Jux Amjibu Chid Benz Kuhusu Tuhuma Za Kutojua Kuimba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva  Juma Jux amemjibu Msanii mwenzake Chid Benz ambaye siku chache zilizopita alisema wazi kuwa hadhani kama Jux anajua kuimba.

Kama utakumbuka siku za nyuma Chid Benz na Jux wameshawahi kuwa na kabifu fulani Hivi baada ya Chidi kudai kuwa Jux alimpigisha shoo kwenye Ziara ya ‘In Love and Money tour’ bila kumlipa chochote kitu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jux amefunguka haya kuhusiana na sakata hilo:

Chid Benz kusema mimi sijui kuimba sidhani kama kakosea maana huo ni mtazamo wake na sio dhambi maana ni uhuru wa kuongea, nilikosea kumwambia Chid Benz nitakucheki maana nilikutana nae kwenye Love and Money tour Dar backstage na aliomba kupanda kwenye stage na alipanda na alivyomaliza nilimshukuru na nikamwambia ‘nitakucheki’”.

Kesho na sikumcheki, kila alipokuwa akinitafuta nakuwa na mambo mengine na baada ya siku tatu nikaona anasema kwenye media nimlipe hela zake, na kiukweli ile show hatukuwa na sponsor na wasanii wote walifanya bure na kutuunga mkono, bado sijamcheki ila nitamcheki”.

 

Juma Jux Atinga Ndani Ya Coke Studio

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux amefanikiwa kufika katika bonge la shoo la Coke Studio ambalo limeshawahi kuwashirikisha wasanii wakubwa Afrika.

Jux anafanya vizuri na ngoma zake kama vile Zaidii” na “Tell Me”, Lakini mbali ya  muziki, Jux pia ni mfanyabiashara akiwa ni mmiliki wa chapa ya T-shirts “AFRICAN BOY”, ni bidhaa za nguo zinazopatikana Afrika Mashariki zikimilikiwa na mwimbaji pamoja na mtunzi Juma Jux.

Jux amesema kuwa moja ya mipango yake kwa mwaka 2019 ni kufanya nyimbo nyingi za kushirikiana na wasanii kutoka nje ya Tanzania. Katika Coke Studio Jux anashirikiana na mwana dada Shellsy Baronet kutoka Mozambique.

Kwenye interview yake aliyofanya Jux amefunguka Mengi juu ya mara yake ya kwanza Kushiriki kwenye msimu mpya wa Coke Studio:

Coke Studio ni jukwaa zuri kwa wasanii kwani inapelekea kubadilishana tamaduni na nchi zingine; ni kitu  kizuri ambacho nafurahi kuwa sehemu ya Coke Studio.”

JUMA JUX ataiwakilisha vyema chapa ya “AFRICAN BOY” katika jumba la Coke Studio kwa mwaka 2019, kuanzia Februari.

 

 

Jux Ajibu Tuhuma Za Kumdhulumu Chid Benz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux ameibuka na kujibu tuhuma nzito alizotupiwa na msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Chid Benz alipodai kuwa amemdhulumu pesa alizopigia shoo.

Siku chache zilizopita Chid Benz alimtuhumu Jux kwa utapeli baada ya kudai kuwa aliperfom Kwenye shoo ya ‘In Love and Money Tour’ lakini hakumlipa hata senti pamoja na kwamba mashabiki waliikubali shoo yake zaidi.

Katika mahojiano yake na Enews ya EATV, Jux amefunguka na kudai kuwa Chid hakuwepo Kwenye listi ya wasanii ambao walitakiwa kuperfom bali alimfuata backstage:

Kwanza kabisa Chid Benz hanidai pesa yoyote kwa sababu ile Show kabla hata ya kufika Dar tulikuwa tumeshapanga wasanii watakaotumbuiza  hatukuwa na mdhamini kwaiyo hata wale wasanii waliotumbuiza Kuna vitu tuliwafanyia lakini hatukuwalipa hela na wengine walikuja kutusapoti tu kama wasanii wenzao.

