Uwoya Ajutia Kuolewa na Mwanaume Asiempenda

Mwanadada Irene Uwoya amefunguka na kuonyesha kuwa mwenye majuto hasa kutokana na ndoa yake iliyovunjia hivi karibuni na kusema kuwa anajutia sana kuolewa na mwanaume ambae hakuwa na mapenzi naye kutoka moyoni.

Irene ambae alishapita katika ndoa mbili tofauti, hakuwahi kuonyesha kujutia au kusema maneno mabaya kuhusu ndoa yake ya mwanzo lakini amekuwa mwenye maneno mengi sana hasa baada ya kuvunjia kwa ndoa yake na Dogo janja.

Ndoa hiyo iliyowahi kuvunja rekodi ilipokuwa inafungwa na hata ilipouwa inavunjika inamfanya Irene kujutia na kusema kuwa anatamani hata kumwambia kila mwanamke kutokusuthubutu kuolewa na mwanaume ambae hayupo katika mioyo yao.

Jamani wanawake wenzangu , hakuna kitu kinauma kama kuolewa na mwanaume ambae hayuko moyoni mwako ni mateso makubwa , hii ilishanitokea na ndio maana ninawasihi, msijaribu kufanya hivyo.Ukitaka kuifurahia ndoa yako olewa na mwanaume unaempenda

 

Uwoya Kumwaga Ajira Waziwazi

Msanii Irene uwoya ameamua kutoa ajira kwa vijana 30 watakaofanya kazi katika club na bar yake ambayo iaanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi huu february.

Irene uwoya mabae alitakiwa kuifungua club hiyo tangu december mwaka uliopita alishindwa kutokana na baadhi ya mambo kutokamilika lakini kwa sasa kila kitu kinaenda kuwa sawa na ataajiri vijana wengi katika bar hiyo.

Akiongea na waandishi, majaji  wa zoezi hilo Mariamu ismail na  Johari chagula wanasema  kuwa mamia ya vijana wamejitokeza katika usaili na wamefanikiwa kuendesha zoezi hilo salama kabisa.

 

Aristotee Aweka Wazi Bifu Lake Irene Uwoya

Aristotee amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na staa wa Bongo movie Irene Uwoya pamoja na kwamba wapo wanaodai hivyo.

Tetesi zilisambaa kuwa Aristoste na Uwoya hawana maelewano Baada ya kumrekodi Dogo Janja akiwa na mpenzi Wake Mpya na kushabikia Penzi hilo wakati akijua wazi alikuwa mume wa Uwoya na ni rafiki yake mkubwa na mteja katika saluni yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Aristote alisema hana tatizo lolote na Uwoya kwa sababu alichokiongea kwenye video iliyosambaa ni kweli licha ya kwamba tangu iliposambaa msanii huyo hajafika tena kwenye saluni yake wakati ndiye staa aliyekuwa akitoa mkwanja mrefu kwa kujipamba.

Kiukweli sijisikii vizuri kabisa kupewa hayo majina (Yuda na mnafiki) nina watoto wanakua kesho wakisikia baba yenu alikuwa anaitwa Yuda yaani msaliti inakuwa haileti maana nzuri kabisa, lakini tangu hayo maneno yasambae mitandaoni hajawahi kuja hapa ofisini kwangu, zaidi ya kukutana naye tu mara moja.

Pia isitoshe hii hainipunguzii kitu chochote kwa sababu naamini Uwoya siyo mtu wa kukaa na kinyongo muda mrefu, pia tatizo kubwa ni hawa wapambe ndiyo wanaomjaza maneno lakini yeye mwenyewe hana tatizo na mtu, ingawa mchumba wa Dogo Janja akija tena kutengeneza nywele dukani kwangu nitamsifia kama kawaida na Uwoya naye akija nitafanya hivyohivyo”.

Siku chache zilizopita Uwoya aliweka wazi kuwa hana Bifu na Aristotee ingawa ameweka wazi kuwa hajawahi kuongea naye kwa muda mrefu.

Uwoya Athibitisha Kuwa Kwenye Mahusiano Mapya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya ameibuka na kukiri kuwa Hivi sasa yupo kwenye mahusiano mapya na mwanaume mwingine ambaye hajamtaja.

