“Sijioni Mzuri Bali Mimi ni Mzuri” Wolper Amtolea Povu Shabiki Aliyemshauri Aolewe

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amerudi Kwenye headlines za mitandao ya kijamii baada ya siku ya jana kuvurugana na shabiki wake na kurushiana maneno mazito baada ya shabiki huyo kumshauri Wolper aolewe.

Sakata hilo lilianza baada ya Wolper kuweka picha ya harusi ya Ay na Remmy na kuisindikiza na makopa kibao kuonyesha sapoti yake kwa couple hiyo lakini cha ajabu shabiki huyo alimtolea povu Wolper ambapo aliandika maneno haya kwenye picha hiyo:

Ufanye na wewe uolewe umekazana kujiona mzuri na pengo lako kama mfereji wa maji machafu”.

Baada kupewa maneno hayo Wolper alishindwa kuvumilia kwani alimjia juu shabiki huyo na kumuibia;

Yaani umeandika kwa jazba mwenyewe kwanza pole, pili sio kwamba najiona mzuri mimi ni mzuri, tatu kuolewa kwangu hakuhusiani na hili pengo ulivyo mjinga unaona hili pengo ndio shida kuolewa wanaolewa vipofu na hawamjui bwana au mke anafananaje mxiuuuui itakuwa pengo langu linalokusanya mate ya denda… We anza kuolewa kwanza kwa niaba yangu    alafu uende kwenye darasa la ndoa ili ukajue ndoa haibebwi na pengo…mshamba wewe”.

Baada ya povu hilo Wolper alimblock Shabiki huyo na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram “I honestly can’t handle anymore stress in my life right now”.

Jacqueline Wolper: Nimepoteza Muda Wangu Mwingi Kufanya Bongo Movie

Muigizaji maarufu wa Bongo movie ambaye hivi sasa amegeuka na kuwa mjasiriamali Jacqueline Wolper ameeleza majuto yake ya kupoteza miaka mingi ya kufanya Sanaa ya Bongo movie.

Wolper amekuwa maarufu Kwenye tasnia ya Bongo movie kutokana na filamu kadhaa alizoigiza kuanzia miaka ya nyuma huko tangu enzi za supastaa marehemu Kanumba.

Miaka ya hivi karibuni upepo umebadilika na kumekuwa na maneno kadhaa ya kuelezea kifo cha Bongo movie huku wadau wengi wa filamu wakilia na suala la hatimiliki kuua soko la Bongo movie lakini watu wengi hasa mashabiki wameongelea suala la ukosefu wa ubunifu na uhalisia kuua soko.

Wolper amefunguka na kusema anajutia kupoteza muda wake kukomaa na Kufanya Bongo movie kwa miaka yote badala yake anaona angejiingiza kwenye ushonaji kama hivi sasa. Wolper anamiliki duka la nguo ‘Boutique’ linalojulikana kama Wolper house of stylish.

Wolper ameongea hayo na Global Publishers ambapo amedai kuwa miaka kumi iliyopita alitumia nguvu kubwa mno kukuza jina lake kupitia sanaa lakini ukweli ni kwamba angetumia nguvu hiyo kukuza kipaji chake cha ushonaji basi bila shaka angekuwa mbali:

Ningejua tangu mwanzo ningekomaa na mitindo maana naona huku watu wananielewa zaidi na ninapata pesa nyingi lakini kwenye filamu nimeishia kujulikana”.

 

Young Tusso Bado Anazimika na Penzi la Wolper

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayejulikana kama Young Tusso ambaye alijipatia umaarufu miaka ya nyuma kwa mara ya kwanza baada ya kutoa wimbo wake aliouita Jacqueline Wolper.

Young Tusso aliupa wimbo huo jina la Wolper kwa sababu wimbo mzima alimuimba Wolper na kufunguka jinsi gani anamkubali na yuko tayari hata kumuoa siku moja endapo atapata nafasi kwake.

Young Tusso Akiwa na Wolper

Baada ya kusikia wimbo huo na kuvuma sana Wolper alikiri kuvutiwa na wimbo na alisema anamkubali Young Tusso kama shabiki wake lakini pia alisisitiza kuwa na yeye pia ni shabiki wa kazi za Young Tusso.

