Huddah- Nimetembea Sana na Mabilionea Lakini Sijawahi Kuwa Bilionea

Mfanyabiashara na Socialite maarufu kutoka Kenya Huddah Monroe ameibuka na jipya Baada ya kukiri kuwa ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wanaume mabilionea Lakini hajawahi kuwa bilionea.

Huddah amefunguka hayo Kupitia mtandao wa Snapchat ambapo ameeleza kuwa amekuwa akijihusisha kimapenzi na watu wenye utajiri mkubwa lakini yeye bado hajawa tajiri kwa sababu amegundua utajiri hauambukizwi kwa kujamiana.

Nimejihusisha kimapenzi na Mabilionea lakini sijawahi kuwa Bilionea, utajiri hauambukizwi kupitia tendo la ndoa ,inabili uwe mtumwa kwa ajili ya vitu vyako kila siku” .

Hudah ambaye Hivi sasa anafanya vyema na kampuni yake ya vipodozi ya Huddah Cosmetics ameongea hayo katika jitihada za kuwahamasisha wasichana wafanye kazi kwa bidii badala ya kutegemea kuwa na wanaume wenye pesa tu.

Huddah Monroe Awatolea Povu Zito Wasanii Wa Kenya

Socialite na mfanyabiashara maarufu nchini Kenya Huddah Monroe amefungukia Sakata la kampeni ya ‘Play Kenya Muzic’ Na kuwatolea Povu wasanii wa Kenya na muziki wao.

Nchini Kenya kwenye vituo mbali mbali vya Radio kumekuwa na kampenzi ya Play Kenya Music ambayo inashinikiza ma Dj na Watangazaji kupiga muziki wa wasanii wa kenya badala ya wasanii wa nchi nyingine zaidi.

Huddah Monroe amefunguka na kuweka wazi kuwa  anapenda sana kusikiliza nyimbo za wasanii wa Nigeria kuliko Kenya.

Huddah kupitia Instagram Stories, amesema kuwa muziki wa Nigeria unahusisha maisha halisi ya kwenye jamii. Huku akiuponda muziki wa Kenya ambao amedai kuwa nyimbo nyingi ni za mapenzi, zina sifia ulevi na madawa ya kulevya .

Unajua kwanini huwa huwa nasikilisa sana muziki wa Nigeria? unaniingia sana moyoni, kwa sababu nasikiliza kile kitu nataka kusikiliza, wenzetu wameamka sana. Ujumbe uliopo kwenye nyimbo zao sio tu mapenzi na madawa ya kulevya, bali wanazungumzia maisha halisia. Kiukweli wananivutia, na hivyo ndio vitu tunataka kusikia. Na sio kila siku kuimbia ngono, mapenzi na madawa ya kulevya”.

Lakini pia katika upande mwingine Huddah amewapongeza wasanii kama Nyashinski, Sauti Sol, Octopizzo na Khaligraph Jones kwa kufanya muziki mzuri na kuitangaza Kenya kimataifa .

Huddah Amtaka Mh,kenyata Kuhararisha Bangi.

Mwanadada maarufu kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe amemuomba mh rais wa nchi hiyo kufanya uhalali wa kilevi cha bangi kila  hata bila kufanya mchakato wa kura za maoni .Mwanadada huyo ambae mara nyingi amekuwa akionekana akitumia kilevi icho kama kiburudisho kwake anasema kuwa yoyote aliye karibu na rais amfikishe taarifa za ombi lake.

katika ukurasa wake wa instagram Huddah aliandika “kabla ya kura ya maoni , tunaomba abgi ihararishwe, nani aliye karibu na rais naomba amfikishie hili”

Huddah hatokuwa mwananchi wa kwanza nchini humo kutaka mmea huo wenye kilevi na unaotambulika katika baadhi ya  nchini kuwa madawa ya kulevya kutaka mmea huo kutumika kihalali kila mahala.Inasemwa kuwa zaidi ya watu  1400 mwaka uliopita walitaka kuunga mkono hoja hiyo iliyowakilishwa bungeni na mmoja wa wanasayansi nchini humo  akisema kuwa ina faida sana kwa wananchi na kwa pato la Taifa pia.

Huddah Agoma Kuwekwa Kundi Moja na Vera Sidika

Socialite maarufu kutoka nchini Kenya Mrembo Alhuddah Njoroge maarufu kama Huddah Monroe amegoma kabisa kushindanishwa na hasimu wake Mrembo Vera Sidika ‘Queen Vee’.

