Kim Nana Amwaga Povu Kisa Penzi la Diamond na Tanasha

Video vixen na mwanamitindo Lilian Kessy  maarufu kama Kim Nana amejikuta akimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu Ex Wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.

Kim Nana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa muda kabla ya kumwagwa chini miezi michache iliyopita na Diamond kuanza mahusiano na Tanasha.

Kim Nana ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la Diamond na Tanasha baada ya Gazeti la Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha.

Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.

 Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?”.

Diamond Ruksa Kumuoa Kim Nana-Lynn

Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia kichupa cha wimbo wa ‘Kwetu’ wa Msanii Rayvanny, Irene Hillary maarufu kama Lynn amefunguka na kusema ni ruksa kabisa Kwa Diamond kumuoa Kim Nana.

Lynn alifunguka hayo siku chache Baada ya warembo hao wawili wanaosemekana kufaidi Penzi la staa huyo wa Bongo fleva kugongana katika shoo ya Wasafi Festival mkoani Mtwara.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa warembo hao ni Kama paka na panya kutokana na wote kumpenda staa huyo hivyo walivyokutana Mkoani Mtwara kila mmoja alipooza na kuonekana wakiangaliana kwa jicho la uhasama.

Kama utakuwa uliwafuatilia walipopanda jukwaani utakuwa uliwashuhudia walivyokuwa wakikatana jicho la ukali.

Lakini Kim anaonekana kuibuka kidedea maana tofauti na Lynn, yeye alionekana mwenye furaha huku akikata nyonga kuashiria hakuwa na stresi kama mwenzake.

Hata wakati wa kurudi Dar, Lynn alipanda gari la wanenguaji na njiani alionekana kabisa hana furaha, tofauti na Kim aliyepanda kwenye gari moja na wanamuziki wa Wasafi na kujitwalia mapozi kama yote hivyo kumaliza kabisa umalkia wa Lynn ndani ya Wasafi”.

Baada ya tetesi hizo za kuwepo wivu wa kimapenzi Lynn alipiga stori na Gazeti hilo na kufunguka kuhusu  mahusiano yake na  Diamond na Kim Nana.

Unajua kuna kitu watu hawakijui kuhusu mimi na Diamond. Mimi na Diamond hatua uhusiano wowote ule.

Diamond ni mshkaji wangu sana kwa hiyo hata akimuoa Kim haiwezi kuniuma kwa sababu atakuwa wifi yangu na nimebariki amuoe tu wala sina tatizo lolote,

Quick Rocka Afungukia Mahusiano na Kim Nana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva  nchini Aboot Rocka maarufu kama Quick Rocka amefunguka kuhusu  mahusiano na mrembo ambaye ni video queen Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana.

Kim Nana alijizolea umaarufu miezi michache iliyopita Baada ya kusemekana kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz.

Quick Rocka ameibuka na kukana kuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo na kusisitiza kuwa mahusiano pekee aliyokuwa naye ni urafiki wa kawaida sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Quick Rocka amefunguka haya:

Ni kweli namfahamu Kim Nana kama mtu niliyekuwa nafanya naye kazi tu lakini hakuna mambo ya mapenzi kabisa.”

Tetesi za Kim Nana kutoka na Quick Rocka zilianza baada ya msanii huyo kuonekana anamposti mrembo huyo mara kwa Mara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kim Nana Adaiwa Kubadili Dini Kisa Diamond

Video vixen anayetrend sana kwenye mitandao ya kijamii Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana ambaye pia ni mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz anasemekana kubadilisha dini kutoka kuwa Mkristo mpaka muislamu kwa ajili ya ndoa na Diamond.

Gazeti la Amani linaripoti stori hiyo ambapo ndugu wa karibu na msanii huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisema kuwa Diamond kwa sasa yupo na uhusiano ambao upo ‘siriasi’ kwani amefikia hatua ya kumbadili dini mpenzi wake huyo ili waingie naye kwenye ndoa.

Nyie hamjui, wanaosema eti Kim Nana ametupiwa virago vyake nje huko Madale nyumbani kwa Diamond na mama yake, wamepitwa na habari, mwenzao Diamond kambadili dini anataka kumuoa kwani hata muda mwingi yupo na mama mkwe wake pale Madale”.

