Linah Awajia Juu Wanaomponda Mtoto Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga ameibuka na kuwajia  juu watu ambao wamekuwa wakimponda binti yake.

Siku chache zilizopita Linah alituhumiwa kwa kuedit  picha za mtoto Wake Paris Tracey mwenye umri wa mwaka mmoja kiasi cha kubadilisha rangi yake na kuwa mweupe kabisa.

Linah ambaye ni mama wa mtoto huyo mmoja, amefunguka ikiwa ni siku chache baada ya picha ya mwanawe kusambaa mitandaoni ikimwonyesha akiwa tofauti na jinsi mama yake anavyomuweka.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba Jumatano, Linah, alisema amekua akitumia uhuru binafsi kuishi na mtoto wake hivyo hapendi jinsi watu wanavyomtuhumu na kutaka kumpangia maisha ya mwanawe.

Ifike mahali kila mtu afanye yale maisha anayoona yanamfaa, mambo ya kupangiana maisha si sawa kwa kizazi hiki, kuna watu wanalalamika na mposti mwanangu tofauti na alivyo wajue nafanya hivi kwa mapenzi yangu na si yao”.

Linah amekua akimwonyesha mwanawe lakini watu wengi wamedai mwanadada huyo amekua akimbadilisha zaidi mtoto huyo rangi ya mwili wake na kuonekana mweupe tofauti na alivyo.

“Sina Habari na Mambo Ya Ndoa”- Linah Sanga

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa.

Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Linah alisema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake.

Mimi ukiniuliza mambo ya ndoa kwa sasa ni ngumu kueleza.. niulize muziki wangu unakwendaje au kuhusu mwanangu”.

Linah amezaa Mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

Nai Atoa Jibu Hili Baada Ya Tuhuma Za Kuazima Nguo Kwa Linah

Video vixen maarufu na Mpenzi wa Msanii wa Bongo fleva Centro Zone Nai au maarufu kama Nai Official amefungukia tuhuma za kumuanika nguo Msanii mwingine wa Bongo fleva Linah Sanga.

Nai amewatolea povu zito mashabiki walioanzisha taarifa hizo za uongo na  kuwataka wafunge midomo yao kwani hawajui wanachokiongelea kwani yeye sio mtu wa kuazima nguo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nai alisema hawezi kuazima nguo kwa mtu yeyote kwani ni bora arudie nguo lakini siyo kuazima, kilichotokea kwake na Linah ni kwamba nguo zimefanana ila kila mtu amenunua kwa wakati wake na ndiyo maana alifanya utani kumshukuru Linah mtandaoni kwa kumpa gauni kwa sababu yamefanana ila watu wakadhani ni kweli amemuazima.

Hizo ni dharau sasa ina maana ndiyo nimefulia kiasi hicho mpaka nishindwe kununua gauni? Nilijua tu watu wataongea ndiyo maana nikafanya makusudi kumshukuru Linah kama amenipa ila nilifanya utani kwa sababu magauni yamefanana, yeye lake alivaa kwenye shoo Iringa mimi nimevaa kwenye bethidei ya Wolper, sasa kama kiwanda kinatoa nguo moja watu wanataka tufanyeje”.

 

Linah Sanga Ataja Hadharani na Bwana Mpya

Msaniibwa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga anadaiwa kutoka hadharani na Mpenzi mpya marabaada ya kuachana na baba watoto wake Shaban Mchomvu.

Gazeti la Ijumaa Wikienda wanaripoti kuwa Linah alijiachia na jamaa huyo mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Iringa alipokuwa anashiriki kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Linah aliachana na baba mtoto wake miezi kadhaa iliyopita alionekana kwa mara ya kwanza na mwanaume mwingine ambapo mashuhuda  waliwashuhudia wakiwa wamegandana kama ruba kwenye kila kona mjini Iringa.