Huddah amekataa kushiriki Tuzo za Black Entertainment Film Fashion Television and Arts (BEFFTA) ambapo yupo kipengele cha International Film and Fashion ambacho hasimu wake Vera Sidika pia amechaguliwa kushiriki na kusema kuwa hawezi kulinganishwa naye hata kidogo.

Huddah na Vera wamekuwa Kwenye mvutano wa muda mrefu na hata kugombana kwenye mitandao ya kijamii na sasa Huddah amegoma kabisa kishiriki tuzo hizo kutokana kuwekwa kundi moja na adui yake.

Kupitia mitandao ya kijamii Huddah ameandika haya kuhusiana tuzo hizo:

Mmenichagua katika tuzo ambazo wala sizifuatilii kabisa nipo bize na mambo yangu na ninafanya mambo yanayonihusu na sipo kwa ajili ya kulinganishwa na hao mlioniweka nao, kwa Afrika sina wakulinganishwa naye yaani sijaona labda USA (Marekani), nipo bize na brand yangu ya HUDDAH na kuangalia vipi naikuza sitaki ushindani na mtu”.

Huddah na Vera wamekataa mara kwa mara kuwa na bifu lakini matendo yao yamekuwa yakionyesha utofauti.

Huddah Awachana Wabongo Kwa Unafiki Amkingia Kifua Jokate

Socialite maarufu kutoka pande za +254 Kenya, Huddah Monroe amewatolea uvivu wabongo kwa vitendo vya kinafki walivyomfanyia Jokate Mwegelo mara baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.

Huddah amewatolea povu watu waliomnanga Jokate baada ya Ali Kiba kumuoa mwanamke mwingine ambaye ni Amina mwaka huu na kusababisha watu kumcheka sana Jokate.

Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Huddah ameandika ujumbe huu:

Ali Kiba alivyomuoa msichana mwingine mapema mwaka huu watu walimcheka sana na kumdhalilisha Jokate. Lakini sasa hivi anapata mafanikio hao hao watu wanageuka na kumpongeza ama kweli mitandao imeshindikana. Hana mashabiki wa kweli bali ni wanafiki tu na wanaondoka kwa upepo”.

Ali Kiba alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Jokate kwa muda mrefu lakini mapema mwaka huu alimuoa Amina.

Wikiendi iliyopita Rais Magufuli alimtangaza Jokate kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe jambo lilipelekea kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa mashabiki mbali mbali na hata wasanii wenzake.

“Nikipiga Picha Za Utupu Nalipwa, Wazazi Waangalieni Watoto Wenu”- Huddah

Socialite maarufu kutoka Kenya mrembo Huddah Monroe maarufu kama Huddah The Boss Chick amewatolea povu wazazi wanaomsema kuwa kuanika picha zake za Utupu Mtandaoni zinaharibu watoto wao wa kike wanaomfuatilia.

Huddah amejizolea umaarufu zaidi kutokana na umbo lake matata Lakini pia anajulikana kwa kuanika umbo lake Kwenye mitandao ya kijamii huku akiwa mtupu kabisa au nusu utupu.

Kutokana na Kuposti picha hizo Huddah amekuwa akikosolewa sana kutokana yeye kuwa maarufu na kioo  cha jamii ametakiwa kuwa mfano mzuri kwa watoto wa kike wanaomfuatilia.

Lakini Huddah ameibuka na kujitetea kuwa anapoweka picha kama hizo Kwenye mitandao ya kijamii ni kwa sababu anakuwa analipwa kufanya hivyo aidha ni kwa ajili ya kutangaza nguo zile za ndani au kutangaza mahoteli ya kifahari.

Wasichana wengi wananiangalia mimi. Sidhani kama nimemshawishi mtu yoyote kupiga picha za utupu. Tatizo linakuwa lipo kwa wazazi wanaoshindwa kulea watoto wao na kijamii Kwenye mitandao ya kijamii kuangalia Huddah kufanya nini”.

Lakini pia Huddha aliendelea kusisitiza kuwa kuposti picha na nguo za ndani ni kazi yake inayomuingizia kipato:

Mara nyingi nikipiga picha na nguo za ndani nakuwa nafanya matangazo ya biashara aidha natangaza hoteli au nguo za ndani nilizovaa na nifanya hivyo kwa sababu nalipwa Sifanyi ovyo ovyo”.

