Juma Nature Amtamani Sana Rayanny

Msanii mkongwe na wa siku nyingi katika game Juma nature , ameshindwa kuficha hisia zake baada ya kuamua kusemwazi kabisa juu ya ufanyajikazi wa msanii rayvanny ambae amekuwa akijituma sana kufanya kazi akitkea katika kundi la wcb.

Juma nature anasema kuwa kama itatokea akapata bahati ya kuchagua ni mtu gani kwa sasa anatakiwa kufanya nae ngoma basi msani wa kwanza kumchagua atakuwa ni Rayvanny kutoka katika kundi la WCB.

Sasa hivi naona vijana wengi wanafanya kazi sana, ila kwa upande wangu mimi , nikipata nafasi nikiwa kama msanii mkubwa nitataka kufanya kazi Rayvanny  na kwa sababu ana kipjai sana.

Pia Juma nature anasema kuwa kati ya muziki wa zamani na wa sasa hivi, muziki wa sasa hivi umekuwa na maendeleo makubwa sana kulinganisja na ule wa zamani hata maisha ya wasanii yaebadilika san.

 

Juma Nature Aungana na Afande Sele Kutoa Madongo Kuhusu Wasafi Festival

Mkongwe wa Bongo Fleva Sir Juma Nature amefunguka na kutoa neno kwa mkongwe mwenzake katika tasnia ya Bongo Fleva Simba wa Morogoro Afande Sele.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nature ameandika ujumbe huo kitu ambacho kinahusishwa na tamasha la Wasafi Festival ambalo linatarajia kufanyika wikiendi hii likitoka mjini Iringa.

Juma Nature kwa asilimia kubwa atakuwepo kwenye tamsha hilo kutokana na kauli aliyoitoa mmoja wa mameneja wa Diamond Mkubwa Fela baada ya kusema ” Mwanangu Juma Nature Kiroboto atakuwepo kwenye Wasafi Festival ya Iringa na Morogoro”

Nature kuitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Mjomba andaa magimbi matamu mwenye chuki anaendelea nachukizake.”

Huu ni muendelezo wa bifu za chini chini zinazoendelea katia ya wasanii  wanaotaka kufanya show na WCB na wale ambao waliotakiwa kufanya show ya fiesta wikiend iliyopita lakini ilishindikana akwa sababu show hiyo ilihairishwa.

Nilitegemea Kuwa Tajiri Kama Diamond:-Juma nature

Msanii Juma Nature anasema kuwa kuwa miaka ya nyuma aliyokuwa akifanya kazi na album zake zilivyokuwa zikifanya  vizuri alitegemea  kuwa kama ingekuwa ni wakati huu basi angekuwa amenufaika sana na kutajirika sana.

Juma Nature anasema kuwa na yeye sasa angekuwa ni moja ya wasanii wachache  wenye mafanikio makubwa sana kama walivyo wakina Diamond lakini ndio muda nao ulishapita.

kwa uuzaji ule wa album kwakwelitulikuwa tunafunikwa funikwa tu wala hatukuwa tunanufaika sana kama sasa hivi na hatukupaswa kuwa hivi.

nilitegemea kwa kipindi kile sasa hivi na mimi ningekuwa hata nina tv zangu kama mnavyomuona Diamond sasa hivi  na viwanda vikubwa vya kwangu mimi mwenyewe.

Juma nature anasema kuwa pamoja na kwamba kuna vitu wanamiliki sasa hivi lakini ni kutokana na kukomaa kwao kama wasanii wa zamani.

 

Q-Chief Anazingua :-Juma Nature

Msanii mkongwe wa muziki Juma Nature amerudi tena baada ya miaka kama mitatu mfululizo aliyokaa kimya na kuamu akutoa wimbo wake mpya.

Juma Nature ameachia nyimbo mbili kwa mfululizo lakini amesema kuwa pamoja na kwamba hata yeye maekaa kimya ka muda lakini hawezi kuacha muziki kama alivyofanya Q-chief kwa sababu kila kitu ni swala la kujipanga.

mimi nilimsikia q-chief akiongea lakin niligundua kuwa alikuwa akizingua tu,mtu ambae anafanya vizuri kwa miaka yote hiyo hawezi kuacha muziki kwa namna hiyo , labda unaweza kukaa kimya kwa miaka kutokana na mambo fulani fulani kisha ukarudi ukajipanga.

Juma nanture anasema kwa sasa yuko kwa ajili ya kazi na yupotayari kufanya kazi na kundi lolote la muziki kama ilivyokuwa kwa TMK.

Juma Nature afunguka kuhusu swala la kuchukiana na Chege Chigunda kwasababu ya mwanamke

Juma Nature ameongelea swala lililowafanya wengi kuamini kuwa hali sahani moja na Chege Chigunda. Msanii huyo mkongwe amekana kuwa mwanamke ndiye chanzo cha beef yake na Chege.

Cha kushangaza ni eti Nature hana beef yoyote na Chege; akizungumza katika kipindi cha eNewz ya EATV, rapper huyo alifunguka na kusema hajawahi kugombana na Chege.

Chege Chigunda

Jibu lake Juma Nature ni bainisho baada ya kuenea tetesi za kipindi kirefu zilikuwa zinawaaminisha watu kuwa mke aliyemuoa msanii huyo ndiye alikuwa mpenzi wa Chege hapo awali mpaka kupelekea kuimba wimbo wenye maudhui ya kumuaga mpenzi huyo uliyopewa jina la ‘Good bye’.

“Mimi sijawahi kugombana na mwanangu, sasa mimi nigombane na damu itawezekana kweli ?, hatuwezi kugombana, tutagombana stejini tu kwa sababu ya usanii lakini hatugombani kama hivyo unavyochukulia wewe”. Alisema Juma Nature.

Juma Nature

 

Juma Nature akana kumlipisha Harmorapa kufanya kolabo naye

Wiki chache zilizopita, rapper mpya kwenye sanaa ya muziki Harmorapa alilalamika kuhusu wasanii wakongwe kuwalipisha wasanii wapya wanapotoa kolabo nao.

“Haipo sawa kwa wasanii wakubwa kutudai sisi ‘underground’ pesa ya kufanyia collabo wakati wanajua bado hata hatuanza kufaidika na muziki wenyewe,” Harmorapa alisema.

Juma Nature, aliyetoa kolabo na Harmorapa, alikana kuwa alimlipisha Harmorapa kufanya kolabo naye. Akiongea na kipindi cha E News cha EATV, Juma Nature alisema Harmorapa hana pesa ya kumlipa.

“Nikisema nimemlipisha Harmorapa pesa kwa ajili ya kolabo nitakuwa nakosea. Mimi ni mtu mzima nilikubali kufanya wimbo na msanii yule kwa sababu ni mkali na anajua muziki pia na imani atafika mbali. Hawezi kunilipa mimi, ana hela gani?,” Juma Nature aliambia EATV.

Harmorapa