Sarah,mpenzi wa Harmonize amjibu Wolper

Ikiwa ni  siku moja tu imepita tangu Harmonize na Wolper waingie tena kwenye bifu  zito baada ya msanii huyo wa lebel kubwa nchi ya wasafi kutoa wimbo ambao ulilenga kutoa siri za mahusiano yake na mpenzi wake huyo wa zamani Wolper ,wawili hao walijikuta katika malumbano mazito ambayo mpaka sasa yanaendelea mitandaoni huku kila mmoja akikataa kushindwa na kunyamaza ,katika post yake aliyotoa jana katika ukurasa wake wa instagram wolper aliandika kumshauri harmonize kuacha kuandika nyimbo ambazo zinamuhusisha yeye bali ajitaidi kuandika nyimbo ambazo hata zitakuwa zikimsifia mpenzi wake mpya anaejulikana kwa jina la sarah, pia Wolper aliandika maneno yaliyodhihirisha kuwa harmonize alimfata Sarah kwa sababu ya pesa.

Akitoa majibu ya post ya Wolper ,Sarah  aliandika hivi katika ukurasa wake wa instagram ” kama nilimpa hela nyingi akakuacha na wewe si umpe hela akurudie”, mwanamke huyo  wa Harmonize alikuwa kimyaa kipindi chote cha malumbano ya wawilio hao lakini sasa nae kaamua kufunguka ,hata hivyo Sarah pia alionesha dharau kwa kumwita mpenzi mpya  wa wolper “msukule”, “mbeba pochi” .Sarah ambae aliambiwa na Wolper kuwa hajui lugha leo anaamua kusema kuwa post hiyo ameiandika kiswahili kwa msaada wa mpenzi wake harmonize na kumtagi kabisa,” nimeandika kiswahili kwa msaada wa Harmonize”

Hata hivyo vita hiyo ya kimtandao sasa inaonekana kuwa kubwa kwa sababu imekuwa ni kati ya Harmonize na mpenzi wake Sarah huku Jackline Wolper ,  na inakuchukua taswira mpya kwasababu inakuwa kama kila upande  unaokuwa na wivu  na upande mwingine.

Ikumbukwe kwamba wawili hao wameachana muda mrefu lakini vita hii imeanza upya baada ya Jackline wolper kuamua kufunguka sababu ya kuachana na harmonize ambapo kati ya mengi aliyoyasema alisema kuwa mwanamke mpya  ambae ndio sarah alikuwa chanzo cha yeye kuachana na mwanaume huyo huko pia hela imetajwa kama kivutio cha mapenzi kutoka kwa mwanamke huyo.Je mpenzi mpya wa Wolper ataingilia kati, au watayamaliza wenyewe….

Harmonize azungumzia kuhusu mjengo wake

Muimbaji kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mjengo wake ambao ni wa ghorofa akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni.

Kulingana na Harmonize mjengo wake unawezekano wa kukamilika mwishoni wa mwaka huu. Hata hivyo, Harmonize alikataa kufunguka kuhusu gharama aliyotumia kutengeneza ghorofa hiyo.

Harmonize alisema;

“Kwa hiyo flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi”

Harmonize aliendelea kwa kudai….

“Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,”

Harmonize aachia picha mpya na mpenzi wake mpya, lakini hana ujauzito!

Muimbaji kutoka Wasafi records Harmonize amewaacha wengi wakijiuliza mimba ya mpenzi wake iko wapi. Hii ni baada ya kuachia picha mpya ambapo anaonekana akistahereka na mrembo huyo.

Hata hivyo Harmonize aliamua kuzima comment section yake ilimashabiki wake wasimchane kwa maneno. Katika picha hizi muimbaji huyo anaonekana akiwa na mrembo wake huyo akicheza pool table mbele ya nyumba ya kifahari inayosemekana wawili hao wanaishi.

Katika moja ya picha hizo msanii huyo aliweka wazi uwanja wa kutuma komenti lakini mashabiki wengi walionekana kuacha komenti mbaya kwa mpenzi wake na kwa hivyo akafunga komenti kwenye picha hizo zingine.

Tazama picha hizo hapa;

Wolper amepata mchumba mwingine baada ya Harmonize?

