Johari Amtaka Hamisa Aachane na Diamond

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Blandina Chagula maarufu kama Johari amempa somo mrembo Hamisa Mobetto kwa kumtaka aachane na Baba watoto wake Diamond Platnumz.

Johari amefunguka na kudai kuwa ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na staa hivyo anajua ni jinsi gani walivyo pasua kichwa hivyo anamshauri Mobetto aachane na Diamond.

Kwenye mahojiano  na Global Publishers, Johari amemtaka  Mobeto, asirudi kwa Diamond, bali angeendelea na maisha mengine maana kurudi ni kuambulia maumivu tu, hakuna cha maana zaidi.

Ningekuwa nimepata nafasi ya kumshauri Mobeto, ningemwambia asimrudie Diamond, lakini ndiyo hivyo nilisikia wako pamoja tena, ninachoweza kumwambia ni awe makini tu maana penzi na staa linaumiza sana. Kwani ni watu ambao hawatulii, atajikuta anajipotezea muda na baadaye kuja kujuta.

Nimewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na staa, uliniumiza sana na ndiyo maana nampa somo Mobeto kuwa makini sana ili kukwepa kuumiza moyo wake na kupoteza muda”.

Johari alishawahi kuwa na uhusiano wa muda mrefu na staa wa Bongo movie Ray Kigosi lakini walikuja kuachana na Ray kuzaa na Chuchu Hansy.

Hamisa Mobetto Ajibu Tuhuma Za Kuazima Nguo

Mwanamitindo na Muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto amejibu tuhuma alizotupiwa wiki iliyopita kuwa ameazima nguo za mtu na kudanganya za kwake.

Sakata hilo lilianza wik iliyopita baada ya Mobetto kuposti nguo aliyovaa Sarah mpenzi wa Harmonize na kusema imetoka kwake jambo ambalo sio la kweli kwani nguo hiyo iliyengenezwa na mwanadada mwingine anayejiita Ab Desgners ambaye alimwandikia ujumbe mwanamitindo huyo kuwa awe mkweli.

Baada ya maneno kuzuka Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimsaka mwanadada anayeitwa Aliyah ambaye alidai ndio mmiliki halali ambaye alifunguka:

Ni kweli nguo ni zangu kwani Mobeto alikuja kwangu na kunieleza kuwa anataka achukue nguo zangu avae alafu atasema zimetoka kwake ili anitangazie biashara, na kusema kwamba akipata wateja aniletee, mimi nilikataa, nikasema kama anachukua nguo anitangazie kwa jina langu la sivyo nimuazime tu arudishe”.

Baada ya Tuhuma hizo Hamisa alifunguka  na kudai kuwa habari hizo ni za uongo na kilichotokea ni kutoelewana tu:

Jamani mimi nilishaeleza sana na hata nilipoweka kwenye mitandao niliandika kuwa nguo hizo zimebuniwa na yeye sasa mimi nashangaa watu wananichafua kwenye mitandao“.

 

Aunty Ezekiel: Sioni Tatizo Kuvaa Nguo Niliyoshonewa na Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu zito watu wote waliomkoso kwa kuvaa nguo aliyoshonewa na Mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Siku ya uzinduzi wa filamu yake fupi ya Mama Aunty alivaa nguo nzuri nyekundu na kupendeza kupita kiasi ambapo baadae aliweka wazi kuwa aliyemshonea nguo ile ni Hamisa.

Mashabiki wengi walimjia juu Aunty kwa kuvaa nguo ya Hamisa huku akijua wazi yule ni adui namba moja wa Zari na pia adui wa shoga yake Wema Sepetu.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Amani, Aunty amekiri kutowaelewa wanaoshangaa ishu hiyo kwa sababu yeye na Mobeto hawana ugomvi wowote na wala hajawahi kukosana naye, sasa kitakachomfanya ashindwe kuvaa nguo aliyomshonea ni kitu gani?.

Mimi ninawashangaa sana wanaoongea kuhusiana na kuvaa nguo ambayo nimeshonewa na Hamisa. Sioni tatizo kwani tofauti zake na mtu mwingine mimi hazinihusu“.