 

Huddah Adai Hiki Ndio Kinachowatoa Udenda Wanaume Kutoka Kwake

Socialite maarufu kutoka 254 Kenya Huddah Monroe amefunguka na kutaja kitu kinachowadondosha wanaume kutoka Kwenye mwili wake.

Huddah ambaye anajulikana kwa umbo lake matata linaloonekana kuwatega wanaume wengi amefunguka na kudai kitu kinachowavuta wanaume ni tabasamu lake na sio vingine kama wengi wanavyodhani.

Hudah alifunguka hayo Kwenye mahojiano na Wasafi Tv baada ya kuambiwa ataje kifungo chake katika mwili wake ambacho huwa kinawavuta na kuwatoa udenda wanaume wengi:

Which part on my body wanaume wengi wapo attractive is….., I think is my smile”.

Huddah alikuja Tanzania wiki chache zilizopita kwa ajili ya kutokea kwenye shoo ya msanii kutoka Label ya WCB Harmonize.

Huddah Afungukia Mahusiano Yake na WCB

Socialite maarufu kutoka Kenya mrembo Huddah Monroe maarufu kama Huddah The Bosschick amefungukia uhusiano wake na Label maarufu nchini WCB.

Huddah alitua nchini Tanzania mwishoni mwa wiki hii na mara moja alionekana akiwa katika ofisi za WCB na CEO wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi The Playlist ya Times FM, Huddah amesema kuwa ukiachilia mbali sababu za kibiashara, amekuwa akivutiwa na uchapakazi wa timu nzima ya WCB.

The vibe is, WCB napenda sana ni watu wanajima, watu wana njaa ya maisha , so for me WCB have the some kind of vibe the i have. Wanapenda maisha mazuri, so they very work hard hawalalai saa 24 wapo kwenye kazi, so that I like that”.

Huddah ambaye ni Mfanyabiashara anayemiliki make up line yake inayoitwa Huddah Cosmetics ambayo imekuwa ikifanya vizuri.

Huddah Monroe alikuja nchini Tanzania kwa ajiili ya ku-host show ya Harmonize iliyofanyika siku ya leo June 16, 2018.

Huddah Monroe Aopoa Njemba La Kiarabu

Socialite maarufu kutoka Kenya Huddah Monroe amefunguka na kudai hivi sasa amefanikiwa kupata mpenzi mpya ambaye ni mwarabu.

Huddah ambaye amejipatia umaarufu kutokana na vituko vyake lakini pia na urembo wake aliweka wazi kuwa kwa sasa yupo Kwenye Mahusiano Kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao mmoja wa burudani nchini Kenya, Huddah alisema  kuwa yupo Kwenye Mahusiano na mwanaume Huyo wa kiarabu na anampenda sana.

Hudah aliweka wazi suala hilo baada ya kuandika kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram, kwamba angekuwa nje ya soko kama asingepata mpenzi na kurudi kwenye uhusiano.

Ninashukuru nimepata mpenzi, ambaye tunapendana. Ni Mwarabu na kiukweli ningekuwa nje ya soko kama ningeendelea kuwa mpweke”.

 

Huddah Amchana Zari na Kamwambia Hana Ubosi Wowote

Socialite maarufu kabisa nchini Kenya, Huddah Monroe ameingia kwenye vita ya maneno mtandaoni tena na Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye ni mzazi mwenza wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Huddah amempanga Zari na kudai anajifanya Bosslady wakati hana lolote hii imetokana baada ya Zari kuweka video mtandaoni inayomuonyesha akionyesha simu zake tatu ambazo anatumia hivi sasa ambazo ni Samsung galaxy s8, Note 5 na IPhone X.

Baada ya kuonyesha simu hizo Zari alidai kuwa yeye ni tajiri na ndio maana amenunua simu zote kali kwa wakati huu huku akionyesha saa yake aliyodai ni Rolex. Baada ya video hiyo kusambaa mtandaoni Huddah alimjibu kuwa yeye amekuwa anatumia IPhone X tangu ilivyotoka mwaka jana hivyo yeye ndio Boss.

Kupitia ukurasa wake wa SnapChat Huddah aliandika maneno yafuatayo:

Funny how people buy iPhone X after it came out long ago and social media can’t sleep…some of us have been using iPhone Z from the day it came out and we don’t flaunt small things like that because we’re used to it! Act like a boss! Tumia pesa ikuzoee”.

