Ningekuwa Diamond , Ningemuoa Zari ;-Gigy

Mwanadada Gigy money ameamua kutao yake ya moyoni kwa kusema kuwa kama yeye ndio angekuwa msanii Diamond platinumz basi wala asingehangaika na wanawake wengine bali angeamua kumuoa Zari kwa sababu ni mwanamke mwenye hela na anajitambua.

Gigy anaonekana kupingana kabisa wa watu kwenye mitandao ya kijamii wanaokaa kutwa wakimsema vibaya mwanamama Zari kuwa amezeeka na ni mkubwa kwa Diampond bila kuangalia umuhimu wa maisha yake kwa msanii huyo.

Gigy anasema kuwa anshangaa kumuona Diamond akiangaika na wanawake wakati Zari alikuwa mwanamke mwenye hela na kama wanegoana wote wangekuwa na pesa na wala wasingesumbuka na kitu chochote kile.

Hat hivyo bado Gigy haonekani kumchukia tanasha kwa sababu amemsifia na kusema kuwa hata yeye alipomuoana siku ya kwanza alimshangaa kwa uzuri aliokuwa nao.

Waziri Shonza Ampa Onyo Kali Gigy Money

Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Mhe. Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kumong’onyoa maadili hapa nchini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mh. Shonza ameitumia kauli hiyo iliyotolewa na Rais asubuhi wakati wa makabidhiano ya kifaa kitakachotumika katika mawasiliano ambacho TCRA wamekabidhiwa ambapo Rais alisema katika moja ya kauli wakati anaelezea madhara ya mitandao ya kijamii.

Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili”.

Baada ya kauli hiyo Mhe.Shonza ambaye ni Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, yaani Naibu anayeshughulikia mambo yaote yanayohusu habari na mawasiliano ameipost kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema:

Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_ogna wenzio,msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa”.

Nilikuwa na Ndoto Ya Kuwa Mwanasheria- Gigy Money

Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money ameibuka na kudai mbali ya kufanya muziki Lakini Ndoto Yake kubwa ilikuwa kuwa mwanasheria.

Gigy Money ameibuka na kudai kuwa alipokuwa mdogo alikuwa ana Ndoto kila siku za kuja kuwa mwanasheria na sio mwanamuziki kama alivyo Hivi sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Gigy Money amesema kuwa alikua akipenda fani hiyo tangu akiwa mdogo kutokana na kuwa na uwezo wa kumsimamia mtu katika ukweli bila kuyumbishwa.

Nilikua napenda sana sheria, sema sikusoma sana na niliishia kidato cha pili lakini ndoto yangu kubwa ilikua kuja kuwasimamia watu kupata haki zao, mambo ya muziki nimeyavamia tu“.

 

Dudubaya Akiri Kumkubali Gigy Money

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Tumaini Godfrey maarufu kama Dudubaya ameibuka na kuweka kuwa anamkubali msanii mwenzake Gigy Money.

Dudu Baya amesema kuwa msichana anayeweza kumuoa na anampenda ni Gigy Money na Lady Jaydee. Japo kuwa ameeleza kuwa Gigy anatabia ambazo bado haweki kumfanya awe mke labda aziache.

Mwanamke ninayempenda ni Gigy Money, Gigy huwa nampenda ila tabia zake ambapo bado siwezi kumfanya kuwa mke yaani mpaka aache zile tabia, tulishazungumza ila hawezi kuacha zile tabia, Gigy mnaweza mkawa sehemu akaanza kucheza akiwa uchi kwahiyo kama mama watoto siwezi.

Lakini tukija mabinti wengine wakike kwenye hustle anajiamini ni Lady Jaydee, kwasababu ni mwanamke mwenye akili timamu kwasababu mimi nampenda mwanamke mbishi kwasababu mimi ni Konki”.

Dudubaya na Gigy Money waliwahi kuibua Tetesi Za kuwa pamoja Baada ya kuonekana karibu kuliko kawaida walipokuwa pamoja kwenye ziara ya Wasafi Festival.

 

Gigy Money Afunguka Kurudiana na Mo Jay

Mwanadada Gigy money amefunguka na kuongelea swala lake la kurudiana na menzi wake ambae pia ni baba wa  watoto wake mo jay amabe pia ni mtangazaji wa clouds media.

Gigy Money anasema kuwa ni ukwlei kuwa hajawahi kuachana na mume wake huyo kwa sababu kuachana ni maneno tu ambayo yamekuwa yakisemwa katika mitandao ya kijamii.

unajua kuachana huwa ni maneno tu ambayo yanaweza kuwa wat wanaongea lakini hakuna ukweli na ukizingatia kuwa sisi ni wazazi,  kwa maadili yetu yule mototo lazimaatatukutanisha tu.

