Idris Sultan na Wema Sepetu waendelea kuwatumbuiza mashabiki wao, wanataka kurudiana? (Picha)

Wema Sepetu ambaye ni Tanzania sweetheart na mwanamke maarufu Afrika Mashariki ameonekana kuonyesha uwezekano kuwa bado mapenzi yake kwa Idris Sultan bado yako.

Hii ni baada wawili hao kuonekana mtandaoni wa Instagram wakiongea kwenye comment section. Hata hivyo wawili hao huwa wakitaniana na kulingana na maoni ya mashibiki wao, wawili hawa wanaweza kurudiana.

Kwa sasa hakuna anayejua mpenzi wa Wema Sepetu ama Idris Sultan lakini wengi wanapaswa kuridiana kwa sababu mapenzi yao hayafichiki. Tazama baadhi ya comments zao hapa chini;

Bado hali ya Mzee Majuto haijabadilika, adai kuwa anaumwa

Mchekeshaji kutoka Bongo anayetambulika kama King Majuto bado hajapata nafuu hata baada ya kufanyika upasuaji kutokana na tatizo la ugonjwa wa ngiri (hernia).

Hali yake bado haijabadilika kulingana na alichosema baada ya wanahabari kuzungumza naye hivi karibuni. Mzee majuto alisema kuwa bado anahitaji muda mwingi kulala, iliaweze kusikia nafuu.

Baada ya Global publisherz kuzungumza naye, Mzee Majuto alisema:

“Bado nimelala jamani na sijui unataka nini tena? Naumwa na ninasikia maumivu sana na sitaki kuzungumza zaidi maana nimechoka, elewa tu kwamba bado naumwa na ningependa sana uniache ili nipate muda mwingi wa kupumzika, ni kweli hivi karibuni nilipata nafuu kabisa na kuanza kutembea lakini ndiyo hivyo bwana, bado hali haijakaa sawa,”

“Gombaneni, roganeni mpaka muuane” Huu ndio ujumbe Nay aliowaandikia Ommy Dimpoz, King Kiba na Diamond Platnumz

Rapa wa bongo Nay wa Mitego hatimaye ameingilia vita mpya ya Ommy Dimpoz, Diamond Platnumz na King Kiba kwa kutoa maoni yake.

Kupitia mtandao wa Instagram Nay alifunguka kwa kusema kuwa hakuna anayemuunga mkono lakini jambo linalomkasirisha ni kuwahusisha wazazi kwenye vita hivi vyao vya utoto. Aliandika kusema;

Gombaneni, roganeni mpaka muuane, napenda kusikia changamoto kwenye gemu, ila tusiwaingize wazazi wetu tafadhali, tukananeni matusi yote wenyewe kwa wenyewe ikibidi piganeni kabisa atakaye kufa tutazika na itakuwa historia kama Big na Pac.

Akaendelea kwa kuongeza kuwa;

“Ila kuwaingiza wazazi ni ujinga, sipo upande wowote si kwa Kiba, Dimpoz wala Diamond, endeleeni na vita yenu kama wanawake mmechukuliana mabwana, ila suala la wazazi mnavuka mipaka,”

Rosa Ree afunguka sababu za kuvalia mavazi ya nusu utupu

Msanii wa hip hop bongo ni mmoja wa wasanii wa kike ambao hupenda kuvalia mavazi yanaonyesha mwili wake.

Sio kwa sababu anajaribu kuuza nyimbo zake, lakini ni kwa sababu anapenda kuvalia nguo kama hizo.

Akizungumza kwenye mahojiano Rosa Ree’ amefunguka kusema;

“Navaa mavazi ya nusu utupu kwa sababu napenda, mimi ni mwanamuziki,  lazima nivae tofauti na watu wa kawaida, kwa hiyo wanataka hata nikienda kuoga nivae suruali? Acha waseme, ninaziba masikio mimi naangalia muziki wangu tu,” alisema.

