Steve Nyerere Amtaja JB Kuwa ‘Bodyguard’ Wake

Muigizaji wa Bongo movie ambaye amebobea kwenye kuingia sauti za viongozi mbali mbali wa siasa Steve Nyerere ameibuka na jipya hivi karibuni Baada ya kudai msanii mwenzake JB ni mlinzi wake.

Gazeti lab ijumaa linaripoti kuwa Tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Hyatt Regency, Posta jijini Dar kulipokuwa na hafla ya kuzindua taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na bidhaa ya manukato ya De La Boss iliyoandaliwa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

Katikati ya hafla hiyo, Steve aliyekuwa ameongozana na JB alijigamba mbele ya watu kuwa kwa sasa analindwa naye jambo liliolofanya wengi kuangua vicheko.

Nina bodigadi huyu hapa (JB) na mimi nimekuwa mmojawapo kati ya wanaolindwa”.

Katika kuonyesha tukio hilo lilikuwa la utani Steve alionekana kumtaka JB amsogezee gari lake ili kumuiga Diamond ambaye alionekana na mabodyguard wawili na walionekana kumfungulia milango ya gari, JB aligoma na kila mmoja kuondoka kivyake.

Irene Uwoya Afungukia Mapenzi Yake Kwa JB

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Irene Uwoya ameibuka na kuweka wazi mapenzi yake mazito juu ya msanii mwenzake Jacob Stephen maarufu kama JB.

JB na Irene Uwoya waliwahi kukonga nyoyo za mashabiki kwenye tasnia ya Bongo movie kutokana na movie zao walizoigiza kufanya vizuri na kupendwa sana watu.

Kupitia ukuraaa Wake wa Instagram, Uwoya alimtumia salamu za Birthday JB lakini katika ujumbe Wake alifunguka na kuweka wazi kuwa anampenda sana:

https://www.instagram.com/p/Bq9a16-h50e/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=13ab3f35zngna

JB na Irene Uwoya wameshawahi kuigiza pamoja kwenye filamu zilizowahi kufanya vizuri Kama vile Oprah.

JB- Siwezi Kuwa Mrithi Wa Mzee Majuto

Muigizaji wa Bongo movie Jacob Stephen maarufu kama JB amesema hata siku moja hawezi kuwa mrithi wa Marehemu Mzee Majuto.

Mzee Majuto alifariki mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu, Ingawa alikuwa na umri mkubwa Mzee Majuto alikuwa mmoja wa komedian mkubwa sana Tanzania.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, JB amesema mashabiki wengi wamekuwa wakimwambia kwamba yeye ndiye mrithi wa Mzee Majuto, lakini haiwezekani kushika nafasi yangu maana alikuwa na ladha yake na yeye ana ladha yake katika uigizaji.

Haiwezekani mimi kuwa mrithi wa Mzee Majuto maana alikuwa na kitu cha tofauti sana na alipendwa na watu wengi hivyo ni vigumu kuwa mrithi wake ila ninawaahidi Watanzania kuwafurahisha kwa kadiri ya uwezo wangu katika kuigiza”.

 

JB- Nimepungua Kwa Sababu Nimepunguza Kula Kula Ovyo

Msanii wa filamu za Kibongo Jacob Stephen maarufu kama JB amefunguka na kudai kuwa siri pekee iliyomfanya mpaka hivi sasa amepungua ni kupunguza Kula Kula ovyo.

Siku chache zilizopita JB ambaye anajulikana kwa kuwa na mwili mkubwa hadi kupewa jina la Bonge la bwana, ameposti picha Instagram akiwa amepungua kupita kiasi.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani hivi karibuni, JB amesema  siri ya kupungua kwake ni kupunguza kulakula hovyo na ndiyo maana ameweza kupungua kwa haraka huku mazoezi pia yakihusika.

Mwanzo nilikuwa napenda sana kula vyakula, ndiyo maana nilikuwa na mwili mkubwa, lakini sasa hivi siendekezi tena kulakula hovyo, na ninahakikisha nafanya sana mazoezi, ndiyo maana unaona nimeweza kupungua kwa haraka”.

Lakini pia Kwenye mtandao wa Instagram JB aliandika siri yake:

JB Afunguka Baada Ya Kukataa Movie Za Wanigeria “Sitafuti Umaarufu Natafuta Pesa”

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Jacob Stephen maarufu kama JB amefunguka na kudai amekataa kufanya kazi mbili kubwa za Wanaigeria kwa sababu ya pesa ndogo waliyotaka kumlipa.

JB amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Bongo 5 ambapo amedai sahivi hatafuti umaarufu wa kuonekana kwenye filamu na Wanigeria bali yupo bize kusaka pesa za ukweli.

Mimi kusema kweli napenda pesa na hata hao Wanaigeria wamekuwa kama mara tatu lakini tuliposhindwana ni kipato tu yaani siwezi kuinuka hapa nikaenda Nigeria halafu nikiangalia pesa ninayolipwa ni  haiwezi kunitosheleza mimi sahivi sahivi sitafuti umaarufu tena natafuta pesa.

Lakini pia  hata ukiniuliza sababu kubwa ya kuacha uigizaji na kuwa producer ni hela tu na siyo kwamba sitamani kuendelea kuigiza ila napata mashabiki zaidi nikiwa producer kuliko muigizaji”.

 

 

Ushauri Wa JB Kwa Wasanii Wenzake Wa Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Jacob Steven maarufu kama JB amewapa usia wasanii wenzake wa Bongo movie.

Miaka ya hivi karibuni soko la bongo movie limeshuka kwa kiasi fulani nikimaanisha ni tofauti na ilivyokuwa miaka michache ya nyuma huku watu wengi wakikosoa filamu hizo zinazotolewa na solo hilo huku wasanii wengi wakilaumu wizi wa kazi zao na bajeti finyu.

Wasanii wakongwe kama JB wamekuwa wakitafuta njia sahihi za kuweza kulikoa soko la Bongo movie, JB kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka yafuatayo;

“Kanuni za uvaaji zinasema kabla hujaambiwa hiyo nguo ni nzuri ni lazima wewe mwenyewe uipende ndio maana mtu akikuuliza kati ya nguo hizi ipi nivae ukichagua nyingine utasikia angalia vizuri hii anakuonyesha anayoitaka hata tukija kanuni za utongozaji zinasema lazima ujikubali mwenyewe ukijichukia yule unayemtaka atachukia zaidi mfano kama kazi yako ni kuzibua choo halafu ukamdanganya mtu wewe ni banker maana take umejichukia, Kwanini nimesema haya ukiangalia account za wasanii wengi wa filamu kwa mwezi mzima anaweza asipost kitu chochote kinachohusiana na filamu, najua wengi wenu ni vijana na ni wakati wenu na lazima mpost mambo yenu lakini nawakumbusha Fulani ndo ziliwafanya muitwe majina hayo”.

Pia JB aliendelea kufunguka kuwa;

“Mashabiki wanawafahamu kwa ajili ya movie tafadhali tusijisahau, walau kwa wiki mara mbili Mimi nimepunguza sana kupost mpira ni movie tu na nimeacha kuwafollow watu wasiohusiana na movie hata mke wangu, nyie msifanye hivyo kama mimi lakini naomba nione post za movie kwenu…tuamke tuzitangaze movie zetu”.

Je unahisi juhudi hizi zitatosha kuokoa soko hili la Bongo movie?

JB Aongelea Kushuka kwa Kiwango cha Bongo movie

Muigizaji wa Bongo movie maarufu JB amefunguka kuhusiana na tuhuma za kushuka kwa kiwango cha filamu za Bongo movies. Watu wengi hasa mashabiki wa filamu hizo wamekuwa wakilalamika kuwa ladha ya filamu hizo imepotea na sio kama zamani na hiyo kuwapelekea wao kushindwa au kuacha kununua filamu hizo na kupelekea kukosa soko kwani watu wengi wamehamia kuangalia filamu za kikorea na kifilipino.

Katika mahojiano aliyoyafanya JB amekiri kuwa kweli filamu hizo zimekosa mvuto kwa watazamaji kwani tatizo ni stori kujirudia rudia na bajet finyu ya kutengenezea filamu hizo.

JB alisema;

“Matatizo ambayo yalikuja kuikumba tasnia ya filamu ukiacha usambazaji ni hadithi, sasa kwa hadithi nyingi hazikuwa siyo nzuri wakati wa kutengeneza filamu, vipi tamthiliya ambayo ni kitu kirefu? ndio maana utaona kuna tamthiliya nyingi sana ambazo zinafanywa lakini hazivumi vile kama ilivyokuwa zamani”.

Mashabiki wengi wa filamu hizo wamekuwa wakiwalaumu waigizaji wa filamu hizo kwa kupoteza mwelekeo wa sanaa na kujiingiza katika vitendo a,bavyo vinaua sanaa zao. mfano wasanii wengi wa kike wamekuwa na skendo nyingi sana ambazo zinawafanya wajulikane sana kwa skendo kuliko vipaji vyao hivyo kupelekea kuua sanaa zao.

Mbali na hayo pia Bongo movie ilipata pigo kubwa sana baada ya kufariki marehemu Kanumba ambaye alikuwa na mchango mkubwa sana katika sanaa hii ambapo alikuwa akivuka boda na kuitangaza bongo movie nje ya Tanzania lakini tangia afariki hajatokea msanii wa kuziba pengo lake.

Je unahisi anaweza kutokea msanii wa kuziba pengo la Kanumba na kuipeleka sanaa hii mbele zaidi ili ikapate soko la nje ya nchi? Tafadhali toa maoni yako.