 

Baada ya Linah na kijana huyo kuonekana wakiwa na ukaribu usio wa kawaida Gazeti la Ijumaa lilimfuata na kumhoji kuhusu uhusiano wao ambapo mara moja alimwaga Povu zito:

Sitaki mambo ya umbeya, kwa hiyo nisiambatane au kukaa na mtu? Kwanza sioni cha ajabu kwa sababu sasa hivi nipo huru na mambo yangu, naweza kufanya chochote ninachojisikia na hakuna wa kuniwekea mipaka katika uhusiano wala kazi zangu, niacheni na mambo yangu tafadhali”.

Linah aliachana na mzazi mwenzake Shabani Mchomvu Baada ya kuzaa naye Mtoto mmoja mwenye mwaka mmoja anayeitwa Tracy Paris huku sababu za kuvunjika kwa Penzi Lao zikiwa hazijawekwa wazi.

“Ugomvi Wa Clouds na Wasafi Haunihusu Naangalia Pesa”-Linah

Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amefungukia tuhuma za kuonekana kuisaliti Clouds Media Baada ya kuonekana akiwa na Wasafi Festival ambapo amekuwa akipiga shoo mbali mbali.

Linah Sanga alianzia safari yake ya kimuziki katika Nyumba ya vipaji Tanzania (Tanzania House of Talents) na kupatia mafanikio makubwa lakini msanii huyo hajaonekana upande huo kwa muda mrefu.

Baada ya kuonekana zaidi na Wasafi Festival Linah ameibuka na kujitetea kuwa yeye hajamind ugomvi uliopo kati ya Wasafi na Clouds yeye yupo kikazi zaidi yeye Kama Msanii anaangalia maslahi yake huku mabifu yao yakiwa hayamuhusu.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Linah Sanga alifunguka haya Kuhusu kuisaliti Clouds na kuhamia Wasafi:

Wakati nipo THT nilifundishwa kuwa mimi ni mfanyabiashara na Mimi ni brand hivyo siangalii nafanya wapi kazi as long as naingiza mkwanja halafu isitoshe hayo maugomvi mimi hayanihusu mimi naangalia pesa ambayo naingiza katika kazi ninayopewa”.

Linah Sanga pia alifungukia picha zake zilizosambaa kwenye mtandao wa kijamii zilizomuonyesha akiwa amevaa vinguo vifupi na kuonekana na Neil I mkubwa tofauti na anavyojiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo amesisitiza picha zile zimetoka vile kutokana na kwamba zilipigwa alipokuwa anatembea.

Linah Sanga agoma Kuolewa Sasa Hivi , Anataka Kula Bata Kwanza

Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa kwa sasa wala haitamani kabisa ndoa kwa sasa anataka kufanya mambo mengine kwanza na kupumzika sana.

linah anayasema kayo ikiwa ni miezi kadhaa tu imepita tanfu alipoweka hadharani kuwa ameachana na baba wa mtoto wake ambae pia alikuwa ni meneja wake kwenye kazi zake.

naatamani sana kupata mwanaume mwenye mapenzi, matunzo na mwenye kujali sana, sitamani hata kuolew akwa sasa nataka nichill tu kwanza

Ikumbukwe kuwa linaha aliwahi kuwa katika mahusiano ambayo alitangaza kuwa yeye na mwanaume huo watafunga ndoa pamoja na kwamba walikuwa na dini tofauti kwa sababu ni baba wa mtoto wake ., lakini ghafal alikuja na kutangaza kuwa hawapo pamoja tena.

Linah Sanga Azidi Kukwepa Tetesi Za Kumwagwa na Baba Watoto Wake

Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Linah Sanga amezidi kukwepa tetesi za kuwa ameachana na Mpenzi na mwanaume aliyezaa naye Mtoto Wake wa kwanza Shaban Mchomvu.

Kwa miezi kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa Linah na baba watoto wake wameachana Baada ya Shabani kuchoshwa na maisha ya kimuziki anayoishi Linah ikiwemo mavazi ya ajabu.

Lakini Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi Enews cha EATV,  Baada ya kuulizwa kuhusu taarifa hizo Linah amekuja juu na kuwataka watu wafatilie muziki Wake na sio maisha yake binafsi.