Wiki iliyopita kuna stori ilisambaa kuwa penzi la Diamond na Kim Nana lilifika mwisho mara baada ya mrembo huyo kutimuliwa nyumbani kwa Diamond Madale na Mama Diamond baada ya kutibuana.

Mama mzazi wa Diamond Bi. Sandra amefungukia tetesi hizo na kusema Kim Nana hajatimuliwa Madale bali yupo pale Kim yupo nyumbani kwake na sasa amebadilishwa dini na mwanaye ambapo anafundishwa kusoma Kuruani na mumewe Maisala Shamte ‘Anko’ na ndio maana wako karibu muda wote.

Kwa taarifa yenu Kim nipo naye muda mwingi na sasa amebadili dini, anafundishwa Kuruani na mume wangu kwa hiyo watu watasubiri sana kama wanadhani ataachwa leo wala kesho, hilo halitatokea”.

Mwanzoni mwa mwaka huu Diamond alimuahidi mama yake hatamaliza mwaka 2018 bila kuoa labda huu ndio muda muafaka wa kumuoa mpenzi wake huyo.

Rommy Jones Adai Mwanamke Pekee Anayemfaa Diamond ni Zari

Kaka wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Rommy Jones ameibuka na kudai mwanamke pekee  anayemfaa mdogo wake ni Mpenzi wake wa zamani na mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari’.

Mahusiano ya Diamond yameendelea kutengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii hasa sasa kutokana na warembo wawili ambao ni Kim Nana na Lynn kuonekana kugombani Penzi la staa huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Rommy Jones, amefunguka kuwa mke pekee ambaye anamfaa mdogo wake huyo ni mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’.

Nasema ukweli ndani ya moyo wangu, Zari ni mwanamke ambaye anafaa kuwa mke na kuwekwa ndani kwa sababu anajielewa na anasimama kama mama kuanzia kwenye ulezi wa watoto wake na kila kitu ndani ya nyumba”.

Rommy amesema anatamani Zari awe shemeji yake wa maisha na ikiwezekana wafunge ndoa kwani ana kila sifa ya kuwa mke na ndiye mwanamke pekee anayeweza kumuweka sawa mdogo wake na akaenda kwenye njia sahihi.

Unajua kila familia ingependa sana kuona mtoto wao anapata kitu kilicho bora, yaani mke ambaye anaweza kusimama vyema kama mama hivyo mimi leo nikiamka Diamond aniambie anamuoa Zari, nitafurahi sana kwa sababu najua atakuwa amepata kilicho bora kabisa”.

Lakini pia Rommy hakusita kuwaongelea Lynn na Kimnana ambapo amesema;

Unajua Diamond kwa hao (Lynn na Kim Nana) ni kama tu zile za mwanaume kutenda kosa na kuchepuka nje, lakini akawa na msimamo na mwanamke wake, kwa hiyo kwa hao siwezi kumuongelea sana kwa sababu pia sisi hata siku moja hatukai na kujadiliana naye mambo yake ya kimapenzi, ila ukizungumzia mke, basi nitakuambia ni Zari tu”.

Husna Ajaribu Bahati Yake Kwa Diamond

Mrembo ambaye aliwahi kufanya vyema Kwenye Mashindano ya Miss Tanzania 2011/2012 Husna Maulid ameibuka na kudai kuwa na yeye ni mmoja kati ya warembo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Sakata hilo la Husna lilitokea siku chache zilizopita baada ya kuweka picha yake Instagram na kusindikiza na maneno ‘Roho Ya Simba’ na kuonyesha yupo Madale nyumbani kwa Diamond jambo lililosababisha mashabiki kumjia juu.

Mashabiki walimshambulia kwa kitendo cha kumuweka na yeye kwa Diamond ilhali anajua kwamba tayari ana wanawake kadhaa tayari Kwenye Mahusiano naye.

Baada ya povu hilo la mashabiki, Husna alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo alimwaga povu kwa watu wanaosema anamtaka Diamond ambaye ni bwana wa Lynn.

Unajua kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, huyo Lynn ni nani, siwezi kumuhofia yeye wala mwanamke mwingine yeyote maana kila mtu na bahati yake, wanaotukana watukane watachoka”.

Hivi Diamond tayari amekwisha mmwaga Lyyn na Yupo Kwenye Mahusiano na Mrembo mwingine anayeitwa KimNana.