Mashabiki ambao ni Team Zari wamekuwa wakimtolea maneno Aunty kwa usaliti aliofanya kwa Zari kwani wengi waliamini kuwa ni rafiki yake lakini kama utakumbuka siku za nyuma Aunty alishasema kuwa hana urafiki na Zari wala Hamisa.

Hatimaye Diamond Amuweka Mtoto Wake na Hamisa Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayefanya vizuri na kibao chake cha kwangwaru ametengeneza gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ya mtoto wake na Hamisa.

Hatimaye kwa mara ya kwanza Diamond ameposti picha ya kwanza ya mtoto wake Dylan ambaye amezaa na Hamisa.

Tangu Dylan azaliwe kulikuwa na mgogoro kati ya Diamond na Hamisa hii ilitokana na Hamisa kuanika video na picha zao za faragha Wakati huo Diamond alikuwepo na Ex wake Zari.

Tangu hapo kilichofuata kilikuwa ni kurushiana vijembe Mtandaoni na kupelekana mahakamani na hata Hamisa alisema kuwa Diamond alikuwa hataki kumuona mwanaye na hata kumuhudumia.

Lakini tangu taarifa za Diamond na Hamisa kurudiana zienee inaelekea mambo yamekuwa tofauti kwani Diamond amesemekana hata kumuona mtoto wake na hata jana kwa mara ya kwanza aliweza kumposti mtoto wake Kwenye ukurasa wake wa Snapchat:

 

Hamisa Mobetto Awajia Juu Watu Wanaombeza Kisa Amezaa na Wanaume Wenye Hela

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Haida Mobetto amewajia juu watu wanaombeza baada ya kusema kuwa yeye sio Single mothers.

Siku ya juzi ilikuwa ni Mother’s Day/ siku ya Mama duniani na Hamisa aliweka wazi kuwa yeye sio Single mother kwa sababu anasaidiwa kulea watoto wake na Baba watoto wake.

Hamisa ana watoto wawili ambapo mtoto wake wa kwanza Fantansy amezaa na Majizzo na mtoto wake wa pili Dylan amezaaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Lakini baada ya video hiyo kuingia mtandaoni watu walianza kumsema vibaya kutokana na yeye kuongelea suala lake la kuzaa na wanaume wawili tofauti ambao wote ameweka wazi wana uwezo.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa altoa povu hili:

Mnatakiwa mjua kwamba Fancy na Dee Mungu ndo alipanga wazazi wa hawa watoto wawe nani..hasira zenu please msinimalizie mie mtoto wa marehemu Mzee hassan..Its getting boring now.”

 

 

 

 

Wema: Hamisa ni Mdogo Wangu Lakini Mazoea Yamezidi

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuongelea uhusiano wake na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto huku akidai kuwa ni mdogo wake ila mazoea yalizidi hivyo aliamua kumuweka kando.

Siku za nyuma Wema na Hamisa walikuwa marafiki sana kwa miaka mingi na hata ni mara nyingi Hamisa amekuwa akisikika akimuita Wema dada yake.

Lakini urafiki huo uliingia shubiti siku za nyuma baada ya Wema kutaka kumtumia watu wampe kichambo Hamisa na hata kudai sababu ya wawili hao kutofautiana ni baada ya kumsikia Hamisa akimsema maneno mabaya.

Kwenye Interview yake na Global Tv, Wema amefunguka kuwa Hamisa ni mdogo wake lakini alizidisha sana mazoea hivyo ilibidi amuweke kando ili heshima iwepo:

Mimi hamisa ni kama mdogo wangu, hivyo yaani waga nasema kila siku Lakini sometimes mazoea yakizidi sana sijui huwa inaleta mushkeri kwaiyo inabidi kila mtu abaki kwenye mipaka yake ili ajue hapa natakiwa nipitilize au hapa nisipitilize”.

Watu wengi walihusisha Wema kugombana na Hamisa na Diamond lakini Wema aliweka wazi kuwa aligombana na Hamisa kwa sababu alimsikia anamsema vibaya kwa watu.

