Picha za Hamisa na Diamond zavuja

Ni zaidi ya mwaka sasa  upite tangu kuwepo na tetesi za kuwepo kwa mahusiano kati ya msanii wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na video queen maarufu wa Bongo Hamisa Mobeto.Hamisa ambae amekuwa akitishia uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na mzazi mwenzie  na msanii  huyo Zari The Bosylady,hata hivyo  miezi michache iliyopita  Hamisa alijifungua mtoto wa kiume aliempa jina la Prince Adbul Nasib  au’ Tanzania baby’, mtoto ambae inasemekana  kuwa ni mtoto wa Diamond Platinumz huku akiongeza idadi ya watoto wa msanii huyo mkubwa kuwa watatu .Tangu kuwepo kwa tetesi hizo Diamond mwenyewe amekuwa akikanusha tetesi hizo na kusema  kuwa hana uhusiano wowote na video queen huyo ,zaidi ya mahusiano ya kikazi tena hasa walipokutana katika kushoot video ya wimbo wa ‘salome’ , wimbo  ambao uliozua mambo mengi na ndipo tetesi za wawili hao kutoka ulipoanza kusambaa.

Zari , mama mzazi wa watoto wawili aliozaa na Diamond amekuwa akijikuta katika vita ya kimtandao na mashabiki na hata Hamisa mwenyewe huku  sababu kubwa ikiwa ni kuwepo kwa   tetesi hizo. Pamoja na hayo yote nata   Hamisa mwenyewe  amekuwa akirusha madongo  hewani bila kudhibitisha  moja kwa moja ukweli wa tetesi hizo.

Wapo mashabiki wanaosema kuwa wawili hao (Hamisa na Diamond ) wamekuwa wakionekana pamoja baadhi ya maeneo, lakini  pia ukiachana na hayo, kipindi ambacho Hamisa Mobeto amejifungua wanafamilia wa Diamond walikuwa ni moja ya watu wa karibu walikwenda kumtembelea Hamisa  hospitali ambapo alilazwa mrembo huyo.

Baada ya tetesi hizo kuwepo kwa muda sasa, zimevuja picha  zinazosadikika kuwa ni picha za Diamond na Hamisa Mobeto wakiwa chumbani , huku mkono wa diamond wenye kuonyesha tatoo yake, hata hivyo picha zingine zinazoendelea kusambaa ni zile zinazimuonyesha Hamisa yupo kwenye chumba ambacho ni chumba cha kulala cha Diamond na mama watoto wake huku eneo ilo likionekana kufafanana kabisa na lile ambalo Zari amekuwa akipost picha katika ukurasa wake wa instagram kama sehemu yake ya kulala pia.

Hamisa Mobetto aendelea kudai kuwa maisha yake na ya Abdul Naseeb yako mashakani

Hamisa Mobetto anaendelea kuhofia kuwa maisha yake na mtoto wake aliyezaliwa Agosti 8, mwaka huu.

Kulingana na marafiki wake wa karibu, Hamisa Mobetto anaishi na wasiwasi kutokana na vitisho anazozipata kila siku kutoka kwa baba ya mtoto wake. Chanzo kimoja kutoka familia ya Hamisa kilisema;

“Unajua baada tu ya kujifungua kulienea habari nyingi kuwa mtoto huyo ni wa msanii huyo hasa baada ya Hamisa kumpa mwanaye jina hilo. Kilichofuata, kwanza msanii huyo alikimbilia kwenye media (vyombo cha habari) kukanusha habari hizo ambazo zimekuwa zikizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu. Unajua jamaa (msanii huyo) alidhani kuna siri chini ya jua kuwa anaweza kuficha jambo hilo maana watu walikuwa wakimchomea kwa mpenzi wake ambaye amezaa naye.

Aliendelea kusema,

“Ili kumziba mdomo Hamisa, msanii huyo aliona ni bora amkane mapema lakini Hamisa siyo wa mchezomchezo maana aligoma kuficha ishu hiyo. Baada ya kuona anaweza akabumburua ishu, msanii huyo alimpiga biti asizungumze na vyombo vya habari kabla ya kumwekea ulinzi wa chinichini kuhakikisha waandishi hawamfikii Hamisa. Sehemu pekee ambayo Hamisa aliona jamaa huyo hawezi kumzuia ni kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii hasa Instagram na Snapchat ‘so’ akawa anaposti vipande vya baadhi ya viungo vya mtoto huyo. Sasa baada ya kuona hivyo, msanii huyo ambaye alikwenda mara moja tu kumuona mtoto huyo alianza kumpigia simu na kumtumia meseji za vitisho. Wewe fikiria Hamisa na kichanga chake sasa anaishi kwa hofu maana jamaa amemuambia kama atafunguka kuwa amezaa naye atamuondoa uhai yeye na mtoto wake. Hali hiyo imeifanya family ya Mobeto iwe na hofu kubwa na ili kujiweka salama, aliona ni bora aende polisi kuripoti ili kama kutakuwa na jambo lolote baya litakalomkuta yeye na mwanaye, basi mhusika atakuwa ni msanii huyo. Mwanzoni tulidhani ni ishu ndogo lakini kwa vitisho anavyopokea Hamisa, vinamnyima raha na kumfanya alie tu.