Ikumbukwe kuwa mwanadada Gigy money aliwahi kusema kuwa alipigwa sana na baba wa watoto wake huyo huku kila mmoja kwa wakatri wake akionekana akiwa na mpenzi mwingine katika mitandao ya kijamii.

 

Gigy Money Adaiwa Kushushiwa Kipigo Kizito na Dudubaya

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money anadaiwa kutembezewa kipigo cha haja  na msanii mwenzake mkongwe Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya.

Global Publishers wanaripoti kuwa Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita jijini Mwanza ambapo inaelezwa ugomvi ulianza kama utani wawili hao wakiwa nyuma ya jukwaa wakati Tamasha la Wasafi Festival likiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo alidai Gigy ambaye mara nyingi ameonekana akiwa karibu na Dudu Baya alikuwa akiongea sana na kutaja mambo ambayo ni matusi mbele za watu huku Dudu Baya naye akiwa na mwanaye.Wakati Gigy akiendelea kumwaga maneno ya chumbani akijihusisha na Dudu Baya, msanii huyo mwenye asili ya utata alikuwa kimya kwa aibu akiwa na binti yake, Maria.

Kukaa kimya kwa Dudu Baya hakukusaidia kitu kwani Gigy aliendelea kutoa maneno makali lakini yalipozidi mwanamuziki huyo aliwaomba waungwana wakamtulize mwanamama huyo.

Yaani maneno ya Gigy yalikuwa yanamfadhaisha sana Dudu Baya na mwanaye  ambapo licha ya kumtaka aache hakusikia, aliendelea tu“.

Kutokana na kuendelea kutoa maneno machafu Dudu Baya alimvaa Gigy na kumshushia kipigo cha ambapo aliokolewa na mabaunsa waliokuwa karibu. Katika varangati hilo Gigy aliangua kilio kutokana na maumivu huku akilalama kupoteza simu yake ya kisasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko Dudu Baya ili kueleza sababu za kumshushia kipigo Gigy na kufunguka;

Huyu Gigy hana akili, nilishamwambia muda mrefu kwamba sitaki utani wake yeye hanielewi, yule ni mwanamke wa ajabu sana”.

 

Gigy Money Afungukia Uwamuzi Wake Wa Kumuachia Mtoto Wema Sepetu

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefungukia uamuzi Wake wa kumuacha Mtoto Wake na Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

Wiki iliyopita Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money aliweka wazi kuwa kabla ya kusafiri kwenda kufanya shoo mkoani Mwanza ameamua kumuacha binti yake na Wema kwani anaamini ni mama mzuri na anapenda sana watoto.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Gigy Money aliyekuwa safarini jijini Mwanza huku akimwacha mwanaye kwa Wema jijini Dar, Gigy alisema amemuona Wema ana upendo na pia anapenda watoto hivyo akaamua kumuachia na kwenda kutafuta maisha akijua yupo mikono salama.

Namuomba Mungu amjalie Wema apate mtoto maana ni mama mwenye upendo ndiyo maana nimemuachia Maira amlee na ninajua atakuwa kwenye mikono salama“.

Wema ameshaweka wazi mapenzi yake kwa watoto licha ya kushindwa kupata Mtoto Wake wa kumtaka mwenyewe.

Dudubaya na Gigy Money Wabambwa Pabaya

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amedaiwa kukutwa chobingo na msanii mwenzake Gigy Money wakiwa wanafanya yao.

Global Publishers wanaripoti kuwa pamoja na ugumu wote ambao Dudubaya anadaiwa kuwa nao lakini alikutwa akiwa anachekeshwa na kukalishwa na Mtoto Gigy.

Wawili hao walinaswa nyuma ya jukwaa la Wasafi Festival katika tamasha lililofanyika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Halmashauri ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa mbapo Gigy alikuwa ameshapanda jukwaani na kuwapa burudani wakazi wa eneo hilo. Katika tukio hilo, wawili hao walinaswa wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba huku kila mmoja akionekana kukolea kwa mwenzake.

Baada ya kuzua gumzo mbele za watu ndipo waandishi wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko liliwafuata wawili hao lakini waliomba waachwe wapumzike kwa madai kwamba walikuwa wamechoka kuhojiwa.

Hebu tuache bwana tupumzike…”.