Lakini tangu hapo Young Tusso hakukomea kumtaja Wolper kwenye nyimbo zake nyingine ameendelea kumtaja Wolper Kwenye nyimbo zake nyingine kama ishara ya kwamba anampenda kimapenzi jambo ambalo baadhi ya wadau wa muziki wamedai inamuharibia biashara.

Kitu ambacho Young Tusso amekataa kata kata kwani amedai anaongea kuhusu mambo mengine mengi zaidi ya kumuongelea Wolper hivyo itakuwa ngumu kwa kufeli kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Young Tusso alifunguka yafuatayo:

Kwanza ukisikiliza wimbo wangu wa ‘Kaza roho’ ni wimbo ambao nimezungumza vitu vingi sana sijui kwa nini watu wameishika sehemu niliyomtaja Wolper  Alafu isitoshe sioni tatizo kumtaja kwani sijamtaja kwa ubaya ni feelings tu ninaepress mapenzi yangu kwake”.

 

Jacqueline Wolper: Msituchukulie Poa Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie maarufu kabisa jacquiline Wolper amewataka wabongo wote hasa wale watu wenye tabia ya kuiponda Bongo movie wasiwachukulie poa kwani wanarudisha heshima yao hivi karibuni.

Kwa muda mrefu Sanaa ya Bongo movie Imesemwa kuwa imekufa na kila mmoja kuinyoshea kidole kwa kukosa ubunifu ambao ni muhimu ili kusaidia kuipeleka mbele ili kuhakikisha inakuwa na kufika level za kimataifa zaidi.

Ni kawaida siku hizi kusikia watu wakiiponda Bongo movie hasa inapofika wakati kuwa kuna makosa kadhaa ya kiubunifu yanafanyika. Imefika kipindi imekuwa hata ni kama soko Lao limekufa kwani sio sawa na miaka mitano nyuma.

Jacquiline Wolper ni moja ya msanii wa kike aliyejipatia umaarufu wake kutokana na kuchepuka filamu kadhaa za Bongo movie ambazo zilimletea umaarufu lakini hivi karibuni imekuwa ni nadra sana kuona wasanii hawa wanacheza filamu zao kutokana na soko Lao kupotea.

Wolper amefunguka na kusema sio kweli Bongo movie imekufa bali ni ilikuwa imelega tu ila hivi sasa wamepata madirector wapya hivyo wanategemea kurudi Kwenye chati kama zamani, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika haya:

Oya msituchukulie poa Bongo movie hii ndio class yetu na tunapeta kazi zinafanya zituweke mjini msidharau jamani…kwanza nasikia Bongo movie tumepata director mpya tutarudi tu chatini”.

 

Jacqueline Wolper Awachana Wanaume Wote ‘Wadangaji’

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amewafungukia na kuwatolea povu wanaume wote ambao wanapenda kudanga.

Kudanga ni neno linalotumiwa sana hapa Bongo ambalo linaweza kumaanisha kuchuna buzi ambapo linawalenga hasa wadada wengi wa mjini ambao wanapenda miteremko katika maisha lakini sahivi mambo yamebadilika kwani hata wanaume wanatuhumiwa sana kwa kudanga.

Wolper amewatolea uvivu wanaume wote ambao wana kawaida ya kuchuna wanawake zao ambao kwa hivi sasa ni maarufu kama vibeni-10, ambapo Wolper amewasihi wawe makini maana wakiendekeza kudanga basi wataishia kuwa mahouse boy.

Wolper alifunguka hayo na kurusha dongi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika:

Naomba mjifunze kitu wanaume wadangaji, mnadanga au mnadangwa mwisho wa siku unageuka houseboy kwa unayoenda kupambana nayo…..sio kila unachokiona kipo kama unavyokiona!”.

Baada ya ujumbe huo kusambaa mitandao ilianza kuenea kuwa hilo lilikuwa ni dongo ambalo Wolper alimrushia mpenzi wake wa zamani anaye julikana kama Brown ambaye alikuwa ni kiben-10 cha Wolper ambapo alikuwa analelewa na Wolper na kuhudumiwa kila kitu lakini baadae walikuja kuachana.