Akaongeza kuwa…

Hamisa Mobetto na mwanae
Hamisa Mobetto na mwanae

“Kiukweli Hamisa anatia huruma sana na anahitaji msaada kwa sababu mbali na msanii huyo pia anapata vitisho kutoka kwa mpenzi wa jamaa huyo. Sasa watu wanajiuliza, wakati anatembea naye hakujua kuwa kinaweza kupatikana kiumbe? Na kwa ustaa wake anashindwa nini kulihendo suala hilo kwa busara ili lisimchafulie kuliko kutoa vitisho hivyo?” kilifunguka chanzo chetu hicho na kuongeza. Hata kwenye ukurasa wake wa Snapchat, Hamisa ameshatahadharisha juu ya kutishiwa kuuawa yeye na mwanaye.”
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa liliperuzi kwenye ukurasa wake huo na kukutana na ujumbe wa Hamisa uliosomeka:
“Mlidhani atafia tumboni enh…au mlijua nitafia leba…. nyie siyo Mungu na hamtakaa kuwa kamwe…& if anything bad and I mean anything bad happens to me or my son hatutawaacha salama!!!”

 

Hamisa na yeye aka sema;

‘MIMI NA MWANANGU TUNAUAWA WAKATI WOWOTE’ Ni kweli mimi na mwanangu tunauawa muda wowote. Nina ushahidi wa kutosha wa vitisho so nimeona ni vyema nitoe taarifa kwenye vyombo vya usalama,”

Diamond Platnumz amchana Hamisa Mobetto baada ya mrembo huyo kumpa mwanae jina “Abdul Naseeb”

Hamisa  Mobetto ameonekana kutojali watakacho sema watu na kumpa mwanae wa siku kumi sasa jina la ‘Abdul Naseeb’ ambalo likedhibitisha kuwa ni mtoto wa muimbaji, Diamond Platnumz.

Mrembo huyo ambaye alitokea kwenye nyimbo ya Salome Hata hivyo hajafunguka kuelezea sababu zake lakini, jana usiku Diamond Platnumz anasemekana kuwa alimchana kwa kuandika;

Hata hivyo Hamisa Mobetto hakujibu kwani Diamond Platnumz hakumtaja mtu yeyote kwa jina. Mashabiki nao kwa sasa wanachochea kusikia atakachosema Hamisa.

Hamisa Mobetto ampa mtoto wake jina Kiowa, Abdul Naseeb

Hamisa Mobetto ambaye ni video vixen na model amewaacha wengi wakijiuliza maswali baada ya kumpa mtoto wake jina la Abdul Naseeb. Jina hili limezua maswali mengi huku wengi wakidai kuwa hii ni dhibitisho tosha kuwa ni mtoto wa Diamond Platnumz.

Abdul Naseeb ambaye alizaliwa Agosti 8 mwaka huu amekuwa akifichwa na Hamisa Mobetto ambaye bado anangoja kuonyesha sura ya baby Dully Dee.

Kwa sasa Hamisa Mobetto amebadilisha jina la akaunti ya Instagram kutoka ‘Tanzania Baby’ na kuandika ‘Abdul Naseeb’. Hata hivyo bado tunangoja kusikia atakocho sema Diamond Platnumz kwa sababu mama yake (mama Diamond) wiki iliyopita aliambia Shalawadu Clouds TV walionekana katika hospitali ambayo alijifungilia mrembo huyo.

Lucy Komba awapasha mashabiki wa Zari wanaomtusi Hamisa Mobetto

Muigizaji wa bongo Lucy Komba amefunguka kwa mara ya kwanza kuwakomesha watanzania ambao wanamtukana Hamisa Mobetto kisa kuwa mtoto aliyezaa ni Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya wengi kudai kuwa kunauwezekano wa mtoto huyu wa pili wa Mobetto kuwa wa Diamond Platnumz ambaye anasemekana aliwahi kutoka kimapenzi na Hamisa Mobetto.

Lucy Komba

Hata hivyo Lucy Komba aliwatoa wengi povu kwa kuandika;

“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,”

Aliongeza,

“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo. GOODMORNING.,”

‘Baba’ ya mtoto wa Hamisa Mobetto ajitokeza

Dennis Louis ambaye ni mshindi wa milioni 50 za Tanzania Movie Talent amejitokeza kudai kuwa mtoto wa Hamisa Mobetto ni wake kupitia mtandao wake wa Instagram.

Muigizaji huyo alianzak kwa kusema kuwa Diamond Platnumz sio baba ya mtoto yule bali yeye ndio baba wa halali. Dennis Louis aliweka post hiyo huku akiwaacha wengi kama wameshangaa. Aliandika;

“Mengi yamesemwa nimevumilia vya kutosha mwenye mzigo nadhani mshanijua!! Kabla hamjaandika mambo zenu muwe na evidence za kutosha!!. Basi wenye wivu watasema Photoshop shubaaamit!!! #babajunior #comingsoon”

Hata hivyo hakuwachia hapo kwani aliweka post nyingine yenye picha yake na Hamisa Mobetto ameandika,

“son you have a bright future behind you…#eyoo! It’s a boy”

Mashabiki nao ambao wamekuwa wakifuatilia akaunti za Hamisa na Tanzanian baby walimshambulia huku wakisema kuwa wanajua kuwa msanii huyo anatafuta Kiki.

Kufikia Sasa Hamisa bado hajaweka wazi mtoto wake huyo wala baba ya mtoto wake.

 

Hamisa Mobetto aandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakijiuliza Kama mtoto anayemtarajia ni wa Diamond Platnumz

Hamisa Mobetto ameonyesha kuwa yeye hamuogopi mtoto yeyote ata Zari Hassan ambaye ni ‘mke’ wa Diamond Platnumz na mama ya watoto wake wawili.

Hii ni baada ya mrembo huyu kuandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakijiuliza ikiwa mtoto anaye mtarajia ni wa Diamond Platnumz. Mrembo huyu aliandika kusema,

Mama Daa…? Mama dee…? Mama dii..? Mama doo..? Mama duh..?

Kulingana na mashabiki wa mrembo huyu, kuna unawezo kuwa Hamisa Mobetto alikasirishwa na video ambazo Zari aliwachia Jana kwenye Instagram yake – huku akionekana akitabasamu Diamond akimchezea gitaa wakiwa wawili huko Afrika Mashariki.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza ya Mobetto kufanya jambo kama hili kwenye mitandao yake ya Instagram. Ingawa hapo awali Diamond Platnumz alikuwa ameilana mimba hiyo….kwa hivi sasa hakuna uhakika nani anasema ukweli.

Tazama post hiyo hapa;

Hivi ndivyo Hamisa Mobetto alivyosheherekea siku ya kuzaliwa ya mwanae

Hamisa Mobetto hajulikana tu kwa sababu ya urembo wake lakini kwa moyo wake mkunjufu na mtu ambae hana neno na mtu yeyote. Ameweza kuiweka maisha yake off mitandaoni na mara moja moja huweza kuposti picha za mwanae ambaye anampenda sana, kulingana na anavyomuongelea kwenye mitandao yake ya kijamii.

Hivi leo mtoto huyo, Fansy amefikisha miaka mitatu tangu azaliwe na kama kawaida Hamisa Mobetto aliziposti picha kadhaa kumsheherekea mwanae kupitia account yake ya instagram. Aliandika kusema…

Happy birthday my Baby nakupenda @misfansy .

Model huyu aliposti picha kadhaa ambazo zimewaacha mashabiki wake wakitamani anavyomlea mwanake. Ata hivyo tazama picha hizo hapa.

Alichosema Mamake Hamisa Mobeto baada ya Zari Hassan kumtolea mwanawe povu

Maneno yamemfika kooni mamake model Hamisa Mobeto baada ya picha kusambaa mitandaoni ikidaiwa bintiye amechora tatuu ya Diamond Platnumz.

Picha hiyo ilizua kero ikuluni,Madale kwa Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari Hassan,hadi matusi na maneno yakaporomoshwa kumchafua Hamisa Mobeto.

Hamisa Mobetto
Hamisa Mobetto

Kuhusu stori hii, mamake Mobeto ameshindwa kujizuia.Na inasemekana amejikuta ashamtolea povu hatari sana Zari Hassan kwa sababu ya matusi aliyomtunukia Hamisa.

Akizungumza na gazeti la Global Publishers,mamake Mobeto alisema,’hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema.

“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya, kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” amemalizia huku akiwa na uchungu mwingi.