Ebitoke Akiri Kumuiba Mume Wa Mama Ashura

Mchekeshaji maarufu kwenye Mitandao ya kijamii Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke amefunguka na kukiri kutembea na Mume wa msanii mwenzake Mama Ashura.

Skendo ya Ebitoke kumuiba mume wa Mama Ashura ambaye alikuwa Meneja wao Timamu Tv, Conrad Timoth zilianza Baada ya Mama Ashura kutimuliwa na Ebitoke kuchukua nafasi yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amefunguka kwamba yeye hakumfuata Timoth ili kuwa naye kwenye mahusiano, licha ya kuwa Bosi wake huyo ni mume wa muigizaji mwenzake, Mama Ashura.

Baada ya kuulizwa tetesi za kugombana na Mama Ashura kwa kumchukulia mume, Ebitoke alikiri haya.

Sasa ananimind mimi ndio nilimfuata Timoth nikamwambia njoo kwangu, Haya mambo yalishapitwa na wakati”.

Miezi michache iliyopita Ebitoke alitangaza kuondoka Timamu kwa Timothy na kufanya Sanaa ya kujitegemea muda michache baadae Ashura alionekana tena ndani ya Timamu.

 

 

Mama Ashura Ajikuta Katika Mgogoro Na Familia Ya Kiba.

baada ya tamasha la fiesta kufanyika jijini Dar Es Salaam, Mama Ashura ambae kwa muda mrefu amekuwa akitoa maoni yake ya kumkosoa msaini wa bongo fleva Alikiba ameibuka tena na kuongelea show aliofanya Alikiba usiku wa tamsha la fiesta lililofanyika pale Leaders Club.

Katika post yake ya kwanza msanii wa vichekesho nchini kutokea katika kundi la Timamu alisema kuwa  amekiona alichokifanya Alikiba katika fiesta na anatoa ushauri kwa Alikiba ili aache tabia ya kubweteka, huku akionekana kutoridhika na show ya msanii huyo aliofanya usiku ule.

Hata hivyo baada ya hapo Mama Ashura aliandika tena kwa undani kile alichokuwa anakimaanisha katika post yake ya awali aliyokuwa ameiweka katika ukurasa wake wa instagram.

Mama Ashura aliweka picha ya Alikiba tena na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsifia Alikiba kutokana na kuwa na ufundi katika sauti yake lakini kumbe kuwez ku-win kimziki  hakutegemei ufundi wa sauti tu bali hata vile unavyoweza kucheza na muziki wako na kuangalia mahitaji ya muziki na mashabiki wako.Aama ashura hakuishia hapo lakini pia aliweza kutoa mfano wa msanii Diamond Platinumz kuwa ndie anaeweza ku-copy na sauti na crowd yake anapokuwa jukwaani.

Hii inakuwa sio mara ya kwanza kwa Mama Ashura kumuongelea Alikiba na hata kuwachana mashabiki wake, hatua ambayo ilifikia kuwa na vita ya kimtandao kati ya mama ashura na Team-Alikiba katika kurasa za instagram.

Baada ya kuongea hivyo, moja ya watu wa karibu wa msanii Alikiba , dada yake anaejulikana kama Zabibu Kiba alijibu maneno ya Mama Ashura kwa namna tofauti kidogo huku akificha kuonyesha nani katupiwa dongo hilo.Zabibu alioneshwa kukerwa na watu wanaokaa na kumpigia kelele  kaka yake ilhali yeye anaona kaka yake anafanya vizuri katika muziki.

ukijua nini unafanya na nani anakutafuta hata dunia nzima ikupinge, utazidi kusonga mbele tukatika mafanikio ili kufika unapotaka  sio kila mbwa anaekubwekea  unatakiwa kusimama na kupigana nae.

hata hivyo mpaka sasa ,Alikiba mwenyewe ajaongea kitu chochote kuhusu tuhuma izo ingawa ndugu zake wameingilia ugomvi huo.

 

Mama Ashura Awapa Makavu Mashabiki Wa Alikiba

Msanii  chipukizi  wa vichekesho kutoka katika kundi la Timamu nchini Tanzania anaejulikana kama Mama Ashura amefunguka na kuwatolea mapovu mashabiki wa  Team Alikiba ambao wanajifanya wanampenda sana msanii huyo kumbe ni uongo.Msanii huyo ambae kipindi cha nyuma kabisa alishawahi kuandika katika mtandao wake wa Instagrma maoni yake kuhusu Alikiba na kumtolea mapovu msanii huyo kuhusu tabia yake ya kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo ni tabia  inayowachosha mashabiki wake, lakini badala yake baadhi ya mashabiki hao wa alikiba walikuja juu na kuanza kumtukana msanii huyo wa vichekesho na kujikuta akiingia katika bifu zito la kimtandao wa watu wanaojiita kama Team Kiba.

Alipokuwa katika mahojino na Times Fm, Mama Ashura  amefunguka na kusema kuwa  mashabiki wengi wa msanii Alikiba hawako real kama yeye anavyodhani bali wanamshabikia kwa sababau ni maadui wa Diamond, hivyo mashabiki hao wanaona njia ya kumuumiza Diamond ni kumsahabikia Alikiba na kuongeza idadi.Hata hivyo Mama Ashura anasema kuwa hata hao mashabiki wenyewe Alikiba hawajui ” hao mashabiki wenyewe Alikiba hawajui, alafu hawapi hata sapoti, mashabiki wa Alikiba sio wale wa real kabisa, ni maadui wa Diamond” anafunguka Mama Ashura

“Wengi wanakuja kwa alikiba na ku-take advantage,  huyo ambae  yupo tofauti na huyo lakini wangekuwa real  wasingekuwa wanatumia matusi katika mitandao kama njia ya kumsapoti msanii wao” aliongezea msanii huyo wa vichekesho

Hata hivyo Mama Ashura alisena kuwa yeye sio team ya msanii yoyote kati ya Diamond na Alikiba ila tu aliongea kama maoni yake na ushauri kwa Alikiba na mashabiki wake,kwa kuongezea Mama Ashura anasema kuwa inabidi msanii awe na shukrani pale ambapo mtu anafanya kitu kwa ajili ya kazi yake  na kutoa ushirikiano kwa watu wanaotoa sapoti kwake katika mitandao ya kijamii “Eric Omond alitoa Cover ya Zilipendwa ya Wasafi na akatoa  Seduce Me ya Alikiba lakini Diamond alicomment  ‘Asante’ kwa Omondi lakini Alikiba hakufanya hivyo” aliongezea msanii huyo