Mange Kimambi na Hamisa Uso kwa Uso Marekani.

Safari ya mwanadada Hamisa Mobeto nchini marekani iekuwa moja ya safari zenye faida kwake kutokana na kukutana na watu mbalimbali ambao kwake wameweza kuwa faraja na wenye kuleta mafanikio kwake.

Kwanza kabisa baada ya kufanya show mbalimbali Hamisa alianza kwa kutuonyesha mpenzi wake mpya ambae wamekutana kwa mara ya kwanza wakiwa marekani na hata kutuhakikishia kuwa huyo ndi mpenzi wake lakini sasa mwanadada huyo amekutana n mwanamashughuli na mwanaharakati mkubwa kutoka Marekani mwanadada Mange kimambi.

Mange ni moja ya wanaharakati wanaotetea sana  wasanii na watu mbalimbali ambao wanaonekena kutokuwa na sauti ya kudai haki zao.

Wawili hao ambao hawakuwahi kuonana , wameonekana kuwa na furaha baada ya kuonana siku ya jana.

Baada ya Kusemwa Kuhusu Daimond, Mange Amtetea Hamisa

Mwanadada Mange kimambi amefunguka na kumtetea hamisa  kutokana na mashambulio ambayo amekuwa akitapokea katika kurasa za instagram kuhusu Hamisa kuwa na mapenzi na Diamond kwa siri na kwamba Diamond amekuwa akimtumia hamisa tu kwa starehe lakini hana mapenzi nae yoyote ,

Mange anawashangaa watu wanaomwambia Hamisa kuwa kama Diamond angekuwa anapenda basi amekuwa akimuweka katika kurasa zak za mitandao ya kijamii lakini kwa sababu hampendi na ndioa maana hana anachomfanyia hadharani,huku kwa maoni ya mange anammwambai hamisa kuwa wengi waliokuwa wakiwekwa katika mitandao wameishia kuumizwa na mwanaume huyo.

Hata hivyo Mange anamshauri hamisa kuwa kama kuna kitu ambacho amekuwa akimpa Diamond basi azidishe kumpa ili amjengee hadi nyumba.

Mange anamwambia Hamisa kuwa kama waliweza kuwa katika mahusiano na Diamond mpaka wakafikai hatua ya kuzaaa mtoto basi aendelee kutokisikiliza maneno ya watu kwa sababu hata hao watu wanaompa manno bado na wao ya kwao yanawanshinda.