Irene atupa Dongo Gizani

Mwanadada aliyewahi kuwa video vixen ambae kwa sasa ni msanii  “IRENE”, ametupa jiwe gizani na kuwaambai baadhi ya wasanii wamekuwa na tabia ya kuwa na majini maubwa katika mitandao ya kijamii lakini utajiri wao haulingani na kile wanachokimiliki kwa hali halisi.

Hata hivyo mwanadada huyo aliwahi kusemwa sana atika mitandao kuwa amekuwa na jina kubwa na utajiri mkubwa usiolingana hata na umri wake.

Irene ambae kwa sasa hivi amejikita katika kuimba haijulikana dongo hilo amemtupia nani lakini amekuwa na utokuwa na maelewanao na baadhi ya wasichana wenzake kama HAMISA.

 

Siwezi Kufanya Kazi na Tunda, Wema wala Hamisa :- Lyn

Mwanadada ambae alianza kuwa kama video vixen lakini kwa sasa amejiingiza katika muziki irene maarufu kama lyn amefunguka na kusema kuwa hawezi hata siku moja kufanya kazi na wasanii wenzake wa kike wema, tunda au hamisa.

lyn anasema kuwa wasichana ahao aliowataja hawawezi kuwa ma-video vixen kwenye kazi zake kwa sababu watu hao hawana mvuto  wa kutokea katika video za wasanii akiwepo yeye.

Alipokuwa akijibu swali aliloulizwa kuwa endao director atamwambia amtumie Wema , Kimnana , Hamisa au Tunda kuwa video vixen wake atafanya nini, lyn alisema kuwa ” hawawezi kuwa katika nyimbo yangu kwa sababu wote hao hawana muonekano wa kukaa katika video, kwa sababu video vixen  wanatakiwa kuwa sex’

Lyn Nae Kufata nyendo za Hamisa Mobeto

Mwanadada irene ambae ni video queen  ambae pia aliwahi kupata umaarufu sana baada ya kusemekana kuwa amekuwa akitoka kimapenzi na mwanamuziki Diamond Platinumz amejikita rasmi katika maswala  ya muziki huku akiachia wimbo wake mpya.

Wimbo guo unaokwenda kwa jina  la chafu umeandikwa na msanii mwenzake marioo na kuwa directed na hanscana huku ikifanyika nchini Afrika ya Kusini.

Mwanadada huyo anasema kuwa kwa sasa amemua kuijiingiza rasmi katika muziki na anaomba sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki zake, huku akisema kuwa ameshatambulika kisheria na BASATA  hvyo hakuna haja ya mashabiki kuwa na wasiwasi na kazi zake.

 

Irene:-Nilimjua Hamisa kwa Kuonyeshwa Kwenye Picha


Mwanadada Irene aefunguka tena kwa mara nyingine kuwa hajawahi kuwa na ukaribu wowote na mwanadada Hamisa Mobeto ambae inasemekana kuwa ni mke mwenzie kutokana na dada huyokuwa na mahusiano na Diamond ambae pia aliwahi kuwa na mahusiano na  Hamisa na kuzaa nae mtoto mmoja.

Wawili hao wanaonekana kuwa na bifu kutokana na teams zao kuwa wakiwakosoa kila mmoja kwa muda wake na kuwasemea vibaya lakini Irene mwenyewe anasema kuwa hajawahi kukutana na hamisa na wala hamjui kabisa.

Sina ugomvi na hamisa kabisa kwanza hatujawahi hata kuongea wala hatujawahi kukitana sasa unakuwaje na ifu na mt ambae hata hamjawahi kukaa na kuongea  au kuonana hata mara moja.ninaweza kuonana na hamisa na tukaongea na kuwa washkaji lakini kwa sababu sijawahi kuongea nae siwezi kusema kitu.

Hata hivyo mwandishi alipomuuliza Irene kama anamjua hamisa na e alijibu kuwa hamjui kabisa na ameazna kumjua baada ya kuwa akienda katika interviews amekuwa akiulizwa kuhusu Hamisa.

ofcourse simjui kabisa kwakweli zaidi ya kuwa naulizwa kuhusu yeye,  na vile kuwa naonyeshwa tu picha kuwa Hamisa ndo huyo lakini nimemjua siku za hivi karibuni tu wala sio zamani.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa mwanadada huyo kusema kuwa hamjui Hamisa kabisa.

 

Kisa Umri Fake, Zari Ashikiliwa Uwanja wa Ndege.

Mwanadada Zari the bossy alikumbwa na mkasa mzito wiki iliyopitaambapo mwanadada huyo alikwenda nje ya nchi kwa ajili ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa lakini kwa bahati mbaya wakati yuko katia uwanja wa ndege wa Heathrow mwanadada huyo alishikiliwa na polisi katika  uwanja huo.

Habari zinazotolewa ni kwamba Zari alikaa hapo kwa muda kabla ya kuanza safari yake kutokana na habari zilizokuwa zikisambaa sana katika mitandao kuhusu umri wake kuwa sio sahihi ukizingatia kuwa passport yake haikuwa na umri sawa na ule uliokuwa ukisemwa.

Zari ambae siku yake ya kuzaliwa haikwenda vizuri baada ya kushikiliwa kwa msaa 16 akieleka London alikuwa akisemekana kuwa  ana miaka 43 wakati yeye akisema kuwa ana miaka 38.

