Mazingira Yasiyoepukika kwa Mwanamke Kutoa Maamuzi

Kuna mambo ambayo wataalamu wengi wamekuwa wakiongelea katika maisha hasa yanayohusiana na hisia, tunapokuja kwenye swala la kutaka kufanya maamuzi tunashauriwa sana kuepuka kufanya maamuzi unapokuwa na hisia fulani, hii inaweza kukuletea matokeo  chanya au hasi lakini mara nyingi unakuwa haujategemea kupata matokeo hayo kulingana na hali uliyokuwa nayo.

Kwa wanawake, hii huwa ngumu kwao kwa sababu kuna hali  ambazo aidha kwa kupenda au kutokupenda anaweza kujikuta tu akifanya maamuzi bila kujali yataleta matokeo gani baadae.

Kwa kumsikiliza pia moja ya wataalamu wa mahusiano kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salam , Chris Mauki anasema kuwa kuna hali ambazo mwanamke hata ufanye nini inakuwa ngumu kwake kuacha kufanya maamuzi pengine apate mtu wa karibu sana kuweza kuzipinga hatua zake.

Baadhi ya hali hizo zinazoweza kumfanya ashindwe kuacha kufanya maamuzi ni pamoja na :-

  • Akiwa mpweke – akiwa na kiu ya kuliwazwa kwenye upweke wake haangalii huyu ni mume wa mtu, mchumba wa mtu, mzazi wa mtu. Yeye anachotaka upweke wake uishe
  •  Akiwa desparate (mwenye kiu ya kuolewa) – mwanamke akiwa kwenye hali hii, basi mwanaume yoyote kwake ni potential husband, awe mume wa mtu au la, akifikia hapa hajali mambo ya kupima afya, mambo ya dini au imani, vigezo na masharti vyote vinafukiwa ardhini.
  •  Akiwa na kiu ya mtoto – Hapa hajaliwi mtu inajaliwa mbegu tu. Kila akiona mwanaume anamwona kama baba mtoto wake, hapa haliangaliwi penzi tena bali mbegu za mtoto. Hapa hata kama ana imani ya kuhamisha milima atakuwa tayari kwenda kwa mganga pale anapoona maombi hayafanyi kazi. Mtoto atatafutwa come what may, come sun come rain

Hali yako na mapito yako yasikufanye ushushe standards zako. Ndio maana taji hata siku moja haitolewi mwanzoni bali mwishoni. Yeye avumiliaye atavikwa taji –

 

 

 

Jinsi Unavyoweza Kujua Uko Kwenye Mahusiano Hatarishi.

Sio kweli kuwa watu wanaokaa muda mrefu katika mahusiano ndio wanaweza kukumbana  na uhatari katika mahusiano , wapo ambao wamekuwa wakianzisha mahusiano kwa maslahi yao binafsi lakini wenzi wao wanapata tabu kujua kwa sababu wanakuwa tayari   wameshapenda.

Hata kama mmekuwa na mahusiano kwa muda wa wiki moja tu, ni lazima kuwa mwangalifu na mtu unaeingia nae katika mahusiano ili kujua kama uko kwenye hatari ya kuumia kwa namba yoyote ile.

Watu wengi hawataki kuamini kuwa kule wanakopenda kunaweza kuwa na hatari ya kuumia , wengi wanaamini kuwa kama mtu anaweza kukuonyesha kukupenda  hasa kwa maneno basi anakuwa tayari ameshachanganyikiwa na hakuna kitu unaweza kumwambia , lakini kumbe kuna mazingira yanaweza kuchunguzwa taratibu na ukagundua baadhi ya vitu kama.

Uthibiti usio wa kawaida (Over Control )

kuna watu katika mahusiano haoni kama mwenzake ana thamani kama inavyopaswa kuwa, yeye anataka kuwa muamuzi wa mwisho katika kila kitu, anataka awe msemaji wa mwisho kwa kila kitu, na kama utabisha basi mnaweza kukaa bila maongezi mpaka atakapojisikia kukusemesha wewe.Mfano yapo mahusiano ambayo , mmoja kati yenu anataka kuwa anajua kila kitu kuhusu mwenzake lakini sio vyake, atataka yako  simu  ajue ni nani anapiga au kutuma sms, atataka kujua unaongea na nani na kwanini.Hii sio dalili ya mahusiano mazuri.

kujipendelea (self-centeredness)

Hakuna maana ya mapenzi kama mwenzi wako anakuwa akijali nafsi yake kuliko yako, maana ya mapenzi ni kujitoa muhanga kwa kila kitu , mapenzi mazuri ni yale ambayo kila upande unakuwa ukifaidi kile mlicholenga kukianzisha , lakini kama mmoja ananungunika na mwingine anafurahia na kuona sawa tu basi hayo sio mapenzi, ONDOKA HARAKA.

Kutaka kujimilikisha

Hatukatai kuhusu kumpenda mtu mpaka kumuonea wivu, lakini kuna ule wivu tunasema ni ujinga, wivu ambao anataka kujimilikisha wewe kuwa ndio wake kwa kila kitu.Wivu ambao kila sehemu na kila kitu chako basi ni lazima kipitie kwake, hii inachosha na kumfanya mmoja wenu akose amani ya maisha na mapenzi pia.

Ukosefu endelevu.

