“Pamoja na Migogoro Yetu Bado Nataka Kumuoa Gigy”- Mo J

Mtangazaji wa Choice Fm ambaye amezaa na msanii wa Bongo fleva Gigy Money, Mo J amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba yeye na Gigy wana matatizo mengi Lakini Ndiye mwanamke anayetaka kumuoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Mo J alisema kuwa mpango wa kumuoa Gigy Money alikuwa nao kwa muda mrefu kwa sababu kwanza ni mwanamke aliyethubutu kubeba mimba yake kwa kipindi chote cha miezi tisa hivyo kumpa heshima ya kuitwa baba.

Gigy ndiyo sababu ya mimi leo kuitwa baba, nampenda sana hayo mambo mengine ya migogoro huwa yanatokea tu kwa bahati mbaya, namshukuru Mungu Gigy ni muelewa hivyo huwa tunaongea na kumaliza tofauti zetu wenyewe, kwa hiyo Mungu akipenda kabla huu mwaka haujaisha nitafu nga naye ndoa”.

Pamoja na Mo j kusema hayo Lakini Gigy ameonekana akiwa na mwanaume mwingine na ameweka wazi kuwa amemuacha Mo J na hawezi kurudiana naye.

Gigy Money na Mo J Mapenzi Moto Moto Tena

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameonekana tena na baba wa Mtoto Wake Mtangazaji wa Choice Fm  Mo J siku chache Baada ya kuachana.

Wiki iliyopita habari iliyotrend kwenye Mitandao ya kijamii ni kitendo cha Mo J ambaye alikuwa kwenye mahusiano Gigy Money kudaiwa kumtongoza mke mtarajiwa wa Mc Pilipili na kumwagwa chini.

 

Kupitia katika kipindi cha Shilawadu Gigy Money alionekana akitoleana Povu zito na Mo J na hata kumtukana kupindukia na kutangaza kuwa amemuacha na yuko single.

Lakini inaonekana wawili hao hawajaachana kwa muda mrefu kwani siku ya Leo kuna video clip inawaonyesha wawili hao wakiwa wamerudiana na wanaonekana wakiwa pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram  Gigy Money anekiri kurudiana  na baba Watoto Wake na kudai kuwa anahisi kuwa amelogwa na Mpenzi Wake huyo.

Yaani mimi najua huyu kaka kaniloga tu jamani na sitaki kuelewa”.

 

Mc Pilipili Alia na Wanaume Wanaomnyemela Mchumba ‘Ake

Mchekeshaji na Mshehereshaji maarufu Bongo Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ amekiri kuwa Penzi lake na mchumba ake Philomena Thadey ‘Cute Mena, linapumulia mashine kutokana wanaume kumtolea macho.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, MC Pilipili alisema kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimsumbua kila kukicha, hali inayomsababishia kukata tamaa.

Hawa wanaume walianza kumfuatilia mchumba wangu muda mrefu kabla hata sijaanza kumtangaza kwenye vyombo vya habari, lakini sasa wamezidi baada ya kumvisha pete ya uchumba.

Pia nimesikia kuna kijana eti yupo kwenye kituo kimoja cha redio (jina kapuni) naye anamfuatilia, nimebaki ninamuangalia tu kwa sababu wanaomfuatilia wapo wengi.

Kuna mwingine yupo Mwanza, mwingine yupo Mwenge, Ubungo, Mlimani City, Sinza, mwingine anatokea kampuni moja hivi ipo Posta, mwingine yupo Usalama wa Taifa na mwingine ni bodaboda sehemu f’lani hivi. Kwa hiyo mwisho wa siku inategemea na yeye mwenyewe kama wakimuingia, akawaelewa, basi nitamuacha aende, ikiwezekana labda hata uchumba pia naweza nikauvunja”.

Siku chache zilizopita Mtangazaji wa Choice Fm Mo J alikumbwa na kashfa ya aina yake Baada ya kusikika kwa taarifa kuwa alikuwa anamtongoza Mpenzi huyo wa Mc Pilipili ilhali yuko katika mahusiano na Gigy Money.

Penzi la Gigy Money na Mo J Lafika Mwisho Kisa Michepuko

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ na Baba Watoto Wake Mo J wameachana tena Baada ya Gigy kumtuhumu Mpenzi Wake kwa michepuko.

Hivi karibuni Mo J alikumbwa na skendo ya aina yake Baada taarifa kusambaa kuwa amekuwa akimfuata mchumba wa Mc Pilipili anayeitwa Philomena na kumtongoza.

Mo J kushoto na Mpenzi wa Mc Pilipili, Philomena Kulia

Inadaiwa kuwa Msichana huyo Ali screenshoot maongezi yao na kusambaza kwenye Mitandao ya kijamii yaliyomuonyesha Mo J akimtongoza mrembo huyo.

Basda ya kupata taarifa hizo Shilawadu walimfikishia Gigy Money ambaye alizua bonge la varangati na kusababisha yeye na Mo J kurushiana matusi ya nguoni na kuachana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy Money ameweka wazi kuwa Penzi lake na Mo J limefika ukingoni kwa ajili ya michepuko:

https://www.instagram.com/p/Bst0Db4nKJ-/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=3mtt5s5dn184

Gigy Money Amesema Hata Mo J Akiamua Kuoa Poa Tu

Video vixen a na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kuweka wazi kuwa hata leo ikitokea mzazi mwenzake anataka Kuoa kwake hana kipingamizi.

Hivi karibuni kupitia  ukurasa wake wa Instagram Mo J  aliposti picha akiwa na mwanamke mwingine huku akiwa amesindikiza maneno yaliyoashiria kuwepo kwa ndoa yao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa, Gigy alisema kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na mzazi mwenzie huyo, hata akiamua kuoa leo yeye hatojali chochote kwa sababu penzi lao liliisha muda mrefu hivyo wamebaki kama wazazi tu.

Hivi unajua mimi na Moj tulishaachana muda mrefu na kama mnavyoona ana mwanamke mwingine na mimi nina mwanaume wangu, kwa hiyo hata akiamua kuoa leo hii sitakuwa na pingamizi lolote ili mradi tu awe anatoa matunzo mazuri kwa mtoto wake”.

Gigy na Mo k walikuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu lakini Penzi Lao Lilivunjika Baada ya kukosekana uamifu Baina yao lakini walifanikiwa kuzaa Mtoto mmoja anayeitwa Mayra ambaye hivi sasa ana miezi sita.

Gigy Money na Mo J Wazidi Kurushana Roho na Wapenzi Wapya

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money na Baba Watoto Wake Mtangazaji wa Choice Fm Mo J wameendelea kurushana roho huku kila mmoja akimuanika Mpenzi Wake.

Gigy Money na Ex Wake Mo J wamelala Mtoto mmoj mwenye umri wa miezi Sita sasa lakini wamekuwa na tabia ya kuachana na kirudiana tangu Mtoto wao alivyozaliwa lakini hivi karibuni Gigy aliweka wazi kuwa wawili ho hawako pamoja tena.

Baada ya kuachana Gigy Money alimuanika wazi Mpenzi Wake ambaye yuko naye kwa sasa na kumtaja Kama Montana ambaye ni Mmarekani ambaye anaishi nchini Kenya.

Baada ya Gigy Money kuonekana akiwa anajiachia na jamaa huyo ingawa mara kwa Mara amekuwa akimsaliti na kurudi tena kwa Mo J hatimaye Mo J naye amechoka na kumuweka wazi Mpenzi Wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo J aemuanika mrembo huyo na kuambatanisha na kiemoji cha pete “? Soon Inshallah ??❤️” kumaanisha ameshibana na mrembo huyo na ndoa inaweza kutokea siku yoyote.

Gigy Money Awekewa Masharti Makali Kwenye Nyumba Ya Kupanga

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Kiki ni Gigy’ Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kunyooshwa na mama mwenye Nyumba yake Baada ya kuwekewa masharti magumu.

Mtandao wa Global Publishers unaripoti kuwa Gigy alipewa masharti hayo magumu na mama huyo ambaye alikuwa anaijua historia ya msanii huyo kwani alikotokea aliwahi kugombana na mwenye nyumba mpaka kutaka kumshushia kipigo.