Uwoya ambaye aliachana na Mume Wake ndoa ambaye ni Msanii wa Bongo fleva Abdul Chande ‘Dogo Janja’ amesema Hivi sasa ana Mpenzi mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi w Habari kwenye sherehe za uzinduzi wa foundation ya msemaji wa Simba Haji Manara,  Irene Uwoya amesema kwamba ni kweli kwa sasa yupo kwenye mahusiano, na mpenzi wake huyo ni mfanyabiashara.

Ofcourse nipo kwenye mahusiano, yeye ni mfanyabiashara ila siwezi kuwatajia jina”.

Ingawa Uwoya amekataa kumuweka wazi Mpenzi Wake lakini kumekuwa na tetesi kwenye Mitandao ya kijamii kuwa mrembo huyo yupo kwenye mahusiano na mfanyabiashara ambaye ana mkwanja mrefu na ndio anamuweka mrembo huyo mjini kwa sasa.

Uwoya Awatolea Povu Wanaosema Kuhusu Mali Zake

Mwanadad Irene uwoya ameamua kuwajibu watu waliokuwa wakizusha baadhi ya maneno kuhusu mahusiano yake ya sasa huku tetesi zikidai kuwa mwanadada huyo kwa sasa yuko katika mahusiano na kigogo mmoja anaefanya kazi katika serikali ya kenya.

Maneno ya mashabiki yamekuwa mengi kutokana na kuwa mwanadada huyo amekuwa akioneana akila bata non stop katika viwanja mablimbali huku akionyesha jeuri ya pesa katika kurasa zake za mitandao.

Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa watu wamekuwa wakiangaika sana kufatilia maisha yake na kusema mara anatoka na huyu mara yule lakini hakuna mwenye ukweli zaidi ya yeye mwenyewe hivyo waache kumfatilia.

mhhhh bongo jamani, mara natembea na john mara na musa , mara uritho mara mafao ya baba yake, mara hana lolote kwakweli kazi mnayo  na ndio maana hamna kazi za kufanya jua likisogea na nyie mnasogea.daaah ..poleni sana kifupi tu ni kwamba mnajisumbua sana fanyeni maisha yenu….

Kigogo Anayesimamia Bata Za Uwoya Aanikwa

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amedaiwa kuishi maisha ya bata ndefu kwa sababu ya Kigogo mwenye pesa zake ambaye ndio mpenzi wa Uwoya kwa sasa.

Gazeti la ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mtu wa karibu na Uwoya amepasua kuwa Uwoya anapewa jeuri ya pesa na  kigogo mzito aliyepo kwenye Serikali ya Kenya.

Ni kigogo (anamtaja jina, tunalihifadhi sababu hatujam­pata kuthibitisha) katika Seri­kali ya Kenya, ndiye ambaye anamuwezesha kwa kila kitu. Hizi sijui kufuru za bethidei yake, sijui kujiachia kwenye boti hadi Zanzibar kigogo huyo ndiye anayemuweze­sha”.

Chanzo hicho makini kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, kutokana na uzito wa kigogo huyo, imekuwa ngumu kujulikana na hata anayejua pia huhofia kusema.

Ni kutokana tu na uzito wa kigogo huyo na bahati mbaya sana ni kwa sababu yupo Kenya, ingekuwa yupo Bongo ingekuwa ni rahisi sana watu kumjua.

Kigogo huyo ndiye anayed­hamini pia zile safari za mara kwa mara za Uwoya nchini Dubai, nafikiri huwa wanaku­tania huko na huyo kigogo kula zao raha.”

Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Uwoya ambaye alifunguka na kuweka wazi:

Hivi kwa nini kila mtu anapenda kumjua mtu wangu maana marafiki wanapenda kumjua, wasanii wenzangu, mpaka ndugu zangu yaani watu wa­nahangaika kweli jamani Lakini Huyo (anamtaja jina) nampenda sana labda niseme hivyo, siku akija Bon­go watu watafunga midomo yao”.

Uwoya alisisitiza kuwa hawezi kumtaka Mpenzi Wake kwa sasa Lakini muda ukifika atamuweka wazi.

