Mkali wa Wasafi records aachia video mpya ‘Dede’ inayowapa wasanii wenzake wasiwasi kutokana na ubunifu wake

Lava Lava kutoka label ya WCB hatimaye ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Dede’ miezi kadhaa baada ya kuachia video yake ya kwanza katika uongozi wa rekodi ya Wasafi, ‘Tuachane’.

Ingawa video yake haina tofauti mingi na Tuachane, nyimbo hii yake imewavutia wengi ambao wanafurahishwa na maudhui aliyotumia kwa lyrics ya Dede.

Video hiyo pia imepata maoni tofauti kutoka kwa mashabiki wake. Hata hivyo itazame hapa na utoe maoni yako.

Chidi Benz akamatwa baada ya kunaswa na Heroine

Chidi Benz ambaye alikuwa ameachia wimbo mpya unaofahamika Kama ‘Muda’ aliyomshirikisha Q Chillah amjipata mashakani baada ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya heroine.

Kulingana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alifunguka kusema kuwa Chid Benz alipatikana baada ya msako na mkali uliofanyika August 12 jioni.

“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”

Chid Benz ambaye ambaye alikuwa anaonekana kubadilika amewashtua wengi kwani hii sio mara yake ya kwanza kupatikana na Sawa za kulevya.

Shilole apata majibu kutoka kwa Dayna

Hapo awali kabla ya kuachia wimbo wake mpya Kigori alifunguka kudai kuwa sababu yake ya kukawia kabla kuachia wimbo mpya ni kwa sababu alikuwa amewapa wasanii wa kike muda kufanyap projects ambazo ni kali kushinda zake lakini, hakuna aliyeweza kumfikia.

Hata hivyo msanii Dayna Nyange amezungumza na E-Newz ya EATV ambapo alijibu ripoti ya Shilole kwa kusema;

“Mimi nafikiri yeye ndio anaweza kuwa majibu yote kwamba kwa nini amekuja kuchukua game yake, labda alikuwa kimya kwa muda mrefu akawa anaona bado nafasi yake ipo. Unajua kila mmoja ana riziki yake kwenye hizi kazi usitengemee kwamba Dayna atakuja kufanya kitu fulani nimpoteze mtu fulani, hapana kila mta na riziki yake na kila mja na wakati wake,”

Akaongeza kwa kusema;

“I think ni wakati wake kama alifanya kitu fulani akaona mafanikio yake lakini akaona huku bado kulikuwa na mafanikio yake au anahitaji zaidi, so ana haki ya kufanya, kusema anachuku game ni misamiti tu ya lugha zetu za kisanii,”

Picha mpya za Vee Money za wazingua mashabiki, Ni kweli kuwa amenenepa? (Picha)

Msanii na mrembo wa bongo Vanesaa Mdee ameachia picha mpya usiku wa kuamkia leo huku akionekana kuwa ameongeza weight katika sehemu ambazo mtu hawawezi kosa kujua.

Vanessa aliwachia picha hizi kupitia mtandaow ake wa Instagram huku akizingua akina idris Sultan na mashabiki wake ambao huwa mkondo wa kwanza kujua anachofanya mkali huyu.

Picha hizi hata hivyo sio siri kuwa ni za kuvutia na nguo yake ya manjano na viatu vyake vya chini.

Rayvanny awachia picha mpya akiwa na mwanae

Msanii wa Wasafi records Rayvanny amewafurahisha wengi baada ya kuachia picha mpya akiwa na mwanae, Jaydanvanny katika mtandao wake wa Instagram.

Picha hii ameiwachia wiki kadhaa baada ya msanii huyu kumueka mtoto wake mitandaoni yake ya kijamii. Hata hivyo iliwavutia wengi hata Diamond Platnumz ambaye alimsifia kwa kuwa yeye ni baba kwa Sasa.

Rayvanny na mpenzi wake Fahyma walibarikiwa na mtoto huyu miezi kadhaai iliyopita na ukilinganisha picha hii na zile za awali;

Zari awapa maneno wanaodai kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond Platnumz (Picha)

Zari Hassan ameonekana kukasirishwa na watu wanaodai kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond kwa kuweka picha huku wakimfananisha na marehemu Ivan Ssemwanga ambaye alikuwa bwana yake kabla kutemana.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Zari aliwapasha watu hawa kwa maneno makali huku akisema kuwa Nillan ni 5star. Aliendelea kwa kuwakomesha kutoa jina la mtoto wake kwenye vinywa vyao.

Mrembo huyu pia aliongeza kwa kusema kuwa yuko busy na iwapo wataendelea atawapa vouchers za bure za vodacom ili waendelee kuongea.

Tazama picha hizi hapa;

Barnaba amjibu aliyekuwa mke wake kupitia ujumbe huu wa Instagram?

Barnaba na aliyekuwa mke wake wameonekana kupashana kupitia mitndao yao ya Instagram. Hii ni baada ya mrembo huyo aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mzazi mwenziye, kuposti picha akiwa na mpenzi wake wa sasa mitandaoni huku akiandika ujumbe unaoelezea sababu za ndoa yao kuvunjika.

Hata hivyo Barnaba naye aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akiwasifia wanawake – lakini mashabiki wake wanaonelea kuwa alikuwa anamjibu mke wake.

Alindika kusema;

“Mama aliniambia ukimtukana mwanamke basi umenitukana na mimi, siku zote nawaona kama mama zangu, hongera wanawake wote duniani, salamu zangu juu yenu Jumapili ya leo nawapenda sana, na wale mliopoteza mama zenu fanyeni ibada juu yao waweze punguziwa adhabu ya kifo au kufutiwa kabisa, Bwana Yesu asifiwe sana Jumapili ya Mungu tumpe Mungu Wakristo wenzangu”

Hii ndio sababu Faiza Alley anasema kuwa wasanii wa Tanzania hawana ubunifu

Faiza Ally ambaye ni mama ya watoto wawili hivi karibuni aliwachana wasanii wa Tanzaniak kwa kudai kuwa hawana ubunifu wowote wa kutafuta Kiki.

Mrembo huyu aliandika haya kupitia Instagram account alisema;

Faiza Alley

“Nilichogundua sasa hivi kutokana na kipindi ninachosikilizaga redioni ni kwamba wasanii Watanzania hawana akili za ubunifu katika kutafuta kiki, zaidi ya wanaume kutoka na wanawake maarufu na wanawake maarufu zaidi ya kutoka na wanaume maarufu.”

Akamalizia kwa kusema;

“Unapokuwa msanii kiki ni moja ya kazi lakini jaribu kuwa mbunifu kidogo zaidi ya uroda! Sema naomba mnisamehe ni ile uhuru wa kuongea tu sijamlenga mtu lakini najua kuna mstari wa kujifunza”

“Labda nina mimba ya Wizkid” Gigy Money asema

Msanii na mrembo wa video Gigy Money amekuwa akisingiziwa kuwa anamimba kitu ambacho aliweza kufunguka kuhusu hivi karibuni.

Akizungumza na FNL ya EATV Gigy Money aligusia kuhusu wimbo wake mpya ‘Papa’, alafu baadae akaongeza kwa kana taarifa zinazodai kuwa anamimba huku akisema kuwa ameiambia FNL ya EATV kuwa anatamani sana kutoka kimapenzi na msanii Wizkid ambaye anaweza kumzalia.

“Kipindi cha sasa hivi na Papa ndio nimetoa?, hapana, ujue mpaka yananishtua maneno haya, you know sina mimba lakini labda nina mimba ya Wizkid unajua mimi natamani ikaenda ikashuka tu.”

Akamalizia kwa kusema;

“Yeah namkubali, unajua dream sio wote wanatimiza ndoto zao, mimi nimetimiza ndoto yangu, nilisema Tekno moyoni siumeona huyu hapa akajaa,”

Dogo Janja afunguka kuhusu mavazi yake

Rapper wa bongo Dogo Janja ni mmoja wa wasanii ambao wanatambulika kuvaa kama mastaa wa uingereza. Yeye mwenyewe huwa na style yake mwenyewe na hapo awali aliwahi kudai kuwa hakuwa msanii ambaye anaweza kufikia kiwango cha kuvalia.

Hivi karibuni alifunguka kuongea kuhusu mavazi yake katika mahojiano na Dj Show ya Radio One. Kulingana na Dogo Janja watu wengi wamekuwa wakidhani mtu anapaswa kuwa na hela mingi ili apendeze kitu ambacho si cha ukweli… Dogo alisema;

“Watu wamekuwa wakilinganisha muonekano wangu na fedha, ninachoamini kuvaa sio fedha nyingi sana ila kuvaa ni passion ya mtu, so kila mtu anavaa ndio maana nikasema ukivaje unapendeza kitu ambacho kipo watu wanavaa huwezi kutembea utupu hata siku moja,”

Nuh ataja sababu itakoyomfanya amchukue mtoto wake baada ya kuwachana na mke wake

Nuh ameweka wazi kuwa ameachana na mke wake lakini msanii huyu hakutaja sababu za kuachana.

Hata hivyo amemruhusua alikuwa mke wake kumlea mtoto wao wa kike aitwaye, Anyaghile. Lakini akizungumza na 5Selekt ya EATV hivi karibuni Nuh alisema kuwa aliyekuwa mke wake ashaolewa tena lakini ameapa kuwa hakuna kitakacho mfunga yeye kumchukua mwanawei wapo atafanyiwa vitu ambavyo si sawa.