Kim Nana Awataka Wadangaji Wajaribu Ujasiriamali

Video vixen anayefanya vyema sasa Kwenye ulimwengu wa muziki wa Bongo fleva Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana amewataka wanawake wadangaji kutafuta biashara ya kufanya.

Kim Nana amefunguka na kudai anawashangaa sana wanawake wanaofanga mjini badala ya kutumia muda wao na nguvu zao kwa ajili ya kutafuta biashara za kufanya.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Kim Nana amesema kuwa anawashangaa wasichana wengi hasa mastaa wanaodanga wakati fursa za biashara zipo nyingi na mbali na biashara kazi za kufanya zinapatikana.

Unajua sisi ambao tuna majina tayari yawe makubwa au madogo ukijaribu kitu kushindwa ni ngumu sana hivyo mimi nawashauri wanaodanga wabuni hata miradi au wajitokeze kwenye makundi yanayofunza ujasiriamali watatoka tu kimaisha“.

Kim Nana pia amewataka watu kufuta dhana inayosambaa kuwa mavideo Queen wote ni wadangaji kutokana na kipato chao kidogo wanachopata kutokana na kazi hiyo.

Kim Nana Awatolea Povu Gigy Money na Lynn

Video Queen anayefanya vizuri kwa hivi sasa Lilian Kessy maarufu kama Kim Nana amewapa kichambo cha maaana warembo wenzake Lynn na Gigy Money baada ya kurushiana matusi.

Wiki iliyopita kuna video clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyowaonyesha Gigy Money na Lynn wakiwa wanarushiana mitusi mizito mizito na hata kudaiwa kupigana.

Kim Nana amewatolea povu wasichana hao kwa kitendo walichofanya mbele ya jamii huku akidai jambo hilo linawafanya watu wawaone walio katika fani ya uvideo Queen ni wahuni tu kama wao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,  Kim Nana alisema hakufurahishwa na wauza nyago hao kusemeana mbovu hadharani kwani ingekuwa vema wakaitana pembeni na kugombana pasipo kuwapa watu faida hasa ikichukuliwa kuwa, wao ni kioo cha jamii.

Unajua wameshindwa kutambua kuwa wao ni kioo cha jamii na  maneno waliyokuwa wakirushiana yanafanya watu waidharau fani yetu na kuona kuwa ni ya kihuni kutokana na kuropoka ovyo mbele za watu“.

 

Mrembo Kim Nana Adai Amber Lulu na Gigy Maney Sio Level Zake

Video Queen anayekuja kwa kiasi ya ajabu Kwenye tasnia Lilian Paul Kessy maarufu kama Kima Nana amewaponda vibaya mno wasanii Amber Lulu na Gigi Money huku akidai hawafai kuwa mavideo vixen.

Kim Nana alijizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video za wanamuziki kama Beka Flavor ameibuka na kudai mavideo Queen hao ambao wameongia Kwenye Bongo fleva hawakuwa level zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, amefunguka na kudai ni bora wadada hao walivyoingia Kwenye muziki kwani hawakuwa na mvuto wa kuwa wauza sura wa Kwenye video:

Amber Lulu na Gigy Money hawanivutii kabisa na hawana mvuto wa kuwa ma-video queen. Bora ‘wa-stick’ hukohuko kwenye muziki walikokimbilia”.

Lakini pia mrembo huyo alijitamba ni bora kuliko mavideo Queen wote kwa Bongo kwa sababu ana muonekano wa kuwa hivyo tofauti na ilivyokuwa kwa Gigy Money na Amber Lulu.

Amber Lulu

Kim Nana alipoulizwa kuhusu tuhuma za mavideo Queen wengi Bongo kutembea na wasanii mbali mbali ili wapate umaarufu alikataa na kudai yeye yupo kikazi zaidi hana time hiyo:

Mimi ninajiheshimu, nikiitwa na mwanamuziki kuhusu kazi, tunafanya halafu basi. Tutaendelea kuwasiliana kwenye mambo mengine, lakini siyo mapenzi. Sijawahi kutoka kimapenzi na staa yeyote Bongo na sitarajii hilo kwa sababu kuwa na uhusiano na mastaa kuna-umiza kichwa. Wengi hawa-jatulia“.