Malaika Afungukia Ukimya Wake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Rarua rarua’ Malaika amefunguka na kuweka wazi sababu iliyomfanya mpaka akapotea kwenye gemu.

Malaika amesema kuwa ameamua kukaa kimya kwa muda mrefu ili kuangalia upepo wa gemu unaendaje kwani gemu inabadilika kila siku.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Malaika Malaika alisema kuwa anajua mashabiki wake wanajiuliza kwa nini hasikiki tena kwenye muziki lakini ukweli ni kwamba yupo anaangalia njia nzuri ya kuwafurahisha mashabiki wake.

Japokuwa nasafiri huku na kule lakini yote hiyo ni kuangalia upepo wa muziki unavyokwenda na ni kitu gani mashabiki wanakitaka kwa hivi sasa kama ni Singeli, Mduara au miondoko mingine yoyote ili niweze kutoka tofauti”.

Uzuri Wangu Haujanibeba Kimuziki- Malaika

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutambana kibao cjha ‘Rarua rarua’ Diana Exavery maarufu kama Malaika amefunguak an kudai uzuri wake haujasababisha mafanikio aliyopata kwenye muziki.

Katika interview aliyofanya na Global PublishersMalaika alisema kuwa anajitambua kuwa yeye ni mzuri lakini anajitahidi kufanya kitu kizuri hata kama akikaa muda mrefu bila kutoa nyimbo lakini kutokana na msingi mzuri aliojiwekea tangu mwanzo hawezi kuanguka kama inavyokuwa kwa wanamuziki wengine.

Unajua hata uwe mzuri kiasi gani kama huna bidhaa nzuri sokoni ni kazi bure lakini uzuri ni kwamba uwe mwanamuziki wa kike mrembo halafu pia uimbe nyimbo nzuri kwa mashabiki wako hapo hata uzuri wa sura yako utaonekana na kukusaidia”.

Lakini pia Malaika amekana tetesi za kuacha muziki bali ameamua kupumzika wakati akijipanga kwa ajili ya kazi yake mpya siku za mbeleni.

Malaika Agoma Kumuanika Mpenzi Wake Licha Ya Usumbufu Mkubwa Anaopata

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao cha ‘Rarua rarua’ Malaika amefunguka na kusema hawezi kumuanika mpenzi wake hadharani ingawa anapata Usumbufu Mkubwa kutoka kwa wanaume.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Malaika ambaye alijizolea umaarufu baada ya kusikika kwenye ngoma ya Chege ‘Uswszi Take away’ amefunguka kuwa hawezi kumuweka wazi mpenzi wake:

Siwezi kumuweka hadharani mpenzi wangu kwani Sidhani kama ni sawa kuweka kila kitu chako binafsi nje, maana wanachotaka mashabiki ni kazi yako na sio uhusiano wako.

Lakini pia Malaika amefunguka kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa Wanaume hasa kwa sababu ya urembo wake:

Usumbufu upo mkubwa na ukizingatia ni msichana mzuri lakini hiyo haifanyi nimuweke wazi mpenzi wangu”.

Malaika ameongelea pia ukimya wake Kwenye tasnia ya Bongo fleva ambapo amesema alikaa kimya kwa muda kutokana na majukumu yake nje ya muziki.