“Mtoto still yupo na ningetamani sana kukaa naye tangu akiwa mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umri lakini nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo si sawa nitaenda kumchukua na kukaa naye mimi mwenyewe,”

Aliongeza;

“Kwa hiyo nampa muda nione, nikienda nikakuta mwanangu amenenepa, ana furaha, yupo poa ataishi naye mpaka umri utakapofika lakini nikienda nikakuta mwanangu amepungua nambeba na kuondoka naye.”

Lucy Komba awapasha mashabiki wa Zari wanaomtusi Hamisa Mobetto

Muigizaji wa bongo Lucy Komba amefunguka kwa mara ya kwanza kuwakomesha watanzania ambao wanamtukana Hamisa Mobetto kisa kuwa mtoto aliyezaa ni Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya wengi kudai kuwa kunauwezekano wa mtoto huyu wa pili wa Mobetto kuwa wa Diamond Platnumz ambaye anasemekana aliwahi kutoka kimapenzi na Hamisa Mobetto.

Lucy Komba

Hata hivyo Lucy Komba aliwatoa wengi povu kwa kuandika;

“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,”

Aliongeza,

“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo. GOODMORNING.,”

Esha Buheti alifungua mtoto wa kike

Esha Buheti ndio mama mpya bongo baada ya kujifungua mtoto wa kike leo. Muigizaji huyo wa filamu za bongo amebarikiwa na mtoto siku kadhaa baada ya Linah, Faiza Ally na Hamisa Mobetto kujifungua salama.

Kulingana na habari zinazoenea, Esha alijifungua Latina hospitali ya Sali International iliyopo ushuani Masaki.

Kama wenzake Esha alithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kupost picha ya mtoto wake chake na kuandika;

“Alhamdullilah ni mtoto wa kike, asante Mungu kwa zawadi hii, asanteni wote kwa dua zenu mimi na mtoto tupo salama.”

“Natamani Kuzaa” Elizabeth Michael ‘Lulu’ afunguka kuhusu kuwa mama

Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni mmoja wa wanawake maarufu Tanzania kwa sababu ya sinema za Kibongo. Hata hivyo wenzake wamekuwa wakizaa na kulingana na mahojiano yake na 4-Tamu pia yeye anatamani mtoto.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lulu kusema haya. Katika mahojiano yake Lulu alisema kuwa imefika wakati na yeye anatamani sasa kuzaa.

Aliendelea kusema kuwa umri wake unamruhusu na akipata mwanaume wa kumzalia basi atajaribu kupata mtoto. Akizungumza na 4-Tamu alisema;

Lulu Micheal

“Natamani tu na mimi nipate mtoto sema ndiyo hivyo bado natengeneza mipango ya mimi kuwa mama tena mama bora,”

‘Baba’ ya mtoto wa Hamisa Mobetto ajitokeza

Dennis Louis ambaye ni mshindi wa milioni 50 za Tanzania Movie Talent amejitokeza kudai kuwa mtoto wa Hamisa Mobetto ni wake kupitia mtandao wake wa Instagram.

Muigizaji huyo alianzak kwa kusema kuwa Diamond Platnumz sio baba ya mtoto yule bali yeye ndio baba wa halali. Dennis Louis aliweka post hiyo huku akiwaacha wengi kama wameshangaa. Aliandika;

“Mengi yamesemwa nimevumilia vya kutosha mwenye mzigo nadhani mshanijua!! Kabla hamjaandika mambo zenu muwe na evidence za kutosha!!. Basi wenye wivu watasema Photoshop shubaaamit!!! #babajunior #comingsoon”

Hata hivyo hakuwachia hapo kwani aliweka post nyingine yenye picha yake na Hamisa Mobetto ameandika,

“son you have a bright future behind you…#eyoo! It’s a boy”

Mashabiki nao ambao wamekuwa wakifuatilia akaunti za Hamisa na Tanzanian baby walimshambulia huku wakisema kuwa wanajua kuwa msanii huyo anatafuta Kiki.

Kufikia Sasa Hamisa bado hajaweka wazi mtoto wake huyo wala baba ya mtoto wake.

 

Harmonize azungumzia kuhusu mjengo wake

Muimbaji kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mjengo wake ambao ni wa ghorofa akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni.

Kulingana na Harmonize mjengo wake unawezekano wa kukamilika mwishoni wa mwaka huu. Hata hivyo, Harmonize alikataa kufunguka kuhusu gharama aliyotumia kutengeneza ghorofa hiyo.

Harmonize alisema;

“Kwa hiyo flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi”

Harmonize aliendelea kwa kudai….

“Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,”