 

Uwoya Atangaza Mauaji Mahusiano Yake Yajayo

Mwanadada Irene Uwoya ametangaza kuwa kwa mahusiano yake yanayokuja baada ya yale yaliyokufa lati yake na Dogo Janja ni lazima kuna mambo mawili yanaweza kufanyika katikati yaani  kuolewa kabisa au kuua.

mwanadada irene anasema kuwa kwa sasa ameshachoshwa na mahusiano yasiyokuwa na tija kabisa hivyo anaona kuwa kama anataka kuingia katika mahusiano kwa sasa inaweza kumfanya kufunga ndoa na kutulia kabisa au kuamua kuua kwa sababu tu yanaweza kuwa yameshinda.

katika ukurasa wake wa instagram, Irene aliandika “My next relationship will either lead to marriage or  my first murder  beacause am tired.”

Florah Afunguka Baada Ya H.Baba Kukiri Kumiss Uwoya

Msanii wa filamu za Bongo movie, Florah Mvungj amefunguka Baada ya mume Wake ambaye ni Msanii wa Bongo fleva H. Baba kukiri kumiss Ex Wake Irene Uwoya.

Siku chache zilizopita H-Baba kupitia  ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya Irene Uwoya kisha kuandika kuwa amemmisi, jambo lililowashangaza wengi kwani siku za nyuma kidogo aliwahi kumponda na kusema haoni ndani kwa mke Wake Flora.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Florah Mvungi amedai haoni tatizo kwa Mume Wake kumkumbuka Aliyekuwa Mpenzi Wake isitoshe amedai yeye hana wivu.

Watu wanakuza mambo sana, mbona ni hali ya kawaida sana, ni kumbukumbu tu ambazo mtu zinamrudia, anafanya anachojisikia, ameona ni vyema kushea kumbukumbu zake na watu kwenye mitandao, sijaona shida yoyote na wala sijahisi wivu“.

 

Kaka wa Uwoya Afunguka Kuvunjika kwa Ndoa ya Dada Yake.

Babuu Uwoya kaka wa Irene Uwoya amesema familia yao kutomkubali Dogo Janja kuwa mume wa Irene Uwoya ndio chanzo cha ndoa hiyo kuvunjika
.
“Hakuna hata mmoja aliyependezewa na hilo suala, na hakuna hata mmoja aliyekuwepo kwenye harusi, sidhani kama ni ndoa, Dogo Janja alikuwa rafiki yangu, kasoma na wadogo zangu, hajawahi kuwa shemeji, mimi shemeji yangu namjua mmoja tu kashatangulia mbele za haki, anaitwa Ndikumana”, amesema Babuu alipoulizwa na East Africa Radio
.
Ikumbukwe miezi mingi iliyopita Mama Irene Uwoya akizungumza na gazeti moja serious hamtambui Dogo Janja Kama mkwe wake kwa madai hana adabu wala heshima ya kuwa mkwe wake

Irene Akanusha Kupewa Talaka na Dogo Janja.

Mwanadada Irene Uwoya anasema kuwa pamoja na yote yaliyowahi kutokea katika mahusiano yake na mume wake na kufikia hatua ya kuachana kabisa lakini bado amekuwa alimpenda na kumkumbuka sana mpenzi wake.

Wawili hao waliofunga ndoa mwishoni mwa mwaka  jana , walifikia tamati ya mahusiano yao baada ya wawili hao kushindwana ndani ya nyumba kwa sababu za usaliti  huku Dogo janja akionekana ndio mkosaji mkuu na kufanya kila mtu kuanza maisha yake.

Hata hivyo baada ya kuachana kwao, Irene amekuwa msemaji sana katika mitandao na vyombo vya habari kila anapohijiwa kuhusu swala hilo huku akikana kuwa hakuwahi kubadili dini ili kuolewa na mwanaume huyio na kusema kuwa hakuwahi pia kupewa talaka.

hata hivyo irene anasema ” sijawahi kupewa tala na dogo janaja na sijawahi kuacha kumpedna hata siku moja lakini kuna mambo mengine lazima maisha yaendelee,  na ndio maana nikasema kuwa sasa hivi niko busy kufanikisha baadhi ya ndoto zangu nilizokuwa nimejiwekea, mambo ya kuolewa nadhani tuwaachie wengine tu”

Hata hivyo irene anasema kuhusu utajiri wake, watu wengi wamekuwa na tabia ya kufuatilia mtu anafanya nini au uanapata wapi ela  bila kujua kuwa kuna wakati unaamua kufanya mambo kimya kimya na baadae yananyooka wanaanza kushangaa.