Gigy Money Afunguka Maumivu Aliyopata Kupitia Mikononi Mwa Mo J

Video vixen na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money amefunguka na kuanika maumivu ya mapenzi ambayo amekuwa akipitia.

Sio mara ya kwanza kwa Gigy Money kutangaza hadharani kuwa aliyekuwa Mpenzi Wake mtangazaji wa Choice Fm Mo J amekuwa akimnyanyasa na hata kumpiga na kumuachia majeraha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy Money amefunguka mazito kuhusu mapenzi yake na kijana huyo ambaye amezaa naye Mtoto mmoja:

https://www.instagram.com/p/BrCAM12nJhr/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=oi1c5qrl358l

https://www.instagram.com/p/BrCEhTVHAaQ/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=g2gq9rv95hng

“Bora Kufanya Kazi na Diamond Kuliko Alikiba”-Gigy Money

Video vixen maarufu na Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford kwa jina la usanii Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ni bora kufanya kazi na Diamond kuliko Ali Kiba.

Gigy Money ambaye Hivi sasa anaonekana akiwa amejiunga pamoja na Kundi zima la Wasafi linaloongozwa na Diamond Platnumz ili kushiriki katika tamasha lao la Wasafi Festival.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Gigy Money ameibuka na kudai kuwa ameona kuna ubora mkubwa wa kufanya kazi na Diamond kuliko kufanya kazi na hasimu Wake Ali Kiba.

Ali Kiba anakunja sana kuliko Diamond  na siku ambayo tulienda kufanya wote shoo Kahama Ali Kiba alinitenga kabisa Backstage”.

Wiki mbili zilizopita Diamond Platnumz na Ali Kiba walifanya shoo zao usiku mmoja ambapo Ali Kiba alipiga shoo mkoani Shinyanga/Kahama na Diamond alipiga shoo yake mkoani Mtwara.

Gigy Money Atoa Siri ya Kupigwa na Mpenzi wake Mpya

Mwanadada Gigy Money ameshindwa kuvumilia kwa kile kilichodaiwa kuwa ni unyanyasaji katika mahusiano baada ya kuweka picha yenye kumuonyesha akiwa na makou shingoni mwake makovu mabayo yanasemekana kuwa ni baada ya kupigwa na mpenzi wake.

gigy mone baada ya kuachana na mo jay aamekuwa na wanaume tofauti tofauti na hata kulingishiana na baba wa mtoto wake huyo katika mitandao ya kijamii kwa penzi hilo jipya lakini mapenzi hayo yanaonekana kumshida hasa baada ya kuonyesha makovu ya kupigwa.

katika picha hiyo gigy aliandika “shingo yangu imeharibikia..wanawake bongo tunaonewa sana…”

Ikumbukwe kuwa gigy moneya amekuwa na mahusiano na wanaume tofauti tofauti na amekuwa akifanya show-off za wanaume hao.

Mimi Kwetu Ndio Tajiri ;-Gigy Money

Mwanadada gigy moeny amefunguka na kusema kuwa ana ndoto za kufanya mambo makubwa katika maisha yake ikiwa pamona na kufungua sehemu ya chakula na salon.

Gigy Money ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Dizzzim Online na kusema kuwa katika familia yake  Yeye ndio tajiri kuliko mtu yoyote hata akiingia kwao yeye ndio anaheshimika lakini huku nje watu hawajui kuwa yeye ana majukumu mengi kama ya kumlea mtoto wake.

Mungu akipenda kwakwei nina mataraajio mengi sana kama kufungua sal;on, kufungua sehemu kwa ajili ya chakula, kuna pesa tu hapa nimekuwa nikiitafuta, pesa sio ngumu ila nina majukumu mengi tu na hata mimi kwetu nikiingia mimi ndo tajiri unaelewa lakini wao hawajui kuwa mimi nina majukumu gani na nina take responsilibities gani kwa mwanangu

 

Gigy Money na Mo J Wazidi Kurushana Roho na Wapenzi Wapya

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money na Baba Watoto Wake Mtangazaji wa Choice Fm Mo J wameendelea kurushana roho huku kila mmoja akimuanika Mpenzi Wake.

Gigy Money na Ex Wake Mo J wamelala Mtoto mmoj mwenye umri wa miezi Sita sasa lakini wamekuwa na tabia ya kuachana na kirudiana tangu Mtoto wao alivyozaliwa lakini hivi karibuni Gigy aliweka wazi kuwa wawili ho hawako pamoja tena.

