Hamisa Mobetto aendelea kudai kuwa maisha yake na ya Abdul Naseeb yako mashakani

Hamisa Mobetto anaendelea kuhofia kuwa maisha yake na mtoto wake aliyezaliwa Agosti 8, mwaka huu.

Kulingana na marafiki wake wa karibu, Hamisa Mobetto anaishi na wasiwasi kutokana na vitisho anazozipata kila siku kutoka kwa baba ya mtoto wake. Chanzo kimoja kutoka familia ya Hamisa kilisema;

“Unajua baada tu ya kujifungua kulienea habari nyingi kuwa mtoto huyo ni wa msanii huyo hasa baada ya Hamisa kumpa mwanaye jina hilo. Kilichofuata, kwanza msanii huyo alikimbilia kwenye media (vyombo cha habari) kukanusha habari hizo ambazo zimekuwa zikizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu. Unajua jamaa (msanii huyo) alidhani kuna siri chini ya jua kuwa anaweza kuficha jambo hilo maana watu walikuwa wakimchomea kwa mpenzi wake ambaye amezaa naye.

Aliendelea kusema,

“Ili kumziba mdomo Hamisa, msanii huyo aliona ni bora amkane mapema lakini Hamisa siyo wa mchezomchezo maana aligoma kuficha ishu hiyo. Baada ya kuona anaweza akabumburua ishu, msanii huyo alimpiga biti asizungumze na vyombo vya habari kabla ya kumwekea ulinzi wa chinichini kuhakikisha waandishi hawamfikii Hamisa. Sehemu pekee ambayo Hamisa aliona jamaa huyo hawezi kumzuia ni kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Snapchat ‘so’ akawa anaposti vipande vya baadhi ya viungo vya mtoto huyo. Sasa baada ya kuona hivyo, msanii huyo ambaye alikwenda mara moja tu kumuona mtoto huyo alianza kumpigia simu na kumtumia meseji za vitisho. Wewe fikiria Hamisa na kichanga chake sasa anaishi kwa hofu maana jamaa amemuambia kama atafunguka kuwa amezaa naye atamuondoa uhai yeye na mtoto wake. Hali hiyo imeifanya family ya Mobeto iwe na hofu kubwa na ili kujiweka salama, aliona ni bora aende polisi kuripoti ili kama kutakuwa na jambo lolote baya litakalomkuta yeye na mwanaye, basi mhusika atakuwa ni msanii huyo. Mwanzoni tulidhani ni ishu ndogo lakini kwa vitisho anavyopokea Hamisa, vinamnyima raha na kumfanya alie tu.

Akaongeza kuwa…

Hamisa Mobetto na mwanae
Hamisa Mobetto na mwanae

“Kiukweli Hamisa anatia huruma sana na anahitaji msaada kwa sababu mbali na msanii huyo pia anapata vitisho kutoka kwa mpenzi wa jamaa huyo. Sasa watu wanajiuliza, wakati anatembea naye hakujua kuwa kinaweza kupatikana kiumbe? Na kwa ustaa wake anashindwa nini kulihendo suala hilo kwa busara ili lisimchafulie kuliko kutoa vitisho hivyo?” kilifunguka chanzo chetu hicho na kuongeza. Hata kwenye ukurasa wake wa Snapchat, Hamisa ameshatahadharisha juu ya kutishiwa kuuawa yeye na mwanaye.”
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa liliperuzi kwenye ukurasa wake huo na kukutana na ujumbe wa Hamisa uliosomeka:
“Mlidhani atafia tumboni enh…au mlijua nitafia leba…. nyie siyo Mungu na hamtakaa kuwa kamwe…& if anything bad and I mean anything bad happens to me or my son hatutawaacha salama!!!”

 

Hamisa na yeye aka sema;

‘MIMI NA MWANANGU TUNAUAWA WAKATI WOWOTE’ Ni kweli mimi na mwanangu tunauawa muda wowote. Nina ushahidi wa kutosha wa vitisho so nimeona ni vyema nitoe taarifa kwenye vyombo vya usalama,”

Aunt Ezekiel aeleza sababu zake za kutotokea kwenye Bongo Movies

Aunt Ezekiel ambaye ni muigizaji wa movie za Bongo hivi karibuni amefunguka kueleza mbona haonekani kwenye movie hizi Kama kitambo.

Mose Iyobo na Aunty Ezekiel

Mrembo huyo ambaye ni mama ya mtoto mmoja na mpenzi wa dancer kutoka Wasafi Records hivi karibuni alifunguka kudai kuwa anapumzika kwa sasa lakini hivi karibuni. Aunt Ezekiel alikiambia kipindi cha Twenzetu cha Times FM.

“Bongo Movie tunaweza kusema ni kama maisha ya binadamu, kuna time analala, anaamka, anapika, so kunakuwa na kazi tofauti tofauti. Naweza kusema kwa sasa hivi Bongo Movie ni muda wetu wa kurelax kwanza kwa hiyo tumepumzika, tumelala tukishaamka nadhani tutakuja na vitu vingi vya tofauti.”

Aliongeza,

“Sio kwamba tukilala ndio hakuna kitu ambacho kitakuja kikubwa zaidi au hakitachukua akili za Watanzania tena, hapana kulala kwa Bongo Movie ni kulala kwa kujipanga ili tunapokuja kurudi tena turudi vizuri, so mimi siamini kama Bongo Movie imekufa, tumerelax tu,”

Hata hivyo aliyekuwa rafiki yake wa karibu Wema Sepetu amekuwa akiachia projects zake mpya pole pole.

Barakah the Prince amjibu Ben Pol baada ya kudai walimpunguza kwenye show

Msanii kutoka Tanzania Barakah the Prince amefunguka kwa mara ya kwanza kumjibu Ben Pol ambaye alidai hivi karibuni kuwa msanii huyu alipunguzwa kwenye show ambayo alitakiwa kutokea na wasanii wenzake Kama Juma Jux.

Akizungumza kwenye interview mpya na kipindi cha XXL cha Clouds FM Barakah alisema kuwa wake Ben Pol alichozumgumzia kwenye interview yake ni uongo, huku alisema;


“Mimi sipunguzwi, nilijitoa nikawaambia nina menejiment ambayo ina utaratibu wake, ninapofanya kazi lazima kuwe na makubaliano na mkataba kwa sababu wao walishindwa kufuata utartibu nikajitoa kwenye hiyo show yao.”

Aliendelea kwa kusema,

“Hatukuwa na muungano wowote kusema kwamba tulikuwa na tour, tulifanya show moja tu ile, show iliyofuata uongozi wangu ukataka utaratibu wa hizo show waliposhindwa nikawaambia mimi sitaweza kufanya. Sema nyimbo yake ni mbaya asitafute sababu ya kujitetetea… utovu wa nidhamu yule (Ben Pol) baba yangu?”

Picha za Zari Hassan akiwa amevalia kama mwanamke anayefuata maadili ya dini ya Kiislamu

Japo sio mara mingi tunamuona Zari Hassan kama amejistiri, kuna picha zake kadhaa ambazo mrembo huyu ameonekana amevalia dera na buibui ambazo wanawake wa dini wa kiislamu huvaa.

Hapo awali mpenzi wake Diamond Platnumz alisema kuwa yeye hana shida na Zari Hassan kuvaa anavyotaka kwani hawezi kumchagulia wala kumbadilisha kwa kumtaka ajistiri.

Picha ambazo nimezipata mitandaoni, Zari anaonekana kupendeza kwa mavazi haya ingawa hii sio style yake.

Tazama picha hizi hapa chini;

Msanii wa Bongo AT asimulia ugomvi wa Diamond Platnumz na Alikiba ulipoanzia

Ni wengi bado wanajiuliza ni nini kilichotokea Kati ya Diamond Platnumz na Alikiba kuwafanya wawili hao kukosana.

AT ambaye ni maarufu Bongo alisimulia tukio la Kiba na Naseebu akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimbaji huyo maarufu wa muziki wa mduara alisema;

“Tulikuwepo tupo Oman kwenye hotel moja inaitwa Dream tulikuwa tuna show, kwa hiyo walikuwa wanacheza game, Alikiba amechagua Real Madrid na Diamond Barcelona, mimi nimekaa pembeni naangali watu wanacheza game yao. Ali akawa amefungwa mbili, akawa anataka kupiga free kiki kwenye game Diamond akamsukuma akamwambia halafu mwanangu nakutafuta siku nyingi. Alikiba akanyanyuka ikabidi na mimi ninyanyuke sasa, nikamuuliza Ali tatizo nini mbona kama mnataka kupigana halafu tupo ugenini wazee vipi?  Akaniambia huyo dogo kuna vitu anavifanya mimi sijavipenda.”

Aliendelea kwa kusema,

“Mwisho wa siku naona kama vile vitu vinaendelea halafu watu wanakurupuka wala tatizo wao hawalijui. Ebu watafute ukweli ulipo, sijui huyo kamtoa kwenye wimbo huyo, kuna jambo lingine ambalo lipo. Kiukweli kuna vitu ambavyo pengine wao wenyewe wanavijua ni vikubwa zaidi,”

Shilole ametaja sifa za Mwanaume anaempenda

Kuna fununu zinazodai kuwa Shilole amepata mpenzi ambaye anataka kumuoa lakini jambo hili halijamsimamisha kutaja sifa ambazo anazozipenda kwa wanaume.

Akizungunza hivi karibuni msanii huyu wa nyimbo za Bongo alisema kuwa yeye anawapenda wanaumbe ambao wanajitambua na ambao ni warefu ikiwa ni jambo la muonekano. Ingawa aliendelea kusema kila mtu ameumbwa vitofauti, Shilole aliweka wazi kuwa hawezi kutoka na mtu ambaye ni mfupi. Alisema,

“Mimi napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa mimi napenda mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana,Sipendi Wanaume wafupi, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti, ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa“

Shilole alisema haya kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV huku akiongezea kuwa anatamani kuoleka kwani hii ni ndoto ya kila mwanamke.

“Hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima”

Ben Pol aweka picha akiwa nusu uchi, mashabiki nao wamponda

Ben Pol hataki mchezo na iwapo haujaziona picha zake mpya basi hautaelewa ninacho sema. Kwa Mara ya kwanza msanii huyu wa nyimbo za RnB ameachia picha zake akiwa uchi lakini anaonekana kama ameketi huku akificha sehemu zake za nyeti.

Picha hizi aliziweka kwenye mtandao wake wa Instagram na mashabiki wake ambao hakuwa wanatarajia jambo kama hili walimshambulia kwa meneno ya kumtusi na wengine wakimueleza kuwa amepoteza muelekeo wake ikiwa hii ndio ndio njia ameamua kuichukua.

Yeye ndiye msanii wa kwanza wa kiume Bongo kuachia picha kama hizi. Hapo mbeleni wengi walikuwa wamemzoea kuweka picha kama amejivalia nguo zake za designer lakini kwa sasa inaonekana kuwa ameamua kufanya mambo mapya.

Mtindo huu sana sana hutumiwa na wanawake lakini Ben Pol ameamua kuonesha kuwa pia wanaume Wanaweza pia. Iwapo haujaiona picha hiyo basi itazame hapa.

‘Hasara Roho’ ya Darassa kuvunja rekodi ya ‘Muziki’?

Iwapo kuna msanii ambaye anatamba Afrika Mashariki sasa ni Darassa. Miezi mitano iliyopita msanii huyu sliachia wimbo wake wa Muziki na kwa mara ya Kwanza alivunja rekodi ambazo wasanii wengi waliokuwa wamemtangulia hawajafika bado.

Muziki ilitazamwa mara mara 7,859,849 kupitia mtandao wa YouTube na nyimbo yake mpya Hasara Roho inaonyesha kuwa inafuata mtindo huo kwani kwa imeangaliwa mara 933,776 ndani ya wiki mbili.

Hata hivyo hapo awali wengi wa mashabiki waske walihisi kuwa nyimbo hii yake haikuwa na tofauti kubwa na Muziki lakini inaonekana kuwa wanaipenda pole pole tu. Video ya wimbo huo hata hivyo ni wa hali ya juu na ndio maana mashabiki wengi wanaendelea kuonyesha wanaikubali.

Balaa! Jux awajibu wanaodhani uhusiano wake na Vanessa Mdee umekwisha

Kumekuwa na uvumi mitandaoni kuwa Vanessa Mdee na Jux Juma wameachana baada ya Vmoney kuonekana akiwa na wanaume tofauti kwenye picha ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni.

Hata hivyo Jux amefunguka kuhusu maneno haya na kusema kuwa yeye anamuamini mpenzi wake kwani hata picha hizi zikichukuliwa yeye huwa akifanya kazi na hana tatizo na hilo.