Aunt Ezekiel aeleza sababu hatoweza kumrudia mwanaume aliyemuoa miaka 4 zilizopita

Baada ya mpenzi wa Aunt Ezekiel wa kitambo Sunday Demonte kurejelea Tanzania kutoka Dubai baada ya kutumikia kifungo cha miaka kadhaa, Aunt Ezekiel amesema kuwa hawezi mrudia mwanaume huyu.

Aunty Ezekiel

Akizungumza kwenye mahojiano na Risasi Mchanganyiko Aunt Ezekiel alisema;

“Ngoja niulize, hivi jamani mbona watu siyo waelewa? Nani asiyejua kama mimi niko na mtu hivi sasa? Na ninaamini kabisa hata yeye (Demonte) anajua? Kwa hiyo hata kama ameachiwa huru na akaja, ukweli utabaki kuwa ndiyo huohuo tu, kwamba tayari nina mtu mwingine maana hata yeye asingeweza kusubiri muda wote huo, hivyo ajue tu hana chake,”

Aliendelea kuongeza kuwa Sasa hivi hawezi kumuacha Mose Iyobo kwa sababu wakona mtoto na maisha yake yamesonga.

Staa huyo aliongeza kuwa, kwa hivi sasa ni vigumu kuachana na mzazi mwenziye aliyenaye kwa kuwa tayari wana mtoto ambaye anapenda kuwaona wakiwa pamoja, hivyo hawezi kumuacha Mose Iyobo. Aunt alisema;

“Hebu fikiria, mtoto wangu amezoea kutuona pamoja mimi na baba yake na ni kitu ambacho anakipenda sana, sasa kwa nini nimuumize?”

 

Ommy Dimpoz amuandikia Barua mamake Diamond Platnumz

Wengi wanapodhania kuwa Ommy Dimpoz ameamua kukaa kimwa – basi msanii huyu wa bongo hivi leo amewaacha wengi wameshtuka baada ya kumuandikia bi Sandra barua kupitia mtandao wa Instagram.

Ommy aliweka picha yake na ya mama Diamond hukua kiandika;

BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU

Salam zako nimezipata mwanagu hivi kweli ww wa kukosa adabu kuamua kunichamba baba yako? Sasa Kosa langu mimi nini????kwani kuna ubaya kumtandikia kitanda Baby wako king?
#unanioneakwakuasijuikurap?
#sijuiNamiminimkatae
#kamayeyealivyokataawaMobeto
#Yaniunamkataamjukuuwangu
#unakubalikuleawatotowa5siowako
#umerogwawwsioburemwanangu
#NilikuwanajuanimezaaSIMBA
#kumbenimezaaKIMBA
#DavidonaeanalalamikuhusuENEKA
#UmeletaJanjaJanjakwenyefallonu
#utakujakuniuakwapreshajomonii
#Nnaedhalilikamimibabayako
#hayanendakatungevesinyingine
#Rahayavitausichanguesilaha
#BABAMALKIA

Tazama post yake hapa;

Msanii maarufu wa bongo aweka picha ambayo imezua utata mitandoni kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Rayvanny

Diamond Platnumz amekuwa mada ya wiki huu baada ya Hamisa Mobetto kufunua jina la mtoto wake, Abdul Naseeb.

Kwa kufanya hivi, Diamond Platnumz alimbumburushia Mobetto matusi huku akimuita ‘bitch’ na kuwafanya mashabiki wake kumponda kwa kitendo hiki.

Hata hivyo, Diamond Platnumz ameonekana kuendelea kumponda Hamisa kwa kumuwekea picha za kuudhi mitandaoni. Akimsheherekea Rayvanny Leo, Mkali huyo wa Wasafi aliweka picha huku akionekana akimbusu Zari na Vanny akioneka kwenye background.

Kwenye picha hiyo, Simba aliandika;

Jus wanted to wish the guy at the back happy birthday…please tag him!!!

Lakini, mashabiki wake wameonyesha kutoridhika.