Muigizaji wa filamu Wolper Stylish anaonekana kuwa amepata mchumba mpya baada kuachana na Harmonize ambaye anatarajia mtoto wake wa kwanza na mrembo wake mpya wa kizungu.

Wolper Stylish
Wolper Stylish

Kuachana kwa wawili hawa kuliwashtua mashabiki wao ambao walikuwa wakitarajia harusi kulingana na walivyokuwa wakipendana. Hata hivyo Harmonize alidhibitisha kuwa uhusiano wao ulikuwa umeisha na sasa alikuwa na mchumba mpya.

Hata hivyo Wolper alikaa kimya hadi Jana alipoandika ujumbe ambao umewaacha wengi wakisema kuwa kunauwezekano kuwa amepata mwanaume ambaye ameituliza roho yake sasa.

Harmonize aonyesha Pete, saa na mikifu yake ya dhahabu yenye dhamana ya mamilioni

Wasanii wa Wasafi Records wanaonekana kuwa wanashika mkwaja wa hali ya juu. Ikiwa sio magari na nyumba ni pete na saa zenye dhamana ya juu.

Harmonize amejiunga miongoni mwa wasanii ambao wanaziweka picha kuonyesha dhahabu zao mitandaoni ya kijamii. Msanii huyo leo hii ameziachia picha na video kuwaonyesha mashabiki wake baadhi ya saa, Pete na mikufu ambazo ameza kuzinunua.

Kulingana na maoni ya mashabiki wake sio wengi walipendezwa na kitendo hiki hasa saa hii Waislamu wamefunguka. Wengi walionelea angewapa maskini pesa hizo angalau wanunue chakula au kujenga msikiti.

Tazama video na picha hapa chini;

https://instagram.com/p/BVHuVKaFRwX/

Harmonize adai kuwa ‘kuna mtoto na kuna mtoto wa kizungu

Harmonize kwa hivi sasa ameweka wazi anatoka na mtoto wa kizungu na kama mwanaume yeyote ambaye amelowa kwenye mapenzi, msanii huyu hajakuwa akificha furaha yake.

Msanii huyo wa Wasafi records alimzindua mrembo huyo hivi karibuni baada ya kuwachana na Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake kwa muda mrefu. Hata hivyo akiongea kwenye kipindi cha 255 ya XXL ya Clouds FM Harmonize alisisitiza kuwa anatarajia mtoto wake atachukua rangi ya mamake.

Alisema,

“Ngoja nikwambie kitu kuna kuzaa mtoto na kuna kuzaa mtoto wa kizungu ni vitu viwili tofauti,” alisema Harmonize. “Naenda Marekani mara moja si unajua mke wangu anatakiwa kusarifi kaniambia kuna ishu tunaenda kufanya sasa mimba ikiwa kubwa atazuiliwa kupanda ndege,”

Wolper aeleza sababu za mahusiano yake kutodumu

Mapenzi ya Harmonize na Wolper yameisha kulingana na fununu zinazotambaa mitandaoni. Wawili hao wameachana kwa sasa na kulingana Wolper, yeye hana bahati kwenye mapenzi.

Akizungumza hivi karibuni Wolper alifunguka kwa kusema kuwa anakipaji cha kukomeshwa na wanaume wote ambao ametoka kimapenzi nao. Alisema,

“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae”

Hata hivyo Harmonize anasemekana kuwa anampenzi mpya ambaye ni mtoto wa Kizungu.

Baada ya kuambiwa mwili wake haufai kuvaa ‘bikini’ Wolper aachia picha ya kuwazingua mashabiki

Hakuna mtu mrembo kama mwanamke ambaye anajiamini. Hii ndio sababu malkia wa filamu za bongo Wolper stylish amekataa kuyaskiza maneno ya mashabiki ambao wanaopenda kumponda kuhusu mwili wake mnene.

Baada ya kutokea kwenye video ya mpenzi wake Harmonize kama amevalia nguo za kuogelea…mwanamke huyu alipondwa kwa maneno ya mashabiki ambao walidai kuwa kuna nguo ambazo mrembo hafai kuvalia kutokana na umbo la mwili wake.

