Karen Afungukia Mahusiano Ya Petit na Baba Yake Gadner

Msanii wa muziki kutoka THT anayefanya vizuri hivi sasa kwenye tasnia ya Bongo fleva na ngoma yake ya ‘Washa’ amesema Baba yake ambaye ni mtangazaji wa Clouds fm Gadner G Habash Hana tatizo na Petit Man.

Kwa wiki kadhaa kulikuwa na tetesi Kuwa Petit Man Ana mahusiano ya kiampenzi na Karen na hata kusemekana kuwa wamefunga ndoa Baada ya picha zilizowaonyesha wakiwa kwenye video shoot ya wimbo wake kusambaa mtandaoni.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Karen amesema ingawa mitandao mingi ilikuwa ikiandika ndivyo sivyo kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na Petit Man, jambo ambalo si kweli Alisema familia yake inajua vizuri ishu hiyo kuwa ukaribu uliokuwepo kati yake na Petit na hata baba yake hakuwa na tatizo naye.

Watu wengi ninaojuana nao na baba anajuana nao vizuri kwa hiyo hata hiyo habari ilivyoanza kuvuma haikuleta shida kwa sababu familia yangu inafahamu kila kitu kuhusu Petit Man”.

 

Karen-Sijapata Mwanaume Wa Kuwa Naye Kwenye Mahusiano

Msanii mchanga kabisa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Washa’ Karen Gadner Habash amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sababu hajapata mwanaume wa kuwa naye.

Karen alitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kusemekana kuwa kwenye mahusiano an kufunga ndoa na mume wa zamani wa Esma Platnumz, Petit Man Wakuache.

Karen amefunguka kuwa hana mahusiano na Petit Man kama ambavyo wengi walidhani bali ni marafiki tu na ni mtu ambaye aliamua kumsapoti kwenye kazi yake baada ya kuona wimbo ulihitaji kuwa na wanandoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Karen ameweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sasa lakini endapo atatokea na katika muda sahihi basi atakuwa hana neno;

Kusema ukweli sina mpenzi kwa sasa nipo single lakini kama atajitokeza na kwa mtu ambaye nitakuwa namuhitaji basi nataka awe muelewa kuhusu kaiz yangu nzima ya usanii na aweze kunisapoti sana lakini pia aipende sana familia yangu hasa wazazi wangu kikubwa aweze kuwaheshimu”.

 

Karen Gadner Afungukia Ndoa Yake na Petit Man

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Karen Gadner amefungukia tetesi zilizomzunguka hivi sasa kwa kuwa amefunga ndoa na mdau wa muziki wa Bongo fleva Petit Man.

Tetesi za Petit kuwa na Mahusiano na Karen zilianza kupamba moto Wiki chache zilizopita baada ya kuonekana kama wanavaliana nguo lakini sakata hilo limechukua Sura mpya baada ya Tetesi za ndoa.

Picha zinazoonekana Kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kama wawili hao wamefunga ndoa lakini kuna taarifa kuwa inawezekana ikawa sio ndoa bali ni video ya wimbo mpya wa Karen wanashoot.

Baada ya sintofahamu Hizi mtandao wa Bongo 5, ulimtafuta Karen na kutaka kumuhoji kuhusiana na tetesi hizo za ndoa na Petit.

Picha nilizoweka zinajielezea tayari kwa kile kilichotokea, kwa sasa siwezi kusema kitu kingine nimechoka Jamani”.

Karen alikataa kufunguka kwa undani zaidi kuhusu kilichotokea na kuwataka watu waendelee kisubiri kwani watajionea mwishoni.