Wolper hivi sasa ana maisha mengine na ameshakuwa mchumba wa mtu baada ya kuvalishwa pete na mwanaume wake anayeitwa Engine ambaye ni msanii wa Bongo fleva.

 

Sitaacha Kuwakomesha Wanawake Wenzangu- Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabishara maarufu  Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hatoacha kuwakomesha na kuwasema wanawaje wenzake wote ambao hawataki kujishughulisha.

Wolper ambaye mbali na kufanya vizuri katika tasnia hii ya sanaa ya Bongo movie bali amejikita ni moja kati ya wafanyabiashara wazuri kwani ana duka lake la nguo/ boutique ambalo anashona na kuuza nguo linaloitwa ‘Wolperstylish’.

Wolper amefunguka na kusema kuwa kamwe hataacha kuwakomoa na kuwasema wanawake wenzake ambao wameishia kujibweteka tu majumbani na hawataki kujishughulisha kwa jambo lolote wala jambo lolote.

Wolper amefunguka hayo kwenye interview yake aliyofanya na Friday Night Live ya East Africa TV ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa mabinti kuacha kutegemea pesa wanazopewa na wanaume na badala yake wajishughulishe ili kutengeneza pesa zao wenyewe:

Nataka niongee na wadogo zangu wa kike 2018 mimi naendelea kuwatia hasira na kuwaambia kuwa hela ya mwanaume sio yako, ukishachukia pesa ya mwanaume Fanya kitu chako ili iwe yako usikubali kunyanyasika kwa pesa za mtu mwingine, kwaiyo wadogo zangu wanawake wenzangu nitaendelea Kuwa inspire ili ufanye kazi ili utambue hela yako, kamwe usitambue hela ya kuhongwa kama yako”.

 

Ndoa ya Wolper Kugharimu Mil.60

Harusi ya staa mkubwa bongo Jackline Wolper inayotegemewa kufanyika siku yoyote hivi karibuni inategemewa kufanyika na kugharimu zaidi ya millioni 60 huku ikisemekana kuwa itakuwa ndoa kubwa ya aina yake itakayofanyika kwa mbwembwe nyingi sana.

Wolper ambae anasema kuwa harusi hiyo itakayofanyika nchini Tanzania na kisha kuhamia Marekani itakuwa ya kuacha historia kubwa sana bongo na sehemu nyinginezo na hata watakapokwenda Marekani haitakuwa ya watu wengi zaidi ya kumchukua rafiki yake wa karibu Aunty Ezekiel.

Milioni kama 60 zitztumika mbapo milioni 50 zitzfanyika kwa ajili ya harusi ya hapa bongo,na nyingine kama 10 kwa ajili ya kule marekani kwa sababu kule hakutakuwa na watu wengi.wasanii ambao nitaenda nao kule watakuwa kama wanne tu,mmoja kati ayo atakuwa ni aunty ezekiel  kwa sababu huwa ananipa sapoti sana katika biashara zangu , hivyo huyo siwezi kumuacha  kabisa. -Alisema wolper alipokuwa akiongea na moja ya waandishi wa gazeti wa kampuni la GPL

Huyu Ndio Mume Mtarajiwa Wa Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper hatimaye alitangaza kuwa ana mpango wa kuolewa wiki iliyopita na hatimaye mume mtarajiwa amejulikana.

Jacqueline aliwashtua watu wengi baada ya kutangaza kuwa ana mpango wa kuolewa ikiwa kiukweli ulikuwa hata gaujapita hata mwezi tangu ameachana na mpenzi wake aliyekuwa naye kwa miezi michache Brown au BFF.

Ingawa aliweka wazi kuwa anaenda kutolewa mahali kwao Moshi lakini pia aliweka wazi kuwa hana mpango wa kumuweka wazi bwana harusi kwa kile alichodai kuwa anaogopa kuibiwa lakini mapaparazi wa mjini wamemtafuta na hatimaye sura yake imeonekana.

Jamaaa huyo aliyemchumbia Wolper kijijini kwao Moshi kwa Bibi yake na inasemekana kuwa kwa jina anaitwa Sadick Athanas lakini jina lake la umaarufu anaitwa Engine na pia ni msanii chipukizi wa mziki wa Bongo fleva.

Gazeti la Amani limeripoti kuwa sherehe ya kuchumbiwa kwa Wolper iliyofanyika wikiendi iliyopita ilizua gumzo la aina yake baada ya muoaji kufanya kufuru ya aina yake inasemekana sherehe hiyo ilihusisha msafara Mkubwa wa magari kutoka Dar es Salaam kuelekea Moshi kijijini.

 

 

Wolper Atangaza Kutolewa Mahari Siku Ya Leo Kwao Moshi

Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper aeweka wazi mipango yake ya kutaka kuolewa hivi karibuni baada ya kusema kuwa siku ya leo anatolewa mahari.

Wolper ni moja kati ya watu waliopitia historia ndefu kimapenzi na watu mbali mbali mpaka kufikia leo hatimaye amepata mwenzi.

Ni mwezi uliopita tu Wolper alikuwa na uhusiano na kijana anayeitwa Brown lakini hsbari za wawili hao kuachana zilitapakaa in tangu hapo Brown amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano na wanawake mbali mbali.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliweka wazi mipango yake ya kuolewa ambapo aliandika:

Nashukuru sana Mungu kwa kuniamini na kwa kuwa na mimi na kutaka kubadilisha historia ya maisha yangu wewe ni mwanaume ambaye umejitoa ili niwe wako umetaka tufike mbali kwanza ndio mambo mengine yafuate (uwende kwa wazazi (ndoa)) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila wewe ni mwanaume uliyemthamini Jacq, nilipotoka niliteswa na mapenzi yaani usaliti, dharau. Pamoja na hayo alishatokea mmakonde mmoja na kunipeleka mpaka mtwara na matembele nikachuma wanakijiji kunipokea na kwa wazazi nikatambulishwa lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umeifikia! Umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali future husband, Nashukuru sana Mungu kwa kunifunza kunyamaza kwenye haya mahusiano kati yangu na wewe, can’t wait kesho Moshi watakavyompokea mkwe wao kwa ajili ya kutoa mahari na mambo mengine najiona mwenye bahati sana kumaliza mwaka kiaina hii  na kuanza mwaka nikiwa na wewe. Mungu akubariki wa kuniona na kuniamini kuwanafaa kuwa mke wako”.

 

Mimi Bado Ni Bikra – Jacqueline Wolper

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper ameibua mzozo mtandaoni baada ya kuandika na kudai kuwa yeye bado bikra.

Wolper amekuwa kwenye vichwa vya habari sana kwa mwaka huu wa 2017 aliuanza mwaka kwa kushangaza watu wengi na kuzua mjadala mzito baada ya kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na msanii kutoka WCB Harmonize lakini uhusiano wao pia uliisha kwa kishindo miezi michache iliyopita huku kila mmoja akimnyooshea mwenzake kidole kwa kujihusisha na usaliti.

Lamini Wolper hakuishia hapo alianza kutoka na kijana mdogo kwake au kwa lugha rahisi ni kiben-10 wake ambaye alijulikana kama Brown lakini nathubutu kusema uhusiano huuhaujawa mrahisi kwa Wolper kwani yeye na Brown wamekuwa watu wa kuachana na kurudiana na hivi sasa wameachana tena .

Wolper amezua gumzo tena kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuanfika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa yeye ni msichana bikra ambapo aliandika “Wallahi I am still a virgin na mavirgin wenzangu tukutane High spirit kesho”. Hii ni kauli ambayo iliwashangaza wengi kwani inaelekea watu wengi hawakuamini kuwa Wolper anaweza kuwa bikra huku wengi wakidai kuwa amekuwa na uhusiano na wanaume wengi mpaka kuwa bado bikra.

Pamoja na hayo yote Wolper amesisitiza kuwa kwa sasa kitu pekee anachojali ni kufanya kaziJac zake na kukuza biashara zake ambapo duka lake la nguo la Wolper house of stylish linafanya vizuri sana

Wolper Amefunguka Sababu Iliyomfanya Mpaka Wazazi Wake Kumtimua Nyumbani

Mfanyabiashara na muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amefunguka kwa mara ya kwanza na kueleza siri iliyomfanya mpaka wazazi wake wakamtimua Nyumbani kwao.