Hata hivyo Wolper inaonekana kuwa hakuwasikiza na ndio maana ameachia picha mbayo imeewaacha wengi wakimsifu na kumtamani mitandaoni. Wolper anaonekana kama amevalia bikini ya kisasa ambayo amependeza sana.

Ikiwa haujaiona picha hiyo basi itazame hapa.

Wolper Stylish
Wolper Stylish

Hizi ndizo pesa Harmonize anapata kupitia YouTube

Harmonize ambaye ni msanii kutoka Bongo amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu pesa ambazo yeye hupata kupitia mtandao wa Youtube kwa Mwezi. Muimbaji huyu ambaye anafanya na Wasafi records alikuwa akiongea na Clouds FM alipotaja pesa mbazo kwa hivi sasa anapata.

Kulingana na yeye anapata kiwango cha Dola 3,500 ambazo zimeweza kuchangia kwa maisha yake ya kifahari. Harmonize alisemakuwa pesa hizi ndiyo zimemuwezesha kutembelea magari ya kifahari ambazo mashabiki hushindwa katoa wapi.

Msanii huyu alisema,

“Namshukuru Mwenyezi Mungu Kupitia muziki umenikutanisha na watu wengi,Umenipa Dili napata riziki kwenye njia tofauti tofauti,sio tu kwenye show,licha ya kufanya show nauza nyimbo zangu kwenye Platform,Mimi akaunti yangu ya Youtube kila mwezi nalipwa Dola 3,500.”

Hata hivyo sio siri kuwa muimbaji huyu amejikaza kimziki na ndio maana maisha yake yamebadilika.

Kuna beef? Idris Sultan na Harmonize wachanana mitandaoni ya kijamii

Inaonekana kuwa Idris Sultan na Harmonize wameanza beef ambayo imewaacha mashabiki kama wameduwaa bila kujua ni yupi watampa support kwa kuwa wawili hawa ni mastaa wakubwa Bongo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Idris Sultan alionekana akimtania Harmonize bila kujua kuwa muimbaji huyu hapendi mchezo. Idris aliandika kusema,

Ogopa rapa wako anapo kiki kuliko wewe. Inabidi mbadilishane wewe ndo uwe rapa.

Harmonize naye hakuchelewa kumjibu Idris Sultan huku akimchana kuwa anaskia kuwa amewekwa na mwanaume mwenzake na kuwa hakuwa na pesa anavyojigamba. Kupitia Twitter Harmonize aliandika kusema….

Nasikia unalala Mbezi kwa mwanaume mwenzio daa huruma. Kwani ulishindaga shilingi ngapi South…??? Mbaya zaidi nasikia unamarinda.

Idris naye kupitia Instagram alimjibu kwa kuposti picha hii na kuandika..

Idris Sultan

Acha nicheke tu, ntafanyaje sasa. Kumpiga nzi risasi ntamuonea maskini. Huyu ni makofi tu ??? #MarindaNimekuaSketiYaShule …. KARIBU KIUMENI ??

Harmonize afafanua script ya video yake mpya kwa mashabiki wasioilewa

Imebidi Harmonize kuwaeleza mashabiki wake uhusiano wa video yake mpya na wimbo wake niambie unaowachanganya wengi. Muimbaji huyu wa Wasafi records amekuwa akiona malalamishi ya mashabiki wake wanoaamini kuwa alikuwa off script kwenye video yake mpya.

Harmonize akiwa na Wolper
Harmonize akiwa na Wolper

Kulingana na lyrics zake za Niambie, Harmonize anaonekana kuwa mtu ambaye hana pesa wala kwake ilhali video ya wimbo huo anaonekana akiishi kwa nyumba ya kifahari na maisha yake kuwa ni ya tajiri kitu ambacho hakiambatani na anachoimba.

Hata hivyo Harmonize alichukua fursa ya kuwafafanulia mashabiki wake alipokuwa kuwa kwenye interview na Prince Ramalove kupitia Kings Fm. Harmonize alielezea maana ya script ya hiyo video kwa kusema…

“Sina mtonyo lakini naishi kwake,sasa nikiishi kwake na yeye ana hela,ntafanyaje?”

Kwa ufupi muuimbaji huyo alikuwa akimanisha kuwa nyumba na magari zinazooonekana kwenye vdeo ni mali za Wolper kwa mujibu wa script.