“Nitakupa style zote” huu ndio ujumbe aliouandika mke wa Roma

Msanii wa bongo Roma sasa hivi anaonekana kufanya vizuri na wimbo wake mpya aliouachia mwezi Agosti 10th.

Baada ya kuweka wimbo huo YouTube mke wa msanii huyo, Nancy, alitoa ahadi ambayo iliwaacha wengi wameshtuka mitandaoni.

Kulingana na Nancy, video ‘Zimbabwe’ mpya ya mumewe ikipata kufikisha views milioni moja angempa style zote.

Sasa, video hiyo Jana, August 20, 2017 video ya hiyo ilifikisha views milioni katika mtandao wa YouTube tangu ilipoweka. Na kama awali, Nacy kupitia mtandao wa Instagram aliandika;

Finally You Made It #1Milion_Views Ndani ya Week 1 Na siku 3!!! Walahi Mume wangu @roma_zimbabwe#LEO_NITAKUPA_STYLE_ZOTE Kwa Furaha Niliyonayo!!! Hongera Mno!! Much Congrat kwa shemela @nicklassm Nakuona Mbali Saaana!!

 

Fid Q amshirikisha Diamond Platnumz na Rayvanny kwenye mix ya ‘Fresh’ na mashabiki wadai wamemchana Hamisa Mobetto

Fid Q ambaye ni msanii wa muziki wa hip hip Bongo sasa hivi ameachia remix wa wimbo Fresh ambapo ameliwashirikisha Diamond na Rayvanny.

Katika wimbo huu Diamond Platnumz anasikika akirap na kulingana na mashabiki, mwanamuziki huyu anawachambua Kiba na Hamisa Mobetto kwenye maneno aliyotumia.

Rayvanny naye alipewa nafasi ya kuimba chorus na kama kawaida, msanii huyu aliweza kuipa nyimbo hii fleva.

Isikize nyimbo hii hapa;

 

 

 

Uwoya aeleza sababu za muvi za bongo kupotea sokoni

Uwoya ambaye ni mmoja wa waigizaji maarufu Bongo hivi karibuni alifunguka kueleza sababu za soko la muvi za kibongo kwenda chini.

Uwoya
Uwoya

Akizungumza na Global Publisherz, muigizaji huyo alisema kuwa kuna changamoto kadhaa ambazo zimechangia huku akiwalaumu wasambazaji wa muvi za kibongo wanazoziuza muvi hizi kwa bei ya chini.

Tazama mahojiano yake na Global Publisherz hapa;

Swali: Labda mimi siyo mfuatiliaji sana, lakini naona kama filamu zimesimama hivi au?

Uwoya: Zimesimama unamaanisha nini? Yaani hazizalishwi tena au?

Swali: Ninamaanisha haziko kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, filamu zilikuwa nyingi sokoni na watu wakizigombea, sasa hivi sizioni.

Uwoya: Ni kweli, sasa hivi wasanii wamepunguza kutengeneza kazi mpya, sababu kubwa ni soko, limekuwa gumu sana.

Swali: Limekuwa gumu kivipi?

Uwoya: Hapa pana changamoto nyingi, kwanza kwa wasambazaji wenyewe na pia kwa wanunuzi. Kwa upande wa usambazaji, wananunua kazi kwa bei ambayo inatuumiza na mara nyingi tunakuwa hatuna jinsi, ni bora tufanye kazi tuonekane kuliko kukaa tu nyumbani.

Swali: Huoni kuwa ubora duni wa kazi zenu ulichangia kwa wasambazaji kununua kwa bei ndogo?

Uwoya: Wakati mwingine uduni wa kazi unatokana na haohao wasambazaji ambao wana bei zao.

 

TID akana kumpachika Recho mimba

Msanii wa Bongo TID anasemakana kuwa alimpachika msanii mwenzake Recho mimba lakini kulingana na mkongwe huyu wa muziki, amekana tetesi hizi.

