Mimi Mars Afungukia Furaha Aliyonayo Kutokana na Kuwa Single

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama kuwa single kwa sababu yupo huru kufanya kazi zake vizuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Showbiz, Mimi Mars alisema, aliamua kuishi peke yake bila mwanaume kwa sababu ameshawahi kuumizwa na aliokuwa akiwapenda hivyo kumfanya kuwa mpweke na kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

Niliishia kuambulia maumivu tu kutokana na kuwa na wanaume wasiokuwa waaminifu, nikaona hapana, kwa nini niendelee kuteseka wakati kuna maisha baada ya mapenzi? Hivyo nimeamua kuishi mwenyewe mpaka pale nitakapompata mtu sahihi, nayafurahia haya maisha kwa sasa”.

Mimi Mars ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Staa wa muziki wa hip hop nchini Kutokea katika Kundi la Weusi Joh Makini.

 

 

Joh Makini Awatolea Povu Wanaobeza Ndoto ya Mdogo Wake.

Msanii wa muziki wa hip-hop nchini Joh Makini amefunguka na kusema kuwa  kila mmoja amekuwa na ndoto katika masiha yake  na inaweza kutimia pale tu anapoamua kuifanyia kazi lakini anawashanga wale waliombeza sana Niki wa pili baada ya kuangaza Ndoto yake ya kuwa rais.

ni kitu kizuri sana mtu kuwa na ndoto lakini kitu cha kuikitisha ni pale ambapo niki alipotangaza ndoto yake kubwa ya kuwa rais kuna vipingamizi vingi sana  kutoka kwa wtu wakiona kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani,inaonyesha ni jinsi gani tuko katika taifa la watu wasiona na ndoto.lazima uwe na kitu kinachoweza kukwambia kuwa ipo siku wewe utakuwa mtu fulani na ukifanyia kazi ndoto hiyo inaweza uja kufanikiwa, na hakuna kinachoshindikana chini ya jua.Kwaio mimi namtakia kila la kheri na ndoto zake ziweze kutimia.

Muda nyuma kidogo uliopia niki alitangaza hadharani kuwa ana ndoto ya  kuwa rais, wapo waliompongeza na pia wapo waliombeza na kumpuuza.

Joh Makini Atoa Sababu ya Kuimba Gospel.

Mwanamuziki Joh Makini Ambae hivi karibuni alitoa wimbo wenye maadhi ya kidini amefunguka na kusema kuwa aliamua kutoa wimbo huo ikiwa kama ishara ya kuwafikishia watu ujumbe juu ya kile Mungu anamfanyia katika maisha yake.

Joh makini anasema wimbo huo hautakuwa wa kwanza kuimba kwa sababu anampangwa kuimba nyimbo za aina hiyo kila mara atakapokuwa akipata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake.

Hakuna mtu ambae hafahamu kuwa mungu ni kila kitu katika maisha yetu,nimeimba wimbo huu kwa mashabiki zangu ili kila mtu ajue kuwa swala la Mungu kuwa anatifanikisha katika maisha yetu sio swala la kumuachia yeye tu, sisi pia tunatakiwa kupambana kwa njia zetu ili na yeye aweze kubariki njia hizo ili kupata kile tunachotamani.”

 

 

Joh Makini Ataja Sababu Za Kutoa Wimbo Wa Gospel

Staa wa muziki wa Hip Hop Bongo Joh Makini maarufu kama Mwamba wa Kaskazini kutokea kundi la Weusi amefunguka na kutaja sababu zilizomsukuma kutoa wimbo wa Injili.

Joh Makini amesema sababu kubwa iliyomfanya mpaka kuimba wimbo wa gospel ni kuonyesha ni Kwa jinsi gani Mungu ana maana kubwa maishani mwake.

Kwenye mahojiano na gazeti la  Risasi Vibes, Joh Makini alisema kwamba wimbo huo kwake ni ‘Hip Hop Gospo’ wenye ujumbe ‘strong’ na si mwisho wa kuimba nyimbo za namna hiyo, ataendelea kila anapopata idea kwa sababu Mungu ni kila kitu kwake.

Hakuna ambaye hafahamu kwamba Mungu ni kila kitu kwenye maisha ya binadamu, nimeimba wimbo huu ili kufikisha ujumbe kwa mashabiki zangu kufahamu kwamba suala la Mungu kutufanikisha kwenye maisha yetu si la kumwachia yeye tu. “Sisi pia tunatakiwa kupambana kwa namna zetu nay eye anabariki nia zetu na kufanya tupate kila tunachotamani”.

 

Nikki wa Pili Sisi Tunamuona Kama Upcoming Artstist:-Joh Makini

Msanii wa hip-hop nchini joh makini amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba ameimba wimbo ambao unawataka watu wajitaidi kwenda kanisani lakini bado hata yeye hakumbuki mara ya mwisho kwenda kanisani.

Akiongea na Wasafi Tv, Joh makini anakanusha pia taarifa za kuwa wasanii wa arusha wamekuwa wakibebwa na media na ndio maana wamekuwa wakisikika sana na kuonekana kuwa wao wanamafanikio kuliko wasanii wengine huku akisema kuwa hata mdogo wake Nikki wa pili sio msanii mkubwa kama watu wanaovyoona lakini ni msanii chipukizi.

Siamini kama kuna sehemu  wasanii wa arusha wanakosea , mimi huwa ninaamini katika nyakati tu na pia hata ukiangalia watu kama kina Motra Future,  mabao mimi ninawaona mbali, lakini pia kuna Nikki wa pili ambae pia tunaweza sema kuwa ni msanii mkubwa lakini kwa age yetu sisi wakina Joh Makini, Lord Eyes tunaona kuwa bado ni msanii chipukizi.

Tuzo ni Kipimo Kikubwa Cha Kazi Ya Msanii:-Joh Makini

Msanii kutoka katika kundi la weusi , joh makini amefunguka na kusema kuwa kutokuwepo kwa tuzo nchin tanzania kuna didimiza sana muziki wa tanzania kwa sababu hakuna kipimo halisi cha ukubwa wa kazi za wasanii.

Joh makini anasema kuwa tuoz inakuwa inampa msanii hamasa ya kufanya kazi kwa umakini zaidi ili aweze kupata tuzo lakini ndani yake anakuwa akifanya muziki mzuri ambao ni faidia kwake na kwa mashabiki pia.

joh Makini anaifananisha tuzo na nafasi ya mwanafunzi anapokuwa shule akisoma kwa bidii ili akae katika nafasi nzuri huku akijua kabisa kuwa kuna zawadi itakuja kwa ajili yake.

Tuzo ni kitu cha msingi na kipimo kikubwa sana kwa nafasi ya msanii kujua ukubwa wa kazi yake,kwa sisi weusi tunajua kabisa kuwa sisi ni wakali na tumekuwa tukifanya vitu vikubwa na vya kushangaza watu

Kwa muda sasaTanzania kumekuwa hakuna tuzo, kutokana na figizu za hapa na pale huku wasanii wengi wakilalamika kuonewa katika tuzo hizo.

Joh Makini Adai Haoni Tatizo Kwa Wasanii Wa Kiume Kuvaa Vikuku

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa staili ya kuchana kutoka katika kundi la Weusi Joh Makini au Mwamba wa kaskazini amedai haoni tatizo kwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku kama wanataka kufanya hivyo.

Joh Makini wameweka wazi kuwa wasanii wa kiume kuvaa vikuku miguuni sio kitu cha ajabu kama watu wengi wanavyodhani kwani anaamini ni fasheni kama fasheni nyingine.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, amesema kuwa wasanii ni watu ambao wanaishi na fasheni na style mbalimbali hivyo msanii kuvaa kikuku ni maamuzi yake na yeye anachukulia kawaida kabisa suala hilo;

Sijui kesho lakini mimi nachukulia kama style yake kama mimi nilivyoamua kuweka Rasta kuna wengine wameamua kuvaa vikuku wengine kutoboa pia na masikio lakini Sioni tatizo lolote kama mtu ameamua kuchagua aina ya maisha anayoishi”.

Wiki iliyopita msanii  wa muziki Diamond Platnumz aliposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akionekana mguuni akiwa amevalia cheni maarufu kwa jina la kikuku jambo ambalo lilisababisha ashambuliwe na mashabiki wake mitandaoni.

Baada ya Davido, Joh Makini Kufanya Kazi na Ice Prince

Mwanamuziki Joh Makini anazidi kupanua wigo wake wa kimuziki kwa kutaka kufanya kazi na ice prince kutoka Nigeria. tetesi za  hapo awali zilikuwa ni Joh Makini kufanya kazi na Davido lakini mambo yanazidi kuwa mazuri kwa kuendelea kufanya vizuri hasa baada ya kutegemea kufanya kolabo nyingine na Ice Prince.

Akiongea na JJ wa Jembe fm , Joh Makini anasema kuwa waliamua kufanya wimbo na Ice Prince pamoja lakini hakutaka kuweka mambo wazi kwa sababu yeye ndie alietafutwa na hii imetokea kama ilivyotokea kwa msanii Davido.

Kuna mtu mmoja tulifanya nae kazi anaitwa eze, tulikutana nae bongo alipokuja kufanya kazi zake ndipo aliniambia kuwa anfanya  kazi na ice prince  na akaniambia kuwa kuna kitu anadhani ni vyema tukafanya nae na mimi nikamwambia why not, na mimi nikakubali.

Joh makini anasema kuwa baada ya mazungumzo hayo siku iliyofuata ice prince alimtumia baet ya wmbo huu na yeye kufanya yake na kisha baada ya hapo ni kufanya mazungumzo na menejiment yake.

Mwisho wa siku nafanya muziki wangu na ninaamini wapo wanaotupenda na wapo watakao amua kutupenda tu, na wapo watakao amua kutotupenda lakini wapo ambao walitujua since day one kabla hatujawa kina Joh makini.

 

 

 

Joh Makini Akana Kupotea kimuziki.

Msanii wa muzii wa bongo fleva kutoka katika kundi la Weusi John Simon maarufu kama joh makini amekana maneno na tetesi zinazozuka juu yake kuwa amepotea kimuziki na huku ikitajwa sababu kubwa kuwa ni wasanii wachanga wanaoibukia na kumfanya yeye kushundwa kusikika kama ilivyokuwa mwanzoni.

Joh mMakini ambae hivi karibuni ametoa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la  mipaka anasema kuwa watu wamekuwa wakiongea maneno bila kuwa na ushahidi kwa sababu hawaangalii vitu vingapi amekuwa akifanya kukuza muziki wake kwaiyo sio kweli kuwa anepozwa na wasanii wachanga.

Sio kweli kuwa nimepoa kimuziki kama vile watu wengi wamekuwa wakisema ,wakizungumza na kuzusha katika mitandao ya kijamii, mimi niko vizuri na kazi zangu  ziko zinafanya poa kabisa  na ninachoataka kuwaambia cha zaidi ni kwamba sitgemei kuchuja hata siku moja.-Alifunguka Joh Makini.

Hivi karibuni Joh Makini alipata skendo ya kutembea na msanii mwenzake mimi mare lakini taarifa hizo walizikanusha na kusema ukaribu wao ni kama kaka na dada kwa sababu wamekuwa pamoja.

 

Mimi Mars Akanusha Tetesi za Mahusiano ya Kimapenzi na Joh Makini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mdee Music Mimi Mars, amekanusha tetesi zinazosambaa juu yake kuhusu mahusiano yake na  msanii mwenzie Joh Makini.Mimi Mars amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha kuwa anatoka kimapenzi na joh makini  bila kujua kuwa yeye na joh makini ni kama kaka yake kwa sababu wamekuwa wanamuona akiwa rafiki ya kaka yake.

