Idris Aongea na Wanaume Wanatumia Neno Kudamshi.

Mchekeshaji maarufu  nchini idris amefunguka na kuoyeshwa kukerwa na tabia ya baadhi ya wanaume wanaotumia neno kudamshi kama kionjo cha kusifia mtu aliyependeza.Kwa msimamo wa idris neno hilo linapaswa kutumia na jisia ya kike na wala sio ya kiume kama ambavyo watu wengi kwa sasa wamekuwa wakilitumia kwa mazoea.

Hata hivyo katika ukurasa wake wa instagram, idris aliandika kuwa amesikia watu wanaotumia neno hilo wamekuwa weng na kama watu hao wapo na wanaume basi anaomba kuwajua kwa majina ili aweze kuwatafuta na kuwavunja vunja.

 

Idris Amuweka Mpenzi Wake Haradharani.

Mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultan ameonyesha baadhi ya picha katika ukurasa wake wa instagram na kumuweka mwanadada ambae kwa muonekano inaonyesha kuwa ni mpenzi wake kwa kuzingatia pia captions alizokuwa ameweka katika ukurasa wake wa instagram.

Katika ukurasa wake huo, Idris alidokeza kwa kusema kuwa ni bora afichwe asiendelee kuonekana ikiwa ni kama kejeli akiwap mashabiki wanaom-follow, lakini pia katika picha yake ya pili Idris aliandika maneno mengi akijaribu kuwatania mashabiki wake kuwa anasubiri maneno makali watakayotokea pindi mashabiki watakapoona picha hiyo.

 

Utani wa Idris kwa Shiloleh

Mchekeshaji Idris Sultan amemtania Shiloleh huku akimsifia kama mwanamke jasiri anaejiamini na kujituma kuliko wanawake wengine waliozoea kuletea kila siku.Hii inakuwa sio mara ya kwanza wa baadhi ya wasanii kugundua umuhimu wa Shiloleh katika jamii.

Pamoja na kwamba Idris aliandika maneno haya kwa njia ya utani lakini imeleta hamasa sana kwa vijana wengine na kuweka gumzo katika mitandao ya kjamii,

Ana nyumba, ana biashara kama tatu, ana watoto watatu na ameolewa  ni marufu na pia ni baby face .mimi nina kiingereza tu hapa , tuendelee kuendekeza ujinga tutajua nani anamcheka mwenzie.

Idriss Akiri Kuogopwa na Wanawake.

Msanii na mchekeshaji  bongo Idris sultan amefunguka na kuelezea kuwa kwa muda mrefu wanawake warembo bongo  wamekuwa wakimuogopa na kumkwepakuwa nae katika mahusino kwa sababu ya umaarufu wake na kazi yake katika jamii.

Idris anasema kuwa wanawake wengine wenye msimamo wa maisha na wasiokuwa tegemezi wamekuwa wakimuogopa sana kutokana na ukweli kwamba wanao kuwa watakuwa maarufu na kufatwa fatwa na mapaparazi  kutokana na umaarufu alionao mwanaume huyo.

Idris anaongezea kuwa muda mwingine huwa anahisi kuwa kazi yake ya uchekeshaji inaweza kuwa chanzo cha yeye kutokuwa katika mahusiano kwa sababu wanawake wanakuwa wanahisi kama vile anakuwa yupo katika utani wa kuanzisha mahusiano ilhali  muda huo anakuwa makini na anachotaka kukifanya.

kabla hajakutana na wewe anakuwa tayari kaisha ku-judge  kila kitu kiasi kwamba anakuwa tayari amshakufikiria kuwa wewe ni kichaa.wanahisi kuwa sisi comedians hatuko makini katika hilo .wanadhani kuwa sisi hatuwezi kupenda kama wengine  lakini cha ajbau wenzetu huko nje wanapata wanawake wazuri tena pisiii kabisaaa.

Idris ana malizia kwa kusema kuwa yeye kuwa mchekeshaji kuna mfanya ashindwe kupata mwanamke anayemtaka.

Idris aeleza kwanini Wema Sepetu hakuenda kwenye uzinduzi wa viata vyake ‘SultanXforemen’

Idris alihudhuria uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu ‘ Heaven Sent’ ambayo ilifanyika Mlimani City takriban wiki moja hivi.

La kushangaza ni kuwa Wema Sepetu hakuhudhuria uzinduzi wa viatu vya Idria zinazoitwa ‘SultanXforemen’. Uzinduzi wa viatu hivyo uliudhuliwa na mastaa kadhaa akiwemo Iren Uwoya, Gabo,Selin, Mc Piilipili, Ally Rehmtullah,Quick Raka lakini Wema Sepetu hakuonekana.

Idris alidhibitisha kuwa alimualika Wema Sepetu kwa uzinduzi huo. Mchekeshaji huyo alifunguka na kusema kuwa alimpigia simu Wema ambaye alimpa sababu ya yeye kushindwa kuja kwa uzinduzi huo.

“Nilimualika Wema sema unajua nyie wanawake mambo yenu hivyo ameshindwa kuja ikabidi ni mpe ridhaa, wakati naongea naye kwenye simu alivyosema sitaweza kufika basi nikamjibu uliza kiatu,” amesema Idris.