Hatimaye Lady Jay Dee Aonekana Kwenye Msiba Wa Ruge

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee ameonekana kwa Mara ya kwanza kwenye msiba wa Ruge Mutahaba.

Kwa miaka mingi imekuwa jambo la wazi kuw Lady Jay Dee na Ruge hawaivi katika changu kimoja Lakini wengi walitegemea jambo hilo lingebadilika mara Baada ya Ruge kufariki.

Siku nne za mwanzo za msiba wa Ruge Lady JD hakuonekana kabisa katika msiba wala hakutoa pole Kupitia Mitandao ya kijamii jambo lililosababisha mashabiki kumjia juu.

Lakini Lady Jay Dee ameonesha kuwa amesahahu yote kwani siku ya jana ameonekana akiwa mkoani Bukoba akishiriki kumzika Ruge Mutahaba ambaye anazikwa mkoani Kagera.

Lady Jay ameonekana kwenye picha ya pamoja na msanii mwenzake wa Bongo fleva Mwana FA.

Lady Jay Dee Azua Gumzo Kipindi Hiki cha Msiba wa Ruge.

Baada ya watu kuhoji sana katika mitandao ya kijamii kwanini   mwanadada Lady Jay Dee ameshindwa kufika katika msiba wa mkurugenzi wa Clouds Media baada ya msiba huo kutokea zaidi ya wiki sasa na kila mtu akiwa na masikitiko na kifo icho.

Hata hivyo baada ya kusemwa sana katika mitandao ya kijamii na watu mbalimbali, mwanadada huyo alionekana kama kuwajibu baadhi ya wanaomsema kwa kusema kuwa hajali kitu kuhusu swala hilo wala maneno yao .Na hivyo aliweka picha yake na kusema

Ikumbukwe kuwa mwanadada Lady jay dee aliwahi kusema kuwa hatokaa kukanyaga katika msiba wa Ruge au Joseph Kusaga na wao wafanye hivyo kwa sababu anaamini kuwa Ruge ndio alikuwa moja ya watu waliokuwa wakiziba sana mianya ya kazi zake kufanya vizuri nje ya nchi.

Hata baada ya kusema hayo miaka mingi iliyopita na hata kusemwa kuwa nyimbo za mwanadada huyo hazikuwa zikipigwa katika Clouds media , bifu hilo liliendelea na hata mkurugeniz huyo amekufa mwanadada huyo hakutokea msibani.

Lady JD Amwaga Povu zito Baada Ya Kukosolewa Kwa Kuvaa Uchi

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama a Lady Jay are amewajia juu watu ambao wamemsema Baada ya picha ya gauni la wazi kusambaa.

Siku ya juzi Lady Jay Dee alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya picha yake iliyomuonyesha akiwa amevaa gauni jeusi lililoacha sehemu kubwa ya maungo yake nje.

Mashabiki walimjia juu Jay D kwa kuvaa nguo iliyomuacha wazi huku wengi wakidai wamechukizwa kwa sababu ni msanii na pia ni Koop cha jamii.

Baada ya Povu hilo Jay Dee ametoa majibu kwa watu hao na kusema wengi wao ni wanafiki kwani hata akivaa mavazi ya heshima huwa hawampongezi pia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lady Jay Dee ameandika maneno haya:

Hivi wale watu wa maadili Mbona picha za Hivi huwa hamlike wala hamcomment kwa wingi mkiwekewa?

Haya maadili hayo hapo sasa inakuwaje? Mbona hamsifii, ila binadamu ni wanafiki sana sijapata kuona”.

 

Gadner Afungukia Tetesi Za Kurudiana na Lady Jay D

Mtangazaji wa Clouds Fm Gadner G Habash amefungukia tetesi zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na aliyekuwa mke wake  Lady Jay Dee.

Siku chache zilizopita Gadner aliposti picha ya kitambo kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mwanamuziki huyo nchini Kenya kwenye sherehe za utoaji wa Tuzo za Kisima. Katika tuzo hizo za miaka hiyo, Jide alitwaa Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike wa Afrika Mashariki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Gardner alisema kuwa anashangaa kwa nini watu waliona ni kitu cha ajabu kwa sababu ni ukweli ulio wazi kwamba hajawahi kuacha kumkumbuka wala hajawahi kumsahau mtalaka wake huyo.

