Wema Sepetu afunguka kueleza kinachomkera kuhusu Tanzania ya sasa

Mrembo wa filamu Wema Sepetu ameonekana kukasirishwa na alichofanyiwa mtu mmoja aliyekutana na yeye mahakamani hivi karibuni.

Wema Sepetu aliweka tweet kadhaa kupitia mtandao wa Twitter huku akionekana kama amekasirika kwa kilichomtokea mtu huyo wakati wa kusikiliza wa kesi ya Mh.Tundu Lissu.

Aliandika tweet hizo akisema;

 

Huu ndio ujumbe ambao Shamsa Ford aliwapa wanaume hawapendi kufanya kazi!

Staa wa muvi za Bongo Shamsa Ford hivi karibuni alichukua muda wake kuwa shauri wanaume amabao hawapendi kujitegemea – haswaa wale ambao huchagua kazi za kufanya.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Shamsa alionekana kukerwa na wanaume ambao wanategemea kufugwa na wanawake wazee kuwashinda.

Shamsa Ford

Katika ujumbe wake msanii huyu alitaja kuwan I vizuri wanaume kujituma na kufanya kazi kwa mikono yao badala ya kutamani maisha ya haraka yasiyo na utamu wowote. Aliandika kusema;

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,”

Akaongeza;

“Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

Ruby amuonyesha mpenzi wake ambaye ni baba ya mtoto anayemtarajia (Picha)

Mrembo na Msanii wa nyimbo za bongo Ruby anamtarajia mtoto wake wa kwanza kulingana na picha ambazo zinaenea mitandaoni.

Ruby aonyesha ujauzito wake

Ruby anaonekana kuwa yuko mjamzito na baada ya kuachia nyimbo kadhaa, mrembo huyu ameamua kuanza familia yake na mpenzi wake aliyemuonyesha kupitia mtandao wake Wa Instagram.

Staa huyo aliamuanika kwa kuiweka picha yake huku akimwandikia ujumbe uliodhibitisha kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wao atakaye zaliwa hivi karibuni. Ruby aliandika kusema;

“My prince charm, my smile maker, Baba princess Ruby”

Tazama picha hapa chini;

Mpenzi wa Ruby

“Akifuatilia ataumia kichwa” Gigy Money amjibu Mzee Majuto!

Gigy Money anaonekana mwanamke ambaye hamuogopi mtu yoyote. Mrembo huyu ambaye ni video vixen wa nyimbo za bongo hivi karibuni aliamua kumjibu Mzee Majuto ambaye alisema kuwa hapendezwi na picha zake za uchi mitandaoni.

Mzee Majuto

Kulingana na ripoti zinazoenea mitandaoni, Mzee Majuto anasemekana kuwa alidai kuwa picha za uchi hazipendezi kwa mwanamke na ndio maana hazipendi picha za Gigy.

Gigy Money
Gigy Money

Hata hivyo Gigy Money hivi karibuni aliamua kumjibu mkali huyu wa movie za bongo. Alisema;

“Kama hapendi swaga zangu ya nini asumbuke kutazama picha zan­gu. Hayo ndiyo maisha n­gu niliyo­chagua, akiyafua­tilia, ataumia kichwa bure, sioni cha ajabu kwangu kwa sababu kuna wasanii wengi tu wanakaa utupu,”

 

Chege Chigunda aeleza kwa nini hana ‘hit song’

Chege Chigunda anaeendelea kufanya kufanya vizuri na muziki wake hivi karibuni alifunguka kueleza kwa nini bado hajatoa hit song kutoka kwa nyimbo zake za hivi karibuni.

Akizungumza na Times Fm katika kipindi cha Twenzetu, Chege alifunguka kutaja sababu kadhaa anazoamini kuwa ni chanzo cha yeye kutokuwa na ‘hit song’ tangu mwaka jana. Chege alisema;

“Unajua kuna mabadiliko ya muziki, ukiangali Marekani nako ni hivyo hivyo, ukiangalia Nigeria ni hivyo hivyo… zamani ulikuwa akisikia ngoma imetoka Fall in love inakuwa Fall in love dunia nzima umeona ukisikia Do Me, basi dunia nzima lakini sasa kilichotokea Nigeria ndicho kinatokea sasa sio kwamba watu hawapigi mziki mkali, kuna vita ya muziki inafanyika,”

Aliendelea kuongeza kuwa

” Zamani ilikuwa unaona singo moja inatoka kwa mwezi ya msanii mmoja au unakuta singo mbili zinatoka, lakini sasa kwa siku zinatoka karibu singo saba hiyo ndio sababu.”

Picha hii ya Diamond Platnumz akiwa mtoto ni dhibitisho tosha kuwa alitambua fashion kitambo

Diamond Platnumz na meneja wake Sallam_SK wanapenda sana kutaniana kupitia mitandao yao ya Instagram. Hivi karibuni msanii huyo mkubwa wa bongo aliweka picha ya yake huku akimtania meneja kuwa yeye alianza kupenda kuvaa jerseys tangu awe mtoto mdogo.

Platnumz aliweka picha hii kwenye mtandao wake wa Instagram huku akimchana Sallam kwa kuwa yeye hajaanza kuvaa shati za strips juzi kama who. Alindika kusema;

Don’t get twister @Sallam_sk I started this strip outfits and chains shit since…..!?
(Mi nawaona tu na nguo zenu za mistari pembeni, na macheni kuyamwaga kwa Shinzo…ila michezo tumeanza kitambo sana?)

Katika picha hiyo, Diamond Platnumz anaonekana akiwa kijana mdogo lakini kulingana na alivyokuwa amevalia, ni kweli kuwa alianza mambo ya fashion kitambo. Tazama picha hii hapa chini.

Chibu Dangote

Baada ya kumchokora kwa muda Shilole hatimaye amjibu Gigy Money

Hapo awali Gigy Money alisema kuwa yeye sio shabiki wa Shilole wala nyimbo sake. Kulingana na mrembo huyu wa video za nyimbo za Bongo, shilole hajui kuzungumza kingereza vizuri na hii pia ndio maana hatamani kuwa shabiki wake!

Gigy Money

Hata hivyo, Shilole ameamua kumjibu mrembo huyu kupitia 5 Selekt ya EATV alipokuwa akifanyiwa mahojiano. Shilole alionekana kuto jali alichosema Gigy money na kwa sababu huyu ni Mudigi wake….hakuona haja ya kujibazana naye. Shilole alisema;

“Ni mdogo wangu kwa hiyo lazima apite kwa dada yake, kwa hiyo watu kama hao wadogo zangu ninawachukulia poa tu, hamna tatizo,”

Shilole aliendelea kwa kukiri kuwa ni kweli hajui kingereza lakini hilo sio jambo la kumsumbua akili;

“Kingereza is not my language, kwa hiyo nikisema bado hainilazimishi kukijua sana lakini najifunza kuongea, na pale panapobidi nitaongea. Hiyo ni kweli hamna shida kama sijaenda (shule) ni sawa, kwani watu wangapi hawajaenda shule, ukiwa umeenda shule na hela uwenayo.”

Shilole atangaza kuwachia wimbo mpya utakao kuwa funzo kwa wengi

Zuena Mohammed anayejulikana kwa umaarufu kama shilole amefunguka kusema kuwa anajipanga kuachia wimbo mpya mwishoni mwa mwezi huu ambao utakuwa tofauti na nyimbo zake zingine kwa sababu una ma­hadhi ya Afropop.

Akizungumza kwenye interview, Shilole alisema kuwa wimbo huu ni wa kipekee kwani maudhui yake ni ya kuwaelimisha wengi. Aliendeleak kusema kuwa ujumbe wake ni mzuri kwa jamii na mashabiki wake watafurahia.

Shilole
Shilole

Mrembo huyu alisema;

“Natarajia kutoa wimbo mpya mwishoni mwa mwe­zi huu, nimeimba mahadhi ya Afropop naamini uki­toka tu na watu wakiusikia utakuwa funzo kwa jamii kutokana na ujumbe uli­omo humo.”