Aliendelea kwa kusema pia yeye kuna wakati yeye hupiga picha na wanawake ambao anafanya kazi (project) na wao na hii haimanishi kuwa anatoka na wao. Jux alisema,

“Si kweli mimi nilimind, sababu kama kupiga picha za namna hizo Vanessa anapiga na watu wengi sana picha za namna ile. Naomba nirudi nyuma kusema hili tena wasichana kwenye tasnia yetu sisi wavulana ndiyo tunatakiwa kuwasupport sana kwa sababu wapo wachache.”

Aliongeza kwa kusema,

Muimbaji huyo ameongeza, “Mimi hata nikipiga picha na wanawake 10 hapa, watu watajua tu Jux anafanya video ila Vanessa akipiga picha hizo watu watasema huyu mwanamke mhuni.”

Hussein Machazi asimulia alivyokutana na mchumba wake kutoka Italy

Mkali wa nyimbo za bongo Hussein Machozi hivi sasa anajikaza kufanya nyimbo ambazo vijana wanafanya na baada ya kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni.

Hata hivyo maisha yake pia yanaonekana yamepata muelekeo mpya baada ya kupata mchumba Muitaliano. Akizungumza kwenye mahojiano muimbaji huyu alikiri kuwa hivi sasa anamchumba mbaye anapanga maisha na yeye.

Hussein Machozi

Hussein alisema kuwa alikutana kwanza na dadake mchumba wake huko Mombasa akipiga shoo. Na kwa sababu alipenda alivyokuwa akipiga show, msichana huyo alimuomba namba na wakaanza kuongea lakini hawakuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi.

Aliendelea kusema:

Ilikuwa Mombasa kwenye shoo, miaka kama mitatu hivi iliyopita, baada ya shoo akaja msichana mmoja Mtaliano akasema amependa kazi yangu, tukabadilishana namba, tukawa tunawasiliana. Baadaye yule msichana akanitambulisha kwa dada yake, tukawa tunawasiliana pia. Sasa siku moja dada mtu akamuuliza mdogo wake kama ana uhusiano wa kimapenzi na mimi, akasema hapana, basi akamwambia yeye amenipenda, tukaanza uhusiano.

 

Ni kweli kuwa Hamisa Mobeto ameinunua rangi yake? (Picha)

Iwapo hauna habari kuwa Hamisa Mobeto ni mmoja wa warembo ambao wanawafanya wengi wakose usingizi, basi sasa hivi umejua. Mrembo huyu kutoka bongo ni model na video vixen ambaye amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz na hivi sasa hakuna anayefikia urembo wake.

Hata hivyo kuna wengi ambao wanadai kuwa rangi yake ya mwili ni ya kununua kwani hakuzaliwa akiwa mweupe. Tetesi hizi zimeambatanishwa na picha zake za kitambo kabla ya ‘filters’ kutokea.

Iwapo tetesi hizi zina ukweli, basi kunauwezekano kwamba Hamisa Mobeto amekuwa akizitumia tembe au mafuta ya kugeuza rangi kuwa nyeupe.

Warembo wengi kwa sasa watumia vitu vingi ilikujibadilisha hata baada ya kujua madhara yao. Kwa sasa hatuna uhakika kwamba Hamisa ni mmoja wa watumizi wa tembe hizi.

Tazama picha hizi mbili za mobeto.

Diamond Platnumz amuandikia Ray C ujumbe kumpa moyo wa kutokata tamaa katika muziki wake

Ni wengi ambao hawakudhania kuwa Ray C atarudi kufanya muziki tena baada ya kupotea ndani ya madawa ya kulevya. Hata hivyo mrembo huyu amewafurahisha wengi ambao hawakuwa wamekata tamaa kwake.

Mmoja wa hawa ni Diamond Platnumz ambaye amemwandikia ujumbe wa kumtia moyo huku akimsihi kuendelea na muziki wake japo ya kukawia sana bila kutoa nyimbo.

Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika kusema…

Ray C

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya….

Diamond aliendelea kwa kusema,

Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku? @rayctanzania

Hata hivyo Ray C ameonyesha kuwa hanamipango ya kuacha muziki tena na kuna uwezekano wa kuenda mbali hivi karibuni.