Wolper ametoa siri ya jinsi wazazi wake walivyomsusa kwa kudai kuwa Kisa anawadhalilisha wakati amekuja Dar-es-salaam kujitafutia maisha.

Wolper amesema kuwa kiuhalisia familia yake ni watu ambao wanajiweza, hivyo alivyoamua kifanya biashara ya umachinga katika soko la Kariakoo familia yake haikupendezwa na kuamua kumtenga:

Wolper alifunguka hayo yote kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 ambapo alizidi kufunguka na kudai:

Kuna baadhi ya mabinti wananiambia wanataka kuwa kama Wolper lakini hawajui mimi nilianzia chini nakumbuka nilianza kuwa machinga Kariakoo nakumbuka nimeshatukanwa sana lakini pia hao watu wanaotaka kuwa kama mimi hawajui kuwa nilichuniwa nyumbani kisa kufanya kazi ya kuuza sabuni kwa sababu wazazi wangu kidogo wana uwezo na walikuwa wana uwezo wa kunitunza mimi na kunipa biashara nikafanya na nikaweza kuendelea na maisha yangu lakini mimi nikaenda kuiza sabuni kama machinga kule kariakoo kwaiyo wenyewe wakaona kama nimewadhalilisha kwa kufanya vile hivyo ikapelekea mpaka wazazi wangu kunichunia kwa mwaka au miaka miwili mizima lakini hizi zote ni changamoto za maisha ambazo lazima uzipitie katika njia yako ya kupata mafanikio”.

Wooler anayefanya vizuri kwenye biashara zake za duka lake la Wolper Stylish lakini pia App yake aliyoizindua hivi karibuni ambayo itaonyesha mambo Mengi kuhusu maisha yake na pia kazi zake sanaa na ujasiriamali.

Wolper Amedai Kuwa Pengo Lake Ndio Linamsaidia Kudanga

Mfanyabiashara na muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper amewajia juu wale watu wote wanao-muedit na kumsema kuhusu pengo lake jeusi na kudai kuwa like pengo ndio linalomsaidia kudanga.

Wolper aliwaacha watu wengi midomo wazi baada ya kuandika maneno hayo lakini kwa habari za chini chini na za kimbea zinadai kuwa Wolper alimrushia dongo lile mrembo mwingine anayejulikana kama Husna Maulid.

Inadaiwa kuwa Husna Maulidi ana uhusiano na mpenzi wa zamani wa Wolper (ex-boyfriend) anayejulikana kama Brown. Sakata hilo lilianzia kwenye mtandao wa Snapchat ambapo Husna aliweka picha ya pengo la Wolper na kumcheka kwa kebehi.

Baada ya kuona hivyo Wolper alimjibu Husna kwa kumuita skeleton kutokana na wembamba wake ambapo aliandika:

Walahi nimecheka mpaka nimepaliwa skeleton unajua kuniua mbavu zangu, nalipenda sana pengo langu aaah najua kinachokuumiza hujatia sign….Hapa kazi tu skeleton”.

Lakini Wolper hakuishia hapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwatolea povu wale wote wanaomkejeli Kisa pengo lmatak kusisitiza lina thamani sana na ndio linamsaidia kudanga.

Ngoja niwaelezeni kitu kimoja ambacho hamkijui kuhusiana na hili pengo….hili pengo nimelipandia ndege kwenda South Africa kwenda kulitoa na kuweka ma silver sasa wewe kunguni unatokea pasipojulikana unakuja kuedit ukadhani nitakasirika am soleee…mimi najipenda nilivyo na ikitokea nimechoka nitanyanyua makalio yangu na kwendaa kuweka jino ili niwe na jino so pliz usitokwe nadamu pliz pengo langu ndilo ninalodanga kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui”.

 

 

Wolper Amsifia Faiza Kwa Picha Yake Ya Uchi Adai Asijali Maana Wabongo Washamba

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo Jacqueline Wolper ameibuka na kumpa tano rafiki take Faiza Ally kwa picha ile ya uchi na kudai asijali maana wabongo ni washamba tu kwa kutoelewa maana ya picha ile.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Faiza aliwashangaza watu wengi baada ya kuamua kurusha picha iliyomuonyesha akiwa uchi kabisa huku sehemu zake za siri zikiwa wazi wakati akizaa leba mtoto wake wa kiume. Baada ya pica hiyo kusambaa ilizua gumzo sana na kusababisha picha hiyo kuenea mtandaoni kama moto wa kifuu.

Baada ya picha hiyo watu wengi walimjia juu Faiza huku mastaa wa mziki kama Snura akimuomba Faiza aitoe picha ile kwa kuwa ilikuwa haimdhalilishi tu yeye kama mwanamke bali wanawake wote maana mambo yanayotokea leba yanapaswa kuwa ya siri kabisa.

Wolper alipohojiwa na kituo kimoja cha habari ili aweze kupima uzito kwenye suala linalo-trend hivi sasa ambalo ni picha ya uchi ya Faiza, Wolper alidai anawashangaa wait wanaomponda Faiza aliyeposti picha hiyo hivi karibuni kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati yeye amevutiwa sana na kitendo hiko na iko siku atamuiga.

Wabongo ni washamba sana ushamba ndio unawasumbua sio kitu kingine kabisa, sioni ubaya wa ile picha hata kidogo eti katudhalilisha sasa pale kamdhalilisha nani? Mimi nimefurahi mno na binafsi ipo siku nitamuiga endapo nitajaaliwa kupata mtoto wangu mwenyewe”.

 

Wolper: Sina Wivu Nimemualika Harmonize na Mpenzi Wake Kwenye Party Yangu

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hana hata chembe ya wivu wa kimapenzi kwa Harmonize na mpenzi wake Sarah na ndio maana amewaalika wote wawili kwenye party ya birthaday yake.

Wolper na Harmonize waliachana miezi michache iliyopita baada ya kuwa pamoja kwa muda. Baada ya kuachana kila mmoja alimtuhumu mwenzie kwa kuchepuka huku Wolper akiweka wazi kuwa waliachana kwa sababu Harmonize alikuwa na uhusian na Sarah kwa sababu ya fedha alizonazo mzungu huyo. Lakini hata baada ya kuachana na kila mmoja kupata mpenzi ambapo Harmonize alianzisha uhusiano na Sarah na Wolper alianza uhusiano na Brown lakini bado wawili hao wamekuwa na bifu la chini chini.

Siku ya jana ilikuwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Wolper ‘birthday’ ambapo yeye mashabiki zake pamoja na ndugu zake walienda kushiriki kula chakula cha mchana na kituo  cha kulelea watoto yatima Temeke. Lakini aliweka wazi kuwa party kubwa ya birthday yake itafanyika leo tarehe saba.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Wolper aliweka wazi kuwa kwa sasa hana tatizo lolote na Harmonize wala  mpenzi wake mzungu Sarah ndio maana amewaalika kwenye sherehe yake:

Nimemualika Harmonize na sio yeye tu hadi mwanamke wake Sarah ili kuonyesha kuwa sina wivu wowote tupo sawa kabisa alafu ningekuwa nasikia wivu kama watu wanavyosema basi nisingewaalika kabisa yaani kwenye maisha mapenzi yanaisha na unatakiwa uendelee na maisha yako sasa mimi nimesha-move on na maisha yangu na nashukuru kwa sasa tumekuwa ndugu na Sarah inabidi tu awe ndugu yangu ili nimsaidie hata kujua kiswahili na pia nimsaidie kama Harmonize akichepuka nimpe nyendo zote ili nimwambie kama anachepuka kwaiyo inafika wakati watu inabidi tu muwe marafiki”.

 

Wolper Amedai Kuwa Anapenda Wanaume Wenye Vibamia Kwasababu Ana sehemu Za Siri Ndogo

Muigizaji wa Bongo movie, Jacqueline Wolper ameibuka tena kwenye headlines wikiendi hii baada ya kuweka wazi kuwa anapendelea kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wenye uume mdogo kwani yeye mwenyewe ni mdogo.