Chid alinifuata backstage akasema anataka kufanya kitu kwa mashabiki na mimi nikamuheshimu kama braza mkubwa akapanda stejini akapiga shoo lakini kesho yake ananipigia simu ananiambia amelogwa shoo lakini hajapata kitu nikamwambia nitampa kitu kutoka mfukoni kwangu lakini haikuwa lazima nashangaa ameenda Kwenye vyombo vya habari”.

 

 

Juma Jux Kucheza Filamu Ndani Ya Bongo Movie

Msanii wa muziki wa Bongo fleva songwritter Juma Mussa maarufu kama Juma Jux ametangaza kucheza filamu yake ya kwanza ndani ya Bongo Movie.

Habari hiyo njema imedokezwa kwa mara ya kwanza Director wa video hapa nchini ikiwemo video nyingi za Jux Hanscana ameweka wazi kuwa hivi karibuni wawili hao wanampango wa kuja na movie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Hanscana ameweka wazi kuhusu Ujio wa filamu hiyo Lakini pia ameweka wazi kuwa Jux alitaka  kufanya siri iwe suprise kwa mashabiki zake.

Jux amekuwa na mchango mkubwa sana Kwenye ukuaji wa Hanscana Brand, alikuwa na uwezi wa kushoot na mtu yoyote yule projects zake lakini akaona Noo why hii riziki nisimpe huyu kijana mwenzangu ili naye asaidie familia yake na vijana wenzake pia.

Shukrani sana Jux mimi nitaendelea kuhakikisha projects zakowsikuangushi bro…Also na movie yetu japo unataka ije kimya kimya lakini natoboa tu kwani kesi bei gani? Movie coming soon..”.

 

Mabeste Afungukia Bifu Lake na Juma Jux

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya muziki wa kurap Venance Mabeste maarufu kama Mabeste aliyewahi kuhit na ngoma zake kama ‘Sirudi nyuma’ na ‘Baadaye sana’ amefungukia bifu lake na msanii mwenzake Juma Khalid ‘Jux’.

Mabeste ambaye aliwahi kuhit sana miaka kama nane iliyopita ameachia ngoma mpya, ngoma inaitwa Chakusema ambayo imefanywa na Prodyuza Rush The Don huku kichupa kikifanywa na Paxpyne.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mabeste amefunguka kuhusu mengi lakini moja kati ya vitu vilivyokiki siku za nyuma kidogo ni bifu lake na Jux na anafunguka zaidi:

Kuna hali ya kutoelewana tu ilitokea huko nyuma na sipendi kuizungumzia sana. Lakini Jux ni mshikaji, tumetoka mbali sana kabla hata hajaenda China kwa ajili ya masomo”.

Lakini pia Mabeste amefunguka kuhusu uhusiano wake na ushkaji wake na Jux kwa sasa unaendaje:

Siyo mbaya. Ninamshukuru, ingawa hatukutani kama ambavyo ilikuwa zamani. Kwa sasa tumekwishakuwa watu wazima, kila mmoja ana majukumu yake, kwa hiyo muda mrefu huwa unapita bila kukutana wala kuwasiliana“.

Jux Atangaza Ujio Wa Albamu Yake Mpya ’The Love Album’

Staa wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux ametangaza ujio wa albamu yake mpya itakayoitwa ‘The Love Albamu’ ambayo anategemea kuiachia hivi karibuni.

Jux ambaye kwa sasa yupo Kwenye Tour na msanii mwenzake ambaye pia ni mpenzi wake Vanessa Mdee amefunguka na kuweka wazi kuwa ingawa hajataja tarehe ya uzinduzi wa Albamu hiyo lakini ni siku za karibuni.

Kwenye Interview yake na Wasafi Tv, Jux ameweka wazi kuwa Albamu hiyo itakwenda kwa jina la ‘In Love’ ambayo itakuwa na nyimbo 18:

The Love album itakuwa na nyimbo 18 tarehe ya kutoka ni bado sijaitangaza lakini wayu wanaokuja kwenye shoo zetu za tour yangu na Vanessa wanapata sana Bahati ya kusikia nyimbo chache za Kwenye Albamu hiyo lakini Tour ikishaisha nitatangaza tarehe ya kutoka kwa Albamu”.

