Diamond Amtambulisha Mtoto wake Aliyezaa na Hamisa

Mwanamuziki Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amemkubali mtoto wake aliyezaa na Hamisa Mobetto na kumuweka wazi ili watu wote wamuone.

Katika mahojiano aliyoyafanya leo Diamond alikiri kuwa mtoto yule no wake na jina lake ni Dylan. Alipoulizwa na waandishi Kama Ana uhakika yule ni mtoto wake na kama amefanana naye Diamond alijibu kuwa ataposti picha baadae ili watu wamuone na waamue wenyewe Kama amefanana naye au la. Japo kuwa mama wa mtoto, Hamisa hakuweka picha ya mtoto huyo Familia ya Diamond ndio ilikuwa ya kwanza kutuma picha hiyo mitandaoni.

Baada ya kumaliza mahojiano hayo, Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alituma picha ya mtoto wake huyo na kusindikiza kwa maneno yaliyosema “Young Lion”.

Faiza Ampongeza Diamond Kwa Kumkubali Mtoto Wa Hamisa

Mwanamitindo Faiza Ally amefunguka na kumpongeza Diamond kwa hatua aliyochukua ya kwenda kwenye vyombo vya habari na  kuweka wazi kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa Hamisa. Kwa muda mrefu katika mazingira mbalimbali Diamond alikanusha kuwa name uhusiano na Hamisa name pia kuzaa naye. Leo kwa kupitia kipindi cha Leo Tena Diamond amekubali kuwa shetani alimpitia na amewahi kuwa name mahusiano ya kimapenzi na Hamisa.

Baada ya mahojiano hayo kuruka hewani mwanadada Faiza kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka new kuandika yafuatayo:

“Nasikiliza Clouds FM Naseeb nakupenda wewe ni mwanaume ea maana  saana sema wanawake wa Uswahilini ni kama ile methali ya Hamisi, yaani unaweza ukamtoa Hamisi shamba lakini usilitoe shamba kichwani kwa Hamisi #hope hutarudia Tena ujinga wako”.

Inasemekana Kuwait suala la Diamond kumkubali mtoto huyo na kumuhusumia limemgusa sana Faiza kwa sababu halo aliyonayo saivi ni Kuwa baba wa mtoto wake hamuhudumii mtoto wake ipasavyo ndio maana ameona kitendo alichofanya Diamond ni  cha kishujaa.

Zari: Majizzo ni baba wa mtoto wa Hamisa sio Diamond

Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii na mashabiki  wanajiuIiza  maswali je Diamond ni  baba halisi wa mtoto wa Hamisa?Ingawa Diamond amekataa tangu mwanzoni kuwa mtoto yule sio wa kwake licha ya Hamisa kumpa mtoto jina la baba ake na  Diamond “Abdul Naseeb”.

Katika mahojiano aliyofanya Zari  nchini Uganda amedai kuwa Diamond sio baba wa mtoto wa Hamisa na amekataa mara nyingi bali baba wa mtoto ni Majizzo,  ambaye tayari ni baba wa mtoto wa hamisa, amedai kuwa sababu pekee inayomfanya majizzo  akatae mtoto ni kwasababu  anamuogopa Lulu Michael ambaye ni mpenzi wake, na pia amedai kuwa Majizzo ndiye anayemlipia  kodi ya nyumba na kumuhudumia kila kitu. Lakini  Zari amefunguka kuwa amekwisha mwambia Diamond kama mtoto atatokea akawa  wake {za diamond} basi itabidi amuhudumie na amkubali ingawa hawezi kumlazimisha kama akikataa mwenyewe.

Diamond amekuwa akihusishwa kimapenzi na Hamisa kwa muda mrefu licha ya yeye kuendelea kukataa. Hamisa  hajamuweka wazi mpaka sasa baba wa mtoto wake, licha ya kuwa kutangaza arobaini ya mtoto itakayofanyika hivi karibu ambapo bila shaka baba wa mtoto atajulikana.

 

Picha ya Hamisa Mobetto akiwa amevaa suruali ya Diamond Platnumz

Kuna riporti zimekuwa zikianaa mitandaoni kuwa Diamond Platnumz ashawai kuwa na mahusiano ya ndani na Hamisa Mobetto, video vixen ambaye alishirikisha kwenye video yake ya Salome.

Hivi majuzi kuna picha iliyoebuka mitandaoni ikimuonesha Hamisa Mobetto kama amevaa suruali ya Diamond Platnumz.

Picha hii imewawacha mashabiki wakiamini kuwa wawili hawa washiakuwa pamoja na hivi ndivyo Hamisa aliweza kuipata suruali hii.

Ingawa hakuna kitu kinachodhibitisha kuwa Hamisa alitoa trouser hii kwa Diamond Platnumz, wengi bado wanaamini kuwa uvumi uliokuwa ukiwafuata Diamond na Hamisa Mobetto ni wa ukweli.

Pia Wengi wanadai kuwa hii ndio maana Zari Hassan and Mobetto hawajaweza kupatana kwa muda sasa.

Hamisa Mobetto hajazungumzia kuhusu picha hii inayoenea mitandaoni lakini mashabiki wa team Diamond Platnumz wamekuwa wakimtag mrembo huyu kwa hiyo picha kuona kama ataweza kusema kitu kuihusu.

Hata hivyo, Tazama hiyo picha hapa chini.

Hamisa na Diamond Platnumz kavaa suruali zinazo fanana
Hamisa na Diamond Platnumz kavaa suruali zinazo fanana