Kwenye mahojiano waliyofanya na mwanamama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Koku alifunguka:

Yaani Gigy alipoingia tu kwenye hii nyumba alipewa masharti makali kama vile kutovaa nguo za ajabu, kulewa, kuvuta bangi na kubadili wanaume hivyo akiwa anatoka kama amevaa nguo za nusu utupu anafunga kanga anaenda kuvua nje.

Sasa nilimwambia kwamba kama anataka kuishi vizuri na mimi hapa nyumbani kwangu sihitaji matusi na nilimpiga marufuku kuvaa vinguo vifupi hapa nyumbani kwa sababu nina watoto wadogo kwa hiyo sitaki waige tabia mbaya, nikamweleza kama anahitaji kuvaa nguo fupi awe anavaa akishatoka nje ya geti lakini siyo humu ndani.

Kuhusu kuvuta sigara na kutumia siwezi nikamzuia mtu kufanya kitu anachokipenda, pengine hiyo ndiyo furaha yake mimi nitajuaje, ila nashukuru Mungu kwa sababu naishi vizuri tu na huyu binti na ni mtafutaji sana, nampongeza kwa hilo“.

Gigy Money alipanga Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Kijitonyama mara Baada ya kumwagana baba wa Mtoto Wake Mo J na kuishia kutimuliwa kwake.

Diva Akana Kuwa Kwenye Mahusiano na Mo J Wa Gigy

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM Loveness Malinzi maarufu Kama Diva The Bawse ameibuka na kukana tetesi kuwa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mo j.

Mo J ambaye pia ni mtangazaji wa Choice Fm amezaa Mtoto mmoja na video vixens na msanii wa Bongo fleva Gigy Money ambaye Mtoto wao anaitwa Mayra.

Wiki chache zilizopita kuna taariza zilisambaa kuwa Baada ya Gigy na Mo J kuachana Diva ameanzisha mahusiano na Mo j ambapo taarifa hizo zilichochewa na video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Diva na Mo J pamoja.

Lakini sasa Diva amekana tetesi hizo na kuweka wazi kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Mo j zadi ya mahusiano ya kikazi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diva ameandika:

Naomba kwa heshima na taadhima nitoe tamko… Leo Ngoja nijibu..sababu nimejisikia afu pia mechefukwa tu yan na baadhi ya vitu na watu . . oky ni hivi Apa juzi kati niliona sana Picha Zangu na @moj360 kwamba tuna mahusiano. Nilipata simu nyingi za waandishi na nahisi niliwajibu sana short n clear sababu pia sikutaka mahojiano na mtu yan…… Yan mechoka kujielezea nilikuwa yan naona fresh whatever…. Truth is sijawahi kuwa na mahusiano na @moj360 yan ata kutongozana hatujawahi tunaheshimiana sana. Ni vile mliona mtu anaefanana nae tukiwa katika video ya Pamoja. Thought i said this once n im saying this again. Sina plan ya kumpost mtu apa uso ata niwe nae vipi. I prefer privacy siku hizi mekuwa. Kwanza medate watu wachache sana in the undustry kiukweli kweli Some zilikuwa stunts si zaid. kwanza nshakuwa mfanyabiashara nawaza hela zaid…and how to protect my brand na kutoka katika midomo ya watu kwa njia mbaya. Negativity stak.. Damn it work so hard to be here aisee. Living to the fullest livin ma life like happy n shit. Hard work y’all kno.. So ndugu jamaa na marafiki na mashabiki poleni kwa usumbufu. Xoxo Lovely Diva #temporarypost“.

 

Gigy Money Afungukia Mahusiano Ya Mo J na Diva

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kuongelea uhusiano unaoendelea kati ya  Mtangazaji wa Choice FM Mo J na mtangazaji wa Clouds Fm Diva The Bawse.

Siku chache zilizopita kuna tetesi zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diva na Mo J ambaye ni mzazi mzazi mwenzake na Gigy Money wapo Kwenye Mahusiano.

Tetesi hizo zilichochewa na video iliyosambaa kwenye social media iliyowaonyesha Wawili hao wakiwa katika mikao ya kimahaba na hivyo kuibua tetesi za uhusiano.