 

 

Irene Uwoya Adai Kuwa Hataki Kuolewa Tena

Msanii wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya ameibuka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu hataki kusikia maishani Mwaka kwa Hivi sasa Kama kuolewa tena au ndoa.

Uwoya amefunguka na kusema kuwa amefikia kwenye uamuzi huo kwani aliyokutana nayo ndani ya ndoa yameshatosheleza moyo wake hivyo kwa sasa yupo kwa ajili ya kuangalia maisha yake na si vinginevyo.

Katika mahojiano yake aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Uwoya alisema kuna vitu vingi anavyo moyoni, lakini pia anaona siyo vyema kuwapa watu faida na ndiyo maana alikuwa anakaa kimya kwa muda mrefu tangu kusambaa kwa habari zake za kuachana na Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Kiukweli kabisa nimeapa moyoni mwangu sitaki kabisa kusikia kama kuna kitu kinaitwa ndoa kwa sababu nahisi hivyo vitu kwenye maisha yangu vimeshapita, sihitaji kuvirudia, naangalia maisha mengine ya kujiendeleza mwenyewe.

Kama sasa hivi nina kazi kubwa ya kumalizia pub (baa) yangu ya Last Minute (ipo Sinza-Mori, Dar). Kwa hiyo akili yote imeahamia huko”.

Irene Uwoya ameshaolewa ndoa mbili ambapo ndoa ya kwanza ilikuwa na Marehemu Ndikumana ambaye alizaa naye Mtoto mmoja na ndoa ya pili ilikuwa na Staa wa Bongo fleva Dogo Janja ambaye wameachana mapema mwaka huu Baada ya tetesi za kutokuwa na uaminifu.

Uwoya Afungukia Tetesi Za Kuiba Mume wa Mtu

Muigizaji wa Bongo movie nchini Irene Uwoya amefunguka na kuongelea skendo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ya kwamba yeye ameiba mume wa mtu.

Sakata hilo lilianza Wiki iliyopita Baada ya Uwoya kuposti picha akiwa na mwanaume mwingine huku akiwa amemziba uso na kusababisha kuzua maneno lakini mambo yalibadilika Baada ya picha za harusi za mwanaume huyo kusambaa akiwa na mke wake na kupelekea Uwoya kutuhumiwa kwa kuiba mume wa mtu.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Uwoya amewajia juu watu waliozusha skendo hiyo na kusema kuwa hawajui wanachokiongelea kwani mwanaume Yule aliyepiga naye picha ni mjomba ale kabisa.

Ndiyo maana siku zote mimi nawaambia watu waache unafiki maana wako macho kuona Irene (Uwoya) anaharibu, lakini wanashindwa kufuatilia ukweli wa jambo hilo hata kidogo tu.

Yule ni mjomba wangu kabisa jamani, inakuwaje anakuwa mwanaume wangu? Huko si ni kuvinjiana heshima? Tena kubwa na isitoshe mjomba wangu huyo alikuwa na mke wake, lakini kwa sababu watu wanapenda kufuatilia mambo, wakaibuka na hivyo”.

Lakini pia Uwoya amedai kwamba alivyoweka picha yake alijua tu yatatokea hayo ndio maana akaamua kumziba sura yake lakini bado watu walifokonyoa Mpaka wakamjua ni nani.

Nilijua tu ndiyo maana nikamziba sura, kuna wanafiki watajitokeza na kuyaleta yao, lakini kwa hapo wamefeli na tena kama ni mtihani wamepata F au ziro kabisa“.

 

Sheikh Mkuu Amjia Juu Uwoya Baada Ya Kutangaza Msimamo Wake Wa Kidini

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Alhad Mussa amemjia juu Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya baada ya kutangaza kwamba hakuolewa kwa dini ya Kiislamu na aliyekuwa mume wake, Dogo Janja.

Sakata hilo lilianza wiki iliyopita Baada ya Uwoya kutoa kauli iliyodai kuwa yeye sio muislam na wala hajawahi kubadilisha dini alipofunga ndoa ya kiislamu na Dogo Janja kama  watu wengi walivyodhania.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani Shekhe huyo alisema, kauli ya Uwoya kudai kuwa yeye si Muislamu inaonesha kuwa wakati akibadili hakuifuata dini bali mwanaume.

