi lakini bado haijatungiwa sera , hivyo ni sawa na kuwa na ofisi isiyokuwa na kanuni, taratibu wala sheria kwa kifupi  bado tunaongozwa na sera ya utamaduni .tunayofura kubwa kwa kutumia siku hii ya wafanyakazi kwa kuikumbusha WIZARA na serikali kwa ujumla kutuundia  sera ili sanaa yetu iweze kuleta tija kwa serikali.

Kwa kuongezea Fid Q anasema kuwa wasanii wamekuwa wakilipa kodi kubwa kwa ajili ya kazi zao lakini kazi zao hazilindwi hivyo hii inahatarisha  uchumi wa wasanii kwa sababu itafika sehemu watakuwa hawana faida wanayoipata kutoka katika kazi zao.

Fid Q Aingilia Kati Sakata la Roma na BASATA.

Rapa Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q ameamua kuchukua jukumu la kuanzisha mazungumzo na Baraza la Sanaa Tanzania baada ya kutolewa kwa adhabu kwa msanii mwenzake wa muziki Roma Mkatoliki na kumfungia kwa kipindi cha miezi sita kutokufanya kazi yoyote ya muziki.

Fid Q alikuwa ni mtu wa kwanza kuonyesha hisia zake za kuumia na hukumu hiyo huku akiamini kuwa miezi sita ni minhi sana kwa msanii roma kutokana na ukweli kwamba msanii huyo ana familia yenye mke na watoto wanaomtegemea kupitia kazi hiyo.

waswahili wanasema mambo ya kusadifu ni kutosheleza haja  ya chunguni , yale yaletayo faida  kama chakula n.k, tunaomba mturuhusu tuje tujadili hii sheria ya kifungo upya siu ya jumatatu ili kumuokoa baba anayetegemewa na familia kwa kupitia sanaa.

Kupitia ukurasa wa Twitter, Baraza la Sanaa pia lilimaua kumjibu Fid Q na kumtaka akaribie kwa ajili ya mazungumzo ya swala la msanii huyo.

milango iko wazi muda wote,Baraza limesukumwa kuundwa kwa umoja  wa wasanii na kujenga mfumo rasmi wa mawasiliano na majadiliano .bahati mbaya wasanii wengi bado wako nje ya mfumo huo.Limekuwa  likiitisha vikao vya mashauriano , lakini mahudhurio yamekuwa hafifu .Kupitia umoja uliopo karibuni.

Fid Q Akerwa na BASATA, Asema huko ni kukomoana.

Msanii mkongwe wa bongo fleva Fid Q, ameshangazwa na uamuzi wa BASATA kwa kumfungia msanii Roma miezi sita ilhali muziki ndio kitu kikubwa anachokitegemea katika maisha yake ya kila siku.kupiti aukurasa wake wa Twitter Fid Q aliosema kuwa BASATA wamekuwa wakifanya hayo yote kama kuwakomoa wasanii lakini sio kuwarekebisha.

Kwa kuendelea kuonyeshwa kukerwa kwake , Fid Q alisema kuwa kufungiwa kwa nyimbo hizo kutokuchezwa katika vituo vya radio na tv ilikuwa ni adhabu tosha kabisa kwa msanii huyo lakini sio kumfungia kabisa.

Maneno ya Fid q yalikuja baada ya msanii wa hip-hop Roma Mkatoliki kufungiwa kufanya kazi zake za sanaa kwa mizi sita baada ya kukahidi agizo la kubadilisha baadhi ya maneno.

Na hili swala la kumfungia msanii asifany kazi kwa muda wa miezi sita kisa tu kwenye muziki wake kuna neno moja au kumi  yeney ukakasi sio sahihi…kuzizuia zisichezwe kwenye radio au tv ilikuwa ni adhabu tosha kabisa.@basatatanzania hii tabia ya KUKOMOANA mmeitoa wapi.H

Hata hivyo baada ya kuandika hivyo basata walikuja kumjibu na kumwambia kuwa lengo lao kubwa ni kuwarekebisha wasanii na sio vinginevyo

Ndugu @Fid Q wewe binafsi hujawahi pata tatizo kama hili,tungo zenye maadili na zisizo na matusi hujenga jamii yenye afya.tukumbushane,tusimamiane, na kufanya sanaa safi.Fuatilia tamko la Naibu Waziri aliyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego.

 

“Alichofanya Diamond Ni Kuonyesha Hisia Zake”-Fid Q

Msanii mkongwe , Farid Kumbanda maarufu kama Fid Q ambae yupo kwenye game tangu miaka ya 90 na mpaka sasa amekuwa akifanya vizuri katika game lake la sanaa ya muziki amefunguka na kumtetea Diamond kwa kila alichokifanya katika wimbo wake aliomshirikisha unaojulikana kwa jina la Fresh Remix.

Katika wimbo huo  Fid Q aliamua kumshirkisha Diamond Platinumz katika remix na  diamond aliimba style ya kuchana , kitu kilichoonyesha kwa mashabiki pia kumbe Diamond anaweza kufanya vitu tofauti tofauti katika muziki, hata hivyo pamoja na wimbo huu kutoka  kuna  baadhi ya mashabiki waliupokea vizuri  lakin pia wapo ambao waliongea vibaya kuhusu wimbo huo na kusema Diamond ameimba taarabu.

Katika wimbo huo ambao kuna baadhi ya mashairi ilikuwa kama anamlenga mpinzani wake katika muziki, ukisemekana ulikuwa una lengo la kurusha dongo gizani na kutoa mapovu kwa mshindani wake huyo.Hata hivyo msanii Fid Q  amefunguka na kumtetea Diamond na kusema kuwa sio kweli kuwa wimbo huu diamond amefanya uonekana kama wa taaarabu ila amefanya sahihi kwa sababu ameimba hisia zake.

‘”kwenye hiphop ukishapanhga kufanya collabo  na mtu na mmeshapanga itoke, hata kama kakuchana inabidi tu itoke,kufuta mashairi ya mtu ni makosa‘” aliongea Fid Q katika kipindi cha xxl cha clouds tv alipokuwa akiulizwa alipokeaje baadhi ya komenti za mashabiki wake

Hata hivyo Fid Q bado alisisitiza kuwa, baaadhi ya nyimbo watu uimba kwa hisia hivyo Diamond kuchana maneno yale kwenye wimbo ni swala la yeye kuonyesha hisia zake” bado nasisitiza alichokifanya baba Tiffah katika wimbo wa Fresh remix ni kitu sahihi kwa sababu zile  ni hisia zake,na maisha yake ya kila siku,ni kitu sahihi wala sio taarabu”

Wimbo huo ambao uliachiwa mwezi Agosti mwaka huu ulileta tafrani kwa baadhi ya mashabiki wa upande wa pili na kusababisha marumbano makubwa ya majibizano kati ya ‘team mbili yaan ‘team kiba’ na ‘team diamond’ huku team kiba wakishtumu msanii huyo kuwa ameimba kwa lengo la kutoa mipasho kwao.Hata hivyo original ya wimbo wa Fresh bado unafanya vizuri .