Sidhani kama mashabiki zangu wanatakiwa kufahamu kuhusu maisha yangu binafsi, wanachopaswa kukifahamu ni muziki wangu tu kwaiyo siwezi kuzungumzia hilo”.

Linah ametangaza kutoa wimbo wake mpya hivi karibuni na kuwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani video ya wimbo huo imeshakwisha kamilika.

 

Penzi la Linah na Baba Watoto Wake Ladaiwa Kuvunjika

Penzi la staa wa Bongo fleva Linah Sanga na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja anayejulikana kama Mchomvu linadaiwa kuvunjika pamoja na kuwa katika tarartibu za ndoa.

Global Publishers wanaripoti kuwa Penzi la wawili hao limeota  mbawa wakati wakiwa kwenye taratibu za kufunga ndoa.

Linah na mzazi mwenzake walianza kuingia kwenye mgogoro baada ya mwanadada huyo kujifungua mtoto wake huyo. Ilisemekana kwamba, mara kadhaa wamekuwa wakikalishwa chini na kuyamaliza mambo yao kichinichini bila mtu yeyote kujua kisha wanaendelea na uhusiano kama kawaida.

lakini inadaiwa kuwa ugomvi wa wawili hao mara nyingi ulikuwa ni wivu wa kimapenzi hivyo hicho ndicho kilichosababisha uchumba wao huo kuvunjika ambapo mpaka sasa kila mmoja anamuona mwenzake mchungu.

Hakuna cha zaidi kilichovunja uchumba ni wivu tu ndiyo ulikuwa ukiwatafuna wote wawili mpaka kufikia hatua ya kuvunjika kwa penzi lao”.

Baada ya taarifa hizo gazeti hilo lilimsaka Linah na kumuhoji kuhusu taarifa hizo ambapo alifunguka na kukiri kuwa hayupo na mpenzi wake:

Hivi kwani ukizaa na mtu mpaka muoane? Ndio hivyo Lakini Sitaki kuongea zaidi kuhusu iyo ishu”.

 

Kuongezeka kwa Mwili Wangu Hakujaathiri Chochote katikaKazi Zangu :-Linah Sanga

Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa swala la kuongezeka kwa mwili wake baada ya yeye kujifungua hakuathiri kazi zake kwa sababu anaweza kufanya kitu chochote jukwaani kuwafurahisha mashabiki wake,

Hii inakuja baada ya moja ya picha yake ya wikiendi hii kusambaaa sana katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha akiwa kama amenenepa sana na kuwa anaweza kushindwa kufanya show nzuri kama zamani,

Akiongea na mtandao wa Clouds fm Linah anasema “mazoezi nayafanya ya kawaida tu, naupenda sana mwili wangu.mimi naona kawaida tu na kuongezeka kwa miwli wangu hakujaathiri chochote katika kazi zangu, napiga show jukwaani na najona mwepesi tu.unajua kuna watu ni wembamba lakin wazito lakini mimi unene wangu haujanipa changamoto yoyote.ninapokuwa jukwaani nawaburudisha mashabiki wangu kama kawaida, lakini ujue pia kuwa mimi sio dansa  naimba nitakavyo sio lazima nianze kuruka ruka,’

Linah Afungukia Mipango Yake Ya Watoto Watatu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuelezea mipango yake ya kuongeza watoto wengine siku za mbeleni.

Linah ambaye tayari ni mama wa mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja amesema anataka kuongeza watoto wawili ili kuwa na watoto watatu hapo baadae.

Kwenye mahojiano na  Risasi Jumamosi, Linah alisema kuwa, atazaa watoto watatu kwani ndiyo anaotamani kuwa nao na kwamba baada ya mtoto wake aitwaye Paris kufikisha miaka miwili ‘atafyatua’ mwingine.

Maisha bila watoto ni magumu, pamoja na kazi yangu ya muziki ninahitaji kuwa mama bora, hivyo nitazaa kama wanawake wengine,” alisema Linah ambaye ameomba mashabiki wake wapokee vema nyimbo yake kwani si ya kuikosa“.

Linah ambaye ameachia wimbo wake wa ‘Nikoleze’ juzi kati na kuachia picha matata mtandaoni iliyowatoa udenda baadhi ya wanaume wakware, alieleza kuwa anapenda sana watoto hivyo mmoja hatoshi.

“Wasanii Wa Kike Tunaombwa Sana Rushwa Ya Ngono”- Linah

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa janga kubwa kwa wasanii wa kike ni kuombwa sana rushwa ya ngono kila kona.

Linah alifunguka hayo baada ya kuulizwa ni sababu gani wasanii wengi wa kike wanashindwa kukaa sana Kwenye gemu na hata wengine kukata tamaa mapema sana.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Linah ameweka wazi kuwa rushwa ya ngono ni changamoto kubwa kwa mafanikio ya wasanii wa kike kwa sababu wanaume wanatumia nafasi hiyo kuwalaghai.

Mimi nafikiri rushwa ya ngono inatembea sana utaenda kwa Dj anataka ngono, utaenda kwa presenter anataka ngono mara utaenda kwa mdau na yeye anataka kwaiyo hiyo inaweza kukurudisha nyuma sometimes.

Wasanii wengi wa kike wanakata tamaa kwa sababu anaona listi ya watu wanaotaka ngono ni ndefu sasa unajikuta unawaza utatumika mara ngapi mpaka ufanikiwe?.

Na kama Kwenye Industry kama kati ya watoto wa kike watatu mmoja anafanya hayo mambo wengine hawawezi kupata nafasi”.

Kwa miaka mingi wasanii wa kike wamekuwa wakilalamika kuwepo kwa vikwazo kwa wao kuweza kufika mbali na kikwazo kikubwa ni rushwa ya ngono.

“Napenda Wanaume Weusi Nikiwaona Nasisimka”- Linah Sanga

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ndege Mnana Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutiwa zaidi na wanaume weusi kuliko wanaume  weupe.

Linah alizua gumzo Kwenye social media baada ya kuweka picha ya mpenzi wake na kuweka wazi kuwa anampenda mwanaume wake kwa sababu ni mweuzi sana.

Kwenye Interview na Millard Ayo, Linah amefunguka na kudai anapenda sana wanaume weusi kwani wana muonekano wa kiume zaidi kuliko wanaume weupe.

Mimi hulka yangu napenda wanaume weusi hata ukifatilia Maex wangu asilimia kubwa ni wanaume weusi Barakah The Prince alikuwa mweusi tii tena amezidi hadi baba watoto wangu na hata Amini naye ukimuangalia ni mweusi”.

Lakini pia Linah ameweka wazi kuwa havutiwi kabisa na wanaume weupe:

Sivutiwi kabisa na wanaume weupe yaani nikaona mwanaume mweusi nasisimka ananivutia kwani naona wamekaa kiume zaidi”.

 

Linah Akiri Kuvutiwa na Mastaa Wa Mbele

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Linah Sanga aka Ndege  Mnana amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutuwa sana na maisha ya mastaa wa mbele hasa Cardi B na Beyoncé.

Linah amesema anavutuwa sana na wasanii hao kwani ameona kuwa pamoja na kwamba wamepata watoto na kuwa wamama lakini wameendelea na maisha ya sanaa kama kawaida.

Beyoncé na Cardi B

Kwenye mahojiano na Kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Linah ambaye tayari ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris amesema kitu hicho kinaendelea kumpa morari ya kufanya Muziki.

Beyonce alijifungua mtoto mmoja na mara ya pili alijifungua watoto mapacha lakini bado akipanda kwenye jukwaa unaweza kusema amepanda mtu ambaye hana mtoto hata mmoja. Ukimwangalia tena Cardi B sasa ana ujauzito mkubwa tu ambao anakaribia kujifungua lakini ebu angalia perfomance yake na the way anavyokwenda.

Kinachonifurahisha ni kwamba hata ile dhana yetu kwamba ukianza tu kuwa na familia umeharibu kwa sababu huwezi kusema wewe ni mwanamuziki usizae, inabidi uwe na familiaa yako na uwe na mume wako lakini uwendelee na kazi yako”.

Wasanii wengi wa kike Tanzania wamekuwa wakikumbana na kasumba ya kutakiwa kuacha kufanya Muziki mara tu wanapozaa na wengine huachana na Muziki pale wanapoolewa.

Alichosema Linah Kuhusu Wasanii wa Kike.

Mwanadada Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa wasaii wa kike wa bongo hawapendi kusaidiana waa kushikana mikono pale inapotokea mmoja wao yuko chini au anahitaji kupata msaada na hii ndio sababu kubwa ya wao kutoendelea .

Linah aliongea hivyo huku akitoa sababu kubwa kuwa wasanii wa kike wamekuwa waoga wa kuzidiana na kwamba wanaona kama wakisaidiana mmoja wao hatamzidi mwingine hivyo hiyo ni roho ya uchoyo, chuki na wivu zinatawala na ndio maana wana fail.

Linah anasema kuwa wasanii wa kibongo wa kike ni wachache sana katika game waliofanikiwa ambao wameanza muziki kitambo lakini wamekuwa na roho za kutokuwavuta wanaoitaji msaada kwa kuoga kuzidiwa katika tasnia.

Wasanii wa Kike Inabidi Tubadilike:-Linah

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini amefunguka na kuwaambia wasanii wa kike kuwa ili kuendelea kimuziki inabdi wabadilike na kukubali changamoto ili kuweza kuendelea.

inaha anasema kuwa wasanii wengi wa kike wamekuwa na tabia ya kuogopa kuthubutu au kuwa na aibu ya kufanya kitu flani kwa kuhofia kuangaliwa wa jamii aua watu wanaomzunguka lakini ili kufanikiwa ni lazima kujitoa na kuji-brand ili kufanikiwa.

Akiongeana na Clouds e ya Clouds Tv, Linah anasema kuwa wasanii wengine wa kike wamekuwa wakitaka kukaa wao katika nafasi hizo, wamekuwa wanaoneana wivu  kwa kushindwa kuwavuta au kuwaachia na wasichane wengien kuwa pale walipo wao.

Linah anasema kuwa wasanii wa kike inabidi waige mfano wa wasanii wkaubwa wa kike kutoka nje , hakuna madaraja ya msanii mkubwa wa kike kuliko mwingine na hiyo yote ni kwa sababu wamekuwa wakisaidiana na  kuvutana kutoka chini.

Wivu wa Mume wa Linah Wamkosesha Mikataba ya Kazi

Mwanamuziki aliyekuwa anafanya kazi nchini Kenya, Mr. Kesho amefunguka na kudai kila wivu aliokuwa nao mume wa Linah ambaye pia ni meneja wake Shaban Mvhomvu unamkosesha mkataba wa kazi na Linah.

Mume wa Mwanamuziki wa Bongo fleva Linah Sanga ambaye pia ni mzazi mwenzake Shaban Mchovu maarufu kama Director Ghost amedaiwa kuwa na wivu sana kwa mkewe kiasi ya kwamba ameshindwa kupata kazi.

Mr. kesho amefunguka kuwa aliporudi kufanya nchini Tanzania alianza kusimamiwa na Adam Mchomvu ambaye pia alikuwa anamsimamia Linah lakini baada ya kutoa wimbo mmoja aliondoka kwenye label hiyo na inasemekana kabisa kuwa chanzo ni ukaribu wake na Linah.

Ukaribu wake na Linah ulisababisha habari kuenea kuwa anatoka kimapenzi na Linah jambo ambalo linasemekana halikumfurahisha meneja ambaye ni mpenzi wa Linah.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Mr. Kesho amefungukia tuhuma hizo za kuwa na Linah na ukaribu wao:

Hapana hakuna kilichoendelea kati yangu mimi na Linah ila tu alikuwa ni mshkaji wangu ambaye nina nyimbo naye tumefanya naye wimbo hakuna mapenzi kati yangu na Linah lakini kama meneja alikataa kurenew mkataba kisa wivu basi sio kosa langu”.