Recho

TID akizungumza na kipindi cha Enewz cha EATV alisema kuwa hatarajii mtoto yeyote na Recho huku akiendelea kusemak kuwa kila mtu anataka kuwa na mimba yake. Alisema;

“Hapana, sitarajii mtoto yeyote na Rachel, sina mimba ya Recho, siyo kweli bwana, hamna mtu mwenye mimba wala nini. Kila mtu anataka kuwa na mimba ya Mnyama, sasa wanawake wangapi wanataka kuwa na ujauzito wa mtoto wangu?”,

Hata hivyo hivi karibuni wawili hao walisemekana kuwa ni wapenzi.

Tazama picha kutoka sherehe ya Romy Jons

Romy Jons ambaye anatambulika kama ndugu mkubwa wa Diamond Platnumz – wikendi hii August 18, 2017 alifanya birthday kubwa huku akivutia wasaniii wengi kusheherekea na yeye.

Waliohudhuria ni wasanii wa WCB, Babu Tale, Vanessa Mdee na wasanii wengine kumpa pongezi Romy kwa kuongeza mwaka Mwingine maishani mwaka.

Kupitia mtandao wa instagram Romy aliwashukuru wote waliohudhuria party hiyo, kwa kuandika

“thanks for everyone who showed up last night…shukran sana kwa kila aliyejitokeza jana!najisikiaga faraja sana kusherehekeaga siku yangu ya kuzaliwa na watu wangu wa karibu na wasiokua wakaribu pia!!!!,”

Tazama picha hizo hapa;

Madee anyenyekea baada ya Wolper kumchambua mtandaoni

Msanii wa bongo Madee amejieleza baada ya ishu kubwa kutokea kati yake na muigizaji wa filamu za bongo Wolper.

Hii ilitokea baada ya Madee kutumia picha ya katuni inayofanana na Wolper kwenye wimbo wake mpya aliomshirikisha Tekno.

Kulingana na Wolper, Madee hakumuomba ruhusa ya kutumia picha yake na ndioi ikasababisha ishu hii.

Hata hivyo, akizungumza na Showbiz, Madee alisema, kuwa Tekno alitaka kutumia msichana mweupe na mwenye sifa tofautitofauti na ndipo Madee aliwaza na kumtumia Wolper. Lakini aliomba msamaha kwa makosa yake alisema;

“Nilikosea kumtumia Wolper kwa sababu kwanza sikumuomba. Wolper ni mshkaji nitawasiliana naye ili tuweze kulimaliza,”

 

 

Mr Nice aeleza kwanini anahisi Wakenya wanamtambua kushinda Watanzania

Lucas Mkena anayetambulika kama Mr Nice amefunguka mara ya kwanza kueleza sababu zake za kupiga show Kenya sana kushinda Tanzania.

Akizungumza na Showbiz ya Tanzania, Mr Nice alifunguka kusema mengi ambayo nimeambanisha hapa courtesy ya Global Publishers.

Isome hapa chini;

Showbiz: Mashabiki Bongo walikumisi kwa muda mrefu wangependa kujua ulikuwa wapi na unafanya nini kwa sasa?

Mr Nice: Maisha yangu kwa sasa yapo Kenya, huko nina zaidi ya miaka mitatu nikifanya muziki wangu, nimeamua kuhamishia makazi huko kwa sababu kule wenzetu mambo ya burudani wako mbali sana hivyo kazi zinapatikana kwa wingi tofauti na Bongo.

Showbiz: Vipi kuhusu mazingira ya huko hayakukupa shida? Mr Nice: Hapana halafu unajua maisha yangu ya muziki yamekuwa ya kwenda hapa na pale nchi mbalimbali hivyo hiyo haikunisumbua. Showbiz: Unazungumziaje habari zilizokuwa zikizagaa kuhusu kifo chako?

Mr Nice: Ni chuki tu za baadhi ya Watanzania wenzangu na ninashindwa kuelewa kwa nini wananichukia kiasi hiki wakati nchi nyingine wananiona lulu? Kwa nini wananifanyia hivyo wakati Kenya naishi kama mfalme maana hata nikiambiwa nije kufanya shoo Tanzania, najifikiria mara mbili mbili kwa sababu naona watu wangu wamenitenga.

