Kivazi Cha Kitenge Kinavyowatoa Wanaume

Ilishazoeleka kuwa vazi la kitenge ni maarufu kwa wakinamama na wakina dada tu, lakini siku hizi mambo yamebadilikakabisa , mishono n mitindo imezidi kuwa mingi, fashion inazidi kupanuka na wanaume nao wameamua kuja na fashion ya vitenge tena imekuwa ikiwatoa isivyo kawaida.hawa ni baaadhi ya wasanii wa Tanzania wa kiume walitokea vizuri kabisa katika kivazi cha kitenge.Raha ya kivazi hiki ni kwamba hakichagui wapi pa kuvaa, unaweza kuvaa kanisani, ofisini na hata katika mitoko mbalimbali.

 

Hemed phd ni mmoja wa wasnii wa bongo fleva, yeye amekuwa mstari wa mbela kabisa katika mavazi ya kitenge, hata katika nyimbo yake mpya amuamua kutoka na kitenge, sio lazima ushone shati tu , hata suruali pia, lakini hata ukivaa full bado unaonekana maridadi.

Diamond Platinumz hivi juzi alituwakilisha vyema kama huku nchi za ulaya alipoenda kuchukua tuzo yake, lakini hakusita kuvaa kivazi cha kitenge ambacho kilimtoa vizuri kabisa, alafu chini akatupia raba kali kabisa.

Mabeste, akiwa ametoka vizuri kabisa na kivazi cha kitenge , aina ya makenzi.vitenge hivi vinapendwa sana hasa kwa wanaume wakivaa mashati

Quick rocka , nae aliamua kutupia kivazi cha kitenge murua kabisa na suruali yake nyeusi .Raha ya kitenge kinakufanya unaonekana maridadi kabisa na umaweza kuvaa sehemu yoyote.

Fahad Fuad ni moja ya wanamitindo maarufu na video model anaefanya vizuri Tanzania akiwa ametupia kivazi chake  cha shati kilichochanganya na  kitenge maridadi kabisa.

Kitu kingine kinachovutia kwenye kitenge ni kwamba sio lazima uvae kitenge chote, msanii Ben Pol aliamua ku-design shati lake akaweka nakshi za kitenge mikononi na baadhi tu ya sehemu na bado aalionekana maridadi kabisa.