“Mashabiki Zangu Hawahitaji Kumjua Mpenzi Wangu”-Lavalava

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri chini ya Label ya WCB, Abdul maarufu kama Lavalava amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kumuanika Mpenzi wake  hadharani.

Tofauti na wasanii wenzake wa WCB, Lavalava pekeee Ndiye ambaye amekuwa akimficha Mpenzi Wake na haijawahi kujulikana ana mahusiano na mwanamke gani tangu alipopata umaarufu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lavalava ameweka wazi kuwa haoni ulazima wa yeye kumuonesha mchumba wake kwasababu sio malengo yake na itaharibu kabisa mfumo wa muziki wake kwasababu watu watavumisha sana.

Nadhani sio lazima sana watu kujua uhusiano wangu kwasababu hayo ni mambo yangu binafsi jamani yaani kama ningekuwa sijatoa ngoma kwa muda mrefu basi ingekuwa ni haki y a o kuhoji lakini u h u s i a n o wangu hauwah u s u kwasab a b u malengo yangu ni kufanya muziki wangu ujulikane zaidi kuliko mahusiano yangu”.

 

Lavalava Afunguka Kushikwa Sehemu za Siri

Msanii kutoka kundi la WCB amefunguk juuu ya video iliyosamba sana mitandaoni wiki iliyopitaikimuonyesha akiwa jukwaani na baadhi ya mashabiki wake wa kike wakimshika na kumingizia mikono katika sehemu zake za siri.

Msanii huyo anasma kuwa hajaona jambo geni kufanyiwa hivyo huku akitoa mfano wa msanii mwenzae kutoka nigeria davido aliwahi kufanyiwa hivyo na hakukuwa na jambo baya lolote.

sijaona jambo geni kwa kufanyiwa hivyo mbona hata wakina davido walifanyiwa vitu kma hivyo, kitu kilichonisikitisha sana ni kuwa kuna moja kati ya wale wasichana ameachwa na boyfriend wake , ni jambo limeacha historia  kwa nchi ya kenya lakini ile imeonyesha jinsi gani tumepokelewa vizuri.

Kwa sasa msanii huyo anafanya vizuri na kibao chake cha niuwe.

 

Lavalava Azimia Jukwaani , ni Baada ya Kupigwa Busu na Shabiki.

Kuna video inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimunyesha msanii kutoka WCB, Lavalva akiwa jukwaani ana-perform na mara akapigwa busu na moja ya mashabiki zake wa kike aliyepanda jukwaani hapa na ghafla msanii huyo kudondoka na kuzimia.

Msanii huyo ambae baada ya kuzimia ilibidi kupatiwa huduma ya kwanza na kisha kusomewa dua na ndipo alipoamka  , haiafahamika kama swala hilo amelifanya kwa kiki au ilikuwa kweli alikuwa katika hali hiyo.

Hata hivyo hakuna kiongozi yoyote katika kundi hilo alielisemea hilo wala yeye mwenyewe kuhushu tukio hilo ambalo liliwashangaza wengi na kuwafanya mashabiki waanze kuimba kwa nguvu kuwa msanii huyo amekufa.

Kisa Cha LavaLava Kuimba ‘Tuachane’ Hiki Hapa

Msanii aneafanya vizuri kimuziki kutoka katika kundi la wasanii wenye vipaji nchini  Wcb-Wasafi ambae ngoma yake ya kwanza kumtambulisha ilikuwa ni ile ya Tuachane ameelezea kiundani sababu ya yeye kuimba wimbo huo .Lavalava ambae anasema kuwa wimbo huo ni moja ya vitu vilivyomtokea katika maisha hivyo aliimba wimbo huo akiwa na hisia za maumivu kutokana na kile kilichomkuta siku za karibuni kabla ya kutoawimbo huo.

Lavalava ambae anasema kuwa alikuwa akiishi nyumba moja na mwanamke ambae yeye alikuwa akimchukulia kama wa kwake kumbe alikuwa na mwanaume mwingine na hata ile nyumba waliokuwa wanakaa ambayo alihisi kuwa analipa mwanamke huyo  kumbe  alikuwa akilipiwa  na mwanaume mwenzie.

Mwezi mmoja kabla sijaachia ngoma ya tuachane nilikuwa na mpenzi wangu ambae tulikuwa  tumepanga na tunakaa pamoja, tulikuwa tumepanga mipango mingi ya maisha kwamba kuan siku nitafika tutafanikiwa  na nitaweza kumuhudumia , afu na yeye akawa ananihitikia tu fresh,kumbe bhana hata pale tulipokuwa tunakaaa kuna mwana alikuwa amempangishia.-Alifunguka mwanamuziki huyo kutoka kundi la Wasafi

Na mimi nikawa ninakaa hapo najiachia, mchizi siku hiyo akarudi akanikuta yaani nilihisi kama nataka kufa  kufa hivi, akaniambia mi ndo baba mwenye nyumba nimerudi hapa kwangu.-Aliendelea kusema Lavalava.

Akiendelea kuongea na Radio Free Lavalava nasema kuwa baada ya hapoa aliwaacha wakaendelea kubembelezana yeye akaamua kondoka ndipo  alipoamua kwenda kutoa wimbo wa Tuachane.

Vijana wengi wa kiume wamekuwa wakikaa na wapenzi wao  wa kike bila kujua kuwa  mwanamke anaeishi nae anakuwa yupo na mahusiano na mwanaume mwingine na hata matunzo anayopata yanatoka kwa mwanaume mwingine, kwa upande wa vijana ambao wengi wanapenda kulelewa  wamekuwa wakiumizwa sana na mambo kama hayo ingawa kwa Lavalava anasema kuwa yeye aliamini kuwa ni mwanamke atakae panga nae maisha kwa ajili ya baadae.

kwa vijana wengi , inabidi ifike sehemu watu waingie katika mahusiano huku akiwa ameshafanya uchunguzi na kumjua vyema mtua aneingia nae katika mahusiano.