Jay Moe Asema Sababu ya Wasanii Kufeli ni Kiburi

Msanii mkongwe wa muziki Jay Moe anasema kuwa sababu kubwa ya wasanii kufeli ni kuwa na kiburi na kujiamini kupita kiasi na kufikia hatua ya kushindwa kuendelea kufanya kazi.jay moe anasema kuwa kwa upoande wake anaona kabisa mpaka sasa ameweza kudumu kwa sababu  ya nidhamu na kuishi na watu vizuri na kuwa na usikivu pale anapokuwa akipewa ushauri.

katika kila kitu ili kidumu ni lazima kuwe na nidhamu,katika game yangu kulikuwa na wasanii wakubwa na maarufu waliokuwa zaidi yangu mimi,lakini labda nidhamu yao ndio iliwaangusha mpaka sasa.

ninachoshukuru mimi ni kwamba niko na mahusiano mazuri na watu ambao nafanya nao kazi kila siku kama media,mashabiki na watu mbalimbali katika industry,na nidhamu ndio kitu kikubwa kwa sababu unaweza kuwa na umaarufu sasa lakini baadae ukapata shindwa ukakosa wa kukupa msaada.

Lakini pia Jay Moe anasema kuwa wasanii wakongwe wamekuwa wakikataa mabadiliko kuwa muziki wa sasa na wazamani una utofauti mkubwa.

Jay Moe- Muziki Umekuwa Biashara

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Jay Moe aliyejipatia umaarufu kipindi cha nyuma kwa staili yake ya kipekee ya kuchana amefunguka na kudai kuwa hivi sasa muziki umekuwa biashara.

Jay Moe amedai kwa sasa kuna vitu vingi ambayo vimebadilika kutoka wa wasanii wa muziki wa hip hop kutoka na muziki kubadilika na kuwa biashara tofauti na zamani.

Jay Moe alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Ladha 3600 cha EFM ambapo alifunguka haya ziadi:

Sasa hivi tunawekeza sana kwenye muziki tofauti na miaka ya zamani tunatoa wimbo tu hakuna uwekezaji wowote ambao tulikuwa tunaweka.

Lakini sasa hivi au miaka ya sasa hivi muziki umekuwa biashara, kwahiyo lazima pia unavyowekeza uhakikishe uwe na target nzuri ya kuweza kujua pesa yangu itarudi vipi”.

Tofauti na miaka ya nyuma wakati Wakina Jay Moe na wasanii wengine wakongwe wanaanza muziki ulikuwa haujapewa nafasi kubwa kiasi hicho lakini sasa mambo yamebadilika na muziki unaendesha maisha ya watu wengi.

 

“Muziki umekuwa mgumu” Msanii mkongwe wa hip hop – Jay Moe akiri

Jay Moe amekiri kuwa wasanii wakongwe kama yeye wameondolewa kwenye ulingo wa muziki kwasababu ya mambo ya kisasa.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM, Jay Moe alieleza kuwa muziki wa sasa umekuwa na mambo mengi kama mitandao ya kijamii, photo shoot na kadhalika ambazo zimechangia kuwaondoa baadhi ya wasanii wakongwe kwenye muziki.

Jay Moe

“Muziki umekuwa mgumu kuliko zamani, ugumu wake ni kwamba zamani ulikuwa hauhitaji kufanya photo shoot, hauhiaji kuji-brand kwenye mitandao ya kijamii kudeal na video ukitoa tu ngoma kama Jua au Mvua, sijui Kama Unataka Demu tuliprint CD tukasambaza kwenye redio tofauti na tukahit na tukaweza kuisha. Lakini ukizunguzia muziki wa sasa hivi unaona wasanii wakali lakini wanashindwa kui ngia ndani yake sababu ya mazingira ya game ilivyo sasa hivi. Game inahitaji vitu vingi, hiyo game huwezi kuifanya mpaka uwe na pesa, mpaka kuwa sign na label kubwa ambayo inaweza kukugharamia,” Jay Moe alisema.

 

Huu ndo ujumbe Rapper Jay Moe alitoa baada ya kusemekana kuwa ako na ubishi na Diamond Platnumz

Mahojiano aliyofanya Jay Moe katika The Playlist ya Times FM umezua utata, blog ya Udaka TZ ulimnukuu Jay Moe akisema kuwa hawezi kujiunga na WCB ata kama lebo hio wanamuitaji.

Blog hio pia lilisema kuwa rapper huyo hawezi peleka ngoma zake kwenye platform ya Wasafi.com ya kuuza muziki kwenye mtendao.

Hata hivyo Jay Moe amejitokeza na kupinga madai ya Udaku TZ, rapper huyo amesema hana ubishi wowote na Diamond.

“@udakutz_ Naheshimu Sana Kazi Za Mikono Yetu,Sijawahi Kufanya Interview Na Nyie Wala Kunicontact For An Interview…Tafadhali Naomba Muache Kucopy Na Kupaste Vitu Namna Hii,I have Huge Respect For @diamondplatnumz Na #WASAFI Kwa Ujumla,Tufanye Vitu Vya Kujenga Sio Kubomoa…Sina Tatizo Na Kupeleka Nyimbo Zangu #wasafidotcom Na Hakuna Sehemu Nimesema Sitopeleka So Dont Get Twisted,Kusema Sitosign Its Because I Have My Own Label #SoFamous So Please Next Time Kama Mnahitaji Udaku Kama Huu Msisite Kinitafuta Lakini Sio Kufabricate Story @udakutz_ Kwa Niaba Ya #SoFamous Napenda Kusema Kwamba Hii Ni Wrong Info.. #Nisaidie_Kushare???” Jay Moe aliandika kwa Instagram.

Jay Moe

 

Huu ndio ujumbe Rapper Jay Moe aliutoa kwa wanamuziki wote wa Nje

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, rapper Jay Moe amejitokeza na kuongelea mambo mbali mbali kuhusu muziki Tanzania.

Alizungumzia kwanza uwezo wake wa kuandika nyimbo na kugusia nyimbo ambazo ameziandika Tanzania moja wapo ikiwa Aseme wa Q Chilah.

Pia alisema angetaka sana kumwandikia Bill Nass wimbo.

Moe amekiambia kipindi cha On The Eight cha TVE kuwa hawezi kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka nje mapaka atakapokuwa na video walau tano ambazo msanii huyo ataweza kuziangalia na kuufahamu uwezo wake zaidi tofauti na ilivyokuwa sasa bado hana video za kutosha.

Hitmaker huyo wa Pesa Madafu ameongeza hata alipokuwa Afrika Kusini mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini P-Funk Majani alimpigia simu na kumtaka kushoot video huko lakini alimwambia kuwa yupo huko kwa ajili ya kushoot video moja ya kutimiza miaka yake 11 bila ya kuwa na video nyingine.

Jay amesisitiza kuwa akifikisha video za kutosha itakuwa ni vizuri kwake hata zikichezwa kwenye vituo vingine vikubwa vya nje ya nchi ikiwemo Nigeria. Rapper huyo kwa sasa ameachia video yake mpya ‘Nisaidie Kushare’ baada ya wimbo wake wa ‘Pesa Madafu’ kufanya vizuri kwenye redio na runinga.