Lakini Jux alifunguka kuhusu wasanii walishirikishwa katika Albamu hiyo:

Asilimia kubwa ya nyimbo Kwenye Albamu nimefanya mwenyewe lakini wasanii ambao nimewashirikisha ni mapema sana kuwataja nadhani siku Albamu ikitangazwa rasmi basi na wasanii watatajwa”.

Jux amesema sababu ya yeye na Vanessa kufanya shoo ya pamoja ni baada ya wote kutoa albamu ambapo Vanessa ametoa Money Monday’s na Yeye anakuja na The Love Album hivyo waliiona ni wakati muafaka wa kufanya shoo.

Mkubwa Fella Adai Hana Kinyongo na Juma Jux

Mdau mkubwa wa  muziki Bongo Mkubwa Fella ambaye alikuwa Meneja wa wasanii kama Wanaume TMK, Mkubwa  wanawe  Yamoto Band na amesema hana kinyongo na aliyekuwa msanii wake Jux.

Mkubwa Fella amesema pamoja na kulea hafanyi kazi za kimuziki na Jux kama ilivyokuwa zamani lakini sio kusema kinyongo na yeye Hapana bali bado anamkubali sana na kazi zake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mkubwa Fella amesema kwa sasa Jux ni mtu wake wakaribu zaidi kwa kuwa anaukubali muziki wake.

Bwana Jux amebaki kama shabiki yangu, kwa sababu tayari ameshakuwa lakini akitaka mawazo nitampatia kwa sababu sasa hivi anafanya kazi na watu wengine lakini kwangu ametoka ameshatoboa.

Yule ni mwanangu wa dhahabu, kwanza mimi ni shabiki yake namba moja kuliko mtu yoyote“.

Jux amesema ameendelea kufanya vizuri na kila ngoma ambayo amekuwa akitoa ambapo kwa sasa anategemea kuanza Tour yake na mpya na mpenzi wake Vanessa Mdee inayoitwa ‘In Love and Money”.

 

Nyanshinski Atangaza Kolabo Yake na Jux

Staa wa Muziki kutoka 254 Kenya Maarufu kama Nyanshinski aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Malaika’ ametangaza ujio wa Kolabo Yake na msanii wa Bongo fleva Juma Jux.

Nyanshinski alifunguka hayo Kwenye mahojiano na BBC alipokuwa anaongelea ujio wake wa Kolabo mbali mbali alizofanya na wasanii mbali mbali kutoka Africa Mashariki.

Lakini nimefanya kolabo na Jux tunangoja tu itoke”.

Lakini pia Nyanshinski aliwataja baadhi ya wasanii ambao amesha fanya nao kazi kutokea Tanzania ni kama msanii mkongwe Ay ambaye ameweka wazi kuwa ngoma yao ipo Kwenye Mtandao wa Youtube tayari.

Nilifanya kolabo moja na AY ilikuwa inaitwa ‘More in More’ ukiitafuta YouTube utaiona”.

Nyanshinski ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa anaangalia zaidi kufanya kazi na wasanii kutoka Rwanda na Uganda kwani hajawahi kabisa kushirikiana nao.

Lakini pia Nyanshinski Aliweka wazi kuwa yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa label ya WCB ili aweze kufanya nao kazi.

Ruby Akiri Kuvutiwa na Jux

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby amefunguka na kuelezea mapenzi yake kwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Juma Jux Kwenye upande wa uimbaji wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ruby amekiri kuwa anavutiwa sana na uimbaji wa Jux hasa kwa sababu nyimbo zake nyingi zinawagusa wanawake huku akitaja wimbo unaoikonga sana nyoyo yake ni utaniua:

Kwa sababu nyimbo za Jux karibia zote zinawashika kwanza wanawake, halafu pia uimbaji wake ni RnB ambayo anaweza kuimba mwanaume au mwanamke, kwa hiyo nafikiri ule uliniingia zaidi”.

Jux ameonekana kama moja kati ya wasanii wa kiume ambao wanavutiwa sana na mabinti kwani kuna watu maarufu kadhaa waliokiri kuvutiwa na Jux ikiwemo Socialite maarufu kutoka Kenya anayejulikana kama Huddah na hata Amber Lulu.