Tazama picha mpya za Elizabeth Micheal ‘Lulu’ zinazo wazingua mashabiki

Muigizaji wa filamu Elizabeth Micheal ni mmoja wa mastaa wa kike kutoka bongo wanaowazingua mashabiki kutoka Afrika Mashabiki.

Hivi karibuni Lulu aliachia picha mpya akionekana amependeza na nguo ndefu kama ya mama yake aliyepigwa picha na true na mdogo wake wa kiume.

Sio siri kuwa Lulu ni mwanamke anayejitambua na mwenye ameumbika kama malaika. Ni wengi ambao wanazinguliwa na uzuri wake na pia roho yake safi.

Tazama picha hizi alizoziachia hivi karibuni huku akionekana na familia yake.

Linah ajifungua mtoto wa kike (Picha)

Mwanamziki Wa bongo Linah anasemekana kuwa amejifungua mtoto wake Wa kwanza. Habari hizi ambazo zinasambaa mitandaoni na pia marafiki wake wa karibu pia wameona kumpa pongezi.

Hata hivyo Linah hajadhibitisha ikiwa taarifa hizi ni za ukweli lakini mpenzi wa Rayvanny pia alimwandikia ujimbe huku akimshukuru kwa kumshukuru kwa kumletea mkwe wake. Fahyma aliandika kusema;

Nashukuru kwa kuniletea mkwe wangu @Officiallinah

Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa msanii huyu hata hivyo Linah bado hajamuonyesha baba wa mtoto wake lakini mashabiki wanatarajia atafanya hivi karibuni.

Tazama picha ya mtoto anayesemekana ni wa Linah.

Diamond Platnumz asema haya kuhusu muziki wa Bongo

Ikiwa umekuwa ukijiuliza kuhusu muziki Wa bongo unaendelea wapi, basi Diamond Platnumz amejibu swali lako. Msanii huyu wa nyimbo za Bongo Fleva, amefunguka kusema kuwa nyimbo za kibongo zimekua na hii ni kutokana na bidii za wasanii kutoka bongo.

Diamond Platnumz alisema kuwa muziki Wa bongo Fleva wetu umeweza kufika sehemu mingi huku akiongeza kuwa tu si muziki bali pia mbuvi. Akizungumza na Bongo 5, Diamond Platnumz alisema,

“Muziki wetu unazidi kukua kwa kwa sababu mpaka Watu wa nje wanakuja kufanya kitu nyumbani lazima tasnia yetu iwe imekua, kwa hiyo tasnia yetu imekua sio tu kwa Wasanii hata Industry nzima Vyombo vya Habari, Wadau kila mtu anayehusika na burudani, tumepiga hatua“

Tazama mahojiano yake na Bongo 5.

Kajala atokwa na machozi baada ya haya kumtokea jijini Mwanza

Muigizaji wa filamu Kajala aliachwa na maumivu mkononi baada ya kunyofolewa kucha na mashabiki waliokuwa wakimvuta akiwa jijini la Mwanza.

Kajala Masanja

Akiongea na Risasi Jumamosi, Kajala alisema kuwa haya yalitokea akiwa kwa harakati za kufanya kazi anayoifanya na kampuni ya mchezo wa kubahatisha.

Kajala alisimulia kusema kuwa kucha yake ilitolewa akigawa tisheti kwa mashabiki ambao walianza mvutano na kwa bahati mbaya, kumvuta mkono mpaka kumbandua kucha aliyokuwa amebandika.

Jeraha hili lilimuacha huku akivuja damu mkononi na kuhisi uchungu ambao ulimfanya kulia. Kajala alisema,

“Yaani mimi nilikuwa sina ili wala lile nagawa matisheti mara wakaanza kunivuta kwa nguvu mpaka wakaitoa kucha yangu, hali hiyo ilinitesa asikwambie mtu jeraha la kucha linauma sana. Maumivu niliyopata yalikuwa ni makali mno kiasi ambacho nilishindwa kufanya kazi yangu, nilipata matibabu ambapo kwa sasa naendelea vizuri,”

Mzee Majuto bado yuko hai!