Kuna mtu anaweza kuwa amekuchoka lakini hataki tu kusema kwa sababu hataki kuwa sababu ,mtu huyu anaweza kuwa ni mwenye vituko na makosa ya kila siku yanayojirudia kila mara na kukufanya kuchoka.Fikiria kwamba amekuwa kila siku akifanya kosa moja ambalo kwa namna moja ama nyingine ameshajua kuwa linakukwaza , lakini cha ajabu kwa sababu ya mapenzi akiomba msamaha Unakuwa laini, Amka na anza kuchukua hatua hapo.

Udanganyifu uliopitiliza.

Ujawahi kusikia kesi ya kuwa mtu anakuwa akifanya kitu sio kwa sababu akili yake inataka afanye kitu fulani, lakini kwa sababu ya ushawishi kutoka kwa mtu anaempenda anajikuta anaweza kufanya chochote tu , hii utokea sana katika mahusiano ya sasa, mmoja wenu anakuwa na maneno ya kukulaghai  na kukufanya ukubaliane na kile anataka yeye wakati mwisho wa siku kitawaingiza katika matatizo tena hasa kwa upande wako.

NB;-Hakuna mtu asiependa amani kwa kila kitu, kuwa kwenye mahusiano au kuwa na mtu unaempenda kusikufanye ukaona kuwa maisha hayana maana kabisa, unachopaswa kujua ni kwamba  , pale unapoamua kuwa katika mahusiano kitu kikubwa cha kuzingatia ni amani ya moyo wako , hivyo tafuta mahusiano yenye afya sio kupelekwa tu kwa sababu unahitaji mahusiano.

 

 

 

 

Jinsi ya Kukabiliana na Maumivu ya kuachana na Mpenzi.

Watu wengi wamekuwa wakimia sana hasa pale wanapokuwa wanasitisja mahusiano na wale waliokuwa wakiwapedna kwa dhati, sio kila unapoachana na mpeniz wako unakuwa unataka kufanya hivyo, mara nyingi zipo sababu kubwa zinaweza kukufanya kuachana nae kwa sababu tu ni lazima kumuacha na kila mtu kutaka kuwa pke yake.

Lakini hakuna mapenzi ya kuachana na usiumie hata kama haukuwa na mapenzi ya dhati na mtu huyo, lakini kuna njia zinaweza kukuponguzia maumivu na kukufanya uwahi  kupata nafuu ya maumivu.

badilisha mazingira.

ni vizuri kuondoka katika mazingira yatakayokuwa yakikupa kumbukumbu kila mara juu ya jyule uliyekuwa nae, jaribu kuwaepuka hata wale marafiki zake ambao wanaweza kukuiliza kuhusu yeye, hii itakufanya kupata nafuu ya maumivu yako.

jifunze kusamehe na kusahau.

ni jambo zuri kujifunza kusamehe na kukubaliana na hali halisi ya kile kilichotokea, inawezekana mliachana kwa hasira kutokana na kile alichokufanyia kwa kipindi icho, jifunze kukubali kosa na moyo wako uwe mwepesi kusamehe kile alichokukosea ili usibaki na hasira.

sitisha mawasiliano.

kuna watu wanakuwa na maumivu na wale waliowaacha lakini bado anaweza kumtafyuta na hata kupigia simu, hiyo inaongeza maumivu kwa sababu yapo utakayokumbuka kuhusu yeye, epuka kuwsiliana nae na hata akikutafuta basi tafuta njia ya kumuepuka mtu huyo.

jipende na kujithamini mwenyewe.

kisaikolojia wataalamu wanasema watu wengi wakiachwa na wapenzi wao au kugombana basi wanaanza kujishusha na kuona kuwa wao hawafai na wala sio  wa thamani sana, kumbe mtu anaweza kuamua kukumiza tu kwa sababu zao na hata bila kujali kama atakuumiza wewe, sasa huu ndio muda wa kujiona bora na kujipenda mwenyewe kuliko maelezo.Achana na fikra kwamba wewe sio bora kuliko yule aliyemfata au kumpata baada yako.

usitafute wa kuziba pengo.

mara nyingi imekuwa ni kawaida kwa watu wanapoumizwa wanakimbilia kutafuta mtu mwingine kwa ajili ya kuziba pengo ili kukwepa maumivu yale ya mwanzo, hii ni mbaya sana kwa sababu ikitokea ukaumizwa tena unapata maumivu makubwa zaidi kuliko yale ya awali.jipe muda kwanza na kisha jitafakari  na jipe muda wa kuponesha makovu yako ya maumivu ya mapenzi.

 

 

Kwanini Mahusiano Mengi Huvunjika kwa Muda Mfupi

Baadhi ya wataalamu wanaohusika na maswala ya mahusiano wanasemaukuwa sababu kubwa ya watu kuvunja mahusiano kwa muda mfupi aidha kabla ya kuingia kwenye ndoa au baada ya kuingia kwenye ndoa huweza kuwekwa katika makundi mawili , yaani kundi  la kwanza ni sababu zile zinazohusiana na mchakato wa maisha ya kila siku kabla ya kuanza kuishi pamoja na pili ni zile zinazotokana  na wawili hawa kukaa pamoja na kukutana na misuguano ya kila siku.

Sababu hizi zinaweza kuwa ni tabia za mtu binafsi anakuwa nazo kabla ya kuanza mahusiano na hataki kuziacha hivyo anaamua kuziendeleza tu,  sababu hizi huweza kuleta kutengana kwenu kwa sababu tu wawili hawa wanakuwa wamechanganya tabia binafsi za mtu mmoja mmoja na zile wanazokutana nazo katika maisha ya kukaa pamoja.

