Harmonize Amjibu T.I.D Kuhusu Kuigiza Nyimbo za Nigeria.

Msanii wa muziki wa bongo fleva anaefanya vizuri  katika muziki  , Harmonize amemjibu msanii tid kuhusu tuhuma alimpa za kuwa amekuwa akiiga kuimba nyimbo za wa Nigeria na kuwa amekuwa akipoteza uhalisa wa nyimbo za Tanzania.

Msanii huyoa aliekuwa akiongea na Wasafi tv, anasema kuwa inawezekana kabisa kuwa T.I.D hakuwa anamlenga yeye kwa sababu kama angekuwa amemlenga yeye basi angemtaja jina na kwa sababu kuongea bila kumtaja jina inaweza kuleta bifu pia hata kwa wasanii wengine tofauti na yeye.

Mimi ninaamini kuwa kuna watu alikuwa akiwalenga lakini sio mimi ila kwa sababu hakutaka matatizo na wasanii wengine akaona  bora apitie kwangu na kutaja jina la mdogo wake harmonize.

 

Shabiki Amtolea Povu Harmonize Kuacha Kumuiga Diamond

Moja ya mashabiki wa msanii Harmonize  amemuandikia msanii huyo barua ndefu na kumshauri jinsi ya kufanya ili aweze kukua kimuziki lakini sio kumuiga meneja wake Diamond kwa sababu kwa kufanya hivyo anakuwa anaua kazi zake za muziki.

Shabiki huyo anaesemekana kutokea Mombasa amemuomba  Harmonize aje na style tofauti na  kuacha kumuiga Diamond kwa sababu anawaboa mashabiki wake wengi.

am from Kenya working in Dubai, shabiki mkubwa naharmonize lakini ananiboa sana anavyokuwa nafanya  kwa sttle zake za kumuiga diamond.naomba aje na style zake tofauti hata kama mond ni boss wake.

Shabiki huyo kutoka kenya hatokuwa shabiki wa kwanza kumtolea povu msanii harmonize kwa kile kinachodaiwa kuwa amekuwa akimuiga boss wake kuanzi akuvaa na hata mavazi wakati mwingine bila kujua kuwa mashabiki wao wanaowapenda wamekuwa wakiwafatilia na kuwashajua kuwa hawana tofauti.

hii inaua soko la muziki hasa kwa upande wao, hivyo  msanii anapaswa kuchuka ushauri huo na kyuona ni wapi alipokosea na panapaswa kurekebishwa.

Harmonize azungumzia kuhusu mjengo wake

Muimbaji kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mjengo wake ambao ni wa ghorofa akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni.

Kulingana na Harmonize mjengo wake unawezekano wa kukamilika mwishoni wa mwaka huu. Hata hivyo, Harmonize alikataa kufunguka kuhusu gharama aliyotumia kutengeneza ghorofa hiyo.

Harmonize alisema;

“Kwa hiyo flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi”

Harmonize aliendelea kwa kudai….

“Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,”

“Usiogope maneno ya watu” Diamond Platnumz amwambia Harmonize

Wikendi hii iliyopita, Diamond Platnumz, Harmonize na warembo wao walifika katika klabu maarufu ya Nairobi, B Club kuwatumbuiza mashabiki wao wa Kenya katika show iliyowavutia wengi.

Wakali hao wawili wanaaminika kuwa marafiki wa karibu waliwapa wengi kitu cha kuongea hasa baada ya kuonekana na warembo wao, Zari na mpenzi mpya wa Harmonize anayetambulika kama Sarah.

Hata hivyo Diamond Platnumz aliwashangaza wengi baada ya kumuandikia Harmonize ujumbe kupitia Instagram huku akimsihi asiogope maneno ya watu kwani wamepata fedha na mali ya kutosha kupitia muziki wao.

Tazama picha hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BXMcjb7FSgD/

Harmonize amshirikisha Mr Nice kwenye video yake mpya!

Mkali wa label ya WCB Harmonize ameachia video mpya ‘Sina’ ambayo inaonekana kuwapendeza wengi baada ya kumshirikisha Mr Nice Kama video vixen wake.

Mashabiki wamemshukuru Harmonize na label ya Wasafi kwa kumuamuni Mr Nice na nafasi hiyo ya kuieleza hadithi ambayo Harmonize anayoielezea kwenye wimbo huo.

Itazame video hiyo ambayo imeongozwa na director Khalfani.