Ruby amerudi kwa kasi ya ajabu Kwenye muziki na hivi sasa anafanya vizuri kwa wimbo wake wa One and only alioshirikishwa na Nedy Music.

African Boy Yamfikisha Jux Mbali Zaidi, Apata Dili Nono China

Kama anavyosema mwenyewe kwamba kipindi anaanza kufanya kazi na kutengeneza brand ya African boy hakutegemea kama ingekuwa kubwa kama ilivyo sasa hivi lakini kutokana na mapenzi makubwa ya mashabiki zake na mapokezi mazuri yalimfanya aendelee kukuza na kuitanua brand hiyo mpaka kufikia alipo sasa.

Leo hii Jux anasherekea mafanikio yake na brand yake kwa kuwashukuru sana mashabki ambao walikubali kuvaa viatu, kofia, t-shirt na kila kilichotoka ambacho walikibatiza jina la African Boy.

Akiwa nchini China, Jux anaandika haya kwa mashabiki zake kuwa onyesha kuwa brand walioanza kuitengeneza na kuipa jina la pamoja sasa hivi imekuwa na kuweza kumpa dili nono nchini China na kufanya iendelee kukua zaidi.

When i started a african boy it was just ana hashtag statement about being an  young african living, hustling and studying in china.the brand became me and I became the brand from T-shirt to backpacks to shoes you named it.Today i signed asmart and crulative  with chinese manufactuer  vendome ,this would have been impossible without you ,You made African boy yours, and you made it global.

Jux Amwagia Misifa Lukuki Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vizuri kwa hivi sasa na ngoma yake ya ‘Fimbo’ amefunguka na kumwagia sifa msanii mwenzake wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Wiki iliyopita Diamond alivunja rekodi kwa kuwa msanii wa Kwanza nchini Africa kwa kufikisha subsribers milioni moja kwenye ukurasa wake wa YouTube huku akiwafunika wasanii wakubwa kama Davido, Wizkid, Fally Ipupa na wengineo:

Jux amefunguka na kumwagia misifa kibao Diamond kwa mafanikio hayo aliyoyapata na kukiri kuwa ni jambo jema kwani kwa upana wake linazidi kuupeleka mbele zaidi mziki wetu wa Bongo fleva.

Jux amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online ambapo alitiririka haya zaidi:

Hiyo ni bahati ambayo sisi Watanzania tumeipata ni kitu kizuri ni sifa pia kwetu kwa sababu kama ni msanii wa Tanzania anakuwa wa kwanza kufanya kitu kama hicho Africa lazima watu watajiuliza huko Tanzania wanafanya mziki gani ndipo wanapoangalia mziki wa Bongo fleva na pia kukutana na wasanii wengine kwa hiyo ni habari njema na sio mchezo maana sio kawaida na watu wasichukulie kawaida maana kuwapata subscribers kama hao kuwapata sio mchezo”.

 

 

Jux Apokelewa Kama Mfalme Nchini Burundi Haijawahi Kutokea

Mwanamuziki wa Bongo fleva Juma Jux amefunguka na kudai mapokezi aliyoyapata nchini Burundi ni makubwa ambayo hakuyategemea na haijawahi kutokea kwa msanii mwingine.

Jux amefunguka na kusema amepata mapenzi mazito kutoka kwa Waburundi alipokuwepo nchini kwao wikiendi iliyopita ambapo alienda kufanya shoo yake.

Jux amesema kuwa licha ya Mvua kubwa kunyesha siku ya shoo yake lakini bado mashabiki zake walijitokeza kumpa sapoti na kuhudhuria shoo hiyo.

Hit maker huyo wa ‘ Uniua’ alionyesha pia kufurahishwa na mapenzi aliyokuwa anapata kutoka kwa mashabiki zake baada ya kurusha video iliyokuwa inamuomuonyesha akivalishwa shanga na  vitu vingine vya asili ya warundi vinavyoonyesha heshima fulani.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Jux aliandika maneno haya kuwa shukuru mashabiki zake wa Burundi.