Zari na Huddah ni maadui wakubwa na sio mara ya kwanza kwa wawili hawa kurushiana maneno mtandaoni wamekuwa wakitofautiana mara kwa mara lakini ustajaabu kujua kuwa mara ya kwanza walikuwa marafiki wakubwa.

Zari na Huddah Enzi za Urafiki wao.

 

Huddah Aweka Wazi Hisia Zake Kwa Juma Jux

Mfanyabiashara na mrembo kutoka Kenya Huddah Monroe amefunguka na kuelezea wazi hisia zake juu ya mwanamuziki kutoka Tanzania Juma Jux.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Huddah amefunguka na kueleza kuwa Jux ni mwanaume anayeweza kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Ninavutiwa sana na style ya mavazi ya Juma Jux, yaani walahi his style is on point yaani mimi binafsi sijawahi kumtumia mwanaume meseji lakini siku moja naangalia picha kwa Instagram nikamtumia meseji nikamwambia unapendeza, yaani kila anachovaa kinampendeza. Mimi napenda mtu awe  na style yake mwenyewe yaani havai kama watu wengine wanavyovaa na akijitahidi hiyo style yake itakuja kumpeleka mbali sana”.

Pia kwenye mahojiano hayo, Huddah aliulizwa kama Jux ni aina ya mwanaume ambaye anaweza akawa na uhusiano naye wa kimapenzi alikiri kuwa anavutiwa naye kimapenzi pia kwa sasa yupo single akimaanisha hana mpenzi yoyote.

Ingawa hiyo inaweza ikawa ngumu kidogo kwa upande wa Jux kwani tetesi zinazoendelea kuenea hivi sasa ni kuwa amerudiana na ex wake Vanessa Mdee ingawa Vanessa amekataa lakini za chini ya kapeti zanadai kuwa Jux na Vanessa waliopo kwenye tour ya Fiesta pamoja inasemekana wana ukaribu uliopitiliza urafiki wanaodai wanao, kwani pia wawili hao walishasema kila mmoja kwa wakati wake bado anampenda mwenzake lakini huwezi jua tusubiri tuone.

Huyu ndiye mwanaume Huddah anayetamani kumuoa

Socialite mkubwa wa Kenya Huddah Monroe hivi karibuni amefunguka kudai kuwa hatamani kuoleka na mwanaume yoyote kutoka Nigeria.

Mrembo huyu alifunguka kupitia Instagram story yake alidai kuwa kwa sasa amewazoea tabia za wanaume hawa na kwa hivyo hawatamani.

Hata hivyo aliendelea kwa kusema kuwa ingawa kwa sasa bado hajapanga kuoleka…yeye anamtamani Wizkid ingawa pia yeye ni mwanaume kutoka Nigeria.

Aliandika kusema,

“Oh and actually forgot Wizzy was Nigerian. There’s an exception on this marriage thing. I will marry a Nigerian if it’s Wizkid. Baba Nlaaaa.”

Harmonize awataja warembo wawili kutoka Kenya ambao wanampendeza sana

Harmonize alisafiri kuenda Nairobi, Kenya kupigia upato nyimbo zake. Staa huyo kutoka Wasafi Records WCB amefanya mahojiana na vitua vya habari kadhaa jijini Nairobi.

Katika mahojiano na kipindi cha Mambo Mseto ya Radio Citizen hapo jana, Harmonize aliulizwa kumtaja mrembo kutoka Kenya anayemgusa sana.

Mzazi Willy Tuva na Harmonize wakiwa Citizen Radio

Harmonize alicheka na kuwaza kwa sekunde chache kabla ya kusema kwamba Kenya iko na watoto wazuri wengi.  Hata hivyo alisema Huddah Monroe and Vera Sidika ndo wanampendeza sana.

“Suppose kama haugekuwa na Wolper alafu ibidi uwe na mchumba hapa Kenya ni mrembo mgani wa humu nchini Kenya ambaye huwa ana ‘Kugusa’ kinyama?” Harmonize aliulizwa.

“Kenya kuna watoto wazuri kabisa… …mtoto VERA hivi…. mtoto MONROE hivi….wako wengi bana, wote wako sawa,” alijibu Harmonize.

Huddah Monroe

 

Vera Sidika