Jacqueline Wolper aamua kurudi shule baada ya Jux kuitimu masomo yake nchini China

Juma Mussa maarufu kama Jux ameitimu masomo yake nchini China. Msanii huyo amepata shahada ya Computer Science aliyosomea kwa muda wa miaka minne.

Jacqueline Wolper amepata changamoto ya kurudi shuleni baada ya kuona picha ya Jux akisherekea baada ya kuitimu masomo yake nchini China.

“Nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…! Hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” Wolper aliandika.

Jacqueline Wolper amsifu sana Saida Karoli baada ya kufanya hili

Wolper amemiminia sifa kwa mkongwe wa muziki ya asili – Saida Karoli. Muigizaji huyo wa Bongo Movies amesema Saida anahitaji heshima kubwa.

Wolper alisema hayo baada ya mwimbaji huyo mkongwe kuachia wimbo wake mpya ‘Orugambo’ inayomaanisha maneno.

Mrembo huyo wa filamu za Bongo alieleza kuwa Saida anastahili heshima kutokana na namna alivyoutangaza muziki wa asili.

“Saida anastahili heshima kubwa kwa muziki wa asili anaoufanya, kwa kweli namuunga mkono sana,” Wolper alisema akiongea na 3 Tamu.

Tazama wimbo mpya ya Saida Karoli hapo chini:

Jacqueline Wolper afunguka kuhusu mpenzi wake wa kitambo – Ali Kiba

Kabla ya Harmonize kuponyoka naye, Ali Kiba ndo alikua mpenzi wake muigizaji wa filamu za Bongo – Jacqueline Wolper.

Mbaka sahi Wolper anakumbuka mambo mazuri kuhusu ex wake Ali Kiba – muigizaji huyo hakuwa na mabaya ya kusema kuhusu Ali Kiba alipomuongelea kwenye mahojiano na gazeti la Amani.

Jacqueline Wolper

Mambo mawili anayoyapenda Wolper kuhusu Ali Kiba ni upole na unyenyekevu wa superstar huyo, vitu ambavyo Wolper anasema wanaume wengine aliyokutana nao hawana.

“Mengi nakumbuka, kikubwa ni upole wake pamoja na unyenyekevu. Ni tofauti na wanaume wengine ambao nimewahi kukutana nao,” muigizaji huyo ameliambia gazeti la Amani.

 

Jacqueline Wolper afunguka kwanini ameshindwa kuvuka ‘border’

Watu wengi watakubali kuwa Jacqueline Wolper ni muigizaji mwenye kipaji kikubwa, lazini mrembo huyo ameshindwa kufanya filamu za kushirikiana na wasanii wa nje.

Nini haswa ndo kikwazo kinachozuia Wolper kuvuka ‘border’? Lugha ya Kiingereza ndo sababu kubwa inayowafanya waigizaji wa Tanzania kushindwa kufanya filamu za kushirikiana na wasanii wa nje

Wolper alikiri kuwa Kiingereza ni tabu kwake, alisema kuwa kwa sasa ana mwalimu kwa ajili ya kuboresha kiingereza chake ili atimize ndoto zake za kucheza filamu na wasanii wa nje kwa lugha ya kiingereza.

“Wasanii wachache ndio wanaojitahidi kwenda kufanya kazi na wasanii wa nje, mimi na baadhi ya wasanii wengine hatuwezi kushirikiana na hao kwa kuwa hatujui Lugha ya Kiingereza kwa ufasaha kwa kuwa filamu nyingi huzungumzwa kiingereza,” alisema Wolper.

 

Jacqueline Wolper afunguka kuhusu sababu ya kuitema CHADEMA

Jacqueline Wolper alifanya kampeni za kumsapoti mgombea uraisi wa chama cha CHADEMA Edward Lowassa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Akiongea katika kipindi cha Kikaangoni la EATV, Wolper alisema kuwa alimuunga mkono Lowassa akiwa CCM kabla hata ya kujiunga na chama cha CCK. Alieleza kuwa yeye husupport mtu wala si chama.

Mrembo huyo alisema kuwa alitema CHADEMA kwasababu chama hicho kilishindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu.

Wolper alieleza kuwa hana ubaya wowote na Lowassa, alisema mwanasiasa huyo akisimama tena kuwania urais atamsupport bila shaka.

Tazama mahojiano aliyofanya Wolper katika EATV hapo chini:

 

Maoni ya Dogo Janja kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo Janja ametoa maoni yake kuhusu uhusiano wa Jacqueline Wolper na Harmonize kufuati matukio ya hivi karubuni.

Kuliibuka uvumi kuwa wawili hao (Harmonize na Wolper) waliachana lakini baadae Harmonize alikuja kuthibitisha ukweli wa mambo.

Dogo Janja alikuwa na mengi ya kusema kuhusu uhusiano wa Wolper na Harmonize; akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, msanii huyo wa Tip Top Connection inayomilikiwa na Babu Tale, alisema kuwa maisha ya watu mashuuri ni filamu.

Jacqueline Wolper na Harmonize

Dogo alisema kuwa mapenzi ya Harmonize na Wolper ulikuwa kama drama ulipokua unaanza lakini mwishowe ukawa ‘serious’.

“Ukishakuwa na mpenzi staa hiyo ni flamu tayari, maisha yenu ni filamu watu wanafuatilia. Kingine mapenzi yao yalivyokuwa yananza watu walikuwa wanachukulia kama Drama lakini mwisho wa siku unakuja kuona kama wapo serious, kwa hiyo ni vitu kama hivyo.

“Mimi kama mimi siko interested nao sana, ni verse tu zile, siko interest nao kwa vile na mimi nina mapenzi yangu , kila mtu ana mitikasi yake” amesema Dogo Janja.

Dogo Janja

 

Jacqueline Wolper afunguka kuhusu unafiki unaolemaza filamu za Bongo

Washikadau katika filamu za Bongomovies ndo wanaochangia kuzorota kwa hali ya mambo katika sekta hio ya uigizaji – Jacqueline Wolper ameeleza.

Mrembo huyo anasema kuwa anakerwa sana na unafiki wa wasanii, anadai kuwa uigizaji nchini umelemazwa na unafiki.

Jacqueline Wolper

“Nachukizwa na unafiki Bongo Movi, kwa kweli unakera sana, hawako kiualisia ndiyo maana kufika tunapotaka ni ngumu sana,” Wolper alisema akizungumza na Showbiz wakati wa maandamano ya kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji na uuzwaji holela wa sinema za nje.

Wolper alisema kuwa wasanii wangekuwa na umoja wangeungana siku hiyo na kuweza kutoa mwelekeo mmoja ambao ugechangia malalamika yao kuskizwa.

 

 

Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

Harmorapa amemfika kooni Jacqueline Wolper – mpenzi wa Harmonize. Harmorapa, ambaye anafanana na Harmonize, aliwashangaza wengi alipomtafuta binti mrembo anayefanana na Jacqueline Wolper.

Harmorapa na Wolper bandia

 

Harmonize na Wolper

 

Wolper sasa amesema kuwa kinachomuudhi kwa Harmorapa ni kitendo cha mpenzi wake Harmonize kumuongelea vizuri lakini yeye anapohojiwa na vyombo vya habari anaponda.

“Jamani yaani kama huna moyo unaweza ukapasuka kwa hasira maana Harmorapa anaudhi sana, wenzie wakimuongelea vizuri yeye anawaongelea vibaya unafi kiri mtu ataacha kukuchukia? Abadilike,” alisema Wolper.