Mwanadada huyo kuchukua uamuzi wa kutaka kuolewa na aliyekuwa mwenza wake hakuridhia kutoka moyoni, hivyo katika ndoa hiyo Uwoya alimfuata mwanaume na wala hakufuata dini“.

Irene Uwoya alifunga ndoa ya Kiislamu na Dogo Janja na kutangaza kuwa, amebadili dini na kuitwa Sheila, hata hivyo baada ya miezi kadhaa wawili hao waliachana kimyakimya bila kuweka wazi ndoa yao kuvunjika.

Uwoya Adaiwa Kuiba Mume wa Mtu

Mwanadada Irene Uwoya ambae hapo siku chache  nyuma alidaiwa kumuweka wazi mpenzi wake mpya walipokua katikaka moja ya shughuli  za kifamilia  wikiendi iliyopita . Mwanadada huyo aliaoneknaha za pamoja ambazo hazikuwekwa katika akaunti ya irene mwenyew.

Kutokana na  ukaribu  wa irene na mwanaume huyo katika shughuli iyo na  hata kupiga picha pamoja,  picha zilianza kusambaa zikiwaonyesha wakiwa  karibu na  ndipo ilipoanza kusambaa kuwa huyo ndio mpenzi wake mpya.

Hata hivyo habari za chini ya kapeti zimevuja na kusema kuwa pamoja na kwamba kurasa za umbea zinasema kuwa   huyo ndio mpenzi wake kwa sasa , lakini  mwanaume huyo ni mume wa mtu.

Pamoja na kwamba ireen hajasema kitu kuhusu tetesi za kuwa na mpenzi mpya lakini wadau wa mambo tayari walitafuta maisha ya mwanaume huyo na kugundua kuwa mwanaume huyo ni mume wa mtu na ana familia yake tayari.

Irene amekuwa akifatiliwa kwa kila kitu anachokifanya kutokana na mahusiano yake yaliyopita kati yake na Dogo janja.

Irene Uwoya Afungukia Mapenzi Yake Kwa JB

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Irene Uwoya ameibuka na kuweka wazi mapenzi yake mazito juu ya msanii mwenzake Jacob Stephen maarufu kama JB.

JB na Irene Uwoya waliwahi kukonga nyoyo za mashabiki kwenye tasnia ya Bongo movie kutokana na movie zao walizoigiza kufanya vizuri na kupendwa sana watu.

Kupitia ukuraaa Wake wa Instagram, Uwoya alimtumia salamu za Birthday JB lakini katika ujumbe Wake alifunguka na kuweka wazi kuwa anampenda sana:

https://www.instagram.com/p/Bq9a16-h50e/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=13ab3f35zngna

JB na Irene Uwoya wameshawahi kuigiza pamoja kwenye filamu zilizowahi kufanya vizuri Kama vile Oprah.

Sijawahi Kubadilisha Dini Yangu na Kuwa Muislamu-Irene Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya ameibuka na kuwatolea Povu zito watu ambao wamekuwa wakimhoji kuhusu kubadilisha dini Baada ya kuachana na Dogo Janja.

Mwaka jana Dogo Janja na Irene Uwoya walishangaza dunia Baada ya kutangaza wamefunga ndoa na kusema Uwoya amebadili dini amekuwa Muislamu na hata jina lake ni Sheila lakini Baada ya kuachana na Dogo Janja amesema hajawahi kubadilisha dini yake ya Kikristo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Uwoya amesema kwa muda mrefu amekuwa akisema kuwa hawezi kubadili dini yake ya Kikristo hivyo watu wafahamu kuwa yeye ni Mkristo na waondoe dhana kwamba alikuwa dini nyingine tofauti.

Nawashangaa sana watu kila kukicha wananiuliza umerudi kwenye dini yako ya awali kama kuna siku hata moja nilishawahi kuwaambia kuwa nimebadilisha dini yangu ya Kikristo yaani siwezi na sijawahi kujaribu”.

Dogo Janja na Uwoya waliachana mwezi uliopita Baada ya tetesi kusambaa kwamba Dogo Janja alichepuka na Msanii Wema Sepetu wakati yupo kwenye ndoa na Uwoya.