Tunda- Sina Bifu na Hamisa

Video vixen maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Tunda Sebastian ameibuka na kuweka wazi kuwa hana bifu lolote na Hamisa Mobetto na wala hajawahi kugombana naye.

Tunda na Hamisa walisemekana lies Kwenye bifu zito siku za nyuma na ikidaiwa kisa kilikuwa ni penzi la staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Inajulikana wazi kuwa Hamisa ana uhusiano na Diamond na hata kuzaa naye mtoto mmoja lakini hapo nyuma ilishasemekana kuwa Tunda alikuwa ana uhusiano na Diamond kwa muda mrefu.

Kuwepo kwa bifu hilo kulithibitika baada ya Tunda kutumia mtandao wa kijamii kumfikishia Ujumbe Hamisa Miezi kadhaa iliyopita na kusema kuwa Diamond hamtaki lakini anajipendekeza.

Lakini pia siku zilizopita Tunda alimpiga Dongo Zito Hamisa baada ya kusikia karudisha majeshi kwa Diamond ambapo alidai ni mjinga kwa kurudiana na Diamond.

Siku ya juzi Tunda kawatolea povu zito watu walioandika stori kuwa yeye na Hamisa wana bifu ambapo amedai kuwa hana ugomvi wowote na Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tunda aliandika ujumbe huu huku akisisitiza kuwa hana bifu na Hamisa:

Hamisa hajawahi kujibu tuhuma zozote na Tunda na hata kumrushia maneno Kwenye mitandao ya kijamii.

“Hamisa Aliniongelea Maneno Mabaya, Sio Rafiki Yangu”- Wema

Staa wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka kuhusu uhusiano wake na Baby mama wa Diamond, Hamisa Mobetto na kusema hana bifu naye lakini pia sio rafiki yake.

Kama utakumbuka siku za nyuma Wema na Hamisa walikuwa vizuri tu Tena walikuwa marafiki wakubwa lakini Ghafla kuna taarifa zilienea kuwa Wema anataka kukodi watu wakumchamba Hamisa.

Lakini pia ilisemekana chuki ya ghafla kutoka kwa Wema kwenda Hamisa ilitokana na taarifa zikivyosambaa kuwa Diamond alikuwa anachepuka na Hamisa kipindi chote alivyokuwa na Mahusiano na Wema.

Wema amewafungukia Global Publishers, Ijumaa Wikienda na kusema yeye hana bifu na Hamisa ila alimchukia pale aliposikia anamuongelea vibaya kwa watu hapo ndio urafiki wao uliishia:

Sina bifu na Hamisa ila siyo rafiki yangu kabisa kwani kuna maneno aliniongelea mabaya sana, tena siyo kwa kuambiwa, kwa kusikiliza sauti, sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda wake na hata tukikutana kila mtu na hamsini zake“.

Wema alipoulizwa kuhusu Zari aliweka wazi kuwa hana tatizo na Zari Tena anampenda.

Hamisa Mobetto na Lulu Diva Kupamba Steji Moja Nchini Uingereza

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Amezoea’ Lulu Diva atapanda steji moja Hamisa Mobetto katika uzinduzi wa Lipstick zake nchini Uingereza.

Mzazi mwenza wa staa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamusa Mobetto anatarajia kuzindua rasmi lipstick zake zinazojulikana Kama “Charmed Cosmetic”.

Kwenye uzinduzi huo utakaofanyika tarehe 5 Mei 2018, utasindikizwa na burudani toka kwa Lulu Diva ambaye ametoa wimbo wake mpya hivi karibuni unaoenda kwa jina la Huba.

Hamisa alitangaza habari hiyo njema kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliandika:

 

United Kingdom get ready. Business marketing my charmed cosmetics lipstick launch coming soon. Live performance by the sexy Lulu Diva. We come for serious business”.

 

“Haters Wanazidi Kunipa Umaarufu na Kuniongezea Dili za Pesa” -Hamisa

Mwanamitindo na Muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto amewatolea povu zito wale wote wanaomsema vibaya na  kumponda kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mwananchi Communication Limited Hamisa amefunguka na kusema anawashangaa zaidi haters ambao wamekuwa na kazi ya kumchafua kila siku hasa wale wanampachika majina mapya kila siku.

