Sijawahi Kutunga Wimbo Kumchamba Mtu :-Isha mashauzi

Msanii wa taarabu nchi  ISHA MASHAUZI amefunguka na kukanusha kuwa amekuwa aktunga nyimbo kwa ajili ya kuwa-attack wasanii wengine ikiwa kama njia ya kugombana nao na kuepuka kuwafata moja ka moja.Isha anasema kuwa yeye ndio amekuwa akitunga mashairi ya nyimbo zake lakini hajawahi kufanya hivyo kwa ajili ya kumsema au kumchamba mtu vibaya.

Isha anasema kuwa kamwe haweiz kufanya hivyo na kama kunamwatu wanakaa na kujaribu kutunga nyimbo ambazo zinakuwa ni kama majibu ya nyimbo zake basi anakuwa akijisumbua kwa sababu yeye hashindai na mtu na kama kuna mtu anakaa akifanya hivyo anakuwa akijisumbua tu.

Akijaribu pia kuwajibu wanaomsema vibaya hasa baada ya kuvaa suruali katika nyimbo zake, anasema kuwa kwa kawaida msanii ni lazima kubadilika badilika hivyo yeye haoni kama anakosea kufanya hivyo kwa sababu yeye ni msanii.

Fid Q Ampa Shavu Msanii wa Taarab

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q amempa Shavu Msanii maarufu wa Taarabu nchini Isha Mashauzi katika kazi yake mpya.

Wimbo mpya wa Fid Q unaenda kwa jina la  ‘Bam Bam’ iliyowakutanisha Isha Mashauzi, Rich Mavoko na Big Jahman huku Wimbo huo ukimya umetengenezwa na Marco Chali toka Mj Records.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Fid Q amefunguka na kusema kuwa ameamua kumshirikisha Isha Mashauzi ambaye amezoeleka kuimba muziki wa Taarabu kwa sababu ya uwezo Wake wa kuimba kwa style nyingi.

Yaani kilichotokea Mpaka nikamfikiria nilikutana naye sehemu anaimba covers na nyimbo nyingine nyingine nikasema HA! Mbona mimi nilijua unaimba taarabu tu wewe, akasema hapana mimi naimba muziki aina tofauti tofauti.

Kwaiyo nilipokuwa studio nilisema nahitaji mtu ambaye ana tabia ya kupita na mistari yangu ndio ilifanya apate attention yangu”.

 

 

Habari Njema: Isha Mashauzi Ajifungua Mtoto wa Kike

Msanii wa nyimbo za taarabu nchini Isha Mashauzi amejaaliwa kujifungua salama mtoto wake wa kike siku ya tarehe kumi.

Baada ya kuficha ujauzito wake kwa muda wa Miezi Tisa na kutosema ana ujauzito pale alipohojiwa na Media mbali mbali hatimaye Isha ametoa siri yake baada ya kujifungua.

Isha ametoa taarifa hiyo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika maneno haya: