Harmonize Aogopa Kuwagawa Mashabiki, Aamua Kufanya Show na Wolper,

Msanii wa muziki wa bongo fleva , Harmonize amefunguka na kusema kuwa ameamua kufanya show yake na kumtumia Jackline kama host katika show hiyo kwa sababu anaona kabisa kuwa kila mmoja ana mashabiki wake na kipindi wapo pamoja waliweza kutengeneza mashabiki pia hivyo , show hiyo itaonyesha wau kuwa wao sio maadui.

lengo la kumfanya jackiline wolpre kuwa katika show yangu ni ili kuwaambia mashabiki kuwa sisi sio maadui, na hauturaki kuwagawa mashabiki weu na kuwa tunaweza kufanya kazi kwa kushirikiana.

kipindi cha nyuma kidogo wawili hao walikuwa katika bifu zito sana na kutukanana sana katika mitandao ya kijamii.

 

Harmonize Kutoa Kikosi B cha List ya Wanaume wa Wolper

Siku chache zimepita tangu Wolper na Harmonize wajibizane na kufikia hatua ya harmonize kutoa list ya wanaume ambao walishawahi kutoka kimapenzi na jackilne ingawa baaada ya hapo Jackline alijibu kuwa list hiyo imekosewa na kuna baadhi ya watu amewacha na wengine amewakosea , lakini kumbe sakata hilo halikuishia hapo tu, sasa hivi Harmonize amewahaidi mashabiki zake tena kuwa  list aliyoitoa mara ya kwanza ilikuwa ni kikosi A na sasa anajianda kutoa kikosi B.

Harmonize amemuahidi Wolper kuwa kuanzia sasa hatokaa amwambai Sarah chochote kuhushu meseji ambazo amekuwa akimtumia za kutaka warudiane lakini pia amemshauri sana akwa kama mwanamke ajiheshimu sana.

kuwa mwanamke ni chombo ambacho mungu amekupa na kukutunuku  jitahidi sana kukitumia vizuri  na sio kukifanya kama kichaka cha kufanyia maovu ukitegemea kuwa mtu atakaa kimya na kutokukujibu  eti kisa ataonekna kuwa ni mdhalilishaji.mama yangu pia ni mwana mke lakini hakai hata siku moja akiziongelea familia za watu  katika mitandao, mwanamke wangu kaishaitwa mlezi wa wana na mimi nilishaitwa mdangaji  utadhani nitaogopa kuitwa mswahili?…. basi fundi cherehani wangu sitomwambai tena sarah  kuwa unanisumbua ….wacha niliambie taifa  sasa kikosi (B) coming soon….

Wolper Afunguka Mazito Juu ya Harmonize

Ni siku chache tangu msanii jackline wolper aamue kufunguka kuhusu sababu ya yeye kuachana na mpenzi wake wa zamani harmonize msanii kutoka katika lebel kubwa ya wcb, ikumbukwe kuwa wawili hao walikuwa katika mahusino ya kimapenzi na walionekana kuwa na mahaba mazito sana.lakini walikuja kuachana na wolper alipozungumza kuhusa sabau ya kuachana kwao alisema sababu ni mahusiano mapya ya msanii harmonize na mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina kwa jina la sarah. Leo imezuka tafrani nyingine katika mtandao wa instagram  baada ya  wolper kutoa majibu ya  wimbo mpya wa harmonize  uliojulikana kwa jina la ‘NISHACHOKA’ ambapo wimbo huo unadhaniwa kuwa ni kibao kilicholenga kumsasambua wolper. wimbo huo unaonyesha kusimulia maisha yao ya kimahusiano na kufichua baadhi ya mambo. Kuna baadhi ya mistari inasema   ‘kisicho riziki hakiliki….naandika huu wimbo usidhani kama nakufikiria..’

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram jackline wopler huku maneno hayo yakionesha yanania ya  kumjibu  maneno yaliyoyasemwa  kwenye wimbo huo.wolper ameonyesha kudharau kipaji cha harmonize kwa kumwambia kuwa sasa ameanza kuingia kwenye taarabu,na kwamba hata yeye akiamua kuimba hawezi kuimba kama yeye.

Wolper amekuwa  amemshushua harmonize kwa maneno aliyoyaimba ambayo yanapinga na ukweli ‘Unanitungia nyimbo alafu unasema ooo unifikirii mtu mpk unaingia studio unaimba mipasho yako si inamaana nimekujaa kwenye koo mpk mwili yani mpk tukikupima group lako la damu tunaweza kupata WOLPER MASSAWE” aliandika wolper

Katika ujumbe huo wolper ameamua kufunguka mazito ambayo yalikuwa yanafanyika katika mahusiano yaoambapo  kwa namna moja ama nyingine hakuwahi kuyaongea kama chanzo cha mafarakano yao “Sikiliza nimelala chini,Nimekufumania,Nimekuta msgz za wanaokutafutia wanawake lkn sijawahi kuongea kwasababu najua nn maana ya mahusiano kuna kuachana ”  ameandika wolper

Hata hivyo wolper amemtaka mpenzi wake huyo wa zamani kuimba wimbo mpya ili azungumze na mengine mazuri aliyokuwa anamfanyia kama kumsubiri studio,kulia sana kwa ajili yake na ikibidi aimbe nyimbo za kumsifia mwanamke wake mpya anaejulikana kwa jina la Sarah.

 

Wolper aeleza sababu za mahusiano yake kutodumu

Mapenzi ya Harmonize na Wolper yameisha kulingana na fununu zinazotambaa mitandaoni. Wawili hao wameachana kwa sasa na kulingana Wolper, yeye hana bahati kwenye mapenzi.

Akizungumza hivi karibuni Wolper alifunguka kwa kusema kuwa anakipaji cha kukomeshwa na wanaume wote ambao ametoka kimapenzi nao. Alisema,

“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae”

Hata hivyo Harmonize anasemekana kuwa anampenzi mpya ambaye ni mtoto wa Kizungu.

Mapenzi ya Harmonize na Wolper yavunjika kwa mara ingine tena….yadaiwa Harmonize kapata mtoto na msichana mwingine

Mapenzi ya Harmonize na Wolper yamekwisha kwa mara ingine tena!

Huo ndio ujumbe unaoenea kwa mitandao ya jamii wakati huu.

Inasemekana mambo iliharibika baada ya Wolper kugundua Harmonize apo na mwanamke mwengine wa kizungu na wanatarajia mtoto.

Kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM leo April 21, 2017 mtangazaji Soudy Brown alibuni kubaini ukweli lakini hakuweza kuwasiliana na wawili hao.

Ilibidi aongee na meneja wa WCB Babu Tale na haya ndio aliyoyasema:

”Tuzungumze biashara ya Chibu Perfume leo. Utakapompata Harmonize utazungumzia hilo. Mimi sio manager wa mapenzi ya wasanii wangu, namanage biashara na kazi zao basi.”