Wolper aliacha watu midomo wazi Ijumaa iliyopita kwenye kipindi cha Friday Night live alipoulizwa kuhusiana na maneno aliyoyaweka kwenye ukurasa wake wa Instagram siku za nyuma kidogo ambapo inadaiwa kuwa alisema kuwa hapendi wanaume wenye vibamia anapenda waliojaliwa lakini siku hiyo alikataa kuandika maneno hayo badala yake alidai kuwa anapendelea vibamia na kusema mwanaume pesa sio mashine kubwa:

Kwenye mahojiano na East Africa Tv kupitia kipindi cha FNL Wolper alifunguka yafuatayo:

Mimi binafsi napendelea mwanaume awe na uume mdogo pia kwa sababu mimi mwenyewe mdogo kwaiyo utaona kabisa siwezi nikapenda vitu vikubwa ambavyo siwezi nikavihimili na kama kuna mwanamke anayekwambia mwanaume mashine huyo ni muongo maana kiukweli mwanaume ni pesa ukishakuwa na pesa hicho kibamia kitapendwa tu na kwa mwanamke aliyepitia mambo mengi maishani atapenda pesa siyo mashine kubwa”.

Mbali na hayo pia Wolper alifunguka kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake Brown na kusema kuwa bado wako wote na wanapendana sana lakini pia ameongelea kuhusu biashara zake hasa inayofanya vizuri sana kwa hivi sasa ya duka lake la fashion.

Harmonize- Namuheshimu Wolper Ameona Utupu Wangu

Mwanamuziki kutoka WCB, Harmonize anayetamba na nyimbo zake mbili zinazofanya vizuri ‘shulala’ na ‘nishachoka’ amefunguka na kusema anamuheshimu sana Wolper kwa sababu ameona utupu wake.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na attention kubwa sana iliyoelekezwa kwa Harmonize na mpenzi wake wa zamani wake Jacqueline na mpenzi wake wa sasa Sarah. Sakata hilo lilianza tangu Wolper alipoachana na Harmonize na kuweka wazi kuwa Harmonize yupo na Sarah kwa sababu ya pesa. Siku chache zilizopita baada ya Harmonize kutoa ngoma yake ya Shulala wanawake hao waliingia kwenye ugomvi mkubwa mpaka kusemekana kuwa Harmonize amerudiana na Wolper kitu ambacho Harmonize alichokataa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Lil’ommy  Harmonize alikataa kuwa wimbo wake wa ‘nishachoka’ amemuimbia Wolper:

Unajua msanii mzuri ni yule anayeimba nyimbo zinazogusa maisha ya watu na mapenzi ni kitu kinachogusa watu wengi kwaiyo ule wimbo mi nimeimba ili niwafurahishe mashabiki wangu lakini sio kweli kwamba nimemuimbia Wolper, kuhusu kumtumia model anayefanana na Wolper halikuwa wazo langu mi nimeimba nyimbo director ndo akachagua model wa kuwepo kwenye video kwaiyo mi sijui lolote itakuwa vizuri umuulize director”.

Harmonize aliendelea zaidi kufunguka kuhusu Wolper na mchango wake;

Kikubwa naomba nimshukuru Wolper kwa kuiposti ngoma yangu na kuisapoti kwani ametumia muda wake, bando lake, image yake kaweka kwenye kazi yako  kwa kweli sio kitu rahisi, mi namheshimu sana na namshukuru sana naomba mwenyezi Mungu amjaalie na ukizingatia vitu vyote vilivyokuwa vinatokea kwenye mitandao ya kijamii yeye ndo alikuwa anazungumza kwenye media kwa sababu mimi sio mtu muongeaji sana alafu mi huwa namheshimu sana mwanamke ambaye ameona utupu wangu siwezi nikakaa nikamzungumzia vitu alivyokuwa anafanya”.

Baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Harmonize amemuimbia Wolper ule wimbo, baadaye  akatoa video ya wimbo wake wa Nishachoka na kuonekana wazi kabisa model aliyetumika anafanana na Wolper.