Mkali wa filamu za kuchekesha za bongo Mzee Majuto bado yuko hai na fununu zinazosambaa mitandaoni kuwa amefariki ni za uwongo!

Hii imedhibitishwa na rafiki wake wa karibu Mboto anayejulikana kama Haji Salum kupitia mtandao wake wa Instagram. Mboto alikanusha taarifa hizi kwa kuweka picha yake na King Majuto huku akiandika kusema,

“Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga,”

Hii ni baada ya wengi kusambaza uvumi kuwa msanii huyu alikuwa amefariki. Hata hivyo, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti kuwa muigizaji huyu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini bado yuko hai.

Harmorapa afunguka kuhusu uhusiano wake na Amber Lulu

Rappa kutoka Tanzania Hamorapa hivi karibuni kudai kuwa yeye na Amber Lulu wanatoka kimapenzi. Msanii huyu alikiri haya baada ya wengi kudhania kuwa uhusiano wao ni wa kiki.

Hii inakuja baada ya Lulu Diva kukana kuwa anauhusiano na Harmorapa. Hata hivyo rappa huyu ameiambia Boys Boys ya TV1 kuwa yeye kama mwanaume lazime awekatika mahusiano. Harmorapa alisema;

“Unajua siku zote kama ni mwanaume, halafu mwanaume rijali ni lazima uwe kwenye mahusiano ya kimapenzi, kwa hiyo mimi nina mpenzi, kuoa bado hata mtoto sina. Kwa sasa ni mtu famous, nilishamtaja ili kuna wengine hawamfahamu ni Amber Lulu,”

Hata hivyo hatujui ikiwa ni kweli hawa wawili ni wapenzi.

Baby Madaha aeleza sababu yake ya kurudi nyumbani kuwaona wazee wake kila mwaka

Muigizaji wa muvi za Bongo, baby Madaha Joseph hivi karibuni alikiri kuwa kila mwaka yeye hurudi nyumbani kwao kila mwaka kuwaona wazazi na wazee wake wanaoishi mashinani.

Baby Madaha

Mrembo huyu alifunguka kudai kuwa true hufanya jambo hili ilimambo yake yaendelee kwanda vizuri. Kutembea kwa wazazi ‘kutambika’ ni jambo muhimu kulingana na Baby Madaha ndio apate baraka.

Aliambia kipindi cha Motomoto new kuwa hivi sasa yuko nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukaa sana mjini bila kuwaona.

“Bila wazee mambo hayaendi kabisa, niko kwetu Mwanza kwa ajili ya kufanya mambo ya kimila ili walau mambo yaende vizuri mjini maana hali imekuwa mbaya sana, nimekuwa nikifanya hivyo kila mwaka na nimeona huwa inasaidia sana,”

Lulu Amber na Jaguar kutoka Kenya kuachia wimbo pamoja?

Lulu Amber ambaye ni msanii mkubwa sasa kutoka Tanzania hivi karibuni alisema kuwa anamkataba na msanii kutoka nchini Kenya,Jaguar.

Amber Lulu

Muimbaji huyu alifunguka kudai kuwa Jaguar atakuwa anasimamia kazi zake wakati wowote anataka kuingia kwenye soko la Kenya.

Akizungumza na Showbiz xtra, ,Lulu alisema hili jambo la kujivunia kupata msanii kama jaguar kumpa shavu. Lulu aliendelea kusema kuwa hakuwa anatarajia jambo kama hilo kufanyika lakini anashukuru. Lulu alisema,

“Namshukuru Mungu kwa hili, nimepata mkataba mnono kwa Jaguar, makazi yangu yataendelea kuwa Bongo, lakini inapotokea nikahitajika Kenya nitakuwa nafika kwa wakati, niwaombe mashabiki wangu waendelee kunisapoti, naamini nitafika mbali zaidi na kuiwakilisha vyema nchi yangu,”

Hata hivyo bado anaendelea kufanya kazi zake za bongo.