Alichokisema Harmonize baada ya kutambulishwa kama mwizi

Harmonize na Rich Mavoko wako na wimbo mpya Show me lakini stori zinazoenezwa mitandaoni ni kwamba waliiba wimbo huyo kutoka kwa msanii KCV.

Msanii huyu, KCV amedaiwa kuwa kwenye WCB ambapo alirekodi wimbo huo.

Harmonize alifikiwa kwenye Whatsapp na Bongo 5 na ndipo akajibu ya kwamba yeye hawezi ongelea jambo hilo hadi ambapo atausikia wimbo huo wa KCV.

Producer wa WCB Laizer pia alikana madai hayo na kusema hamfahamu KCV hata kamwe.

 

Jah Prayzah aingia studio na Harmonize baada ya kutoa collabo kali na Diamond

Kila mtu anakumbuka ‘Watora Mari’ – wimbo huo bado ni hit kubwa mieze nane baada ya kuachiliwa. Msanii Jah Prayzah alishirikiana na Diamond kutoa wimbo huo.

Umaarufu wa Jah Prayzah ulienea barani mzima baada ya kumhusisha Diamond kwa wimbo wake. Msanii huyo kutoka Zimbabwe alinyakulia tuzo ya Listener’s Choice Awards ya MTV MAMA mwaka jana.

Jah Prayzah sasa imeingia studio na Harmonize – ujumbe aliouandika kwa mtendao wa Instagram unashiria ujao wa collabo yake na staa huyo kutoka WCB Wasafi.

“In the studio again with another Tanzanian big star @harmonize_tz .Zimbabwe neTanzania ?,” Jah Prayzah aliandika.

 

Harmonize awataja warembo wawili kutoka Kenya ambao wanampendeza sana

Harmonize alisafiri kuenda Nairobi, Kenya kupigia upato nyimbo zake. Staa huyo kutoka Wasafi Records WCB amefanya mahojiana na vitua vya habari kadhaa jijini Nairobi.

Katika mahojiano na kipindi cha Mambo Mseto ya Radio Citizen hapo jana, Harmonize aliulizwa kumtaja mrembo kutoka Kenya anayemgusa sana.

Mzazi Willy Tuva na Harmonize wakiwa Citizen Radio

Harmonize alicheka na kuwaza kwa sekunde chache kabla ya kusema kwamba Kenya iko na watoto wazuri wengi.  Hata hivyo alisema Huddah Monroe and Vera Sidika ndo wanampendeza sana.

“Suppose kama haugekuwa na Wolper alafu ibidi uwe na mchumba hapa Kenya ni mrembo mgani wa humu nchini Kenya ambaye huwa ana ‘Kugusa’ kinyama?” Harmonize aliulizwa.

“Kenya kuna watoto wazuri kabisa… …mtoto VERA hivi…. mtoto MONROE hivi….wako wengi bana, wote wako sawa,” alijibu Harmonize.

Huddah Monroe

 

Vera Sidika

 

“Mimi Harmonize hawezi kuniacha” Wolper

Wolper alikuwa kwenye mtandao wa Central Filamu wiki hii ambapo alizungumzia uhusiano wake na Harmonize.

Alidai ya kwamba woko pamoja na hakuna ataye watenganisha.

“Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper.” Alisisitiza.

Hao wawili wamerudiana wiki kadhaa tu baada ya kusemekana wameachana.

Harmonize azungumzia madai ya kwamba ana maringo

Mwanamuziki wa Wasafi Harmonize leo katika kipindi can East Afrika Mashariki, humo Kenya alizungumzia madai ya kwamba ana maringo mengi na hataki kuhusiana na watu.

Akiongea katika show ya Mzazi Willy Tuva, alieleza ya kwamba yeye hana marigo mbali ako busy tu na mambo yake. Alieleza ya kwamba label yake ya Wasafi imetengezea time table ambayo anaifuata kwa ukamilifu.

Kama hayuko ofisini akifanya muziki ako nyumbani kwenye gym ama chumbani mwake akilala. Yeye hana haja yoyote ya kutembelea vyumba vya viburudisho.

Harmonize awajibu haters walio mkashifu baada ya kutoa video yenye utata

Harmonize aliweka wimbo wake mpya ‘Niambie’ kwa YouTube tarehe 16 Machi 2017. Wimbo huo umezua utata kwa sababu kuna watu wanasema haijaendana na maudhui ya audio.

Watu wengi wakitoa maoni yao walisema kuwa audio inajenga picha ya umaskini lakini kwenye video Harmonize anaonekana kwenye maisha ya kitajiri sana.

Akionge kwenye kipindi cha Prince Ramalove kupitia ya Kings FM, Harmonize alifafanua kuwa kwenye video yeye alikuwa kijana maskini ambaye alikua na mpenzi tajiri aliyempa kila kitu.

“Sina mtonyo lakini naishi kwake,sasa nikiishi kwake na yeye ana hela,ntafanyaje?”Alifafanua Harmonize.

Tazama hio video hapo chini:

Harmonize aeleza hofu aliokuwa nayo na uamuzi wa lebo ya WCB Wasafi

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Harmonize alisema alikuwa na hofu na  lebo ya WCB Wasafi baada ya uongozi wake kumtaka kuachia wimbo wake mpya kwenye tovuti ya Wasafi.com badala ya kuachia kwenye TV na redio kama ilivyo desturi.

Harmonize alikiri kuwa alidhani WCB Wasafi walitaka kumpoteza katika ramani ya muziki ndiyo maana hawakutaka atangulize wimbo wake mpya kwenye TV na redio.

Ata hivyo Harmonize amefurahia uamuzi huo, anasema kuwa wimbo wake umepokelewa vizuri na mashabiki wake kwenye tovuti ya Wasafi.com.

“Unajua mimi WCB ni kama chambo kwa sababu hata lebo ilipoanzishwa mimi ndiye niliyekuwa msanii wa kwanza kusaini na nikafanya vizuri wengine wakaja, hata hivyo kwenye mauzo ya muziki kwenye mtandao nimetangulizwa mimi na namshukuru Mungu kazi zimepokelewa vizuri. Uongozi ulikuwa na mtazamo chanya tofauti na nilivyowaza,”alisema Harmonize.

 

New Video: Harmonize aachia video yake mpya aliyomshirikisha mpenzi wake kama video vixen

Msanii wa Tanzania Harmonize ameachia mpya video ya wimbo wake mpya Niambie aliofanya miezi 6 baada ya Matatizo.

Harmonize ambaye anafanya kazi chini ya uongozi wa Wasafi records amefurahisha washabiki kwa wimbo huu uonawagusa kidani maana ameimba kuhusus mapenzi, kitu ambacho mashabiki wa bongo hupenda.

Katika video yake, Harmonize alimshirikisha mpenzi wake wa dhati, Jacqueline Wolper. Kwa kufanya hivi, mashabiki wengi wameachwa wakifikiria kuwa mapenzi yake na Wolper ni ya kiki.

Hata hivyo, alifutilia maneno haya mbali alipokiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM Jumatano hii, kuwa kuna wakati alipogombana na mpenzi wake lakini sasa wamesuluhisha kila kitu.

“Kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa, lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi. Sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki,”

Hata hivyo, tazama video yake mpya hapa.

Msanii kutoka Wasafi Harmonize azungumza mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wolper

Msanii Harmonize juzi alikuwa kwenye Clouds fM na alizungumzia mambo mengi kuhusu wimbo wake na sana sana kuhusu uhusiano wake na Wolper.

Harmonize aliulizwa na Mami baby kama ilikuwa kiki au nini baada ya kudaiwa kuachana na Wolper na ukaribu wao kurejea leo wakati anaachia wimbo wake mpya.

Harmonize

“kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi ila sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na Mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki nilianza naye nikiwa sina hata gari”  Harmonize alieleza.

Alihakikisha lakini hawakuwa pamoja;

“Ukiona mtu anatumia nafasi yako kuvuma ni jambo la kumshukuru Mungu, sikatai yupo kwenye miahangaiko atatoka, Mungu amjalie najua wote tunatoka kwenye familia za kimaskini ni wakati wake sasa kuonyesha alichojaliwa” Alimtakia Wolper kila la heri.