Asanteni sana Burundi sitaweza kijamii kusahau upendo wenu kwenye maisha yangu japo mvua kubwa ilinyesha lakini bado mkakubali mnyeshewe na miaka kwa wingi kabisa kwenye shoo we made history nashukuru kwa heshima yenu ya kuniimbia wimbo wa taifa kama heshima yenu kwangu ni hii haijawahi kutokea kwa msanii yoyote aliyewahi kufika Burundi… Asanteni sana”.

 

Huddah Aweka Wazi Hisia Zake Kwa Juma Jux

Mfanyabiashara na mrembo kutoka Kenya Huddah Monroe amefunguka na kuelezea wazi hisia zake juu ya mwanamuziki kutoka Tanzania Juma Jux.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Huddah amefunguka na kueleza kuwa Jux ni mwanaume anayeweza kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Ninavutiwa sana na style ya mavazi ya Juma Jux, yaani walahi his style is on point yaani mimi binafsi sijawahi kumtumia mwanaume meseji lakini siku moja naangalia picha kwa Instagram nikamtumia meseji nikamwambia unapendeza, yaani kila anachovaa kinampendeza. Mimi napenda mtu awe  na style yake mwenyewe yaani havai kama watu wengine wanavyovaa na akijitahidi hiyo style yake itakuja kumpeleka mbali sana”.

Pia kwenye mahojiano hayo, Huddah aliulizwa kama Jux ni aina ya mwanaume ambaye anaweza akawa na uhusiano naye wa kimapenzi alikiri kuwa anavutiwa naye kimapenzi pia kwa sasa yupo single akimaanisha hana mpenzi yoyote.

Ingawa hiyo inaweza ikawa ngumu kidogo kwa upande wa Jux kwani tetesi zinazoendelea kuenea hivi sasa ni kuwa amerudiana na ex wake Vanessa Mdee ingawa Vanessa amekataa lakini za chini ya kapeti zanadai kuwa Jux na Vanessa waliopo kwenye tour ya Fiesta pamoja inasemekana wana ukaribu uliopitiliza urafiki wanaodai wanao, kwani pia wawili hao walishasema kila mmoja kwa wakati wake bado anampenda mwenzake lakini huwezi jua tusubiri tuone.

‘Vannessa hata akitembea na mtu barabarani ni mtu wake’-JUX

Tukirudi katika kumbukumbu vannesa mdee na juma jux walikuwa ni moja kati ya couple pendwa na ya kupendeza hata jwa kuiangalia kwa picha za mitandaoni huku wawili hao walikuwa wakionekana wapo katika mahaba mazito kabisa.lakini hali ilikuja kubadilika baada ya ibirisi kuingulia mapenzi ya wawili hao na mapenzi yao mazito kukoma.Na hivi karibuni kumekuwa na uvumi mitandaoni kuhusu mahusiano mapya ya msanii vannesa mdee na mtu  mwingine maarufu kutoka katika kundi kubwa na maarufu la Wcb wasafi ingawa msanii huyo mpaka sasa bado hajajulikana wazi kuwa ni nani ,jux mpenzi wa zamani wa vannessa mdee nae amezungumzia ilo.

Alipokuwa akiongea  na mtangazaji wa Ayo Tv usiku wa  tarehe 9 septemba katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume mkoani Arusha katika uzinduzi wa tamasha la fiesta, jux  amesema kuwa kwa sasahivi kila mtu ataongea lake na kila atakaeonekana kuongozana na vannessa basi ataonekana  anatembea nae”kila mtu atakaeonekana na vee utaaambiwa hivyo,leo itakuwa huyu,kesho huyo..” alisema jux. hata hivyo alipoendelea kuulizwa alisema kuwa hawezi kuliongelea swala ilo kiundani labda aliongelee vannessa mwenyewe.