HASIRA KALI

kwa kawaida hakuna mtu asiekuwa na hasira, lakini hasira mbaya ni ile ambayo inakuwa ya hapo kwa hapo na kuleta madhara makubwa (short temper) , hii hufanya mtu kuwa na maamuzi ya ajabu sana yanayoweza kupelekea maumivu makali sana kwa mwenzi wake ingawa baadae anaweza kupoa na kuomba samahani lakini tayari haiwezi kuponyesha jeraha lilisababishwa na hasira yak hapo nyuma

kadri haisra na matukio haya yanapokuwa yanajirudia inaleta chuki na kupungua kwa mapenzi kwa upande mmoja mpaka kusababisha mmoja wapo kujiengua mahali hapo.

HISIA ZA MAUMIVU NA MACHUNGU.

Kuna muda mtu anakuwa na hisia za machungu muda wote na hii husababishwa sana na matatizo au maisha yeti ya nyuma kwa upande wa malezi, familia au mahusiano yetu ya nyuma,mara nyingi kuna kuwa na makumbusho ya kile kilichowahi kutokea nyuma na hii inaweza kufanya kuwa na negative reflactions ya kile kilichowahi kutokea hapo nyuma.

hali hii ufika sehmu uchosha , kama huzuni ya mwezi na hasira za mara kwa mara huendelea inaweza kufanya mtu kuchoka kuonyesha mapenzi ambayo hayarudishwi kwa hisia.

KUTOFAUTIANA KATIKA MATUMIZI YA PESA.

Fikiria kuwa kuna mtu unampenda na umeamua kumshirikisha kwa kila kitu kwa sababu tu unajua kuwa huyo ndio mwenzi wako lakini cha ajabu ni kwmaba anakuwa hana ushirikiano katika swala la pesa, hawezi kutoa pesa zake kwa matumizi yenu wawili, labda pia kipato chenu hakiwezi kufanana na kile mwenzi wako anataka kukitumia kila siku.

Anakuwa na matumizi makubwa na wala yasiyo ya lazima kila siku,  anapoulizwa  anakuwa mkali na hataki kutoa maelezo kuhusu hilo, mapenzi ya aina hii hayana muda mrefu zaidi sana yupo anayehumia sana kuliko mwingine.

Angalia mnategmea kupata pesa na mnaamua kukaa chini kupanga vipaumbele vya pesa yenu lakini cha ajabu mwenzi wako hataki kutanguliza kile cha muhimu, muda mwingine anaweza kukubali wazo lako lakini pesa inapofika mikononi mwake anafanya mambo mengine.

 

Zijue Faida na Hasara za Majibizano Katika Mapenzi.

Sidhani kama kuna ambaye hajawahi kujikuta kwenye majibizano na mpenzi wake. Hata wakati mnaingia katika mlipuko wa majibizano hata mnashindwa kujua sababu ya kujibizana kwenu.

Vitu kama vile mmoja kuchelewa kurudi nyumbani, kushindwa kuwasiliana sawa na mwingine alivyotarajia, kushindwa kutoa msaada pale ulipohitajika, hisia za kuwapo kwa mahusiano pembeni, tabia zisizoeleweka baina ya mmoja na simu yake ya mkononi au ndugu zenu kuingilia uhusiano wenu kwa namna yoyote ile.

Haya ni baadhi tu ya maeneo ambayo wengi wetu tumejikuta tunapishana kimaneno na wapenzi wetu. Mara nyingine inatokea mmepanga kwenda kula au kunywa nje ya nyumbani “outing” mnafika tu sehemu husika mkiwa mnasubiria chakula au mmeshaanza kula mara mmoja wenu anatoa neno moja linaloamsha majibizano makali na ghafla raha ya kuendelea kuketi na kula pale inaisha, mnaamua kukiacha chakula na kuondoka tena ikiwezekana kila mmoja kwa njia yake.

Najua kama ingekuwa tuko darasani nikasema wanyooshe mikono wale ambao hali kama hizi au zinazofanana na hizi zimewahi kuwatokea wengi wangenyoosha mikono.

Inabidi kuwa makini kwasababu kutofautiana katika maneno kunaweza kuwa na muendelezo bila hata ya nyie kugundua na baadaye kuwapeleka pabaya. Kwa mfano, wapenzi hawa wawili wanaanza taratibu katika maongezi yao “leo tunakula nini” mmoja anauliza, mara anajibiwa “kwanza kila ukimaliza kula unaacha vyombo mezani badala ya kunisaidia hata kuvisogeza wakati unajua tuko wawili tu?” Baada ya muda kupita na majibizano kama haya kuendelea, mmoja anaanza kuchoka na kumwambia mwenzake “mimi naona tunatofauti kubwa sana kwenye mambo ya majukumu ya hapa ndani na kwa jinsi hii sioni kama tutawezana bora kila mtu afuate ya kwake”.

Kukosa mazingira ya kutofautiana katika uhusiano kunaweza kuwa na madhara makubwa kuliko kuwa na mazingira ya kutofautiana, wenye kukosa kutofautiana kimaneno wanaweza kuwa na tabia kama ukatili wa kimyakimya, kununiana na kunyimana tendo la ndoa.

Tabia hizi zina madhara katika uhusiano. Kama mazingira ya kutofautiana yapo na ni dhahiri, kwa nini msitofautiane? Cha muhimu ni kuchagua kutofautiana kwa namna inayojenga na sio inayobomoa.

Zijue Sababu za Baadhi ya Wanawake Kuolewa Mapema.

Kuolewa ni moja ya jambo ambalo ni muhimu sana katika maisha hasa kwa mwanadamu aliekamilika, lakini unapozungumzia ndo unazungumzia mambo mengi hasa tabia, mapenz na masiah ya nyuma kwa jinsi ulivyolelewa kunaweza kukupelekea katika mapenzi.

Wengine wamekuywa wakikataa kuolewa kwa sababu tu ya maumivu waliowahi kuyapata katika mapenzi, lakini pia wengine hawaolewi kutokana na tabia ngumu za kibinadamu zinazowafanya washindwe kupata wenzi wenye kudumu nao mpaka kupelekea ndoa.

Lakini pia yapo mambo yanayoweza kuchangia kupata ndoa mapema , ingawa kama Mungu anapanga muda mufaka hata hizi sababu haziwezi kuwa kitu kwake.

Hana tamaa ya pesa

kwa jamii za sasa hivi wanawak wengi wamekuwa wakitanguliza pesa kuliko kitu kinhgine, hakuna asiependa pesa lakini iwe   kwa kiwango cha kusaidia katika mahusiano na isionekne kuwa mmoja yupo kwa ajili ya mwingine tu.

Awe anapenda Watoto.

sio lazima watoto wawe wa kwao, lakini angalia mara kwa mara anapokutana na watoto wa rafiki zake au hata mtaani, anaweza kuwa mtu wa kununulia zawadi watoto wa rafiki zake au jirani lakini pia pma hata maongezi yake  juu ya muonekano wa watoto anaokutana nao.

Heshima kwa kila mtu.

Jaribu kuangalia kam mwezi wake anaheshimu kila mtu, mtoto kwa mkubwa, mwenye nacho na yule asiekuwa nacho pia, mwenye kujari maisha ya wengine na kuonewa huruma wengine hata kama yeye hana kitu.

Anajishusha

Angalia, kuna wanawake wanapenda sana usawa kwa kila kitu na hapendi kuwa chini kwa lolote lile, katika ugomvi au hata mabishano na marafiki anaweza kutaka kuwa mshindi kila mara, huyo ni ngumu kuwa na mtu anaeweza kukaa nae katika mahusiano.

 

Kwa Wanawake ;-Fahamu Wanaume Unaopaswa Kuwaepuka

Kuna wanaume kuwa nao kwenye mahusiano wanaweza kukupotezea sana muda na, hakuna mwanaume mbaya hata siku moja na kwamba hakuna mtu mkamilifu katika mapenzi lakini inapofikia wakati inabidi  kutambua kuwa mwanaume uliyenae ni sahihi kwako au la.

kwa wanawake, sio kila mwanaume anaekufata na kukutongoza anakuwa anataka kuwa na wewe, unaweza kuwa na mwanaume na kudumu  nae katika mahusiano kwa muda mrefu lakini  kichwani  mwake anajua kuwa wewe sio mkewe na muda wake wa kuoa ukifika anakuachilia mbali.

Hivyo basi ebu jaribu kukaa mbali na watu hawa :-

Wanaume wapenda ngono.

Wapo wanaume wanaoamini kwamba hakuna upendo wa kweli bila kufanya mapenzi. Hili ni kundi ambalo kwa mantiki ya haraka hawana lengo la ndoa bali wanalenga kutimiza tamaa za mwili. Japokuwa wapo wanaojihusisha na ngono kabla ya ndoa na kufanikiwa kuoana, hilo halitakiwi kusifiwa au kupendekezwa kwa namna au sababu yoyote ile na jamii yetu.

Wanaume wapenda ngono wana mbinu kali za ushawishi, huanza taratibu kwa mambo madogo madogo, huonesha uaminifu mwanzoni lakini kwa namna ya masihara hujikuta wamekuangusha kwenye uzinzi. Watu wa namna hii wanajua kujali, hawajui kuonya ukikosea, ni wepesi kuitikia hitaji lako, anaweza kuahirisha kazi ili tu achati na wewe anapogundua u mpweke.

Wanaume “watoto

Wanaume ambao wanaanza mahusiano lakini wana akili za kitoto. Si ajabu kumkuta mwanaume ambaye hawezi kufanya maamuzi bila mchango wa wazazi wake. Ukiwa na mwanaume kama huyo ujue dakika yoyote atakapoambiwa we humfai utaachika bila sababu. Kifupi hawapendi kuzungumzia ndoa. Kuna tofauti kati ya wanaochelewa kuoa na wasiopenda ndoa, hapa nazungumzia wasiopenda kujadili kuhusu ndoa. Hukwepa kwa sababu kisaikolojia wao bado ni watoto.

Wanaume “wapenda ukamilifu”

Lugha nzuri tunaweza kuwaita “perfectionists” na sio vibaya ukawajumuisha na “judgementalists” kwenye kundi hili. Hawa ni wanaume ambao wanataka kila kitu kiende sawa sawa na kilivyopangwa.

Judgementalists ni wanaume wanaopenda kujudge kila kitu, yaani hakuna kitu utafanya wasiulize maswali. Hawajui kutia moyo, kusifia au kupongeza. Kuishi na wanaume wa namna hii ni lazima ujipange. Ni wepesi kubadili maamuzi bila kujali muda na rasilimali mlizotumia kwenye mahusiano yenu.

Wanaume wenye mtazamo hasi (Negative minded men).

Mara nyingi wanaume wanapenda wanawake wabadili tabia ili kuwafaa wanaume na sio kinyume chake. Sababu za kuwa na mtazamo hasi ni nyingi kutokana na mtu mmoja na mwingine. Wengine ni kwa sababu ya kutojiamini, wengine ni kutokana na mambo ambayo umewahi kumfanyia kwenye mahusiano yenu, wengine historia za maisha yao ya utotoni na wengine ni kwa sababu ya wivu uliopitiliza kwa hiyo anawaza kuibiwa tu na mengine mengi.

Wanaume wanaoigiza maisha (pretenders)

Hawa ni wanaume ambao hawajakubali hali zao za maisha. Kama ni maskini atataka aonekane tajiri. Akijuana na mtu maarufu basi na yeye anataka aonekane maarufu. Wanaume wa namna hii ukiwagundua hawaoni shida kuvunja mahusiano ili kuficha aibu yao.  Kifupi hawa ni wanaume ambao hawana mikakati thabiti ya maisha yao, hufuata upepo na mara nyingi hawana uwezo wa kweli wa kutunza familia.

 

 

Makosa Wanayoyafanya Wanaume Wakati wa Kutongoza.

Kuna vitu vinahitaji uangalifu mkubwa sana unapokuwa unafanya hasa katka swala la mahusiano,  wapo wanaokaa na kujiuliza kwanini kila anapojitahidi kumuingia mwanamke kwa ajili ya kuanza nae mahusiano inakuwa vigumu, lakini kumbe hajui kuwa kuna kitu anakosea na hawezi kufanikiwa mpaka aweze kukiweka sawa.

Basi haya ni baadhi ya mambo unayotakiwa kuyaacha pindi unapotaka kumu-win mwanamke kimahusiano ;-

  • KUMPONDA MWANAMKE WAKE ALIYEPITA
    Mwanamke anakuuliza kwanini uko single,unaanza kumponda ex wako kwa maneno ya kashfa hali kama hii inaweza kumtisha kisaikolojia umtongozae.
  • KULALAMIKA
    Unamtongoza mwanamke huku unalalamika juu ya mapenzi oooh mara sijawahi kupendwa mjomba hapo unaonyesha udhaifu wako.
  • PAPARA
    Wanaume wengi tumekuwa na haraka sana tunapokuwa tukitaka kuaproach hali inayomfanya mwanamke akuwekee ugumu.mfano umekutana na dada mzuri mmesalimiana hapo hapo unamuomba namba yake.mjomba hata akikupa ujue utasumbuka sana kumpata coz atakufikiria sana juu ya uharaka wako.
  • KUJIFAKE
    Wanaume wengi tumekuwa tukijipandisha au kujionyesha tofauti na hali zetu.ukiwa unaaproach jaribu kuwa real.huwezi kumwambia mdada unafanya kazi benki afu uko na techno
  • KUTOSOMA MOOD YA MWANAMKE
    unapomuaproach mwanamke lazma usome mood yake coz sometime unaweza kutoswa coz hujamsoma mwanamke unamtongozaje mwanamke asubuhi

Maswali Unayoweza Kumuuliza Mpenzi Wako Na Kujenga Mahusiano.

Hakuna mapenzi yenye raha kama yale ambayo  wowote wawili mnaweza kuwa marafiki na mkawa huru sana katika kusema kile unachokuwa unajisikia kwa mwenzako.Kuna maswali yanaweza kuwa ya ajabu au yanaweza kuwa ya kufurahisha na yenye kuchekesha sana lakini yanaweza kuwa ndio yanajenga sana mahusiano yenu .

Jaribu kutenga muda wa utani na maswali ya masihara kwa mwezi wako kama ;-

  • Unakumbuka nini cha utotoni ambacho uliwahi   kufanya?
  • kwenye hii tamthilia unampenda mwigizaji gani?
  • nafikiri nimepoteza namba yangu ya simu , naweza chukua ya kwako?
  • ni kipi kinachoweza kukufanya ucheke zaidi katika maisha yako?
  • .kwa mfano wewe ungekuwa muhudumu  ungechagua watu  wa jinsia gani wa kuwahudumia ?
  • umewahi kutuma maombi ya urafiki kwa rafiki wa kike?
  • kabla ya mimi umewahi kuwa na nani?
  • je unaweza kukosa kitu unachokipenda  kwa ajili yangu?
  • kama ukijikuta umeangukia kwa mwanamke , utaitumiaje hio siku wewe kama wewe?
  • wewe ni wangu?
  • unampenda nani?
  • unaamini kama kuna mungu?
  • unawezaje kumjua mtu kama ni rafiki wa kweli?
  • Unapenda kuwa smart au ni vyovyote tu?
  • je unweza kukaa na mtu usiempenda?

 

 

 

Tabia za Mwanamke Mhuni , Asiyetulia Katika Mahusiano.

Siyo rahisi kupenda

Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.

Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha

Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.

Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote

Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka. Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.

Ana marafiki wa kiume kwa manufaa

Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale. Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.

Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka

Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake. Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka

Mambo Wanawake Wanayotaka Katika Mapenzi Lakini Hawezi Kusema.

Mara nyingi wanawake wamekuwa watu wa kukaa kimya bila kusema wanataka nini ili kuridhishwa katika mapenzi na mbaya zaidi katika swala zima la mahaba, sasa basi kama wmwanaume inabidi kujua nini mwanamke wake anataka kabla ya tendo husika.

Mwanamke anapenda ufate anachotaka.

Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu. Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanya vile wanavyovipenda.

Hupendela tendo la ndoa lidumu muda mrefu.

Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda kuungana na wewe kihisia kupitia kushikana, kubusu nakadhalika. Wakati wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka. Kwa hiyo wanapenda tendo la ndoa lidumu lakini lisichoshe.

Usitumie nguvu katika mapenzi.

Wanawake wanataka wanaume walio jasiri wa kufanya nasio wanaotumia nguvu na ubabe. Wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu na mwisho kuwaumiza wapenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. Wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri kwamba sio kutumia nguvu na ubabe.
wanawake wengi hawafanani.
Wanawake wanapenda wanaume wajue kuwa sio wanawake wote hupenda vitu sawa. Wanaume wengine hufikiri kuwa kwa sababu mpenzi wake wa zamani alikua anapenda kufanyiwa alikuwa basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta njia ya kukukwepa. Kwa hiyo mwanamme anatakiwa amjue mpenzi wake kibinafsi yeye kama yeye na sio kumjua kwa kumfananisha na wanawake wengine. Mwanamme amfanyie mpenzi wake kama anavyopendelea na sio kama anavyofikiri wanawake wanapendelea.

Siri Ambazo Mwanamke Hawezi Kuzisema Anapokuwa Katika Mahusiano.

Idadi ya wapenzi wake wa zamani.

Ni vigumu sana mwanamke kukwambia idadi ya wapenzi wake wa zamani kwa sababu kitu hicho huwa kina mkera sana, ingawa wanaume wanapenda sana kuulizwa swali hilo.lakini jua kuwa kamwe hawezi kukwambia ukweli kuhusu swala hilo.anaweza kukujibu lakini ikawa ni uongo.

kasoro na mapungufu yako.

Mwanamke hawezi kuongea mapungufu yako kwa mtu yoyote hata kama ni rafiki yake, hata kama zinamkera kiasi gani ni vigumu sana kuweka wazi swala hilo.ni watu wanauwezo wa kuvumilia mambo mengi sana na ndio maana hata ikitokea mkagombana ni wanawake wachache sana huweza kufichua mabaya yako kwa sababu wao hawao hivyo.

Kukulinganisha na mpenzi wa zamani.

Wanawake wengi wana tabia ya kuwalinganisha wanaume zao na wale wa zamani, ingawa hawezi kukwambia waziwazi lakini mara nyingi ufanya hivyo na ikitokea una mapungufu mengi kuliko yule wa nyuma basi mahusiano yanaweza yasidumu sana.

Haumridhishi katika tendo la ndoa.

Sio rahisi mwanamke kulalamika kwamba hauko vizuri katika swala la tendo la ndoa, mara nyingi hukaa kimya wanavumilia , wanawake wengi wanahitaji muda sana kufika pale wanapopataka katika mapenzi tofauti na wanaume ambao wao kwao kila kitu huwa rahisi.Lakini usitegemee ataweza kukutamkia waziwazi na kama akiongea basi ujue amevumilia vya kutosha.

 

 

 

Ishara za Mwanamke Mwenye Hisia za Kimapenzi na Wewe.

Sio kila mara mwanaume anaweza kuwa wa kwanza kumpenda mwanamke, mara nyingine mwanamke  anaweza kuvutiwa sana na mwanaume lakini kawa hana njia rahisi ya kuweza kukwambia hisia zake kamili badala yake anakuwa na ishara  na matendo ya kukufanya ujue hali aliyonayo.

Inaweza kuwa ngumu sana kwa sababu hata matendo hayo yanweza kuwa ya siri sana na ya aibu sana muda miwngine , lakini unaweza kugundua baadhi kama;-

Hawezi kuzuia tabasamu muda wote.

mara nyingi mwanamke wa aina hii anapoongea na mwanaume anakuwa na aibu, lakini pia hawezi kujizuia kutabasamau mara kwa mara ingawa unaweza kugundua kuwa kama haukuwepo eneo husika naweza kuwa alikuwa akicheka kwa nguvu na pia alikuwa akiongea vizuri lakini ghafla ukifika na yeye nabadili sura ghafla.

Anakujali muda wote.

mwanamke anapokuwa na hisia na wewe anataka kukujali na kujua shda zako muda wote, kwa mafno kama mmekuwa mkishindwa mahali pamoja muda mwingi atataka kujua kula yako, anaweza hata kutaka kukuletea chakula mara nyingine.kama ni kwenye simu hashindwi kukuuliza kila inapofika muda wa kula, lakini pia atataka kujua wanini umenuna au kwa nini unaonekana hauko sawa.

Ishara za mwili wake.

kuna muda anaweza kutumia hata mwili wake kukufanyai madoido ya hapa na pale ili tu kukuonyesha kitu, mara nyingi anapojua kuwa mahali unapoenda upo basi pia mavazi yake yanaweza kuwa ya mitego mitego sana.angala tembea yake mbele yako, na jinsi anavyokaa na kujiweka ukiwepo unaweza kugundua kitu.

