“Usiogope maneno ya watu” Diamond Platnumz amwambia Harmonize

Wikendi hii iliyopita, Diamond Platnumz, Harmonize na warembo wao walifika katika klabu maarufu ya Nairobi, B Club kuwatumbuiza mashabiki wao wa Kenya katika show iliyowavutia wengi.

Wakali hao wawili wanaaminika kuwa marafiki wa karibu waliwapa wengi kitu cha kuongea hasa baada ya kuonekana na warembo wao, Zari na mpenzi mpya wa Harmonize anayetambulika kama Sarah.

Hata hivyo Diamond Platnumz aliwashangaza wengi baada ya kumuandikia Harmonize ujumbe kupitia Instagram huku akimsihi asiogope maneno ya watu kwani wamepata fedha na mali ya kutosha kupitia muziki wao.

Tazama picha hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BXMcjb7FSgD/

Ruby afunguka baada ya kudaiwa kuwa ujauzito wake ni wa Alikiba

Mwanamziki wa bongo Ruby anadaiwa kuwa na mimba ya Alikiba, hata hivyo hakuna aliye na uhakika wala dhibitisho tosha kuhusu uvumi huu.

Akizungumza na Bongo 5 hivi karibuni Ruby alikiri kuwa amesikia maneno Hata, lakini kulingana na yeye huu ni uvumi usio na ukweli wowote.

Ruby aonyesha mimba yake

Ruby aliendelea kuongeza kwa Sasa amezoea kusikia watu wakidai kuwa yeye ni mpenzi wa Kiba, lakini hana la kusema kwa sababu uhusiano wake na Kiba ni wa urafiki tu.

Tazama mahojiano yake na Bongo 5 hapa;

Harmonize amshirikisha Mr Nice kwenye video yake mpya!

Mkali wa label ya WCB Harmonize ameachia video mpya ‘Sina’ ambayo inaonekana kuwapendeza wengi baada ya kumshirikisha Mr Nice Kama video vixen wake.

Mashabiki wamemshukuru Harmonize na label ya Wasafi kwa kumuamuni Mr Nice na nafasi hiyo ya kuieleza hadithi ambayo Harmonize anayoielezea kwenye wimbo huo.

Itazame video hiyo ambayo imeongozwa na director Khalfani.

Wema Sepetu afunguka kueleza kinachomkera kuhusu Tanzania ya sasa

Mrembo wa filamu Wema Sepetu ameonekana kukasirishwa na alichofanyiwa mtu mmoja aliyekutana na yeye mahakamani hivi karibuni.

Wema Sepetu aliweka tweet kadhaa kupitia mtandao wa Twitter huku akionekana kama amekasirika kwa kilichomtokea mtu huyo wakati wa kusikiliza wa kesi ya Mh.Tundu Lissu.

Aliandika tweet hizo akisema;

 

Z-Anto amtaja mnigeria atakaye shirikiana na yeye hivi karibuni

Z-Anto ambaye ni mmoja wa wasanii ambao walianza muziki zamani ameonyesha uwezo wa kurudisha nyimbo kama za hapo mbeleni baada ya kuachilia nyimbo kadhaa.

Hata hivyo bado hajapata nafasi ya kushirikiana na wasanii wengi lakini kuna uvumi kuwa staa huyu wa Bongo Fleva, huenda akafanya kolabo na pacha wa Kundi la P-Square, Peter Okoye.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Z-Anto alianza kuupongeza uongozi wake wa South For Life (SFL) kwa kumsaidia kuachia nyimbo mzuri zinazovuma kwa sasa. Aliendelea kuwashukuru kwa kkumuunganisha na wasanii wakubwa akiwemo Peter Okoye. Z-Anto alisema,

“Ni furaha ya juu niliyonayo. Yote kwa sasa nawaachia South For Life kwani nipo chini yao, endapo mipango itakaa poa basi mtanisikia nikipaa kimataifa,”

Mashabiki wake Wa Afrika mashariki kwa hivi sasa wanaingojea kuiona project yake.

Hawa kutoka ‘Nitarejea’ alioshirikishwa na Diamond adaiwa kupotelea kwenye vileo!

Nitarejea ni wimbo ambao bado unafanya vizuri Hata baada ya kuachiwa mwaka Wa 2013. Diamond Platnumz alimshirikisha muimbaji anayejulikana kama Hawa na kutokana na sauti yake nzuri, mrembo huyu alitarajiwa kwenda mbali lakini hivyo sivyo mambo yalienda.

Hawa anasemekana kuwa alipata mtoto wake Wa kwanza anayedaiwa kuwa mtoto wa Diamond Platnumz na baadaye akafunga ndoa na mwanaume mwingine ambaye amemsababisha kuingilia vileo kutokana na ‘stress.’

Sasa hivi mrembo huyo amekiri kuwa maisha yake ilipotelea kwenye unywaji wa pombe kali aina ya gongo, kiasi cha kumfanya apoteze mwelekeo maishani mwake.

Akizungumza na Global TV Hawa alisema kuwa alijipata kwenye maisha haya baada ya mumewe kuondoka na kumuacha bila mawasiliano yoyote kwa muda wa miaka miwili baada ya kukaa kwenye ndoa yao kwa muda mfupi.

Kutoka na kufikiria sana, Hawa alitafuta namna ya kutoa ‘stress’ na akaingia kwenye vileo ambavyo vimemdhoofisha kimwili. Amedai kuwa amekonda huku akiomba msaada kutoka kwa mashabiki na wadau kumsaidia kuepuka maisha haya ambayo yanampeleka vibaya.

 

Profesa Jay atajavitu ambavyo vilimpendeza katika harusi yake

Msanii na mbunge kutoka bongo Profesa Jay alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Grace – huku akiwavutia wengi kutoka Tanzania.

Sherehe ya harusi yake ilihudhuriwa na wasanii kama Diamond Platnumz, AY na wengi waliotumbuiza wageni na wazazi wa Profesa Jay na Grace.

Hata hivyo hivi karibuni msanii huyu alifunguka kutaja mambo matatu yaliyomvutia Profesa Jay katika harusi yake. Akizungumza na FNL ya EATV Profesa alisema,

“Chakwanza ni support kubwa ya watu wangu wa mtaa, nikaona watu wote wapo pale especially wasanii wenzangu walikuwepo sana sana, wengine walishindwa kuja kwa sababu mbali mbali,”

Aliongeza kusema;

“Pili media ime-play part yake vizuri sana, lakini kikubwa mbacho namshukuru Mwenyenzi Mungu mbele za haki nimejitahidi hata kuungainsha siasa zetu za Tanzania. Viongozi wote waliopata kuongea  walisema huyu jamaa ametuunganisha, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote walikuwepo pale, ni kitu kikubwa namshukuru Mungu,”

Huyu ndiye mrembo anayetoka na Gnex_thebaddest Wa Clouds FM?

Kuna fununu kuwa mtangazaji wa CloudsFM Gnex_thebaddest anatoka kimapenzi na mrembo mmoja ambaye ni mwanahabari kutoka Kenya, Kamene Goro.

Hii ni baada ya Gnex_thebaddest kuachia picha kadhaa kupitia mtandao wake Wa Instagram huku akimsifia mchumba wake kwa maneno matatu.

Kamene Goro pia amekuwa akiweka picha za Gnex_thebaddest akiziambatanisha na ujumbe unaodhibitisha kuwa wawili hawa wanauwezekano wa kuwa wapenzi.

Mrembo huyu wa Kenya anafanya kazi na kituo kinachoitwa Ebru Tv na ni mtangazaji wa habari za adhuhuri na anatambulika sana kutokana na umbo lake linalowatia wengi wasiwasi. Tazama picha zake hapa:

 

Sababu ya kesi ya Masogange kutosikilizwa mwezi huu

Agnes Gerald anayetambulika kama Masogange bado anangoja kusikilizwa kwa kesi yake baada ya kutofika mahakamani Jana, Julai 13, 2017 kama ilivyohutajika.

Kulingana na wakili wa mrembo huyu, inasemekana kuwa hangeweza kufika kutoka na kuumwa kwa mwili. Wakili wake, Reuben Simwanza akizungumza na hakimu aliomba radhi kwa mteja wake.

Agnes Masogange
Agnes Masogange

Hata hivyo wakili wa Serikali, Constantine Kakula, hakufurahishwa na maneno haya huku akikumbusha mahakamani kuwa hapo mbeleni Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, alikuwa amepeana amri ya kuwa kesi hiyo ianze kusikilizwa Jana.

Agnes Masogange

Wakili wa Masogange aliweza kuisihi mahakama kuihairisha kesi kesi hiyo hadi July 25, 2017. Masogange hata hivyo ameshtakiwa kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroine na Oxazepam na Heroine.

County Boy aeleza mipango yake ya kuwa kutanisha Alikiba na Diamond Platnumz

Mwananziki Country Boy kutoka Tanzania amefunguka kudai kuwa ana mipango ya kuwakutanisha Diamond Platnumz na Alikiba – kitu ambacho tunajua ni ngumu kufanyika.

Msanii huyu akizungumza na Daladala Beat ya Magic Fm alidai kuwa kwa hivi sasa anataka kuwashirikisha wasanii hawa kwa wimbo wake mpya, huku akitarajia kuwa watasikizana. Country Boy alisema;

“Round hii nataka nilete different sound kwa sababu tayari am rapper nataka nitengeneze sound mpya. Nawataka hawa malegendary wawili, hapa Alikiba, hapa Diamond ila siwashirikishi katika track moja, kila mtu na ngoma yake,”

Aliendelea kwa kusema…

“Kila mtu na upande wake natengeneza sound mpya, nahisi nitaleta kitu kikubwa. Ninachoshukuru kwa Mungu mimi nipo flexible naweza kurap katika beat yoyote,”

Hata hivyo wacha tuone Kama Country Boy ataweza kufanya hivi.

Aunty Ezekiel aachia picha mpya kuonesha Princess Cookie alivyokuwa mkubwa!

Muigizaji wa filamu Aunty Ezekiel anafurahia kumuona Cookie akiendelea kuwa mkubwa kila kuchao.

Cookie

Mrembo huyu hivi karibuni aliachia picha mpya za mtoto wake kupitia mtandao wa Instagram huku mashabiki wakiduwaa kumuona alivyokuwa.

Sasa hivi cookie ako karibu kufikisha miaka minne na tunavyojua ni kuwa mtoto huyu amejiunga na shule ili kujifahamisha na wenzake.

Hata hivyo, Ezekiel anaonekana ameipa kazi yake ya uigizaji ili kumpa mtoto wake attention. Tazama picha zao mpya hapa chini;

Chini Bees amjibu Chid Benz baada ya kumchana

Baada ya Chid Benz kumwambia msanii mwenzake Chin Bees awembunifu na kutafuta jina lingine…. Chin Bees ameamua kumjibu mwenzake.

Wawili hawa ambao wanaonekana kuwa na beef kutokana na kufanana kwa majina yao, uenda wakakosana baada ya Chin Bees kusema kuwa hawezi kubadilisha jina ili kumkwepa Chid Benz.

 

Akizungumza kwenye mahojiano na E-News ya EATV, Chin Bees ambaye ni mmoja wa wasanii wanaotamba kupiti nyimbo zake za bongo Fleva aliweka wazi kuwa hana mipango ya kubadilisha jina kwa kuwa hata yafanani. Chin Bees alisema,

“Mimi siwezi kubadilisha jina kwa sababu ya Chid Benz kwa sababu halifananini, very different. Mimi nafanya muziki wangu, siwezi nikakaa nipiganie jina, hivyo bro kama anahitaji jina dah!, sidhani kama jina langu linaendana na lake  me am do my thing.”

Haya basi tutazame tuone watakachafanya sasa!

Nuh Mziwanda afanyiwa upasuaji wa shingo

Msanii wa Bongo Nuh Mziwanda ameandika ujumbe kuwashukuru madaktari wa hospitali ya Mwananyala kwa kumfanyia upasuaji wa shingo baada ya kupata maumivu makali shingoni.

Nuh Mziwanda anayejulikana kwa hit song yake ya Jike Shupa, aliweka picha huku akionekana na bandage shingoni na tabasamu usoni kwa upasuaji salama.

Ingawa bado hajafunguka kusema kilichotokea, Nuh aliandika ujumbe kusema,

“Thanks Jesus….thanks MY SUPER DR KIWALE BINGWA kabisa wa upasuaji ‘Na MWANANYAMARA HOSPITAL kwa surgery (Upasuaji)uliokua chini ya shingo yangu’ bila kusahau MAMA yangu na ndugu zangu waliokua pamoja na mimi.naomba Maombi yenu Mashabiki wangu nirudi katika hali yangu na Kazi ziendelee.Love you.”

Msanii mpya wa Wasafi Records Lava Lava azindua video ya wimbo wake-Bora Tuachane

Lava Lava ameachia wimbo mpya Bora Tuachane ambao unawazingua wengi Afrika Mashariki. Tangu Diamond Platnumz kumtambulisha kama msanii wa Wasafi…Lava Lava amepata mashabiki wengi kwa muda mfupi kuonyesha kuwa yuko tayari kuwatumbuiza wengi.

Hata hivyo Lava Lava ameachia video yake ya kwanza tangu kuingia Wasafi. Video hii imekuja siku mbili tangu kuachia audio.

Mashabiki nao pia wameonekana kumpa support msanii huyu ambaye kwa hivi sasa anawazingua wengi. Sauti yake pia ni ya kumtoa nyoka pangoni na inaonekana kuwa atawapa Harmonize, Rayvanny na Rich Mavoko competition ya kutosha. Tazama video hiyo hapa.