Picha ya Queen Darleen akiwa na bunduki ya zua utata mitandaoni

Queen Darleen ni mmoja wa wasanii kutoka Wasafi records na ingawa yeye pia ndio mwanamke pekee katika label hiyo ya Diamond Platnumz mrembo huyu ni kama dada yake.

Hivi karibuni Queen darleen aliweka picha huku akionekana kuwa amebeba bunduki ambayo imeletautata mitandaoni. Kulingana na mashabiki bunduki hii inaonekana kuwa sio ya kweli, huku wengine wakidai kuwa alitaka kujionyesha kwenye mitanondi.

Hata hivyo, Queen Darleen hakuwajibu mashabiki wake kuzuia kujibishana na wengi wao ambao hawakukifurahia kitendo hiki. Tazama picha hiyo hapa:

?DUNIA SimamaNishukee ???? #duuuuuuuuushwa?????

A post shared by Queen Darleen (@queendarleen_) on

Beka Flavor aeleza baadhi ya changamoto alizopitia Yamoto Band

Beka Flavor amekuwa akijishughulisha na projects mbalimbali baada ya kutoka Yamoto Band. Kama Aslay ambaye walikuwa wakipiga kazi za mkubwa na wanawe Pamoja, pia anafanya nyimbo zake akiwa Solo.

Hii inakuja baada ya wasanii hao kuamua kuwa wangefaidika zaidi ikiwa wangefanya projects zao wakiwa Kama solo artists. Hata hivyo Beka Flavor hivi karibuni amefunguka kudai kuwa kuimba Kama bendi ilikuwa na Changamoto zake.

Akizungumza na kipindi cha Dj Show cha Radio One, Beka alisema…

“Vitu vingi vilikuwa vinanizuia, kwanza nilikuwa si-enjoy kwa sababu nilikuwa naimba verse fupi, mwenywe nilikuwa natamani niimbe verse ndefu lakini wenzio wataimba wapi, hicho ni kitu cha kwanza kilikuwa kinanibana,”

Aliongeza kusema,

“Kuna vitu vingi vimefunguka kupitia mimi mwenyewe, kwanza ilikuwa mtu akinihitaji ni lazima apitie kwa mtu mwingine na mwingine, au kuna kitu kingine ambacho mimi napenda kufanya zaidi ila uongozi unakuta unabana lakini sasa hivi vile navyopenda kuvifanya nafanya na uongozi upo.”

Young Dee afunguka kuhusu uhusiano wake na mama ya mtoto wao

Young Dee ambaye anatambulika na warembo wengi amefunguka kwa mara ya kwanza kuzungumzia uhusiano wake na mamisa ambaye ni mama wa mtoto wao.

Kama inavyojulikana…Young Dee alikana kutoka kimapenzi na mrembo huyu huku akisisitiza kuwa hawakuwa wamepanga kupata mtoto Paloma. Aliendelea kwa kudai kuwa kwa sasa yuko single na uhusiano wake na mamisa umebaki kama ilivyokuwa hapo mbeleni:

 

“Am single and am buys, sina mahusiano, ni kitu ambacho naweza kusema kibinadamu kinatokea kama baraka tu kwa sababu hakuwahi kuwa mpenzi wangu, imebaki kama ilivyokuwa mwanzoni.”

Hata hivyo pia alizungumzia mziki wake mpya kwa kusema,

“Kikubwa imedhihirisha kuwa watu bado wanapenda muziki mzuri, watu bado wanapenda muziki wa hip hop. Kwangu mimi ni kitu ambacho kimenipa faraja na nguvu ya kuendelea kufanya kazi nzuri.”

Rayvanny azindua video ya wimbo wake mpya – Mbeleko

Msanii kutoka Wasafi Records Rayvanny ameachai video yake mpya wiki kadhaa baada ya kuachia wimbo wake wa Mbeleko.

Kulingana na views ambazo amezipata kupitia YouTube kuna uhakika kuwa mashabiki wake wameupokea vizuri Kama nyimbo zake za hapo mbeleni.

Mbeleko ambayo imepata umaarufu Afrika Mashariki ni wimbo ambao wengi wameweza kuuelewa na video yake pia inavutia kwenye macho.