Showbiz: Kuna siku ulikuwa ukiimba wimbo wako wa Mama huku ukibubujikwa na machozi na kusema unaumia watu wanasema una ugonjwa wa Ukimwi, unazungumziaje hilo?

Mr Nice: Ni kweli watu walinipakazia hivyo na wimbo ule wa Mama unaniliza kwa sababu najua mama yangu angekuwepo angewakemea waache kuzungumza maneno hayo maana mastaa wenye mama zao wakisakamwa tu, mama zao wanaibuka kukanusha.

Showbiz: Kwa nini unasema baadhi ya Watanzania wanakuchukia?

Mr Nice: Kwa sababu wamekuwa ni watu wa kunidharau, kunidhihaki kwa sababu heshima ambayo ningeipata hapa nyumbani naenda kuipata nchi nyingine.

Showbiz: Mashabiki wako wangependa kufahamu huko Kenya upo na familia yako?

Mr Nice: Kenya, nafanya kazi tu, familia yangu yote ipo Tanzania, lakini sijaoa na wala sitegemei kufanya hivyo kwa sababu tayari nina watoto wawili ambao nataka kuwalea bila karaha ya mama wa kambo.

Showbiz: Najua muigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ huko nyuma alikuwa ni mpenzi wako vipi unazungumziaje kuhusu matatizo yaliompata?

Mr Nice: Namuombea ila kwa upande wa Watanzania, waache kushabikia mtu anapopatwa na janga na kuanguka. Wamuombee na waache manenomaneno.

Showbiz: Ni faida gani umeipata mpaka sasa kutokana na muziki?

Mr Nice: Nyingi sana, kwanza nina mijengo ya maana minne, nina usafiri wangu na nina mashamba kutokana na muziki huohuo na miradi yangu mingine mingi.

Diamond Platnumz amchana Hamisa Mobetto baada ya mrembo huyo kumpa mwanae jina “Abdul Naseeb”

Hamisa  Mobetto ameonekana kutojali watakacho sema watu na kumpa mwanae wa siku kumi sasa jina la ‘Abdul Naseeb’ ambalo likedhibitisha kuwa ni mtoto wa muimbaji, Diamond Platnumz.

Mrembo huyo ambaye alitokea kwenye nyimbo ya Salome Hata hivyo hajafunguka kuelezea sababu zake lakini, jana usiku Diamond Platnumz anasemekana kuwa alimchana kwa kuandika;

Hata hivyo Hamisa Mobetto hakujibu kwani Diamond Platnumz hakumtaja mtu yeyote kwa jina. Mashabiki nao kwa sasa wanachochea kusikia atakachosema Hamisa.

Mume wa Aunt Ezekiel arejea Dar baada ya kutumikia kifungo chake Dubai

Aliyekuwa mume wa Aunt Ezekiel anasemekana kurujea Dar baada ya kukawia Dubai alikokuwa akitumikia kifungo chake kutokana na kuishi kinyume cha sheria huko Dubai.

Aunt Ezekiel

Habari hizi zilienezwa na Chanzo kilichodhibitisha kuwa Sunday Demonte yuko Tanzania. Hata hivyo Risasi Mchanganyiko ilizungumza na mdogo wa Demonte, ambaye alisema;

“Sunday mbona ameshatoka kitambo, yupo zake uraiani kwa raha zake, ni mwaka huuhuu ametoka japo sikumbuki ulikuwa mwezi wa ngapi maana sikuwepo, kwa sasa yupo hapa Dar, hayupo Dubai, ukitaka kujua mengi ni vizuri nikuunganishe naye mwenyewe ukamuhoji,” alisema.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Hata  hivyo bado wengi wanangoja kusikia atakachosema Aunt Ezekiel ambaye sasa anatoka kimapenzi na dancer wa Wasafi records, Mose Iyobo.