Jux aliyekuwa akionekana anajibu kwa wasiwasi kidogo kuhusu tuhuma hizo  na alikuwa akikataa katukatu kuendelea kuuliza maswali  kuhusu mahusiano ya vannesa huku akimtaka mtangazaji kumuuliza maswali hayo mhusika ambae ni vannnesa.na hata alipotakwa kuuliza swali lolote la kimziki kwa vannessa alishindwa na alikataa kabisa kuchimbwa kiundani kuhusu mpenzi wake huyo wa zamani.

jux na vannessa walikuwa katika mahusiano mazito ya kimapenzi na hata baada ya kuachana kumekuwa na utata mkubwa wa nani atasema ukweli na kufunguka kuhusu sababu kubwa ya kuachana kwao,huku kila mmoja kwa nafasi yake akionekana kukiri kuwa bado anampenda mwenzio.

katika interview hiyo pia Jux alitoa taarifa tena kuhusu kubomolewa kwa duka lake la nguo lenye brand ya ‘African boy’ ila amewahakikishia wateja wake kurudi kwa duka hilo hivi karibuni maana pameshapatikana mahali pengine,ivyo wateja wakae mkao wa kula.

Jux: “Bado nampenda Vanessa”

Mwanamuziki Juma Jux amekiri kuwa bado anampenda mpenzi wake wake wa zamani Vanessa maarufu kama V-money , Jux na Vanessa waliachana miezi mitano iliyopita baada ya kudumu kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda wa miaka minne.  Jux aliweka wazi  kuwa wimbo wake mpya “Utaniua” aliouachia  hivi karibuni  alimuimbia Vanessa, Lakini katika mahojiano tofauti aliyofanya Vanessa alisema wimbo wake mpya wa “Kisela” ulihusu maisha yake binafsi na hisia alizopitia katika mahusiano yake na Jux.

Katika mahojiano aliyoyafanya Jux hivi karibuni alikiri kuwa bado anampenda vanessa na ataendelea kumpenda na itakuwa ngumu kwake kumsahau na itamchukua muda mrefu sana. Moja kati ya vitu mashabiki wengi wa wasaanii hawa wamekuwa wakijiuliza na wakitaka kujua ni sababu gani iliyopelekea wawili hao kufikia uamuzi huo wa kuachana, Jux aliweka wazi kuwa muda na umbali uliokuwepo baina yao  ulikuwa kikwazo kikubwa katika mahusiano yao na alisisitiza kuwa kati ya yeye na Vanessa hakuna hata mmoja wao aliyechepuka (kuwa na wapenzi wengine).

Jux amesisitiza kuwa yeye na Vanessa hawana uadui wowote na wataendelea kuwa marafiki wa karibu japokuwa saa nyingine bado ni ngumu kwake kumuona Vanessa kwenye mitandao ya kijamii mpaka kufikia hatua ya kuamua “kum-block “. Lakini amekiri kuwa “Vanessa amenifundisha vitu vingi sana na amenipa changamoto sana kwani yeye ni msanii mzuri kwaiyo nilikuwa siwezi nikaona yeye anatoa nyimbo na video nzuri alafu mimi nikabweteka bali alinipa changamoto ya kuwa mtafutaji”

Jux amemalizia kwa kusema hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa ameamua atumie muda wake kufanya muziki na pia amekiri akisikia Vanessa ana mpenzi mwingine itamuumiza sana.

Vanessa Mdee: Mapenzi yangu na Jux hayakuwa ya kisela

Wiki mbili zimepita sasa tangu Vanessa Mdee kuachia wimbo wake mpya wa kimapenzi ‘Kisela’ aliyomshirikisha Peter Okoye wa P Square.

Mdee, ambaye aliwachana na mpenzi wake Juma Jux, alifunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki huyo.

Mrembo huyo alieleza kuwa mapenzi yake na Jux hayakuwa ya kisela kwani walikua wako na mapenzi ya dhati ingawa iliisha katikati.

“Mapenzi yangu na Juma hayakuwa ya Kisela, lakini pia sitaki na ninakemea kwa nguvu mapenzi ya kisela. Kuhusu kuimba wimbo huu nikwamba nimewasaidia wanawake wenzangu ambao huwa wanaingia kwenye mahusiano bila kujua ni mahusiano ya aina gani waliyonayo. Lakini kwenye uhalisia mimi siishi maisha hayo,” Vanessa aliambia EATV.

Tazama wimbo wa Vanessa Mdee ‘Kisela’ hapo chini: