Monalisa: Sina Bifu na Kajala

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa ameibuka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na msanii mwenzake Kajala Masanja bali watu wanataka tu kuwagombanisha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Monalisa alisema watu wamekuwa wakizungumza maneno mengi ambayo yanaweza kusababisha wagombane wakati wao wako vizuri, hawana tofauti yoyote kama watu wanavyosema.

Sina bifu na Kajala ila naona watu ndiyo wanataka kutugombanisha, naomba watu waache maneno jamani ili maisha mengine yaendelee maana kila siku ni hilohilo tu“.

Monalisa amesema Baada ya sakata la matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka Wiki chache zilizopita amvbapo Watoto wa wasanii hao walikuwa wanasoma shule moja Lakini Baada ya Mtoto wa Kajala Kufeli na Mtoto wa Monalisa kufaulu kuna maneno ya uchochezi yalizungumzwa kupelekea kuonekana kama wana bifu.

Monalisa Amefungukia Video Ya Kajala na Mwanaye

Msanii mkongwe wa Filamu za Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kupima uzito video ya Kajala na Mtoto Wake Paula.

Siku chache zilizopita and Kajala na binti yake wa miaka 16 Paula walitengeneza headlines Baada ya video yao iliyowaonyesha wakikata mauno kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Monalisa ambaye ana ukaribu na Kajala Lakini pia Watoto wao wamesoma wote amefungukia Sakata hilo na kusema kuwa haoni tatizo mama kucheza na Mtoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya mtandao wa Millard Ayo, Monalisa amedai kuwa pamoja na kwamba hajaiona video hiyo Lakini pia hajaona tatizo Kama ni mama tu anacheza na Mtoto Wake.

Kajala Ajitetea Kwa Kukata Mauno na Mtoto Wake

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja ameibuka na kujitetea Baada ya video iliyomuonyesha akikata mauno na binti yake Paula kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Kajala alisema kuwa video hiyo haikuwa na lengo baya kama watu wanavyomshambulia mitandaoni bali ilipigwa alipokuwa akicheza na mwanaye huyo kama kujifurahisha tu.

Watu wanatakiwa kujua video hiyo haina ubaya na wala haijavujishwa na mimi wala Paula, siku hiyo nilikuwa nyumbani nimelala kwani nilikuwa naumwa kwa muda mrefu.

Akaja Paula na rafiki yake msichana aliyekuwa akisoma naye akaniomba niamke ili nichangamke kidogo kwani alinionea huruma kwa kukaa kwangu ‘siriasi’.

Basi tukaweka muziki tukawa tunacheza kama mama na watoto wake. Baada ya hapo yule rafiki wa Paula alirekodi video na kuitupia kwenye group la wanafunzi wa shuleni kwao na kuiwekea maneno kuwa anatamani kuwa na mama kama mimi.

Hapo ndipo watu wakaanza kurushiana na mwisho ndiyo ikafika kwenye mitandao ambako imezua mjadala mbaya”.

Kajala amesisitiza  kuwa video hiyo haikuwa na nia mbaya au hakutaka kumkuza mwanaye mdogo kama wengi ambavyo wamekuwa wanadai bali ilikuwa ni katika kujifurahisha.

Video ya Kajala na Mwanae Yazua Gumzo

Kuna video imekuwa ikismbaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha msanii kajala akiwa na mtoto wake wa kike paula wakiwa wanakatika na video hiyo kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii na kufanya mahsabiki kuongea sana.

Hata hivyo baada ya wawili hao kusambaza video hiyo, mashabiki walikuwa na maneno mengi ya kusema huku wakisema kuwa kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na maadili ya watoto watakuwa wakiharibiwa sana na wazazi wao kutokana na malezi.

Video hii pia inawarudisha nyuma mashabiki wao na kuanza kusema kuwa inawezekana pia kuwa hata kufeli kwa mtoto huyo kumekuwa kukichangiwa sana na malezi ya mama huyo kwa mtoto wake.

kajala aliwahi kufunguka na kusema kuwa aliumia sana  baada ya mashabiki kumuandamana mtoto wake huyo kutokana na ukweli kuwa amefeli lakini hawakupaswa kumsema vibaya katika mitandao, lakini kwa swala hilo la kusambaza video hiyo watu wanaona kuwa swala hilo ni sawa tu.

https://www.instagram.com/p/Btvz1UxBlEp/

 

 

 

Kajala Atoa Tamko Baada Ya Mtoto Wake Kufeli

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kutaka watu waache kumuongelea binti yake Paula kuwa amefeli kwani atahakikisha anafika chuo kikuu.

Wiki chache zilizopita Mtoto wa Kajal anayeitwa Paula alitengeneza headlines Baada ya matokeo yake ya kidato cha nne kutoka na kuonyesha kuwa amefeli mashabiki kwenye Mitandao ya kijamii walimjia juu na kuanza kumsema vibaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Kajala  ameamua kufunguka akishangazwa na watu kufuatilia na kutokwa povu na matokeo ya mwanaye, Paula.

Nafahamu kila kinachoendelea huko mtandaoni kuhusu matokeo ya Paula, niliamua kukaa kimya kwa kutojibizana na watu ili mwanangu abaki kuwa salama. Watu wanatakiwa kufahamu kuwa Paula ana wazazi wake, sio yatima hivyo kamwe hatakuwa mpweke.

Nashangazwa na inaumiza watu wanaacha kazi na kuanza kumrushia maneno makali mwanangu kwa lengo la kumkatisha tamaa, yaani kama ndio waliokuwa wakimlipia ada na huduma zingine. Watambue kuwa siwezi kumuacha mwanangu alie peke yake, nitakuwa naye kumtia moyo na kujipanga upya katika eleimu yake na atasoma hadi chuo kikuu“.

Lakini pia Kajala amesema kuwa matokeo yake kuwa mabaya hazina kabisa mahusiano na malezi anayolelewa nyumbani.

Unajua jambo linapotokea basi utayasikia mengi sana, Paula sio mtu wa starehe ya kwenda klabu sasa wamemuona wapi? Au ni malezi gani wanayataka nimlee mwanangu kwa sababu namlea kwenye maadili mema au hawataki niwe karibu na mwanangu ama kuwa na akaunti ya instagramu ni nongwa?.

Naomba wamuache mwanangu jamani, imetosha sasa na hao wanaotoa kauli za kejeli wenyewe wamesoma, narudia tena Paula atasoma hadi chuo kikuu na atakuja kuwashangaza“.

 

Kajala Afunguka Baada Ya Mwanaye Kufeli

Muigizaji wa filamu za Bongo movie Kajala Masanja maarufu kama Kay amefunguka kwa Mara ya kwanza tangu Wiki iliyopita matokeo ya Mtoto Wake Paula yalivyotoka na kuonyesha kuwa amefeli.

Stori iliyotrend Wiki iliyopita Baada ya matokeo ya kidato cha kutoka ni matokeo ya Mtoto wa Kajala na mtayarishaji wa muziki mkongwe Pfunk Majani, Paula kutoka kuwa amepata daraja la nne.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Kajala alisema kuwa inasikitisha kuona watu wazima wanamrushia maneno makali mtoto wake na ya kumkatisha tamaa lakini yeye kama mzazi hawezi kumuacha asimuendeleze kwa sababu tu kafeli mtihani ambao anaamini hata wanaomtolea maneno mwanaye walifeli pia.

Mimi kama mzazi siwezi kufurahi maneno wanaomrushia mwanangu kwa sababu hata kufeli kwake siyo sababu ya kushindwa kumuendeleza kielimu na mimi kama mama nitamsimamia Paula, mpaka atafika chuo kikuu na watu hawataweza kuamini na kingine wamuache mtoto wangu jamani”.

 

Mfahamu Cassie Kabwita , Mwanadada Alietaka Kuchora Tatoo ya jina la Kajala

Mwanadada Cassie Kabitwa kutoka nchini Zambia ni moja ya wasanii waaofanya vizuri katika maigizo nchini humo huku kwa hapa tanzania akiwa ni rafii mkubwa wa masnii Kajala Masanja.Kajala na cassie walishafanya kazi nyingi pamoja na wamekuwa na urafiki mkubwa hata wa kuwa kama mtu na dada yae kutokana na ukaribu wao huo.

Cassie  anasema kuwa amekuwa akimpenda sana Kajala kiasi kwamba alitaka kuchora tatoo yenye jina la kajala lakini hakuruhusiwa na Kajala mwenyewe baada ya msanii huyo kumkalisha chini Kajala na kumwambia hasara za kuchora tattoo mwilini.

Cassie anasema , hakuona ajabu kuchora tattoo kuonyesha mapenzi kwa rafiki yake huo ambae kwa sasa amekuwa kama dada, lakini kajala nae hakutaka kuonyesha mapenzi ya kinafiki kwa kutaka kuchorwa tattoo ilhali anajua hasara za tattoo hivyo alikaa nae chini na kumuelezea swala hilo na waliweza kuelewana kabisa.

Matokeo ya Mtoto wa Kajala Yatafutwa Kama Pesa

january 24 , matokeo ya kidato cha nne yalitoka na kuibua hisia tofauti kwa watu kutokana na kwamba watoto wengi waliakuwa wakitegema amvuno ya kle wakicgokipanda shuleni kufanikiwa.katika mitandao ya kijamii imezua sura mpya baada ya msanii monalisa kuonekana mwenye furaha sana baada ya mtoto wake wa kwanza wa kike sonia kuondoka na division one tne aya A ya hesabu.

Lakini swala hili linazidi kuwa kubwa na kuzua maneno kwa sababu pia mtoto wa msanii wa bongo fleva kajala masanja anaejulikana kama paula pia amemaliza mwaka aliomaliza mtoto wa mona lisa na inasemekana kuwa walisoma shule moja.

Kama ilivyokuwa kwa monalisa na wazazi wengine kuwa na furaha na kuyatangaza matokea ya watoto wao, hii imekuwa tofauti kwa kajala kwa sababu hajasema chochote ilhali siku ya mahafali aliweka picha za kusherekea huko.

Basi kila mtu amekuwa akiongea lake hku page za udaku yakitafuta kwa hali na mali matokeo hayo ili kuyaweka hadharani.

 

Kajala Akiri Kuchukizwa na Ubonge Wake

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukizwa sana na mwili wake ulivyokuwa kwa sasa Baada ya kunenepa sana.

Kajala ameweka wazi kuwa kati ya vitu ambavyo anavichukia kwa sasa ni pamoja na mwili wake kuwa mnene kupitiliza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kajala amesema kuwa ubonge wake kwa sasa umefikia kiasi cha kumnyima raha kwani hata nguo zake nyingi ameshi-ndwa kuzivaa kwa sababu hazimpiti mwilini.

Jamani huu mwili mpaka nahofia naweza kupata presha au gonjwa lolote linalotokana na kunenepa sana maana hata mazoezi naona sasa yamedunda, najitahidi kupambana ili niweze kurudi kama zamani”.

Kajala ametangaza kuongezeka mwili kutokana na maisha ya stare he anayoishi kwa Hivi sasa hasa kutokana na mkataba Wake na Biko ambao unamuingizia mkwanja mrefu.

 

Kajala Atangaza Kujiweka Mbali na Mabifu Kwa Mwaka Mpya

Staa wa filamu za Bongo movie Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuwa amedhamiria kuumaliza mwaka 2018 vizuri bila mabifu na watu na pia kuuanza mwaka 2018 vizuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Kajala amefunguka na kusema kuwa anamuomba mno Mungu aanze mwaka ujao akiwa hana adui na hata kama kutakuwa na mtu amemkosea, ataenda kumuomba msamaha kwa sababu anataka kufunguliwa mambo yake.

Kabla ya kumaliza mwaka huu, sitaki kuwa na bifu na mtu na hata kama kuna mtu nitakuwa nimemkosea, nitamfuata mwenyewe na kutaka mwaka unaokuja tuuanze vizuri, mambo ya mabifu yanafunga bahati na mambo mazuri“.

Kajala ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa na mwaka mzuri wa 2018 ikiwemo kuwa na kazi nzuri na kujiheshimu kwa kuepuka skendo kwenye mitandao ya kijamii.

Kajala Ataja Masharti Ya Yeye Kuingia Kwenye Ndoa Tena

Msanii wa Bongo movie na balozi wa Biko nchini Kajala Masanja ameibuka na kuweka wazi vigezo vya mwanamke ambaye anaweza kufunga naye ndoa kwa Mara ya pili.

Kajala amefunguka na kuweka wazi kuwa atakuwa tayari kwa ndoa endapo tu atapata mwanaume ambaye ni mkweli na mwaminifu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Kajala amesema kuwa yeye kama mwan­amke bado anatam­ani kuingia kwenye ndoa na akitokea mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ataolewa kwa mara ya pili.

Nilishaolewa mara ya kwanza, la­kini kama mwanam­ke bado ninahitaji kuolewa, suala hilo lipo akilini kwangu, akitokea tu mwa­naume mkweli, naolewa”.

Kajala ambaye ni mama wa Mtoto mmoja wa miaka Kumi na Sita amekwisha watu kuolewa miaka ya nyuma na mwanaume anayejulikana Kama Faraji Chambo lakini ndoa hiyo ilivunjika baada ya mwanaume huyo kuhukumiwa kifungo jela.

Kajala Masanja Akiri Kumtembezea Bakora Mwanaye

Muigizaji wa Bongo movie na Balozi wa Biko nchini Kajala Masanja maarufu Kama ‘Kay’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kwenye malezi ya mwanaye wa pekee Paula haoni hatari kumpa kichapo pale inapobidi.

Kajala amezaa Mtoto mmoja Paula na mtayarishaji wa muziki mkongwe nchini P Funk majani na Bongo huyo Ana umri wa miaka kumi na Sita.

Katika interview aliyofanya na Global Publishers, Kajala amefunguka kuhusu malezi ya Mtoto Wake huyo na kusema:

Wengine hawawezi kujua ni jinsi gani ninaishi na Paula. Unajua mimi ni mama kijana, lakini lazima mtoto wangu anitii na aishi vile ninavyotaka au ninavyomuelekeza na akinizingua ninamfundisha adabu. Lakini pia kuna wakati tunaweza kuzungumza tukacheka na kutaniana.”

Kwenye mahojiano hayo Kajala alifunguka na kuweka wazi kuwa huwa anamchapa mwanaye pale inapobidi kufanya hivyo:

Nampiga tena siyo kitoto, anaponikosea mimi ni mkali sana. Siku zote nilifundishwa na mama yangu ‘akupigaye ndiye anayekufunza’. Paula anapokosea ninamfundisha na panapostahili kumchapa nafanya hivyo japokuwa siyo mara nyingi maana Paula ni mkubwa sasa, tunakaa tunazungumza na ananielewa vizuri na kuna kipindi tunakuwa marafiki sana.”

Lakini pia Kajala alifunguka kuhusu Changamoto za kulea Mtoto Kama Single mother kwani yeye na baby daddy wake waliachana kitambo sana:

Ni magumu kwa sababu sidhani kama kuna mama anapenda kulea mtoto bila baba ila kwa sababu imenilazimu kuwa hivyo, sina jinsi na uzuri Mungu kanipa nguvu ya kusimama kama mama ingawa huwa anakwenda kwa baba yake anapopata nafasi.”

Kajala Masanja Amkingia Kifua Wema

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Kajala Masanja ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Wema Sepetu baada ya kukosolewa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kusambaza picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

Kajala ameibuka na kusema kuwa huu si wakati wa kushangilia kilichomtokea msanii mwenzake ambaye pia alikuwa rafiki yake wa karibu, Wema Sepetu bali inapaswa kumpa moyo na kuwa naye karibu.

Kwenye interview aliyofanya na Gazeti la Ijumaa kuhusu suala la kuvuja kwa video za Wema na mpenzi wake aitwaye Patrick Christopher ‘PCK’ wakiwa faragha, Kajala alisema kuwa kila binadamu anakosea kwa sababu hawezi kuwa mkamilifu katika maisha yake yote hivyo kukosea ni jambo la kawaida hivyo anampa moyo Wema, asijione mkosefu sana na kukata tamaa ya kuendelea kufanya kitu chochote.

Sioni kama ni sawa kila mmoja kumuona Wema kama ni mkosefu kupitiliza kwa sababu najua wazi hakuna aliye mkamilifu hata kidogo na siku zote kuteleza sio kuanguka ni wakati tu wa kumpa moyo na kuwa naye karibu”.

Tangu sakata hilo litokee baadhi ya wasanii ambao walikua marafiki wa Wema wamemgeuka na kutaka afungwe ili liwe fundisho mmoja wapo ni pamoja na Steve Nyerere na wasanii wengine kama vile Ray Kigosi, Esha Buheti na wengineo.

Kajala-Umri Umenikatisha Tamaa Ya Kuzaa Mtoto Mwingine

Msanii wa filamu za Bongo movie na mtangazaji na balozi wa Biko, Kajala Masanja ameibuka na kuweka wazi kuwa amekata tamaa ya kuzaa mtoto mwingine kutokana na umri wake kumtupa mkono.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Kajala amesema kuwa, kipindi cha nyuma alikuwa akisaka mtoto mno, lakini ilishindikana hivyo umri unasogea na pia mtoto wake ameshakua ni msichana mkubwa hivyo inabidi aangalie maisha mengine na siyo kuzaa tena.

Nilitamani sana kupata hata watoto wawili, lakini ilishindikana kwa wakati, hivyo nimeona bora sasa kuangalia kitu kingine mbele maana nimekata tamaa kabisa ya kuongeza mtoto mwingine, ninajikita kwenye kumuwezeshe Paula asonge mbele kielimu”.

Kajala ameweka wazi kuwa kwa sasa ana umri wa miaka 36 hivyo anajiona tayari ameshakuwa mtu mzima sana. Kajala amezaa mtoto mmoja na mtayarishaji legendari wa muziki wa Bongo fleva P funk Majani.

Kajala Awaonya Wasanii Wanaoendekeza Bata

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Kajala Masanja amefunguka na kuwatolea uvivu Wasanii Wenzake ambao wamekuwa wakijianika Kwenye mitandao ya kijamii wakila bata tu.

Kajala amefunguka na kusema zama za kutafuta sifa kwa kuonekana unakula sana bata zimepitwa na wakati kwani hivi sasa watu wanaangali zaidi kazi na kufanya mambo ya maendeleo.

Kwenye mahojiano yake Gazeti la  Risasi Jumamosi, Kajala alisema yeye kuna wakati alijisahau na kujikita kwenye mambo hayo lakini sasa ameshtuka na ndio maana hawezi kuonekana viwanja ‘akitumbua’ pesa.

Unajua huu ni wakati wa mastaa kushituka na kufanya mambo yatayowasaidia wao na familia zao siku za baadaye. Mimi nimestuka, niliyokuwa nayafanya siyo mazuri ila sasa nafanya yale ambayo mtu makini anatakiwa kuyafanya“.

Kajala ni mmoja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakionekana busy kabisa na kupiga kazi kama mtangazaji na balozi wa Biko Tanzania.

Kajala Amwaga Milioni 16 Kununua Vito Vya Thamani

Muigizaji wa Bongo movie na Mtangazaji Kajala Masanja ameweka wazi kuwa ametumia zaidi ya Milioni kumi na Sita kununua vito vya thamani.

Kajala ameteketeza Milioni kumi na Sita kununua saa yake ya mkononi ambayo inamchanganyiko wa dhahabu na almasi pamoja na bangili ambazo amedai alizipenda sana.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Kajala alisema kuwa, alinunua saa hiyo na bangili wakati akiwa nchini Dubai na alifanya hivyo kwa sababu aliipenda sana seti hiyo na ni moja ya vitu ambavyo anapenda kuwa navyo.

Unajua naweza kupenda kitu leo nikawa nachanganyikiwa nacho kabisa maana nilitokea kuvipenda nikasema nikirudi mara ya pili nitanunua maana mara ya kwanza hela yangu haikutosha”.

Kajala anatajwa kuwa na mkwanja mrefu kutokana na kazi yake ya ubalozi wa Biko Lakini pia kupitia sanaa ya uigizaji.