Anatafuta ukaribu.

Msichana mwenye hisia na wewe haogopi kujitenga mbali na wewe hata kama mko wengi, mara nyingi anataka muwe pamoja na kufanya vitu vingi pamoja , mfano kama mko kundi la washkaji wengi basi anaweza kutafuta sababu tu kuwa karibu na wewe lakini sio wale wengine.

Anaibia kukuchunguza.

kuna muda unaweza hata usijuae kama kuna kitu anafanya mkiwa wote, anaweza kuwa akikuangalia sana kila moves bila wewe kujua  na hata akiona unageuka basi anajifanya kama hakuwa anaangalia kwako.Muda mwingine anaweza kutaka kujua unachati na nani au unaongea na nani kwenye simu au kwanini uko karibu na msichana fulani lakini ukiraka kujua kwanini anafanya hivyo hawezi kuwa muwazi zaidi.

Ajali za kujitakia muda wote.

kila mara anawea kutafuta sabau ya kutaka mshikane au muwe karibu, hapa anaweza kuona kitu kidogo na akajifanya kuogopa tu ili umsaidie au umshike  au akukumbatie.

Atatafuta njia ya kupata Attention yako.

kuna muda anaweza kulalamika kitu ambacho kwa uelewa wako wa kawaida unaona kabisa kuwa haikuwa na sababu ya kulalamika, atakwabia kwanini ufanyi hivi kwake au hivi na hii mara nyingi utokea katika mawsiliano ya simu, kwanini nimekutumia sms haujajibu , au mbona nimepiga haujapokea, ulokuwa wapi, unafanya nini , ukiona hivyo basi ujue kuna kitu kinaendelea katika akili ya mwanamke huyo.

ANGALIZO. Endapo mwanamke anakuwa amejitahidi kukuonyesha njia zote za kuwa katika mahusiano na wewe na bado usiweze kuelewa swala hilo, na mahusiano kati yenu yakashindikana, mara nyingi wanawake hao huwachukia wanaume wanaokuwa wamepata nao CRUSHES, hii utokea kwa watu wengi na baada  ya hapo anakuwa kama mwenye hasira na wewe.

 

Kwanini Wanaume Wengi Wanaongoza kwa Kusaliti.

Ni ukweli mchungu ambao ni lazima tujadiliane kuhusu namna ya kuukomesha. Utafiti usio rasmi, unaonesha kwamba japokuwa wanawake na wanaume wote wanasaliti, lakini idadi ya wanaume wanaosaliti ni kubwa zaidi kuliko wanawake.

Kabla ya kujua sababu hizo, ni vizuri ieleweke kwamba katika kila usaliti unaotokea, kuna mambo mawili yaliyosababisha; matatizo katika uhusiano wa kimapenzi au matatizo ya mtu binafsi.

Kama tunakubaliana katika hilo, hebu kila mmoja ajiulize, kwa nini wanaume wanaongoza kwa usaliti? Kwa nini wanaume wanawasaliti wake zao? Wanawake ambao wanafanya kila kitu kwa ajili yao?

TENDO LA NDOA

Sababu kubwa inayofanya wanaume kuchepuka, ni kukidhi tamaa zao za kimwili. Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa masuala ya kimapenzi, Dk Tamy Wilson wa nchini Marekani, unaonesha kwamba wanaume ambao wanatimiziwa haja zao za kimwili mara kwa mara bila vikwazo, wana nafasi ndogo ya kusaliti ukilinganisha na wale wanaopata haki ya ndoa kwa ‘mbinde’. Kwa jinsi miili ya wanaume ilivyoumbwa, kadiri mtu anavyokaa muda mrefu bila kushiriki tendo, ndivyo tamaa za kimwili zinavyo ongezeka na kama akishindwa kuwa makini, anaweza hata kutembea na hausigeli ‘mchafu’ wakati ndani anaishi na mke mrembo mwenye sifa zote.

TABIA MBAYA

Ukiachana na wale ambao wanasaliti kwa sababu hawana jinsi, lipo kundi lingine la wanaume ambao kihulka wana tabia mbaya tu! Atapewa kila anachokihitaji kwa mkewe, atahudumiwa kimwili, kiakili na kihisia lakini kwa sababu ana tabia ya kupenda kudanganya, kufanya mambo kwa siri na kukosa uaminifu, atasaliti tu.

Watu wa namna hii wanakuwa na matatizo ya kisaikolojia na mara nyingi, huwa hawadumu katika uhusiano hata mwanamke awe mvumilivu kiasi gani.

KUKOSA KUJIAMINI

Sababu nyingine inayofanya wanaume wawe na tabia ya kusaliti mara kwa mara, ni kukosa kujiamini.

Anaishi na mke au mpenzi mwenye sifa zote nzuri lakini moyoni mwake hajiamini, anahisi ipo siku mwanamke atamkimbia na kwenda kwa wengine, kwa hiyo kukitokea ugomvi kidogo ndani, anakimbilia kutafuta mwanamke wa pembeni akijidanganya kwamba hata mkewe akimkimbia, atakuwepo wa kumfariji.

Yupo tayari hata kumpangia nyumba mchepuko ilimradi tu awe na sehemu ya kukimbilia inapotokea ameachana na mkewe.

 

 

Namna ya Kuishi na Mpenzi Anaependa Pesa

Mahusiano mengi yamekuwa  yakivunjika kutokana na watu wengi kukosa kile walichokuwa wakikitegemea katika mahusiano hayo, wasichana  wengi walikuwa wakipenda kuwa na mahusiano na wanaume wenye pesa laki ni sasa hii sio upande mmoja tena bali hata wanaume wanapenda sana kuwa na mhausiano na wanawake wenye pesa na kazi nzuri ili isiwe shida kuhudumian na ikibidi hata mwanaume kuwa anamtumia mwanamke huyo kamachanzo chake cha mapato.

Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.”

Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.

Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia.

Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili.

Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah.

Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone.

MWELEZE UKWELI
Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile.
Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

JENGENI KUSAIDIANA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake.
Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi.

ACHA UFUJALI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!

Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

BAKI NA HILI
Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.

Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.

 

 

 

Sababu za Wanaume Kupenda Wake za Watu.

Kumekuwa na tabia ya wanaume wengi kutaka kuingia katika mapenzi  na wanawake mambo tayari wameshaolewa na hivyo hivyo kwa mabinti kutaka kuwa  na mahusiano na wanaume za watu bila kuogopa kuwa kitu hicho kinaharibu mahusiano ya ndoa ya watu hao au kuvunja familia kabisa.

Kwa bahati mbaya zaidi  kwa maisha ya sasa hivi kuhusu mahusiano unaweza kukutana  na mwanamke naye licha ya kwamba ameolewa lakini naye anajihisi kumpenda mwanaume huyo na  sababu kubwa huwa ni kwamba anakuwa  hapati kile ambacho alikitarajia kwenye ndoa yake. Na hi uwaweka wengi katika njia panda, lakini sababu kubwa ya watu kutembea na watu waliopo katika ndoa huwani :-.

PENZI LA DHATI

Baadhi ya wanaume si kwamba wanaonyesha kuwa wao hawajatulia kwa kuwatokea wake za watu. Baadhi yao penzi la dhati walilonalo dhidi ya wale ambao wameshaingia kwenye ndoa ndilo huwasukuma kufanya hivyo.

Wanachokifanya wao ni kueleza hisia zao bila kujali kuwa, mlengwa ana mtu au laa. Ndiyo maana mtu huyo anaweza kuwa anajua ukweli kwamba fulani ni mke wa mtu lakini kwa kuwa anaamini huyo ndiye wake, analazimika kujaribu zali.

Siyo dhambi kueleza hisia zako lakini ndugu yangu kama unajua kabisa huyo uliyempenda yuko ndani ya ndoa yake au ana mpenzi wake, pambana na hisia zako. Jizuie kwani kumpa usumbufu mke wa mtu ni kujitafutia matatizo bure.

HAKUNA GHARAMA

Baadhi ya wanaume wanawatokea wake za watu kwa kuwa hawatapata usumbufu wa pesa za matumizi, vocha, mavazi na vitu vingine. Wao wanaamini watakuwa wanatoa penzi tu lakini mambo mengine mwenye mke atahudumia.

Lakini wengine wanataka kuanzisha uhusiano na wake za watu kimaslahi. Kwamba mwanaume anaweza kuona mwanamke flani ameolewa na mwanaume mwenye nazo lakini mke anaonekana kutopata penzi analolihitaji. Yeye anatupa ndoano, akiamini akimridhisha kimapenzi, atakuwa anahongwa yeye na maisha yake yatakuwa poa.

Tahadhari. Kama unatokea kumpenda mke wa mtu ili umchune au ili kukwepa kugharamia, tamaa yako hiyo itakuponza. Acha utegemezi, mwanaume aliyekamilika ni yule mwenye uwezo wa kumtunza mtu anayempenda, usikimbie majukumu na kutaka vya mteremko. Kumbuka wengi walioingia kwenye uhusiano na wake za watu kwa tamaa za pesa na mali, yamewakuta makubwa.

USUMBUFU HAKUNA

Kuna wanaume ambao hawapendi kusumbuliwa kwa mambo ya wivuwivu na wapenzi wao, mara nyingi mwanaume anapoanzisha uhusiano na mtu ambaye ana mtu wake anahisi hatasumbuliwa.

Yale mambo ya; ‘uko wapi baby’, uko na nani, nataka tuonane leo’ yanakuwa si kwa kiwango kile ambacho kinakuwepo kwa mtu ambaye hana mtu.

HAKUNA KUGANDANA

Wapo wanaume ambao wao wanataka kila mwanamke mzuri bila kujali ameolewa au yuko singo. Lakini pia wapo ambao hawataki kuingia kwenye uhusiano na mwanamke ambaye atagusia future. Kwa kifupi wanaume wa staili hii wanaamini wakiwa na wake za watu, hawawezi kugandwa wala kuulizwa juu ya ‘future’.

SIFA TU

Wapo wanaume ambao wakitembea na mke wa mtu wanaona sifa sana. Akimtongoza mke wa mtu, akakubaliwa, roho yake inakuwa fresh. Na wengine hawawezi kubaki na siri, kila atakayekutana naye atamwambia; ‘yule mbona nishampitia’.

Hiyo yote sifa. Mtu yuko tayari kutumia gharama yoyote ili mradi atembee na mke/ mpenzi wa mtu, aandike historia kwamba fulani licha ya kwamba ni mke wa mtu lakini ameshatembea naye