Yawezekana Hii ni Sababu ya Kutumbuliwa kwa Jokate

Habari zilizo chini ya kapeti na ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa kutumbuliwa kwa mrembo jokate katika nafasi yake ya kaimu katibu wa uhamisishaji kwa vijana wa UVCCM kumesababishwa na nafasi hiyo kuatak kupewa msanii mweingine wa kike bongo ambae amehamia CCM hivi karibuni.

Pamoja  na kwamba baaada ya kutumbuliwa kwa mwanadada huyo hakutaa kusema kitu chochote kuhusu sababu iliyofanya atolewe katika nafasi hiyo lakini watu mbalimbali wameanza kusema kuwa kutokana na Wema Sepetu kuhamia CCM wa sasa inawezekana nafasi hiyo itakuwa imewekwa wazi ili aweze kupewa yeye baada ya muda.

Akitoa habari hizo moja ya watu wa karibu  amesema kuwa inawezekana kabisa kuwa nafasi ya jokate atapewa wema na kisha wema atapewa nafasi kubwa zaidi ingawa kwa sasa  jambo hilo limekuwa ni siri kwa sababu ni mambo ya uongozi na muda mwingine inabdi kutunza siri.

Hata kaimu katibu mkuu wa UVCCM, amesema kuwa swala la kuondolewa kwa Jokate ni kitu cha kawadia kabisa  kwa kuwa mpaka wanafanya maamuzi hayo ni kwamba walishajiridhisha na maamuzi hayo na sababu za kumtoa zinakuwa zimewaridhishwa wanakamati wote.

 

Jokate Kumuongoza Ramsey Nouah Kwenye Kongamano La Vijana

mwanadada mrembo kabisa Tanzania ambae anazidi kungara kutokana na moyo wake wa kujitoa katika maswala ya kijamii leo ataweza kuambatana na msanii mkubwa wa kimataifa kutoka nchini nigeria Ramsey Nouah katika kongamano la viajana litakalo fanyika katika viwanja vya chuo kikuu UDSM.Wasanii hao watakuwa wagenni wakuu  wazungumzaji  katika kongamano la vijana  maeneo ya chuo kikuuu cha Dar Es Salaam.

Ramsey Nouah  ni moja ya wasanii wakubwa kimataifa ambao ambao wameipeleka tasnia ya movies za nigeria mbali zaidi,ramseya alishawhi kufanya kazi na msanii wa bongo movies marehemu Steven Kanumba iliyojulikana kama  Evil Kingdom iliyofanya vizuri katika tasnia ya movies za Afrika.

Rasmsey Nouah akiwa na msanii Idrisa Sultani.

Kongamano hilo ambalo linalengo la kuwahamasisha vijana na kuwainua katika sanaa litafanyika na kuhuduriwa na mastaa wengie akiwepo Idriss Sultan  aliyewahi kuwa mshindi wa BBA miaka ya nyuma.

Wasanii hao wataanza na mahijiano maalumu yanayofanyika sasa hivi katika kituo cha Radio cha East Africa.

 

 

Jokate:Napenda Watu Wanijue Kutokana Na Kazi Ninazofanya

Mwanadada mrembo ambae amekuwa akifanya kazi nzuri katika jamii hasa ya kurudisha fadhila  na kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii amefunguka na kuongelea vitu ambavyo vimekuwa vikimkera hasa katika matumizi ya mitandao na maswali ambayo amekuwa akiulizwa na waandishi wa habari kuhusu maisha yake.

Jokate amesema kuwa ukiachana na yeye kuwa maarufu  lakini hapendi kwenda katika interviews na kuanza kuulizwa maswali binafsi yanayohusu maisha yake ya ndani  na ndio maana amekuwa ni mtu asiependa kuwaweka ndugu na watu wake wa karibu katika mitandao ya kijamii labda iwe ni kikazi au swala linalomlazimu kufanya hivyo.

Hata hivyo Jokate amesema kuwa anapenda watu wamjue na kumuongelea zaidi kuhusu mambo anayoyafanya katika jamii yeye na brand yake na sio maisha yake binafsi.

Sipendi kuulizwa kuhusiana na maisha yangu binafsi na hata ukiangalia katika page zangu  siposti mchumba, siposti wazazi na wala siposti nduguy kivile kwa sababu najua ukishawapost unakuwa unawaweka katika situation ya watu kutaka kuwaongelea na kama unavyojua watu wengi online wanakuwa na uwezo wa kuongelea kitu chochote kile  kwaio napenda kuwalinda sana watu wangu wa karibu, lakini pia napenda watu wanijue kupitia kazi zangu na vitu vya muhimu ambavyo nimekuwa nikivifanya kwa jamii yangu na vitu kama hivyo – Aliongea Jokate alipokuwa akiojiwa na Millard Ayo Tv

Jokate ambae hivi karibuni amekuwa akionekana akifanya mabo mengi yanayohusiana na jamii amesema kuwa anataka kuwa mfano wa kuogwa kwa mambo mengine mazuri na ndio maana hataki kuwa anaweka maswala yake binafsi katika media.