Mahusiano yangu   na Joh Makini ni ya kikaka na dada,kwa sababu Joh Makini  ni mtu ambae tumekuwa tunamjua kutokana na ukaribu wa kirafiki na kaka yetu mkubwa.Alikuwa rafiki yake mkubwa na kaka yetu kwaio kama vile ambavyo kaka yetu amekuwa wakitushauri ndivyo Joh Makini  anafanya, kwaio ni kaka na ni mshauri hayo maswla ya mahusiano sijui yametokea wapi.

Lakini pia Mimi Mars anawasema kuwa watu wanatakiwa kuwa wanaongea yale wanayokuwa na uhakika nayo kwa sababu mara nyingine inaweza kuahribu mahusiano ya watu bila wao kujua kuwa maneno yasiyokuwa na ushahidi yanaweza kubomoa kabisa.Mimi Mars anasema kuwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote.

Joh Makini- Mimi ni Tofauti Ya Wasanii Wote Bongo

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya Hip hop Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’ amefunguka na kudai kuwa yeye ni msanii tofauti sana na wa kipekee ukilinganisha na wasanii wengine wote Bongo.

Rapa kutoka kundi la Weusi amesema tungo anazozitumia kwa sasa kwenye muziki wake ni kutokana na mabadiliko ya muziki na anaonyesha sanaa zaidi kwenye nyimbo zake na kusisitiza kuwa anayetaka kumfatilia afuatilie mziki wake kwa kuwa maisha yake binafsi hayamhusu na wala yeye sio mtu wa show-off.

Job Makini amefunguka hayo na zaidi kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitia kipindi chao cha Enews:

My personal life style ni my personal life style sipendi kuweka kwenye media ninachokiweka kwenye media ni hii sura ya Joh Makini brand ya Joh makini basiii na ninafanya hivyo sio kwamba labda kuna kitu nahofia hapana hivi ndivyo mimi nilivyo Joh Makini ndio yuko hivi nipo tofauti na wasanii wengine wote. Mimi nafanya mziki mzuri nawapa mashabiki zangu lakini maisha yangu binafsi hakuna mtu anayehitaji kujua wala sidhani kama kuna mtu namnyima haki kwa kufanya maisha yangu binafsi tabaki kuwa binafsi”.

 

Jay Z atajikuna kichwa akiskia alichosema Joh Makini

Joh Makini amesema yuko katika kiwango ambayo hakuna rapa mwingine nchini Tanzania ambaye mashabiki wanaweza mfananisha na Jay Z.

Alitoa maoni haya baada mashabiki zake kumfananisha na msanii huyo wa Marekani ambaye ako na ushawishi mkubwa duniani mzima.

Jay Z

Joh anasema ufananisho wake na Jay Z ni dhibitisho tosha kuwa muziki wake upo katika kiwango kingine ambacho wasanii wengine bado hawajafika.

“Jay Z ni ‘role model’ wangu…mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika ‘level’ ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye…Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z ‘yeah i like it’ kuliko ungenifananisha na mtu mwingine,”Joh Makini alisema.

Joh Makini: Davido alinifwata kutafuta collabo na mimi

Joh Makini aliwaahidi mashabiki wake kufanya collabo kubwa na Davido – msanii anayetajika sana nchini Nigeria na barani Afrika.

Davido alidhibitisha collabo yake na Joh Makini kupitia mitendao ya kijamii. Kwenye Instagram yake, Davido alipost  picha akiwa pamoja na Joh Makini na kuandika maneno yalisomeka “Back to work On set shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ  x NAIJA”

Joh Makini amefunguka na kueleza kuwa Davido ndiye aliyemfwata na kupendekeza wafanye collabo – wengi walikua wanadhani Makini ndiye aliyemwomba Davido kushirikiana naye kimuziki.

“Mimi naona ni kwasasabu alikuwa excited sana kufanya kazi na mimi, halafu wakati wa kufanya hii ngoma yeye ndiye aliyekuwa wakwanza kuniapproach mimi. Kwa hiyo nafikiri ni mtu ambaye alinifuatilia na akaupenda muziki wangu ndiyo maana hata chemistry imekuwa nzuri na tumefanya kitu kikubwa,” Joh Makini alisema.