Nuh Mziwanda azionyesha picha za mwanawe na mke wake

Wasanii wengi sasa hivi wameamua kuanza familia zao kwani hawana muda wa kungojea tena. Mmoja wao ni Nuh Mziwanda ambaye alibarikiwa na mtoto wa kike hivi karibuni na kama wasanii wengine ameweka picha ya mwanawake akiwa na mke wake.

Msanii huyu aliposti picha hizi katika mtandao wake wa Instagram akiziweka fikra zake wazi kupitia ujumbe aliomuandikia mtoto wake Anya na mamake. Mtindo huu pia tumeona na Diamond Platnumz na pia Rayvanny ambaye alibarikiwa na mtoto wa kiume hivi karibuni.

Nuh Mziwanda aliandika kusema…

Mungu pekee anajua jinsi gani moyo wangu na mihangaiko yangu inakulenga wewe Mwanangu #ANYAGHILE nasali sana Mungu akupe hekima ,busara ,upendo ,heshima kwa kila rika na upeo wa kujua baya na zuri ‘Nakupenda Mwanangu ANYA nipo kwa ajili yako kipenzi changu haijalishi nitaenda magharibi wala kusini katika hii dunia ? @iam_mrs_mziwanda #anameremeta video link on my bio @89studios #MariaStopesMwenge #DkSele

Tazama picha hizi hapa chini.

Picha ya Rayvanny akiwa na msichana mwingine yazua maswali mitandaoni

Rayvanny ambaye sasa hivi yuko ziara Sweden amewaacha wengi na maswali baada ya kuonekana amemkumbatia msichana mrembo katika picha moja inayosambaa mitandaoni.

Msichana huyo ambaye anafanana na Fahyma anasemekana ndiye anayekula bata na muimbaji huyo Sweden. Hata hivyo hakuna aliyena ana ushahidi kuwa Rayvanny anauhusiano wowote na msichana yule.

Hata hivyo ukitazama picha hiyo haina mabo ya kimapenzi lakini binadamu ni binadamu. Mashabiki wa Fahyma pia wameonekana kuchangia kwenye picha hiyo huku wakimsihi Rayvanny asiivunje roho ya Fahyma kwani amejifungua juzi.

Tazama picha hiyo hapa:

 

Ommy Dimpoz aeleza sababu zake za kukaa kimya kwa muda mrefu

Mkali wa nyimbo za bongo Ommy Dimpoz amekaa miezi kadhaa bila kuachilia project mpya. Japo anasemekana kuwa amepotezwa na vijana wadogo ambao wamekuwa wakionekana wamevalia sare zake na viatu muimbaji huyu ametoa stori nyingine.

Akizungumza katika interview Ommy Dimpoz alifunguka kwa kusema kuwa anauchukua muda wake kutengeneza kitu ambacho akiachilia mashabiki wake watafurahia.

Ommy Dimpoz

Aliendelea kwa kuongeza kuwa hajapotezwa na mtu yeyote kama watu wanavyosema. Alihaidi kuwa hivi karibuni ataachilia nyimbo mpya miezi kadhaa baada ya kufanya kazi na Alikiba.

“Siyo kweli kuwa nimepotea, kwanza najiandaa kuachia kazi mpya ambayo ina ubora wa hali ya juu, wanaosema nimepotea wasubiri waone maajabu yangu,”

Hata hivyo, Ommy Dimpoz ameonekana kunyamaza wakati ambao wasanii wa bongo wanapepea na nyimbo mpya.

Mastaa wa Bongo wajitokeza kwa wingi kumzika baba ya Bella 9

Bella 9 na wanamuziki wa Bongo walijitokeza kwa wingi jana kumzika marehemu mzee Darmian ambaye alifariki usiku wa Machi 18 baada ya kugongwa na pikipiki.

Kulingana na taarifa Mzee Damian alipoteza damu mingi baada ya piki piki kumgonga na kumvunja mguu. Hata hivyo alipelekwa hospitalini ambapo alifariki dunia baada ya dawa zilizokuwa zinahitajika kukosa kupatikana.

Kumpoteza Mzee Damian ni pigo kubwa kwa Bella 9 na ndugu zake kwa kuwa alikuwa ni mwalimu muhimu katika maisha Yao.

Hata hivyo wasanii na marafiki waliohudhuria mazishi haya walimpa Bella 9 nguvu ya kuendelea na maisha yake kwa kuwa ingawa babake alifariki bado maisha yake yatabidi yaendelee.

Tazama picha ya Mazishi haya.