Hata hivyo ni wachache tena hasa watu maarufu kama Jokate wanaoweza kuendesha maisha yake hasa binafsi kwa siri kubwa, tangu Jokate isemekane kuwa ameachana na Ali Kiba amekuwa kimya sana kutaka kuwaonyesha watu mahusiano yake ya kimapenzi hadharani.

Jokate anapaswa kuwa mfano wa kuigwa sio kwa watu maarufu tu lakini pia kwa watu wote ambao waliweza kupewa nafasi ya kujulikana na bado wakaichezea nafasi hiyo, ukiachana na urembo ambao Jokate umekuwa ukimfaidisha lakini sasa Jokate ameamua kurudi na kusaidia jamii yake katika maswala mbalimbali yanayoikabili ikiwepo na sekta ya elimu.

Mrembo Jokate Kutumia Nafasi Yake Kutetea Wanawake na Watoto

Mwanadada Jokate Mwegelo aliyekuwa mwanamuziki napia mshiriki wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 na kufanikiwa kushika nafasi ya pili, amefunguka na kudai kuwa anategemea kutumia nafasi aliyonayo katika chama chake na umaarufu katika jamii katika kuhakikisha anasimamia haki za wanawake na watoto.

Jokate ni moja tu kati ya mastaa walioamua kugeukia siasa, ambapo kupitia chama cha mapinduzi anashikili nyadhfa fulani. Jokate amesema kwa kupitia nafasi aliyonayo atahakikisha kuwa anapambana awezavyo kuhakikisha anapambania haki za wanawake pamoja na watoto kwa ujumla.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha Star Mix, Jokate alidai kuwa kuna umuhimu sana kila mmoja mwenye nafasi kwenye jamii atambue umuhimu wa mwanamke kwani wao ndio wenye nafasi kubwa kwenye jamii na hivyo wakazane katika kuhakikisha wanawapa elimu.

Unajua watu wengi wanajisahau kuhusu mwanamke na mtoto lakini kwa upande wangu nawaona wana nafasi  kubwa sana ya hasa mwanamke akipewa elimu bora na kupewa nafasi nyingi za kuongoza huku watoto wakipewa haki inayostahili”.

Jokate ambaye anamiliki kampuni yake ya kidoti inayofanya vizuri amezidi kung’aa na mafanikio take kuonekana hadi nje ya nchi hasa pale ambapo mapema mwaka huh alichaguliwa kama mmoja Kati ya vijana 100 mwenye ushawishi nchini Afrika lakini pia ameamua kugeukia siasa na siku za hivi karibuni ameonekana akijikita zaidi katika kuisaidia jamii katika mambo mbali mbali yenye umuhimu na yenye kujenga taifa letu.

Jokate Awasihi Vijana Watumie Mitandao Ya Kijamii Kutafuta Fursa

Mwanamitindo Jokate Mwegelo amewafungukia vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kuiona Kama fursa ya kuweza kuboresha maisha yao badala ya kutumia kwa udaku tu.

Jokate aliongea hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na Sam Misago ambapo alitoa ushauri kwa vijana ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia mitandao ya kijamii kuboresha maisha yao.

“Nafikiri vijana watumie zaidi mitandao ya kijamii kuweza kujielimisha kwa sababu katika ulimwengu wa sasaivi kupitia mitandao ya kijamii tumeona kuna habari nyingi ambazo zinawekwa na pia kumekuwa na fursa nyingi sana kwa vijana kwa mfano kuibuka kwa biashara kama lebo kubwa tu za nguo za nchi za nje kwasababu tu wameweza kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa iyo Vijana waone mitandao ya kijamii kama fursa ya biashara isiwe sehemu tu ya kupiga umbea na udaku na kutafuta umaarufu ambao hauna faida”.

Jokate aliendelea kueleza umuhimu wa mitandao ya kijamii katika biashara;

“Mitandao ya kijamii tukiitumia vizuri inaweza kutunufaisha na tukaweza kumsaidia raisi wetu kutimiza adhma yake ya kuona Tanzania inakuwa nchi ya viwanda, kwaiyo vijana tupende kujifunza kwenye hii Mitandao tuitumie tu vizuri  kwa kunyanyuana zaidi ili tuzidi kuona fursa mbalimbali zilizopo kuliko kutumia kwa kupiga umbea na kufuatilia maisha ya watu binafsi”.

Jokate pia ni moja kati ya watu ambao ametumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kufanya biashara, Jokate ambaye ni miiliki wa kampuni inayotambulika kama ‘Kidoti’ ameweza kutumia mitandao ya kijamii kuitangaza na kuikuza biashara yake.