Tangu Gigy Money  ameachana na Mo J ameweka wazi kuwa hawana maelewano mazuri licha ya kumlea mtoto wao pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy amefunguka baada ya kuulizwa anajisikiaje baada ya kuona Diva Yupo Kwenye Mahusiano na Baby daddy wake ambapo alijibu:

Kawaida sana maaana sina mkataba nao, Hata wewe kipenzi unaweza ukapita naye kiroho safi”.

Lakini pia Gigy Money amesisitiza kuwa hawezi kurudiana Tena na Mo J na hata kuzaa naye Tena hawezi kuthubutu.

“Siwezi Tena Kuzaa na Mo J Bora Nitoe Kizazi”- Gigy Money

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kusema hawezi Tena kuzaa na Baba mtoto wake mtangazaji wa Choice Fm Moj.

Gigy Money ambaye amezaa mtoto mmoja wa kike na Moj anayeitwa Myra amemwaga povu hilo baada ya kuulizwa Kwenye mtandao wa Instagram kama atakuwa tayari kuzaa mtoto mwingine na Mo j.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money aliandika maneno haya:

Bora nitoe kizazi kuliko kuzaa na Punga Sese kama yule siwezi kabisa”.

Kama utakumbuka baada ya kujifungua mtoto wake alipokuwa bafo na Mo J Gigy alifanya Interview na kusema atakuwa tayari kumzalia hata watoto kumi Moj maana ni Baba mzuri.

Gigy Money na Mo J Warudisha Mapenzi Kama Zamani

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gigy Money amerudisha penzi kwa aliyekuwa mpenzi wake mtangazaji wa Choice Fm Mo J.

Wiki chache zilizopita Gigy Money na mpenzi wake wa Muda mrefu Mo J walitengeneza headlines za mitandao ya kijamii baada ya kurushiana maneno Kwenye vyombo vya habari.

Baada ya kutibuana mara tu baada ya kujifungua Gigy Money alitangaza kumuacha Mo J huku alisisitiza mtoto sio wake na akimtaja mpenzi wake mpya kuwa baba wa mtoto.

Lakini  mambo yanaonekana shwari kwa sasa kwani  siku ya jana wawili hao walionekana wapi pamoja mara baada ya Gigy kuposti video iliyowaonyesha wakitembea pamoja na mahaba tele.

Na baadae Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy aliposti picha iliyowaonyesha wawili hao wakiwa nisu utupu kuonyesha kwamba wapo vizuri na kusindikiza kwa caption iliyosomekaa “Mzazi mwenzangu ?♥“.

Gigy Money Aomba Radhi Baada Ya Kumwaga Povu Zito

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameomba radhi baada ya ugomvi wake na Baba mtoto wake Mo J.

Gigy Money alimtolea maneno makali Ex wake ikiwemo kuweka wazi kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo kuwa mtoto wake Myra sio wa Mo J kwani alikuwa na mwanaume mwingine.

Gigy Money na Ex wake Mo J walirushiana maneno makali baada ya Gigy kumtuhumu kiwa hakuwa alimfunza kipindi cha ujauzito na kudai alihama na kila kitu baada ya kuachana.

Baada ya sakata hilo Mo J aliongea na vyombo vya habari na kudai kuwa ana uhakika kuwa mtoto wao ni wa kwake ingawa Gigy kwa ajili ya hasira anampa  mtoto mpenzi wake wa sasa.

Baada ya povu hilo Gigy Money ameibuka na kuomba radhi kwa maneno aliyoongea huku akidai ilikuwa ni hasira ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka ujumbe huu:

Baby Shower ya Mtoto wa Gigy Money Majanga

Video queen aliyegeukia muziki wa Bongo fleva na kusumbua vibaya mno na kibao chake cha ‘Nampa papa’ Gigy Money amepata wakati mgumu baada ya aliyotarajia kumfanyia mtoto wake aliye tumboni kuota mbawa.

Gigy Money aliushangaza ulimwengu alipotokea ofisi za Basata alipoitwa na Waziri Julianna Shonza akiwa na ujauzito mkubwa wa miezi saba aliouficha kwa muda mrefu.

