Harmonize Amwagia Povu Zito Wolper Baada Ya Tetesi Za Kurudiana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amejikuta anamtolea povu zito aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper baada ya kusambaa kwa taarifa za Kurudiana.

Siku chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wolper na Harmonize wamerudiana baada ya Wolper kuposti jina la Harmonize.

Sakata hili lilianza baada ya Wolper kuposti picha kadhaa alizoziambatanisha na Jina la Raj ambalo lilikuwa ni Jina alilomuita Harmonize kipindi cha Mahusiano jambo lililoibua tetesi za wawili hao Kurudiana.

Lakini kabla ya Tetesi hizo kusambaa vizuri Harmonize alimjia juu Wolper baada ya kuulizwa na mashabiki zake kama kweli amemtosa Mzungu wake Sarah na kuamua kuwa na Wolper ambapo alijibu:

Anajitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe bila hata haya wakati tuma msiba wa ndugu yetu, na mwingine katekwa yeye analeta pombe zake hapa”.

Tangu Harmonize man wolper walipoachana wamekuwa maadui wakubwa huku mara kwa mara wakirushiana vijembe Kupitia social media na mara ya mwisho Harmonize alianika Orishas ya wanaume wote ambao Wolper alibanjuka nao.

Wolper- Wanaume Wengi Wanatumia Wasanii Wa Kike Kwa Kiki

Muigizaji wa Bongo Movie na Mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper ameibuka na kudai ni ngumu kwa Mastaa wengi wa kike kupata wanaume wenye mapenzi ya dhati kwani wengi wao wanataka kuwa nao kwa ajili ya umaarufu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Wolper alisema kuwa mara ny­ingi wanaume wamewachuku­lia wasanii kama daraja la kusonga mbele au kukuza majina yao lakini siyo mapenzi ya dhati.

Ni hivi mas­taa wengi hasa kwenye tasnia ya uigizaji wameamua kufanya maisha yao wenyewe na kusahau kabisa kama kuna jambo la kuolewa na ndiyo maana unaweza kukaa hata miaka mitano bila kusikia msanii wa kike ameolewa”.

Wolper amekuwa na Mahusiano na wanaume kadhaa ambao kiukweli aliwapa umaarufu wakati wa Mahusiano yao kati yao ni pamoja na staa wa Bongo fleva Harmonize ambaye alijizolea umaarufu sana alipokuwa na Wolper na muziki wake kukua.

Wolper Awaombea Msamaha Soudy Brown na Maua Sama Wanaosota Rumande

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Mrembo Jacqueline Wolper ameibuka na kuwaombea msamaha mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown na msanii wa Bongo fleva Maua Sama.

Maua na Soudy wamewekwa ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips wakiwa wanakanyaga pesa.

Wolper amejikuta akiguswa na kitendo hicho cha kuwekwa ndani ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema anaomba viongozi wakubwa wa nchi wawaachie wasanii hao kwani walikuwa kwenye utafutaji na badala yake adhabu waliyoipata kwa siku hizi tatu liwe funzo kwa wengine.

 

Katika utafutaji Kuna mitihani Mingi Sana. Nachoweza kusema Nikuomba Tuu wakubwa muwasamehe vijana wenzetu Naamini katika Hili lililotokea Basi wengine wengi watajifunza kitu kupitia hili Naomba niwaombee masamaha wa Dhati kabisa Ndugu zetu Na wawe huru kuendelea Na majukumu yao inshallah. Maua & Soudy na wengine wore mliopo Ndani Juu ya hili sio sawa kutaja wote lakini hawa niwawakilishi poleni saanaa Jamani Ndani sio kuzuri“.

Mpaka sasa inadaiwa wawili hao bado wapo ndani bila dhamana.

Wolper Amwaga Povu Zito Kisa Muna

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper amejikuta akiporomosha mvua ya matusi pale alipoulizwa kuhusu sakata la Muna.

Muna ametawala vichwa vya habari kwa wiki kadhaa kufuatia skendo yake ya kumtelekeza mtoto wake wa kwanza anayeitwa Brian na majibizano a familia yake Kwenye vyombo vya habari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Jacqueline Wolper amewajia juu watu wanaoingilia ugomvi wa familia za watu wanaowaona Kwenye mitandao ya kijamii.

Watu wa Instagram ni washenzi na hawajielewi, tena ni wapuuzi na wapumbavu. Kazi kufuatilia maisha ya watu tu, kwa nini wasimuache Muna mambo yake na familia yake, kila mtu abebe msalaba wake”.

 

Nina Ndoto Ya Kumvalisha Rihanna Kwenye Video Zake-Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Jacqueline Wolper ambaye amekuwa akishona nguo zake kama fundi cherehani amefunguka na kudai anataka kumvisha staa wa kimataifa Rihanna.

Wolper amevaa cha watu midomo wazi baada ya kusema Yupo katika harakati za kumtafuta Mwanamuziki wa kimataifa kutoka Marekani Rihanna ili aweze kumshonea nguo ili aweze kuvaa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Waandishi wa habari katika red carpet ya event ya Jibebe Challenge Wolper alifunguka:

 Kwa sasa bado naendelea kusoma nikimaliza nadhani nitaendelea na preocess za kumtafuta Rihanna kwa ajili ya kumvalisha na shukurani kwa mitandao ya kijamii ambayo imenipa wepesi wa kumtafuta Rihanna”.

Wolper ameswashangaa wanaodai haitawezekana kwake yeye kuwavalisha mastaa wakubwa kama Rihanna na kusema kila kitu kinawezekana ni kuweka juhudi Kwenye kazi.

Wolper Awashukia Wasanii Wanaoishi Maisha Feki

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Jacqueline Wolper amewatolea povu mastaa ambao wamekuwa wakidanganya maisha yao kwa kuweka vitu feki Kwenye mitandao ya kijamii.

Wolper amefunguka na kudai huu ndio mwaka wa mastaa hao kutupilia mbali maisha feki feki wanayoishi na kuanza maisha yao ya kihalisia waachane na yale ya mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Wolper alisema wengi wanajipotosha wenyewe kwa kudanganya maisha waliyonayo, jambo ambalo siyo sawa kwa sababu wanapaswa kubuni vitu vingi vya maendeleo kuliko kujionesha kwenye mitandao kuwa maisha yao ni bomba kumbe hakuna chochote

Hakuna kitu ninakichukia kama maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii, ninayachukia kwa sababu ipo siku mtu atakuja kuona maisha yangu halisi ashangae hivyo inapaswa kila mmoja kuishi vile Mungu amempangia na siyo kuigiza, hayo maisha feki tuyatupe kule”.

 

Wolper- Mapenzi na Ali Kiba Yalikuwa Bora Zaidi

Staa wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Jacqueline Wolper ameibuka na kudai hakuna mwanaume ambaye alikuwa mpenzi bora kwake kama ilivyokuwa kwa staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Wolper ambaye siku za nyuma amewahi kukiri kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa muda mrefu na Ali Kiba ingawa hawakuyaweka hadharani na kujulikana na mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyiwahi kufanya na East Africa Television, Wolper amefunguka na kuongea haya:

Katika Mahusiano yangu yote ambayo nimewahi kuwa nayo, ambayo naweza kuyapa namba moja na yalikuwa mazuri na ni the best ni yale nilipokuwa na Ali Kiba. Lakini sio kwamba namiss hapana ila tu ninasema yalikuwa Mahusiano bora niliyowahi kuwa nayo”.

Mbali na Ali Kiba, Wolper ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mastaa wengine kama Harmonize, Juma Jux na wengineo.

Wolper-Wanaume Wote Nilioachana Nao Bado Wananipenda

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Diva Jacqueline Wolper ameibukana kudai kuwa katika Mahusiano yake yote ambayo amewahi kuwa nayo wanaume anaoachana nao bado wanakuwa wanampenda.

Wolper amefunguka kuwa katika maisha yake yote anapokuwa anaachana na wanaume aliokuwa nao Kwenye Mahusiano wote wanakuwa bado wanamuhitaji licha ya yeye kuwatema na kutowahitaji tena.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Wolper ambaye ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mastaa kadhaa Bongo ikiwemo staa wa Bongo fleva Harmonize amefunguka:

Ujue mimi kila nikiachana na mwanaume anakuwa bado ananipenda, pale nilikimbia kwa sababu nikiachana na boyfriend, huwa sipendi niendelee kuwasiliana naye wala kusogeleana naye, sipendi kusalimiana na X.

Ilishawahi kutokea X ananihitaji kwa ajili ya mambo ya kibiashara lakini kwa sababu nakuwa sihitaji kabisa kuwasiliana nao nili-crash halafu nikakosa dili, hilo ni pepo ambalo ninalo nadhani nitamwambia mchungaji aniombee”.

Lakini pia alizungumzia sakata la kutemwa kama jaji wa shindano la Miss Lake Zone na amedai kuwa waandaji wa shindano hilo walitumia jina lake kutafutia kiki baada ya Shindano lao kubuma.

Wolper Atangaza Kuokoka na Kumrudia Mungu

Msanii maarufu wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kudai ameamua kumrudia Mungu na kuokoka ili aweze kuishi maisha ya wokovu.

Wolper amedai kuwa hivi sasa amemrudia Yesu na kumtumikia kiukweli kweli na kusema anampenda sana Yesu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers , Wolper alisema ameamua kuokoka kwa sababu anatambua mbali na maisha ya duniani kuna maisha ya mbinguni, kwa hiyo ni vyema akaandaa maisha hayo pia na siyo kujisahau kana kwamba hataondoka duniani.

Kiukweli kwa sasa nimeamua kuokoka na kumrudia Mungu, nina uhakika kwa kufanya kwangu hivi niko kwenye mikono salama na mambo yangu yataninyookea zaidi kuhusu uvaaji wangu siyo tatizo kwa sababu siku hizi tunaokoka kisasa”.

Lakini pia Kwenye Interview hiyo Wolper aneweka wazi sababu iliyomfanya ahamishe makazi yake kutoka Tanzania kwenda nchi ya jirani ya Kenya ni masomo kwani kwa sasa anasomea masuala ya ngozi na urembo.

Wolper Atamani Mahusiano Ya Kimapenzi na Raisi

Msanii wa filamu za Bongo Movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kudai anatamani sana kama angetoa Penzi lake kwa Raisi.

Wolper amedai anaona ni bora kama atakuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa sasa statute Penzi pa Raisi yoyote Afrika kwani atakuwa salama zaidi kuliko kufaidi Penzi na wadananda wengine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Wolper alisema mara nyingi amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume ambao mwishoni wanamsaliti jambo ambalo halipendi na linamkera, lakini anaamini akimpa moyo wake wa upendo Rais yeyote Afrika anaona atakuwa salama.

Unajua ndoto yangu mimi ningependa kutoa penzi langu kwa Rais maana najua kabisa, kwanza atakuwa ananiheshimu na itakuwa ni ngumu sana kunitenda kama wafanyavyo wengine na hapo nitatulia kabisa wala sitakumbuka wanaume wazugaji“.

Wolper amekuwa muwazi kuhusu maumivu anayokutana nayo Kwenye  mapenzi yake ambapo uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Harmonize uliisha baada ya kumuacha na Harmonize kuanza Mahusiano na sarah ambaye ana kipato kikubwa.

Jacqueline Wolper: Sina Tatizo na Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hana bifu na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Zari The Bosslady.

Wolper amefunguka hayo siku chache baada ya Zari kuingia kwenye bifu zito baada ya kuwaambia wasanii hao wasikanyage kwake maana watachafua na wasanii kadhaa wa Bongo movie ambao ni Wema,Aunty Ezekiel, Faiza Ally, Shamsa Ford na wengineo.

Wasanii hao ambao wamerushiana maneno na Zari Mtandaoni wameweka wazi kuwa hawawezi kwenda Tena Kwenye Birthday ya Tiffah huko nchini South Africa kutokana na maneno ya Zari.

Jacqueline Wolper yeye alidai kuwa hana tatizo na Zari kabisa, wanaheshimiana iwapo atakuwa amerejea kutoka shule ambapo anasoma kwa sasa, atakwenda tu.

Shule ndio inaweza kunizuia lakini nikiwa nimerejea nitakwenda tu kwani sina tatizo na Zari“.

 

Wolper Adai Hataki Penzi La Mwanaume Ambaye Sio Mtanzania

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kudai hawezi kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mwanaume ambaye sio Mtanzania.

Wolper ameweka wazi kuwa hawezi Tena kuwa Kwenye Mahusiano na mwanaume ambaye sio Mtanzania kwani alishajifunza siku za nyuma hivyo hawezi kurudia tena.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Wolper alisema kama ni kumpata mpenzi ambaye anaamini atamfaa basi lazima atoke ndani ya nchi yake japokuwa kuna watu walianza minong’ono kuwa alipokuwa nchini Kenya hivi karibuni, alikuwa na mpenzi raia wa nchi hiyo.

Sifikirii kabisa kutoa penzi langu kwa mwanaume ambaye siyo raia wa nchi yangu kwa sasa kwa sababu huko nyuma nilipitia huko lakini sasa sihitaji tena kama nimeamua kupendana na mwanaume basi atakuwa ni wa nchi yangu tu”.

Wolper ambaye kwa sasa aneweka makao nchini Kenya ameshawahi kuwa Kwenye na raia wa Kongo.

Wolper Amkingia Kifua Steve Nyerere Kwenye Suala la Rambirambi

Msanii wa filamu za Bongo Movie Jacqueline Wolper ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Steve Nyerere na kumtaka asivunjike moyo kusaidia wengine.

Steve Nyerere amekuwa Kwenye headlines za mitandao ya kijamii kwa muda sasa huku skendo ambayo imekuwa ikimuandama ni ya kila pesa za rambi rambi anazokusanya Kwenye misiba ya watu.

Na ishu hii imerudi  kwa kasi Tena mara baada ya Steve Nyerere kuonekana akiwa mstari wa mbele siku ya leo kwa ajili ya kuandaa msiba wa msanii Mzee Majuto.

Wolper ameibuka na kumkingia Steve na kumpa moyo kwa kazi nzuri anayofanya ya kuwasaidia watu ambao ni wafiwa na kumtaka ayapuuze maneno ambayo yamekuwa yakisemwa juu yake:

https://www.instagram.com/p/BmPJJuDlj1d/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=gh0ae9yptkq7

Jacqueline Wolper Akiri Kuteswa Na Mapenzi

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kutaja vitu ambavyo vinamtesa akiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Katika Interview yake na Wasafi Tv, Wolper ameweka wazi kuwa vitu viwili ambavyo ni  muda na uongo ni vitu vinavyomtesa akiwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi.

Kitu kinachonitesa na kunipa stress kwenye kwenye mahusiano ni uongo na muda. Nafanya sana kazi lakini nahitaji sana muda wa kuwa na mtu wangu, kwa hiyo uongo na muda ni tatizo sana kwenye mahusiano.

Mtu akiaanza kunidanganya au kunipa muda mchache wa kuwa naye na kuwa out of mood kabisa na ninaweza nikaamka nikamwambia it’s over bila kujali chochote”.

Lakini pia Wolper amesema uongo pekee ana kukubali Kwenye Mahusiano ni uongo mzuri:

Uongo ninaouhitaji mimi ni ule kunidanganya kuwa unanipenda, tangu nizaliwe sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe, huo ndio uongo unahitajika kwa kila mwanamke”.

 

Wolper Amwaga Povu Baada Ya Tetesi Za Kutoka na Mr. Nice

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemwaga povu baada ya tetesi kusambaa anatoka kimapenzi na msanii mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice.

Siku chache zilizopita Wolper na Mr. Nice walionekana pamoja wakila bata Kwenye club moja Nairobi nchini Kenya huku wakionyesha kuwa na ukaribu fulani.

Kwenye video ambayo iliwekwa Mtandaoni na Jacqueline Wolper iliwaonyesha wawili hao wakila bata yaani Wolper akivuta shisha huku Mr. Nice akinywa pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.

Baada ya Tetesi hizo za Mahusiano gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni mmoja.

Watu wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja, projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa bado ni mapema kuitangaza”.