Video hiyo ambayo imeongozwa na Joowezy imeachiliwa wiki hii baada ya Rayvanny na Khaligraph Jones kutoka kenya kuachia wimbo wao mpya.

Itazame hapa chini;

Huyu ndiye mwanaume Huddah anayetamani kumuoa

Socialite mkubwa wa Kenya Huddah Monroe hivi karibuni amefunguka kudai kuwa hatamani kuoleka na mwanaume yoyote kutoka Nigeria.

Mrembo huyu alifunguka kupitia Instagram story yake alidai kuwa kwa sasa amewazoea tabia za wanaume hawa na kwa hivyo hawatamani.

Hata hivyo aliendelea kwa kusema kuwa ingawa kwa sasa bado hajapanga kuoleka…yeye anamtamani Wizkid ingawa pia yeye ni mwanaume kutoka Nigeria.

Aliandika kusema,

“Oh and actually forgot Wizzy was Nigerian. There’s an exception on this marriage thing. I will marry a Nigerian if it’s Wizkid. Baba Nlaaaa.”

Tunda aeleza sababu ambazo wasanii wengi hawatoi nyimbo baada ya kufunga ndoa

Tunda ambaye ni msanii mkubwa kutoka Bongo amefunguka kuelezea sababu ambazo wasanii wengi hukawia bila kuachia muziki baada ya kuoa.

Msanii huyo aliambia Bongo 5 kuwa wasanii wengi hukawia ndio warejelee na nyimbo ambazo wake zao na jamii wanaweza kusikiza. Aliendelea kwa kusema kuwa kuna wasanii Kama Mr Blue ambao wameweza kuachia nyimbo zinazofanya vizuri hata baada ya kupata bibi.

Alisema,

“Msanii akioa eti anapotea kwenye muziki hizo ni dhana potofu, kuna wasanii wengi wameoa na bado wanafanya vizuri, wapo akina Mr Blue wanafanya vizuri. Mimi najua msanii anaweza kupotea kama anatoa nyimbo za kumuimbia mke wake, mke wako unatakiwa kumuimbia ndani mwako, na jamii inataka muziki wao,”

Harmonize aonyesha Pete, saa na mikifu yake ya dhahabu yenye dhamana ya mamilioni

Wasanii wa Wasafi Records wanaonekana kuwa wanashika mkwaja wa hali ya juu. Ikiwa sio magari na nyumba ni pete na saa zenye dhamana ya juu.

Harmonize amejiunga miongoni mwa wasanii ambao wanaziweka picha kuonyesha dhahabu zao mitandaoni ya kijamii. Msanii huyo leo hii ameziachia picha na video kuwaonyesha mashabiki wake baadhi ya saa, Pete na mikufu ambazo ameza kuzinunua.

Kulingana na maoni ya mashabiki wake sio wengi walipendezwa na kitendo hiki hasa saa hii Waislamu wamefunguka. Wengi walionelea angewapa maskini pesa hizo angalau wanunue chakula au kujenga msikiti.

Tazama video na picha hapa chini;

https://instagram.com/p/BVHuVKaFRwX/

Ni kweli Hamisa Mobetto anaujauzito wa Diamond Platnumz?

Hamisa Mobetto amejipata tena akisingiziwa kuwa yeye na baba Tiffah wanatoka kimapenzi. Kuzidisha mara hii mrembo huyu anasemekana kuwa anamtarajia mtoto na mkali huyo wa Wasafi records.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Kulingana na fununu mitandaoni hii ndio shida ambayo imemfanya Diamond Platnumz na Zari Hassan kutosikilizana. Hapo awali ilisemekana kuwa wapenzi hao walikosana baada ya Diamond Platnumz kutohudhuria mazishi ya Ivan Don lakini inaonekana kuwa kuna taarifa ambazo mashabiki hawajui kwa sasa.

Hata hivyo hakuna anayejua ikiwa Hamisa Mobetto anamtarajia mtoto wake wa pili na kama ni kweli, hatujui ikiwa mtoto huyu ni wa Diamond Platnumz.

Mamake Diamond Platnumz pia anasemekana kuwa ameridhia mwanae kuwa na Hamisa Mobetto na iwapo hii ni kweli basi Nillan akokaribu kupata mdogo wake!

“Namtambua Young killer toka zamani” Lava Lava

Mkali mpya wa Wasafi Records Lava Lava amedai kuwa anamtambua Young Killer toka zamani wakati alikuwa aki hustle na THT.

Lava Lava ambaye kwa sasa amepata maarufu tangu kuachia wimbo wake mpya ‘bora Tuachane’ alifunguka kwa kusema kuwa wakati bado alikuwa anatafuta njia ya kuingia kwenye Bongo Industry aliweza kukatana na young killer ambaye kwa hivi sasa hamkumbuki kwa kuwa wakati huo hakuwa maarufu.

Akizungumza na Bongo 5, Lava Lava alisema,

“Msodoki mimi namkubali sana lakini pia ni mtu ambaye nilikuwa nakutana naye. Young Killer hanijui mimi lakini leo namwambia, kipindi nahustle THT alikuwa kwenye Super Nyota walikuwa wanakuja sana THT kuweka kambi hadi tukafanya tangazo fulani wote, lakini hakumbuki, yeye akaweka sauti yake mimi nikaweka yangu. Kwa hiyo mimi namjua kwanzia kule chini kabisa lakini yeye katika kutokumbuka kwake tukikutana tunaheshimiana.”

Mpenzi wa Vanessa Mdee amwadikia ujumbe huu kumsheherekea siku ya kuzaliwa

Msanii wa Bongo Juma Jux amewaacha wengi wakiulizana maswali baada ya kumuandikia mpenzi wake Vanessa Mdee ujumbe wa kufurahisha roho kumsheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Ujumbe huu umekuja wakati ambao mashabiki wengi walidhani kuwa wawili hao waliluwa wameachana. Kwa kufanya hivyo Juma Jux amedhibitisha kuwa mapenzi yake kwa Vanessa bado yako na kutupilia mbali fununu hizo.

Jux aliandika kusema,

Happy birthday ?#eastafricanqueen @vanessamdee more life n God bless you mama #bestfemaleartist #moneymondays,”

Harmonize adai kuwa ‘kuna mtoto na kuna mtoto wa kizungu

Harmonize kwa hivi sasa ameweka wazi anatoka na mtoto wa kizungu na kama mwanaume yeyote ambaye amelowa kwenye mapenzi, msanii huyu hajakuwa akificha furaha yake.

Msanii huyo wa Wasafi records alimzindua mrembo huyo hivi karibuni baada ya kuwachana na Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu. Hata hivyo akiongea kwenye kipindi cha 255 ya XXL ya Clouds FM Harmonize alisisitiza kuwa anatarajia mtoto wake atachukua rangi ya mamake.

Alisema,

“Ngoja nikwambie kitu kuna kuzaa mtoto na kuna kuzaa mtoto wa kizungu ni vitu viwili tofauti,” alisema Harmonize. “Naenda Marekani mara moja si unajua mke wangu anatakiwa kusarifi kaniambia kuna ishu tunaenda kufanya sasa mimba ikiwa kubwa atazuiliwa kupanda ndege,”

Aliyekuwa meneja wa Juma Nature aeleza sababu ambazo msanii huyo hafanyi vizuri kwenye muziki kama zamani

Juma Nature ni msanii ambaye amekuwa akifanya muziki kwa muda mrefu sasa. Hata hivyo muziki wake wa hivi sasa unaonekana kutofanya vizuri kama hapo mbeleni.

Meneja wake wa zamani, Mkubwa Fella hata hivyo aliweza kuweka sababu za Juma Nature kufeli hivi karibuni katika interview yake.

Kulingana na Mkubwa Fella, msanii huyu amekosa kampani mzuri ambayo itamuelekeza kufanya muziki ambao unawafurahisha mashabiki wake kama kitambo. Fella alifunguka na kusema
“Juma Nature muziki wake haujapungukiwa chochote, yule kapungukiwa kampani yangu. Kwa sababu alichokuwa anafanya ni kile kile, ila kwa sasa amekosa kampani yangu,” alisema Mkubwa Fella. “Mimi naweza kuongea na mwenye redio vizuri, mimi naweza kuongeza na Dj vizuri. Juma Nature anaimba vizuri pia ni mtunzi mzuri kwahiyo mimi nachoweza kusema kwa Nature ni hilo,”

Steve Nyerere asema asihusishwe na scandal ya audio ya Wema Sepetu

Rafiki wa karibu wa Wema Sepetu amefunguka kudai kuwa hataki watanzania wamuhusishe na audio ambayo Mrembo huyo anasikika akiongea na Mbowe.

Steve Nyerere ambaye ni mchekeshaji anayejulikana sana Afrika Mashariki alitaka Watanzania wajue kwamba hawezi kumfanyia rafiki wake wa karibu jambo kama hilo alipokuwa akizungumza na Bongo 5. Steve alisema,

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile, Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,”

Mbowe hata hivyo amekana kuwa sauti hiyo sio yake lakini kwa sasa watalaamu wanafanya uchunguzi kujua nani aliyesambaza audio hiyo.

Matonya awachia video mpya – ‘Nifungulie’

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, muimbaji wa Tanzania Matonya ameachia wimbo mpya uitwao Nifungulie.

Wimbo huu unamaudhui ya mapenzi na kwa mara ya kwanza ameambatanisha video ya kufurahisha macho. Matonya anasimulia mapenzi ambayo anaona awache baada ya kuumizwa sana na mpenzi wake.

Anaendelea kwa kumsihi mrembo wake amfungulie kwani amechoka kuumizwa na mapenzi haya yasiyo ya heri. Tazama wimbo huu hapa chini;

Jokate asimulia jambo ambalo lilimfanya kulia sana hivi karibuni

Jokate ambaye anajulikana sana Afrika Mashariki kwa filamu zake za uigizaji amefunguka kwa mara ya kwanza kueleza kitu ambacho kilimfanya kulia hivi karibuni.

Akizungumza kwenye interview Jokate alisema kuwa anavunjika roho kumuona mamake mzazi akimshughulikia baba yake ambaye kwa hivi sasa ni mgonjwa. Mrembo huyu aliendelea kwa kusema kuwa mama yake anatumia nguvu zake zote kuhakikisha kuwa baba yake amepona.

Aliendelea kwa kusema kuwa jambo hili linamuumiza sana kumuona mamake akijishughulisha sana kumsaidia baba yao ambaye a naumwa. Jokate alisema…

Kusema kweli hivi karibuni nimelia sana, baba yangu anaumwa sasa mama yangu anatumia nguvu kubwa kumuudumia kwa sababu baba anahitaji uangalizi wa karibu sana,”

Hata hivyo aliongeza kusema kuwa anatamami kuwa na familia yake lakini kwa hivi sasa bado hajampata.

Miss Tanzania Diana Edwards adai kujiunga na filamu za Bongo

Diana Edward ambaye ni Miss Tanzania 2016/7 ameonyesha uwezo wa kujiunga na filamu za Bongo kama Wema Sepetu. Mrembo huyu ambaye amepata sifa nyingi baada ya kuibuka mashindi wa Miss Tanzania kwa sasa anaolea kufanya mambo na filamu.

Mrembo huyu alifunguka kwenye kipindi cha Twenzentu cha Times FM na kusema kuwa kila kitu kimepangwa na kile anachongoja ni kuanza kuigiza.

Aliendelea kwa kusema kuwa yeye amekuwa akiigiza kwa muda mrefu kwa hivyo haitakuwa ngumu kufanya filamu yoyote. Alisema,

“Kila kitu kipo tayari, nimeshafanya mazoezi sasa hivi nasubiria mambo yangu yakikaa sawa nianze kutengeneza. Napenda action movie kwa sababu am so addicted in action movie, staki kusema mengi sana kwa sababu nasubiria maamuzi kutoka kwa meneja wangu itakuwaje, kwa hiyo msubiri. Mimi nilikuwa naigiza kuanzia muda mrefu ingawa sikutoa movie yoyote.”