Labda niseme wazi kwamba mimi sijawahi sijawahi kumsahau Lady Jaydee, ndiyo maana mtu akiniambia nimemkumbuka, nashangaa kwa sababu mtu unayemkumbuka ni yule uliyemsahau. Lakini kwangu yeye (Jide) sijamsahau hata kidogo, yupo tu siku zote kwenye akili yangu”.

Gadner alipoulizwa kama kuposti picha huko kunaashiria dalili za kurudiana na kurejesha ndoa yao upya, Gardner alicheka mno na kusema alifurahishwa na jambo hilo, lakini kwa sasa angeomba liachwe hivyohivyo.

Hilo la kurudiana? Kwa kweli naomba tuliache kwanza, tuliache hivyohivyo tu”.

Gardner na Jide walifunga ndoa Mei 14, 2005, lakini hawakubarikiwa kupata mtoto. Baada ya mvutano wa muda mrefu, wawili hao walifikia hatua ya kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo ya Manzese jijini Dar na mahakama kuamua kuvunja rasmi ndoa yao ya Kikristo na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka Agosti, 2014.

Lady JD Kuwapa Shavu Wabunifu Wa Mavazi na Mitindo

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady jay Dee ametoa fursa kwa wabunifu wa mavazi na wanamitindo atakaowatumia kwenye video ya wimbo wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lady Jay Dee ametangaza kuanza kuchukua maombi ya watu ambao atawatumia kwenye kazi yake:

Nita shoot video yangu ya kwanza kwa mwaka 2019 nchini Afrika ya Kusini siku ya Alhamis 10th January 2019. Nakaribisha Stylists wapya wa nguo, Jewelry, Viatu n.k kwa siku ya leo na kesho tu,”

Lakini ni pia Jay Dee ameweka wazi masharti ya watu atakaoweza kufanya nao kazi:

Unaweza kuniandikia email na kutuma picha ya vitu unavyotaka vionekane, au kutuma kwa WhatsApp kwenye number iliyopo kwenye profile yangu. Zingatia uafrika zaidi katika designs utakazotuma na u modern kidogo ukiwemo sio mbaya“.

https://www.instagram.com/p/BsXjejBB2tS/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=15912avzwe84t

Baada ya Kumpoteza Mama, Jay dee Afungua Kituo cha Matibabu ya Cancer

Mwanadada Lady Jay dee amefanikiwa kufungua kituo kwa ajili ya matibabu ya cancer ikiwa kama njia mpja wapo ya kuwasaidia watu wenye matatizo hayo kwa sababu amekuwa akijua shida na mapito wanayopitia wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wa ugonjwa huo.

Ikumbukwe kuwa mwaka huu huu msanii mwanadada huyo aIipoteza mama mzazi kutokana na matatizo ya ugonjwa huu wa cancer na kumpa uchungu mkubwa wa kutaka kufanikisha kusaidia wenye matatizo ya ugonjwa huu.

Lady jay dee anasema kuwa wazo  hilo limekuja baada ya mwanadada huyo kuangaika sana na ugonjwa wa mama yake kwa muda mrefu huku akishuhudia maumivu aliyokuwa akiyapata mama yake mzazi mpaka anapatwa na umauti.

Lady Jay Dee alisema “yesterday i openned a ward under my name at  Texas cancer center in Nairobi Kenya, This made me cry.kuuguliwa na mama yako  na kumuuguza na kumuangalia mpaka anakufa sio swala la mchezo, sijui nitacha lini kulia, nikisikia neno cancer tu  ninalia hadi asi na pia nikikumbuka tena naanza kulia hata masaa matatu  mfululizo ,…ila Mungu ataponya maumivu …yasikie kwa jirani wala usiombe yakakukuta.”

 

Lady JD Afungukia Tetesi Za Kuachana na Mpenzi Wake

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva mrembo Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake msanii kutoka nchini Nigeria Spicy hawajaachana.

Tetesi za wawili hao kuachana ziliznza baada ya kutoonekana pamoja kwa muda mrefu lakini pia hata mitandao ya kijamii hawakuonekana wakiposti mapicha picha ya mahaba kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Kwenye mahojiano na kituo cha habari cha East Africa, Lady Jaydee amesema kwamba hajaachana na Spice, isipokuwa wawili hao wanafanya kazi ambayo inawalazimu kuwa mbali mbali kwa muda mrefu, ikichangiwa na kuwa raia wa nchi mbili tofauti.

Unajua sisi ni wanamuziki, na wanamuziki ni watu wa kusafiri, na hatuishi nchi moja, kwa hiyo yeye yuko kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu, ni sawa na mume na mke, mume anaenda kazini na mke anaenda kazini kwake, haimaanishi kila siku muwe mnafuatana, leo hayuko hapa lakini ni mtu ambaye nashirikiana naye kwenye mambo mengi, kama kunisaidia kumpata UTI na kuhakikisha amefika hapa Tanzania”.

Lakini pia Jaydee ameendelea kwa kusema kwamba licha ya Spicy kuwa mbali, amechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha tamasha la #VocalsNight2018, kwa kuweza kumuunganisha na msanii UTI ambaye  alikuwa MC wa siku ile.

Lady JD Ataja Kitu Kinachoua Muziki Wa Bongo Fleva

Msanii Mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kuweka wazi kitu ambacho kimekuwa kikiua muziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha habari, Lady Jay Dee ameitaja mitandao ya kijamii kama kitu kinachoua muziki wa Bongo fleva kulinganisha na miaka ya nyuma Wakati mitandao haikuwepo:

Kitu kimoja ambacho nimeangalia ambacho kinaharibu tasnia ni kufikiri kwamba kuangaliwa YouTube ndio kufanya vizuri kwenye kiwanda cha sanaa, YouTube sio kipimbo cha wimbo kuwa mzuri au kufanikiwa.

kwa sababu kuna vitu vingi sana mtandaoni, kuna mtu anaweza kuwa anaenda kuangalia ni nini”.

Kwa sasa Lady Jaydee yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya show yake ya Vocals Night itakayofanyika October 28, 2018 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

 

Tamasha la Jide Kuwashusha Nyumbani Wasanii Wakubwa Afrika.

Mwanadada Lady Jay Dee ameamua kukamilisha kile alichokuwa amekihaidi kwa muda mrefu baada ya mashabiki wake kusubiri kwa muda mrefu sana tamasha hilo lililoanza kutangazwa muda mrefu nyuma.

Lady Jay Dee ambae aliwahi kusema kuwa kuna kitu kinakuja kati yake na Juliana kanyomozi kutoka Uganda, basi kitu icho kinaenda kukamilika kutokana na tamasha la Vocal nights kufanyika October 26 mwaka huu na kuleta wasanii wengi.

Akizungumza na Show biz , Lady Jay Dee anasema kuwa tamsha hilo litawaleta wasanii wengi akiwemo Zahara kutoka Afrika ya kusini na pia Juliana kanyomozi kutoka uganda.

Jay De anasema”nina lengo la kulifanya onyesho hilo kuwa kubwa na la kila mwaka, na lengo kubwa ni kuwakomboa wale wanawake ambao wamekuwa wakilazimishwa kuuza utu wao ili kufanikiwa katika kazi zao.kama unavyojua kuwa wanaume wameshika karibia kila sehemu ya hii sanaa. “

Jay dee anasema kuwa wasanii wengi wa kike wana vipaji lakini hawasikiki kwa sababu hiyo anasema kuwa tamasha hil litakuwa kama daraja kwa baadhi yao huku akimtolea mfano Grace Matata.

Kama mtu anakuwa hayuko tayari kutoa rushwa ya ngono basi hawezi kufanikiwa kwaio mimi nataka kuwa darala kwao, ndo maana nimeamua kumchukua Grace matata maana anafanya kazi nzuri lakini hasikiki.

Mbali na wasanii hao pia atakuwa aliyewahi kuwa mshiriki wa big brother miaka iliyopia UTI NWACHUKU ambae atakuja kwa ajili ya kunogesha tamasha hilo.

Uti pia ni msanii kule kwao kwaio nimemleta pia ili kuchanganya radha ya tamasha,ninategemea kupata sapoti kubwa kutoa kwa mashabiki ambao kila mara wamekuwa na mimi kwa kila jambo.

 

Jay Dee Asema Alitaka Kunywa Sumu Kutokana na Anayoyapitia.

Mwanadada Lady Jay Dee amefunguka na kuweka post katika akaunt yake na kusema kuwa siku kadhaa nyuma zilizopita alitaka kunywa sumu  kutokana na yake anayoyapitia lakini alikuja kuwaza vitu vingi na kujiona kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa alishayapitia mengi kabla ya haya.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Jay Dee aliandika “jana nilitaka kunywa sumuila kabla sijafanya nikajisuta na kukumbuka  kuwa nitakuwa mjinga kiasi gani , nikajisikitika na kisha nikaacha na hadi leo nipo kigumu gumu  ila bado nipo.

 

Mwanadada huyo ni moja kati ya wasanii wa kike wanaoangaliwa sana historia zao za maisha kutokana na kuwa muhamasidhaji bora wa watu wnegine hasa katika muziki.kuna mengi watu wanapitia na hata yeye yapo mngi aliyopitia pengine yalitaka kumkatisha tamaa.

Lady Jay dee , Juliana Kanyomozi Kuwafikia Mashabiki October 2018

Mwanadada  mwenye heshima zake katika sanaa ya bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady jay dee ametangaza ujio wake mpya na msanii mwingine mkongwe kabisa na mataalamu wa muziki kutoka Uganda mwanadada Juliana Kanyomozi mwaka huu .

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Lady jay dee aliweka picha yake na mwanadada Juliana na kuandika maneno yanayoashiria kuwa kuna kitu wanataka kufanya na kuweka verification ya muda kuwa itakuwa ni mwaka 2018 October.

Lady jay dee  na Juliana wanaweza kusemwa kuwa na historia moja ya muziki ingawa kila mmoja ana nafasi yake katika nchi yake , hii ni kutokana na ukubwa wao katika muziki lakini pia wamekuwa wasanii wa  muda mrefu na wamekuwa wasaidizi na mfano kwa kuigwa wa wasanii wachanga wanaoingia katika game la muziki.

Hata hivyo chochote wanacghotaka kufanya wasanii hawa kinaaminika kuwa na manfaa kwa nchi zote mbili na kwa muziki wa nchi zote lakini kubwa zaidi ni burudani nzuri kwa mashabiki.

Lady Jay Dee Akiri Kuwakubali Ben Pol na Vannesa Mdee.

Msanii wa kizazi kipya wa muda mrefu katika game amefunguka na kuonyesha hisia zake za kuwakubali wasanii Ben pol na Vanesa mdee katika game la muziki bila kigezo cha muda wao katika game lakini kwa kuangalia ufanyaji wao wa kazi unavyokwenda.

Sio swala rahisii sana kumuona msanii Lady Jay Dee akisema hadharani na moja kwa moja kuwa anawakubali wasanii flani lakini nadhani pale anapoongea anakuwa amemaanisha , hii inawezekana kabisa ni kutokana na ukubwa wake katika muziki na jinsi alivyouzoea muziki hivyo napomuona msanii na kumsifia basi ni kweli msanii huyo yuko sahihi.

katika ukurasa wake wa twitter, lady jay dee aliandika “Ben pol na Vannesa Mdee mapenzi yao yako real. na mapenzi yangu kwao hayana kikomo, hivyo tu yaan wadogo zangu.”

Hii inaweza kuthibitika zaidi ambapo wikiendi iliypita Vannesa alikuwa na show jijini ambapo Lady jay dee hakusita kwenda kumsapoti mdogo wake huyo.

Lady Jay Dee na Gadner Uso Kwe Uso Msibani

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amekutana uso kwa Uso na aliyekuwa mume wake mtangazaji Gardner G Habash katika msiba wa mke wa Kibonde siku ya jana.

Lady Jay Dee na Gadner walikuwa wanandoa kwa miaka kama kumi kabla ya kuachana na kupeana miaka michache iliyopita kwa sababu zisizojulikana kwa watu wengi.

Lakini baada ya wawili hao kuachana kulitokea bonge la bifu baina yao hadi kufikia hatua ya Gadner kumwagia Matusi Lady JD hali iliyopelekea kupelekana mahakamani.

Lakini baada ya talaka kutoka Lady jay Dee alitangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hana bifu kabisa na Gardner na kuomba kila mtu aendelee na maisha yake.

Siku ya jana wawili hao walikutana Uso kwa Uso huku Lady JD akiwa na mpenzi wake mpya Spicy Muziki Wote wawili walipeana mikono na kisha kumfariji mfiwa.

Lady Jay Dee Afunguka Mahusiano Yake ya Spicy.

Mwana dada Lady Jay Dee amefunguka na kuelezea kwanini kwa muda mrefu sasa hajakuwa akimpost mwanaume wake anaejulikana kwa jina la Spicy ambae ndio mwanaume wake kwa sasa.Lady jay dee anasema kuwa pamoja na kwamba wao ni wapenzi  lakini mara ya kwanza alikuwa akifanya hivyo kwa sababu walikuwa kaika promotion ya wimbo wao wa together remix na ndio maana walitakiwa kufanya hivyo.

Watu wasisahau kuwa mimi ni lady jy dee, na ile oage ni ya lady jay de sio ya spicy ,kwaio kuna baadhi ya mambo yaabaki kuwa private , kama kuna ulazima wa kuwekwa katika page yangu basi nitamweka na atapostiwa.

ila sipendi sana mambo yangu na page yangu ijae picha ya mtu mwingine,na watu wasipomuona tu huyo mtu katika ukurasa wako wanaanza kuuliza ooh , yuko wapi mtu flani, maisha yangu kama lady jay dee yatabaki kuw hivyo na maisha yang ya mapezni na mahusiano yatabaki kuwa yalivyo.

 

Sina Mpango wa Kuolewa-Lady JD

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kusema watu wasitarajie kuona ndoa yake hivi karibuni maana hana mpango wa kuolewa.

Lady JD alifunguka hayo alipokuwa anamuongelea mpenzi wake msanii kutoka Nigeria anayejulikana kama Spicy Music, baada ya kutomposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram tangu Tarehe 4 April.

Lady JD ameweka wazi kuwa yeye na Spicy Music hawajaachana kisa tu hamposti Kwenye page yake ya Instagram bali hajaona sababu ya kumuweka humo kwani kipindi anamposti sana ilikuwa ni kwa sababu ya kazi ya wimbo wao pamoja.

Lakini Kwenye mahojiano yake na Bongo 5 Lady Jay Dee ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba yupo Kwenye Mahusiano lakini watu wasitegemee kumuona anaolewa anytime soon:

Watu wasitarajie kuona ndoa yangu anytime soon wasisahau kuwa sio kwamba mimi sijawahi kuolewa, au kuwa nataka sana kuolewa. Kuolewa ni jambo la kujipanga na kwa sasa siko tayari kuolewa na mtu yoyote naweza kuwa na Mahusiano na mtu lakini siko tayari kwa ndoa! Sio sasa”.

 

Tanzia: Mama Mzazi Wa Lady Jay Dee Afariki Dunia

Mama mzazi wa staa mkongwe wa Bongo fleva Judith Mbibo maarufu kama Lady Jay Dee anayejulikana kama Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya  Alhamisi Aprili 26, 2018.

Taarifa hizo zimetolewa na Kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, ambaye amethibitisha na amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu.

April 01, 2018 Lady Jaydee alizungumza kuhusu kuugua kwa mama yake mzazi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika;

Nauguza mama mzazi lakini naendelea kupambana na maisha vilevile, usinione naimba au natabasamu ukafikiri nina raha sana.

Sina raha wala nini, lakini pia lazima nifanye kazi ili niweze kuishi, bila kuangalia kama watu watani judge vipi!, Kwani bado naamini Mungu atamponya na kumnyanyua kwenye kitanda alicholala kwa zaidi ya miezi 2, Kwani Mungu pekee ndio anaeweza.

Bi. Mbibo alianza kuugua tangu mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo alipatiwa matibabu hapa nchini na nje ya nchini (India).