Hata Wakisema Ninadanga Hainiharibii Kitu.:-Irene

Video queen irene amefunguka na kusema kuwa anashngaa sana watu wanamsema kuwa amekuwa akidanga na kutembea na wanaume tofauti ili kuendesha maisha yake.irene anasema kuwa pamoja na kwamba wanamsema anadanga lakini kwake haimuharibii kitu kwa sababu kwake ina faida.

Irene anaeonekana kama anamjibu mtu aliyempa dongo hilo la kudanga anasema kuwa kama wao wanaona kudanga ni kazi rahisi basi na wao waende wakadange ili wanufaike kama anavyopata yeye.

Hata wakisema kuwa mimi nina danga kwangu hainiharibii kitu, eeh so ninadanga okay so wats up.sijui wengine wanachukuliaje kudanga lakini mimi nina enjoy na ninapenda tu. na yeye kama anaona ni rahisi kudanga akadange.

Video ya Lynn na Mbwa Yawatatiza Mashabiki.

Mwanadada Irene charles maarufu kama Lynn amejikuta katika skenndo nzito baada ya kuachia video katika mtandao wa kijamii akionyesha akiwa na mbwa wake aliyekuwa akimlmamba midomo na kuwachefua mashabiki zake.

Lynn ambae aliwah kutoka kimapenzi na msanii Diamond Platinumz alipata kashafa hiyo  ya kuwa inawezekana akawa na mahusiano ya kimapenzi na mbwa huyo , huko hiyo ikionekana ni kitu cha kuzoeleka kwa wasanii hasa wa kike.

Kuna wasanii wa kike wakubwa kama Wema sepetu na Irene uoya ambao nao pia waliwahi kuoekana wakifuga mbwa na kuwapa mapenzi makubwa sana tofauti na vile inavyotegemewa.

GPL, liliamua kumtafuta moja ya wataalamu wa afya na kumuuliza swala hili limekaaje kwa sababu inaonekana ni kitu cha kawaida kwa wasanii wetu:

Mbwa ana bacteria wengi sana sasa mate yangu yanapogusana na ngozi ya binadamu anamwachia bacteria wengi zaidi,hivyo huwa inashauriwa sana binadamu kukaa mbali na mbwa na hata yake manyoya yake mara nyingi husababisha ugonjwa wa kifua.

 

 

 

Zari ni nani, Simjui Hamisa Mobeto;-LYNN

Mwanadada Irene anazidi kuwashnagaza watu katika mitandao ya kijamii kutokana na kile anachosema kuwa hawajui wanawake wanaotembea na Diamond platinumz. Irene ambae alikumbwa pia na skendo ya kutokakimapenzi na Diamond Platinumz na kusemekana kuwa alipata ujauzito na kuchoropoa anasema kuwa hawajui wanawake hao hata mmoja.

akiongea katika refresh ya wasafi tv, irene anaulizwa kama anajua chochote kuhusu mahusiano ya zari , hamisa na diamond  na anajibu  bila uoga” Zari ndo nani mbona simjui,  mimi simjui hata huyo hamisa mobeto kwa sababu mimi ni lynn mimi ndo simba na mimi ndio lion”

Hii sio mara ya kwanza mwana dada hyo kuulizwa kuhusu mahusiano yake na Diamond na amekuwa akisema kuwa hawajuiwanwake wengine wa Diamond na kuhusu ndoa kama Mungu kapanga yeye kuolewa na Diamond basi ataolewa kwake hana papara.

 

Sina Papara Kuolewa na Diamond;-LYNN

VIDEO Queen Irene Charles ‘Lynn’ ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na msanii wa muziki Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema ametulia na hana papara kwani kama Mungu amepanga aolewe na msanii huyo, lazima itokee!

Akizungumza na Risasi Jumatano, Lynn alisema, hawezi kuleta drama kwenye mitandao kuhusiana na suala lake na Diamond ila anachojua yeye kama Mungu amepanga aolewe naye, itakuwa hivyo na kama siyo basi ataolewa na mwingine aliyepangiwa.

Unajua siku zote ndoa hupangwa na Mungu hivyo kama Dai (Diamond) alipangwa kuwa wangu basi atakuwa wala sina papara, kama hajapangwa kuwa wangu atakuja mwingine,” alisema Lynn.

Bifu la Gigy Money na Irene Lapamba Moto

Msanii wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money aliyewahi kufanya vyema na ngoma yake ya ‘Papa’ amejikuta Kwenye bifu zito na video Queen Irene wa Kwenye wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’.

Siku ya jana kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyowaonyesha warembo hao wawili wakirushiana maneno ya kejeli na matusi ambapo inadaiwa wawili hao walipeana kichapo cha haja.

Kisa cha ugomvi wao kinawemekana kuwa ni kugombania mwanaume Lakini pia inasemekana kuwa kisa ni Diamond kwani Gigy Money ni rafiki wa karibu wa Mobetto ambaye ni mpenzi wa Diamond Lakini pia inasemekana Diamond anatoka na Irene.

Gigy Money na Irene walianza kurushiana maneno Kwenye mitandao ya kijamii muda mrefu lakini hatimaye bifu lao lilichukua sura mpya baada ya wawili hao kukutana Uso kwa Uso wikiendi iliyoisha.

Gigy Money Ametangaza Tena vita na Irene ambapo kupitia ukurasa wake wa Snapchat ameandika ujumbe huu: