Shamsa Ford: Sina Bifu na Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kusema hana bifu lolote na staa wa muziki wa Bongo fleva Harmonize hata baada ya kumdhalilisha mume wake .

Wiki chache zilizopita Harmonize alikuwa kwenye vita kali ya Ex wake Jacqueline Wolper na katika ugomvi wao alimtaja mume wa Shamsa Chidi Mapenzi kama mmoja wa mpenzi wa zamani wa staa jambo ambalo lilimkera Shamsa.

Shamsa aliweka wazi kuwa hajafurahishwa na maneno ya Harmonize kumuingiza mume wake Kwenye bifu lake na Wolper na kumdhalilisha wakati anajua wazi kuwa ameoa tayari.

Kwenye mahojiano na FNL ya EATV, Shamsa amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.

Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao.

Nilipaniki lakini mwisho wa siku simchukii na sina bifu naye niliongea nilichokuwa najisikia na yameisha na hata tukikutana tunasalimiana vizuri kwa sababu hatuna bifu. Sisi ni vijana tunahitaji kuweka nguvu nyingi sana katika kufanya kazi na sio mabifu”.

 

Jacqueline Wolper Amvulia Kofia Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemvulia kofia aliyekuwa mpenzi wake msanii wa Bongo fleva kutoka WCB, Harmonize na kukubali bifu lao liishe.

Kwa muda wa wiki nzima sasa Wolper na Harmonize wamekuwa Kwenye vita ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii huku kila mmoja akidai mwenzake bado anampenda na bado anamtaka.

Wolper ameamua kupiga kimya ili bifu lao lilikuwa linaendelea liishe tofauti na juzi na siku zilizopita ambapo alikuwa akipewa Dongo lolote na Harmonize alikuwa anajibu.

Siku ya jana Harmonize alihaidi kuendeleza mtanange huo baada ya kudai anataka kuweka listi nyingine ya wanaume waliotembea na Wolper baada ya mara ya mwisho kuweka listi ya wanaume kumi na mbili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliandika ujumbe huu kuashiria hatomjibu Tena Harmonize:

Mungu nifundishe kunyamaza, we ndio unaujua ukweli #Najifunzakuheshimkilangaziiliyonifikishanilipo
#NdiomaanataupambanesiwezkushukaatanishushaMungupekee #jifunzekuheshimkilangaziiliyokufishaulipokamweutoteterekakwajarbulolote
#MunguwanguwaushindiwewenijbuToshaNimekukabidhiwewekilakitu

 

Harmonize Amlipua Wolper na Kumuanikia Listi Nzima Ya Wapenzi Wake

Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize ameingia Tena Kwenye bita ya maneno na Ex girlfriend wake staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.

Siku ya jana kuna video ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Wolper akimrushia Dongo Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita Mlezi wa wana baada ya taarifa kusambaa kuwa kamtosa Harmonize na kumchukua Mwarabu Fighter.

Baada ya kuona video hiyo, Harmonize alitokwa na povu zito kwani kwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema yeye sio Mlezi wa wana ila Wolper ni Mlezi wa Wana na kuambatanisha na listi kamili ya wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano.

Hii sio mara ya kwanza kwa Harmonize na Wolper kuwa na sintofahamu na hata Wolper na mpenzi wa Harmonize Sarah.

Wolper Amtupia Dongo Zito Sarah Wa Harmonize na Kudai ni Mlezi Wa Vijana

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amemtupia Dongo zito Sarah baada ya habari zake za kumtosa Harmonize na kumchukua Bodyguard wa Diamond, Mwarabu Fighter.

Siku mbili zilizopita stori iliyotrend kupita zote ni ya mpenzi wa Harmonize Sarah kumtosa mpenzi wake na kumchukua Mwarabu Fighter.

Inasemekana Sarah amefufa ameoza kwa Mwarabu kiasi ya kwamba anamuhudumia ipasavyo yaani kampangishia hadi nyumba yaani zile huduma zozote alizokuwa anapata Harmonize zimehamia kwa Mwarabu.

Kama utakumbuka Kuwa Sarah na Wolper ni maadui wakubwa na kisa kikiwa ni penzi la Harmonize na juzi tu wametoka kumgombania Harmonize.

Baada ya tetesi hizo za usaliti kusambaa mitandaoni Sam Misago Tv walimsaka Wolper na kumuuliza nini maoni yake juu ya ishu hii kumuhusu Sarah na Wolper ameishia kumtupia dongo zito Sarah:

Duh iyo ishu mbona ni exclusive kabisa sijaisikia lakini freshi tu mbona yule demu ni Mlezi wa wana labda kachoka kumlea mwana kaamua kumchukua mwana mwingine freshi tu”.

Bifu laWolper na Sarah lilianza baada ya Sarah kuanza kuchepuka na Harmonize wakati Wolper yupo Kwenye Mahusiano na Harmonize.

 

Harmonize- Nipo Tayari Kumuoa Sarah

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kumuoa mpenzi wake Sarah.

Kwa muda mrefu kumekuwa na maneno mengi kuhusu Mahusiano ya Harmonize na Sarah huku wengi wakidai Harmonize hana mapenzi ya kweli kwa Sarah bali yuko naye kwa ajili ya pesa.

Huku dhana hiyo ikiwa imepandikizwa na Ex wa Harmonize, Jacqueline Wolper ambaye alisema Harmonize alianzisha Mahusiano na Sarah wakati wako pamoja kwa sababu alikuwa anamuwezesha kifedha.

Lakini Harmonize ameibuka na kuweka wazi kuwa anampenda Sarah na hivi sasa yuko tayari kumuoa mwanamke wake huku akipuuzia maneno yote ambayo yanasemwa na watu.

Kwenye mahojiano na The Playlist ya Times Fm, Harmonize aliweka wazi mipango yake ya ndoa baada ya kuulizwa na Lil Ommy kama ana mpango wa kumuoa Sarah:

Ndiyo nataka nimuoe Inshallah”.

Harmonize anafanya vizuri na nyimbo zake mbili ambazo ni Kwa ngwaru aliyomshirikisha Diamond Platnumz na wimbo wake mpya Dm Chick ambao amemshirikisha Sarkodie.

Wolper Atabiri Kifo Cha Bongo na Kuwataka Wasanii Waache Unafki

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Masawe maarufu kama Jacqueline Wolper ameibuka na kuweka wazi kuwa Bongo movie imekufa na kuwataka wasanii waache unafiki.

Wolper alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kutokana na uhodari wake katika sekta ya kuigiza lakini siku za hivi karibuni amegeukia ujasiriamali na kujiingiza Kwenye ufundi cherehani.

Wolper ametoa povu zito kwa wasanii wenzake kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwaasa waache unafki ili sanaa isonge mbele Lakini pia ametabiri kifo cha tasnia hiyo:

Natamani Bongo movie Tupendane saana yani saaaaana, kiukweli na syo kinafk kiasi kwamba ata mtu akitokea akamuongelea bongo movie vibaya basi wote tusimame nae paka ajute kwanini kafanya hlo tukio, lakini maskin ya Mungu mchawi wetu kafa atujui kaburi lake tukamuombe Radhi atusamehe tuwe huru..yani Mtu akikosea ndio kwanza Tunakandamiza nakuonyesha wasioliona lile kosa ichi ni kilio nanimsiba mkubwa R.i.p Bongo movie.
Acha nipambane na cherehani zangu niangalie nijinsi gani nakomboa mafundi chereani na Tuheshimike Tanzania hope Mafundi chereani amtoniangusha na amtokua wanafki”.

 

 

Wolper Awatolea Mate Cardi B na Rihanna

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper ameibuka na kuweka wazi kuwa anawakubali sana wasanii wawili wakubwa ambao ni Cardi B na Rihanna angependa siku moja awavalishe.

Wolper anamiliki duka lake la mavazi ama boutique inayojulikana kama House Of stylish na amewavalisha wasanii kadhaa na nguo zake anazovaa anahusika mwenyewe kuzishona.

Wolper amefunguka na kuweka wazi ndoto zake kubwa katika sekta ya fashion ni kufika mbali kimataifa zaidi mpaka kuwavalisha wasanii wakubwa duniani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo5 Wolper amesema moja ya ndoto zake ni kuja kuwavisha wasanii wakubwa Marekani kama Rihanna na Cardi B.

Rihanna na Cardi B ndio wana swagger zangu kwa hiyo ni watu ambao ninatamani kuwavalisha, na ninajua one day yes..

Mitandao inaonyesha na inathibitisha kwamba nimebuni kitu one week akaja akavaa Rihanna, nimebuni kitu one day, kesho yake anakuja anavaa Cardi B”.

Kibongo Bongo Wolper ameshawavalisha mastaa kama msanii wa Bongo movie Aunty Ezekiel na wasanii wengine kama Gigy Money na wengineo.

Wolper: Siwezi Kusapoti Tena Kazi Za Harmonize

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hawezi hataweza kukaa na kusapoti kazi za Harmonize sababu anamuonea huruma mpenzi wake Sarah.

Siku chache zilizopita Wolper alitengeneza headlines kwenye mitandao ya kijamii baada ya yeye na mpenzi wa Harmonize Sarah kurushiana vita ya maneno kwenye Instagram.

Ambapo Sarah alimtaka Wolper aache kumtumia Meseji za kumtaka Mpenzi wake Harmonize jambo ambalo lilinkera Wolper kwani aliweka wazi kuwa akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa hivyo hakuwa yeye aliyekuwa anatuma Meseji.

Kwenye mahojiano aliyofanya leo na Sam Misago Wolper amesema kuwa ameamua kuacha kabisa kusapoti kazi za Harmonize:

Mimi sio mswahili na wala sina uswahili tulianza mapenzi kwa mimi kusapoti kazi zako lakini sasa naona ili nisikwaze mahusiano yako naona bora nisisapoti kazi za Harmonize kwa sababu yule mwanamke wake anahitaji kuhurumiwa”.

Lakini pia Wolper amesisitiza kuwa amefikia uamuzi wa kumblock Harmonize na Sarah kwenye Instagram ili aepushe maneno maneno.

Wolper: Nisha Hana Vigezo Vya Kutembea na Brown

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa Salma Jabu  maarufu kama Nisha Bebe hana vigezo vya kutembea na Ex boyfriend wake Brown.

Wiki iliyopita picha za Nisha na Brown zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa wanakumbatiana na hata kubusiana jambo lililozua maneno huku ilisemekana kuwa ni wapenzi.

Lakini mwishowe Nisha aliachia wimbo wake wa Bachela ambapo ilionekana kuwa Brown alikuwa ni video king Kwenye video hiyo na wawili hao baadae walikana tetesi zozote za Mahusiano ya kimapenzi wakidai ilikuwa ni kazi tu.

Hatimaye Wolper amefunguka kuhusiana na Mahusiano hayo na kuweka wazi kuwa haamini kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Wolper amedai kuwa Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.

Wolper: Sarah wa Harmonize Ana Matatizo Ya Kisaikolojia, Anahitaji Msaada

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu, Jacqueline Wolper amemtolea povu zito hasimu wake namba moja Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Ex boifrendi Harmonize.

Siku ya jana Wolper na Sarah waliongia kwenye vita ya maneno kwenye mitandao ya kijamii baada ya Sarah kwa mara nyingine kumtuhumu Wolper kwa kumtaka Harmonize.

Sarah alimpa onyo Wolper na kumtaka aache kuongea na Harmonize ambapo alitupia screenshots za meseji ambazo amekuwa akimtumia Harmonize huku imeonekana wazi kuwa hamjibu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Wolper amemjia juu Sarah huku akidai lazima atakuwa na ugonjwa wa kisaikolojia na kutaka watu wampe msaada:

Hivi ni vitu vya kuona huruma na kusamehe kwa sababu yule dada ana wasi wasi maskini anaamini kwamba nitachukua chombo chake wakati mimi muda huo sina lakini anajua mimi ni kiboko yake kwaiyo anaamini kuwa nitamchukua kitu ambacho siwezi mimi nikipita nimepita siwezi kumchukua tena na cha muhimu yule dada anahitaji mtu wa kumpima akili yule dada sio mzima ana matatizo ya kisaikolojia haiwezekaani kitu kidogo analipuka vile”.

Wolper amefunguka kuwa akaunti yake ilikuwa hacked na mtu ambaye ali hack alikuwa anatuma meseji kwa watu mbali mbali dm ikiwemo kwa Harmonize.

Wolper na Sarah Warudi Vitani Kwa Ajili Ya Penzi la Harmonize

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper na Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

Baada ya kutolewa povu hilo, Wolper alimrudishia kombora hilo Sarah na kuandika maneno haya:

 

Hii  sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

Sijawahi Kuachwa na Mwanaume Hata Siku Moja- Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kuachwa na wanaume.

Kumekuwa na stori nyingi Za kimbea mtandaoni ambazo zinaongelea kufeli kwa mahusiano ya Wolper na wanaume mbali mbali anaokuwa nao kwenye mahusiano.

Kiukweli kabisa Wolper ni moja kati ya watu waliokuwa na bahati mbaya kwenye mahusiano inawezekana ikawa pia ni wanaume ambao anachagua kuwa nao.

Kwa mwaka Jana pekee Wolper alikuwa kwenye mahusiano na wanaume watatu tofauti ambao ni Harmonize, Brown na Engine.

Lakini hivi sasa Wolper anaweka wazi kuwa mahusiano yake kuvunjika sio yeye mwenye makosa na wala hajawahi kuachwa yeye ndio anaacha kwenye mahusiano.

Wolper amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na The playlist ya Times FM ambapo ameongea Mengi zaidi:

Kiukweli kabisa naamini kuwa hakuna siku ambayo Ex wangu hata mmoja ambaye ameshawahi kuja kuniongelea vibaya Kwenye Interview yoyote kwaiyo kama ningekuwa na matatizo wangekuwa wanakuja kuniongelea vibaya kwaiyo mimi na wao ndio tunajua ukweli kuwa nani ana matatizo  Lakini pia sipendi sana kuongelea maex ila kikubwa ambacho kipo kwangu sipendi ujinga na sipendi kuonekana mpumbavu kwa sababu mimi ni mzuri najiamini natafuta hela yangu napenda kazi yangu na napenda kuheshimiwa kwaiyo kama ukinizingua nakufuta na by the way sijawahi kuachwa”.

 

 

Wolper- Cardi B Ndio Kaniiga Vazi Langu

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeuka Mwanamitindo Jacqueline Wolper anayemiliki boutique lake la mavazi linalojulikana kama ‘Wolper House Of Stylish’ amedai Cardi B kamuiga kuvaa vazi lake.

Wolper amedai kuwa staa wa kimataifa rapper kutoka Marekani Cardi B anayefanya vizuri hivi sasa ameiga vazi lake alilolishona mwenyewe na kulivaa siku ya Jumamosi kwenye Vikings Night Show ya Papii Kocha.

Wolper ameibuka na kusema Cardi B amemuiga kwani yeye alivaa vazi lake siku ya Jumamosi tarehe kumi na Cardi B alivaa gauni lake Jumapili tarehe 11 kwenye iHeart Music Awards.

Wolper ametokwa na povu na kuwalaumu Watanzania kwa kuwa na Double standards kwani Cardi B alivyovaa lile gauni wamemsifia lakini yeye wamemponda na kudai kama anataka kupaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper alitokwa na povu hili:

Young Lunyo Afungukia Tetesi za Kulimendea Penzi la Wolper

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayechipukia kwa kasi ya ajabu Young Lunyo anayeunda kundi la OMG amefunguka na kumuongelea msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper na uwepo taarifa za mahusiano kati yao.

Wolper ni moja kati ya mastaa wa Bongo movie ambaye mara kwa mara amekuwa akihusishwa na wanaume wadogo kiumri maarufu kama viben-10 au serengeti boys kwaiyo watu walivyoona wana mazoea sana hasa kwenye Instagram utaona Young Lunyo anamposti sana Wolper.

Bongo 5 wanaripoti kuwa Young Lunyo amekana tetesi hizo na kudai hazina ukweli wowote ila zimesababishwa na ukaribu ambao walionao wawili hao kwa ajili ya mazoea waliyojijengea:

Wolper ni dada yangu ambaye ananipa sapoti katika muziki wangu na nilivyopata hizo taarifa sikujisikia vizuri kwa kweli, nilijisikia vibaya kwa kuwa tunaheshimiana sana, sijashangaa sana kwa maana ni msanii kwaiyo lazima ingekuwa Ivyo”.

Lakini Young Lunyo amedai kwa upande wake tayari ana mpenzi wake lakini pia Wolper amedai ana mpenzi lakini asingependa kumuweka wazi kwa sasa mpaka muafaka utakapowadia.

Jacqueline Wolper Akemea Wasanii Wanaovaa Nusu Uchi

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amewajia juu wasanii wenzake wa kike ambao mpaka leo wanaendelea na tabia ya kuvaa nusu uchi kwenye mitandao ya kijamii.

Mapema mwaka huu serikali iliingilia kati suala la wasanii kuvaa nusu uchi kwenye mitandao ya kijamii na hata Raisi John Pombe Magufuli aliliongelea hilo suala na hata kusema kuna baadhi ya watangazaji wana tabia ya kuvaa nusu uchi.

Baada ya kutangaza mapambano dhidi ya wasanii ambao wana tabia ya kuimba nyimbo zisizo na maadili ya Kitanzania lakini pia serikali imetilia mkazo suala la mavazi ya heshima kwa watoto wa kike.

Wolper amewatolea povu wasanii wenzake ambao bado wanaendelea kuvaa nguo fupi ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika maneno haya:

Haki ya kweli yule kiongozi wa kukomesha vichupi yuko wapi? mbona bado tunaona makalio ya watu Instagram? au ndio sanaa every where I go me I wonder mpaka Jasho la damu linanitoka chaaa…..hakuna aliyenihach nauliza swali”.

Mapema mwezi wa jana Naibu wa Waziri habari na sanaa Bi. Juliana Shonza alitangaza vita dhidi ya wasanii wote watakaonekana wanavaa nusu utupu moja kati ya wasanii ambao walitajwa alikuwa msanii Preety Kind ambaye aliishia kufungua kufanya sanaa kwa miezi Sita na Gigy Money.

Sijawahi Kuumia Kisa Mapenzi, Nina Foleni ya Wanaume: Wolper

Muiguzaji mashuhuri wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hajawahi kuumizwa na mapenzi hata siku moja kwani kuna wanaume wamepanga foleni.

Wolper ambaye mwaka jana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii kutoka WCB Harmonize lakini waliachana na baadae akaingia kwenye mahusiano na mwanamitindo Brown kisha naye akaachana naye ndipo inasemekana hivi sasa anatoka na msanii anayeitwa Engine.

Wolper amefunguka na kusema kuwa hajawahi kulia kisa mapenzi bali kinachomuumizaga akiachana na mtu ni kwa sababu tu ametangaza na si vinginevyo kwani kuna kuwaga na msururu na foleni ya wanaume wanaokuwa wanamhitaji muda wowote.

Wolper amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Global Tv alipohudhuria baby shower ya Gigy Money siku ya Jumamosi iliyopita:

Sijawahi kuumizwa na mapenzi yaani nisikufiche kabisa sijawahi kuumia kuachana na mtu ila naumia kwa nini nilimtangaza kuachana kuumia hapana kwanza kwa sababu nina foleni ya wanaume wamejipanga wananisubiri nitoke kwenye Mahusiano kwaiyo mimi ndio ninachagua nimchukue nani”.

Wolper amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa anaelekeza nguvu zake zote kwenye biashara yake ya nguo na filamu ataweka kando kwa sasa kwani anataka biashara yake imfikishe mbali.