Hamisa amedai hivi sasa ameshayazoea majina yote anayopewa na mashabiki Kwenye Instagram kwani ameona hayampunguzii kitu katika maisha yake labda cha zaidi yanamuongezea umaarufu unaozidi kumpa deals mbali mbali za kuingiza pesa.

Kutokana na bifu mbali mbali za mtandaoni na mashabiki kugawanyika kimakundi huunda timu zao binafsi kama Teamwema, Teamzari na teamMobetto. Ambapo Hamisa amepewa majina mbalimbali kama Tununu, laki mbili, ruba hata mbu.

Baada ya kuzaa na Diamond Hamisa alipata haters wengi ambao walimtunga majina mbali mbali na kumsema vibaya ambapo amesema vimemsaidia kumpa mafanikio kwani hivi sasa ana mafanikio mengi ikiwemo kuwa balozi wa website ya Mzuri ya Kenya na hata kufanya Safari nchi mbali mbali kama Dubai, South Africa, na hata Uganda kwa kazi.

“Unajiona Mzuri na Mdogo Lakini Huwezi Kupata Mwanaume Wako” Zari Amrushia Hamisa Dongo

Mfanyabiashara na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi tena kwenye headlines baada ya kumua kufumua bifu lake na baby mama mwingine wa Diamond, Hamisa Mobetto.

Inaelekea bifu la wazazi wenza wa Diamond  limerudi upyaaa kwani Zari kaamua kulianzisha tena baada ya kimya kirefu juu ya suala hilo na tofauti tulivyodhani kuwa huenda wamemaliza tofauti zao kama ambavyo Diamond na Hamisa walivyomaliza mahakamani.

Siku ya jana Zari kutumia mtandao wa SnapChat alimrushia Hamisa madongo upya kama ilivyokuwa siku za nyuma ambapo ameongelea kuhusu suala la Hamisa kuzaa na Diamond na pia taarifa za Hamisa kuchumbiwa na Diamond.

Siku za nyumba Hamisa ameshawahi kudokeza kuwa aliwahi kuchumbiwa au kuvalishwa Pete ya uchumba na Diamond na hata kuna taarifa zilienea kuwa huenda Diamond na Hamisa walifunga ndoa habari ambazo hazijawahi kuthibitishwa.

Mzuri, Mdogo lakini pamoja na hayo yote huwezi kupata mwanaume wa peke yako…..Eti amekuvalisha pete ya uchumba lakini hajawahi kukubali wala kukukubali hadharani! Dada jiangalie sana ….Anafanya Interview redioni eti mwenye mimba atoke blah blah”.

 

Lakini ni pia Zari ametangaza ujio wa kipindi chake kitakachoonyesha maisha yake halisia (reality show)  kitakachoitwa Life of Zarithebosslady ambacho mashabiki wake watapata kuona kila kitu kuhusu maisha yake.

 

Hamisa Mobetto Amefungukia Sababu Inayomfanya Asisherekee Valentines Day

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto amefunguka na kueleza sababu inayompelekea mpaka asiweze kusheherekea siku hii ya Valentine’s Day.

Ikiwa leo ni siku ya Wapendanao duniani ambako inasheherekewa na dunia nzima na watu wote ambapo wanaonyeshana upendo na wapendanao ambapo wanapeana kadi, maua, na Zawadi nyingine nyingi.

Lakini siku ya leo sio nzuri sana kwa baadhi ya watu ambapo mmoja kati ya watu hao ni Hamisa Mobetto ambapo amekiri kuwa hawezi kusheherekea siku ya leo kama watu wengine wengi kwa sababu ni siku ambayo inamkumbusha machungu mengi kwani ni kama siku ya leo ambayo alimpoteza Baba yake mzazi.

Hamisa amekiri kuwa siku ya leo kila mwaka wakati watu wanasherekea na pilika pilika nyingine yeye hawa katika wakati mgumu sana kwani siku za nyuma alikuwa a napenda kusheherekea lakini siku hii iligeuka Chungu baada ya kumpoteza Baba yake mzazi tarehe 14 mwezi wa pili.

 

“Sina Mpango wa Kuolewa Ndio Maana Nimezaa Nje ya Ndoa Mapema”- Hamisa

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto ambaye pia ni ‘babymama’ au mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz Amefunguka na kukiri kuwa hajafikiria na wala hana mpango wa kuolewa kwa hivi sasa.

Hamisa ambaye alikamata headlines mwaka jana kwa kuwa mchepuko wa Diamond kwa miaka Tisa na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume anayeitwa Dylan. Lakini tangu aseme ukweli kuhusu mahusiano yake na Diamond wamekuwa hawana maelewano mpaka jana walipopatanishwa mahakamani.

Hamisa ana umri wa miaka 24 lakini katika umri wake mdogo amejaliwa kupata watoto wawili ambao mmoja ndio Dylan aliyezaa na Diamond na mwingine ni Fantansy aliyezaa na mkurugenzi wa Efm Majey au Majizzo.

Siku ya jana Hamisa alipokuwa anatoka mahakamani kusikiliza kesi ya madai ya malezi ya mtoto aliyemfungulia mzazi mwenzake Diamond katika mahakama ya watoto Kisutu alifunguka na kusema hana mpango wa kuolewa tena na yeye ni mtu ambaye haamini katika ndoa.

Kusema kweli sina mpango wa kuolewa any time soon yaani kabisa kabisa am not ready siko tayari kufunga ndoa kabisa kwa hivi sasa lambda ikitokea mbeleni huwezi jua lakini mimi ni moja kati ya wale watu ambao hawaamini kuhusu kufunga ndoa ndio maana unaniona nimezaa watoto nje ya ndoa mapema kabisa”.

 

Zari na Hamisa Wajibu Tuhuma za Kupata Umaarufu Kupitia Kuzaa na Diamond

Wazazi wenza wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Mfanyabiashara Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ na muigizaji Hamisa Mobetto wameongelea tuhuma walizorushiwa kuwa wanapata umaarufu zaidi kupitia kuzaa na Diamond.

Hamisa na Zari wana ufanano wa kitu kimoja tu nacho ni kuwa wote wamezaa na Diamond lakini zaidi ya hapo ni maadui wakubwa kupita kiasi hilo lilidhihirika mwezi uliopita pale wote walipokuwa na shoo nchini Uganda ambapo waliishia kurushiana maneno ya kashfa mtandaoni hadi kufikia hatua ya kutukanana.

Diamond ni msanii mkubwa sana sio tu Tanzania bali hata nje ya Tanzania kwenye nchi nyingi za Africa hata nje ya bara la Africa kumekuwa na maneno mengi yanayosemwa huku watu wakidai kuwa warembo hawa wanafurahia hizi kiki za kuwa na Diamond kwani na wao wanapata umaarufu wakujulikana.

Kuna maneno yamekuwa yanasemwa kuwa Zari yupo na Diamond sio kwa ajili ya pesa bali ya umaarufu kwani inasemekana kuwa anapenda sana fame na kiki.

Zari ali[ohojiwa na Millard Ayo Tv alifunguka kuhusu tuhuma hizo kama ifuatavyo;

Naweza kusem ndiyo na hapana, ndiyo kwa sababu sahivi tumekuwa couple yenye nguvu (power couple) watu wanapenda kutuongelea sana na vitu kama hivyo hata hivyo kabla kulikuwa kuna watu walikuwa wanamjua Diamond mimi hawanijua na kuna watu walikuwa wananijua mimi na Diamond hawamjui kwaiyo nahisi tumesaidiana kujulikana”.

Hamisa naye alifunguka tuhuma hizo kwani tangu amezaa na Diamond amekuwa akisafiri nchi kama Kenya, Uganda, na Nigeria, Dubai kwenda kufanya shughuli mbali mbali:

Habari hiyo ni ya kweli kwani Diamond ni mwanamuziki mkubwa lakini mwanzo nilivyokuwa na mimba nilikuwa sijui nini kitatokea lakini tangia hapo sijapata jina kubwa tu au umaarufu lakini pia changamoto ambazo zinanilazimisha nipambane maana maisha nayo magumu”.

 

Zari Kwa Hamisa “Ulijua Kuwa Diamond Ana Familia Lakini Bado Ulimpanulia Miguu Yako”.

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ameendelea kutawala tena headlines baada ya bifu lake na Hamisa kuendelea kupamba moto mtandaoni.

Hamisa na Zari waliingia vitani wiki iliyopita baada ya kukutana nchini Uganda ambapo kila mmoja alikuwa ameenda kuhost party. Tangu wiki iliyopita wawili hao wameendelea kirushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya jana kupitia mtandao wake wa snapchat Zari amemrushia dongo jingine Hamisa huku akimtaka aachane na Diamond kwani wameshasamehana na wanapendana sana:

Ulijua wazi kabisa kuwa alikuwa ni mwanaume wa mtu  na ana familia na watoto lakini bado ukaenda kumpanulia miguu yako na kuzaa naye unafikiri hilo gundu litanipata mimi? Kwa kipi nilichofanya hilo linakurudia mwenyewe. Ukitaka rusha picha video zote za zamani hamna shida sisi tumesha sameheana tumesahau ya nyuma sahivi tunaangalia mbele  ule uchawi wote uliokuwa unamwekea unaisha sahivi amerudi katika akili zake za kawaida. Eti unajiita mtoto mdogo mimi nauzee wangu ndo namridhisha na kanikubali. Mpaka sahivi una watoto wawilo kila mmoja na baba yake hivi ukifikisha umri kama wangu utakuwa na watoto wangapi na kila baba wa mtoto anakukataa? Kwa nini unamng’ang’ania  Baba Tigfah na Nillan kwa nini sio Baba Fancy? Una wazimu”.

Zari ameendelea kumpa madongo Hamisa kwenye mitandao ya kijamii huku akimuonyesha kuwa yuko na Diamond nchini South Africa ambapo wanakula bata.

Mimi na Hamisa sio Marafiki- Zari

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz Zari the Bosslady ‘Zarinah’ amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na hasimu wake namba moja Hamisa sio marafiki na wala hawawezi kuwa marafiki.

Warembo wao wawili wapo kwenye bifu kali baada ya Hamisa kuzaa na Diamond miezi michache iliyopita. Tangu kipindi cha nyuma kabisa kulikuwa na tetesi za Diamond kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Hamisa kitu ambacho Diamond alikikataa kata kata lakini mara tu baada ya habari za ujauzito kuenea na hatimaye mtoto kuzaliwa Diamond alikiri kumsaliti Zari na kuzaa na Hamisa.

Lakini baadae Zari na Diamond walisameheana na kuendelea na mahusiano yao lakini tangu kipindi hicho Zari na Hamisa wamekuwa maadui na bifu hilo lilidhihirika zaidi wiki iliyopita pale wote wawili walipoandaa party zao siku moja nchini Uganda.

Kwenye interview aliyofanya na Millard Ayo Tv Zari amefunguka kuhusu hali iliyopo sasa na hasimu wake Hamisa Mobetto:

Mimi binafsi sina ugomvi na Hamisa chochote kilichotokea kati yake na Diamond watajuana wenyewe mimi hivyo vitu havinisumbui wala sijali nina maisha yangu nina nina watoto wangu nina kazi zangu nina mambo mengi ya kufanya sawa kina mambo yalitokea kati ya Baba Tiffa na Hamisa lakini natakiwa nijiulize nataka nifike huko? Yaani nimuache mume wangu kwa ajili yake? Hakuna kitu kama hicho lakini mwisho wa siku mwanaume ni mwanaume utampa kila kitu lakini akitoka atatfuta hata mifupa hivyo sina time ya kumuangalia anachepuka na nani sijui. Ila mimi  na Hamisa sio marafiki na hata tukikutana siwezi hata kumsalimie”.