Baada ya kuachana Gigy Money alimuanika wazi Mpenzi Wake ambaye yuko naye kwa sasa na kumtaja Kama Montana ambaye ni Mmarekani ambaye anaishi nchini Kenya.

Baada ya Gigy Money kuonekana akiwa anajiachia na jamaa huyo ingawa mara kwa Mara amekuwa akimsaliti na kurudi tena kwa Mo J hatimaye Mo J naye amechoka na kumuweka wazi Mpenzi Wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo J aemuanika mrembo huyo na kuambatanisha na kiemoji cha pete “? Soon Inshallah ??❤️” kumaanisha ameshibana na mrembo huyo na ndoa inaweza kutokea siku yoyote.

Gigy Money Awekewa Masharti Makali Kwenye Nyumba Ya Kupanga

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Kiki ni Gigy’ Gift Stanford ‘Gigy Money’ amedaiwa kunyooshwa na mama mwenye Nyumba yake Baada ya kuwekewa masharti magumu.

Mtandao wa Global Publishers unaripoti kuwa Gigy alipewa masharti hayo magumu na mama huyo ambaye alikuwa anaijua historia ya msanii huyo kwani alikotokea aliwahi kugombana na mwenye nyumba mpaka kutaka kumshushia kipigo.

Kwenye mahojiano waliyofanya na mwanamama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Koku alifunguka:

Yaani Gigy alipoingia tu kwenye hii nyumba alipewa masharti makali kama vile kutovaa nguo za ajabu, kulewa, kuvuta bangi na kubadili wanaume hivyo akiwa anatoka kama amevaa nguo za nusu utupu anafunga kanga anaenda kuvua nje.

Sasa nilimwambia kwamba kama anataka kuishi vizuri na mimi hapa nyumbani kwangu sihitaji matusi na nilimpiga marufuku kuvaa vinguo vifupi hapa nyumbani kwa sababu nina watoto wadogo kwa hiyo sitaki waige tabia mbaya, nikamweleza kama anahitaji kuvaa nguo fupi awe anavaa akishatoka nje ya geti lakini siyo humu ndani.

Kuhusu kuvuta sigara na kutumia siwezi nikamzuia mtu kufanya kitu anachokipenda, pengine hiyo ndiyo furaha yake mimi nitajuaje, ila nashukuru Mungu kwa sababu naishi vizuri tu na huyu binti na ni mtafutaji sana, nampongeza kwa hilo“.

Gigy Money alipanga Nyumba hiyo ambayo ipo maeneo ya Kijitonyama mara Baada ya kumwagana baba wa Mtoto Wake Mo J na kuishia kutimuliwa kwake.

“Nilikuwa na Ndoto Ya Kuwa Mwanasheria”-Gigy Money

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu Kama Gigy Money ameibuka na kudai ndoto yake kubwa maishani ilikuwa kuwa mwanasheria.

Gigy Money ambaye alijizolea umaarufu kutokana na Umbo lake matata na vituko vyake kwenye mitandao ya kijamii lakini wimbo wake wa Nampa papa ulimtambulisha zaidi kwenye tasnia ya Bongo fleva.

Lakini hivi sasa Gigy Money anadai muziki haukuwa kwenye ndoto Zake Bali ameuvamia tu kutokana na maisha lakini yeye ndoto yake kuu ilikuwa kuwa mwanasheria.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari hivi karibuni Gigy Money amefunguka kuhusu ndoto hizo na kusema alikuwa anaipenda fani hiyo tangu akiwa mdogo kutokana na kuweza kumsimamia mtu kwenye ukweli bila kuyumbishwa.

Tangu mdogo nilikuwa napenda sana sheria sema sikusoma sana kwa sababu niliishia kidato cha pili lakini ndoto yangu kubwa ilikuwa kuja kuwasimamia watu kupata haki zao”.

 

Wema Achukuliwa Hatua Kali na BASATA Baada Ya Kuvujisha Picha Chafu

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amejikuta katika upande mbaya wa sheria za nchi baada ya kuvujisha picha zake za faragha alizokuwa na mpenzi wake PCK.

Pamoja na kuomba radhi siku ya jana kuhusiana na picha hizo chafu Kwenye mitandao ya kijamii lakini tayari BASATA wameamua kumchukilia hatua kali Wema pamoja na wasanii wote walioachia picha chafu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni.

Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya  filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pamoja na Wema kusambaza na video zake chafu Lakini pia Gigy Money amedaiwa kuachia picha yake chafu Lakini pia video vixen Amber Rutty ameachia video yake ya ngono Mtandaoni.