Lakini tangu ujauzito wake auweke wazi pia Gigy Money amepitia majanga mengi sana ikiwemo kuweka wazi kwenye mtandao wa kijamii kuwa baba mtoto wake ambaye ni mtangazaji wa Choice Fm, Mo Jay anatabia ya kumtembezea kichapo.

Gigy Money alikiri kuwa mpenzi wake huyo anampiga wakati yu mjamzito kitendo alichodai kimempelekea kufikia uamuazi wa kuachana naye na kuwa single mama, uamuzi ambao ulidumu kwa siku chache kwani baadae walirudiana.

Baada ya kuwa katika nafasi nzuri na baby daddy wake Gigy alianza kuandaa baby shower yake kabla hajajifungua mwezi ujao lakini amejikuta anashindwa kufanya shughuli hiyo kutokana na mambo ya kifedha kutokaa vizuri.

Habari za chini chini zimekuwa zikidai kuwa Gigy alikuwa hana mpango wa kufanya baby shower kwa muda huu alikuwa anasubiri mpaka atakapo jifungua lakini baadhi ya marafiki zake wakamshawishi aifanye jumamosi iliyopita lakini siku zilipokaribia hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya kidogo.

Baada tetesi hizi kusambaa gazeti la Global Publishers lilimtafuta kwa ajili mahojiano na alifunguka haya:

Nilikurupuka kuandaa shughuli ndani ya wiki moja wakati nataka iendane na hadhi ya jina langu, nikaona isiwe tabu nikasogeza mbele hadi wiki ijayo”.

 

Gigy Money Alia Kutembezewa Kichapo na Baba Mtoto Wake Wakati Mjamzito

Msanii wa Bongo fleva Gigy Money amefunguka mazito sana yanayomsibu kwa hivi sasa ambapo amedai kuwa baba mtoto wake mtarajiwa ambaye pia ni mpenzi wake wa muda mrefu anayejulikana kama Mo j ana tabia ya kumpiga na amefikia hatua ya kumpiga hivi karibuni akiwa mjamzito.

Gigy Money alitangaza ujauzito wake hivi karibuni baada ya kuuweka Siri kwa muda wa miezi saba huku akiweka wazi kuwa baba wa mtoto huyo ni mpenzi wake ambaye pia ni mtangazaji wa Choice Fm, Mo j.

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money amlimtupia tuhuma nzito mpenzi wake kwa kudai anamtesa wakati yu mjamzito ambapo amedai kuwa ana tabia ya kumpiga na hata kutembea na wanawake wengine, kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka yafuatayo;

Kusema ukweli leo nina stress sana ndio maana nimeona bora niseme  kwani ninachokiamini sio peke yangu ninayeyapitia haya katika makosa ambayo naamini nimeyafanya ni kupenda ingawa najua kupenda sio dhambi nimepitia mengi sana kwenye mapenzi hadi kufikia hatua ya kupingua mwili, baadhi ya watu walio karibu na mimi wanaweza wakawa wanajua baadhi ya mateso na utumwa wa mapenzi niliowahi kupitia, mara nyingi unaweza ukatokea kumpenda mwanaume mwenye uwezo wa kawaida ukiamini mapenzi sio pesa lakini wanaume wa Bongo jeuri unabeba mimba dharau atakufanyia mwanamke wake wa nje atakuonyesha kiukweli inauma ndio lakini naamini ni hatua za maisha na ni ukuaji naamini nimedondoka hatua moja lakini nitainuka hatua nane. Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kuwa na single mothers sio baba wote wamekufa wengi wetu tunwakimbiza watoto wetu mbali na maisha ya mateso tuliowahi kiyapitia kwa baba zetu ukiona naandika haya yote ujue mambo yamezidi kuwa mabaya”.

Lakini pia Gigy Money amefunguka na kuandika “Nachukia mwanaume anayepiga mwanamke mjamzito, nachukia mwanaume mnyanyasaji na sio kila mwanaume anafaa kuitwa mume”. Lakini Gigy amemfungukia mmoja wa shabiki zake na kusema ni kawaida ya Mo j kumpiga zamani lakini sahivi ameshindwa kuvumilia kwa sababu ni mjamzito.